Ajali ya treni iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kwenda Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kigoma kupata ajali eneo la Mazimbu- Mkata Stesheni baada ya mtu asiyefahamika kufungua nati kwenye mataluma.
Kamanda wa Kikosi cha Reli Tanzania , Ruth Makelemo, ( kushoto) akiangalia taarifa ya abiria waliojeruhiwa katika ajali ya Treni ya Tanzania Railways Limited (TRL) iliyokuwa ikitokea Dar kwenda Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kigoma kupata ajali eneo la Mazimbu- Mkata Stesheni baada ya mtu asiyefahamika kufungua nati kwenye malaaluma ya reli Ijumaa usiku Mkoani Morogoro. Kulia ni Mwenyekiti wa Taifa TRAWU, Bakari Kiswala

Baadhi ya abiria wakisubiri usafiri mwingine baada ya treni kupinduka. TRL walitoa mabasi 10 kwa kusaririsha abiria hao. Taarifa toka eneo la tukio linasema safari zimeanza kamakawaida baadfa ya mabehewa hayo kuwekwa kando. na majerhu wawili walioumia ajalini wanaendelea vyema katika hospitali ya taifa ya muhimbili.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. kwa mtindo huu...bongo hatufiki.....

    ReplyDelete
  2. Hao bila shaka ni majambazi ambao wameshazoea kuona treni ikipata ajali tu wanawahi kuiba,,,Tanzania kweli tunatia aibu..wala sitamani kurudi huko puuuu.

    ReplyDelete
  3. kuna Uwezekano ni staff wa TRA wamekata mataruma ya reli, si unajuwa jamaa alikuwa kwenye mgomo wa kudai mafao yao. Serikali muwe fair walipeni hawa jamaa. Haya mambo hayatatokea. Pili Serikali wawafikirie wahathirika wa mabomu mbagala hii si vizuri watu wanalala kwenye mahema na watoto wadogo, wakati watu wengine wanalipa pesa za kufuru.

    ReplyDelete
  4. We anon wa pili kwani nani kakuambia urudi? nyoooo! Wala hatukutaki maana una mawazo ya kitumwa! Mkataa kwao ni mtumwa!Hata ukirudi utakuwa mzigo tu bora ubaki huko huko!

    ReplyDelete
  5. Hizi ni hujuma. Kuna baadhi ya watu au vyama wanataka kuharibu jina la serikali iliyopo madarakani. Hawezi tokea mtu ni mtu tuu akafungua hizo reli. Majambazi sio rahisi kama majambazi walikuwa wanataka kuiba si wangeiba?? Treni siilipinduka mbona hawajaiba?? Hakika nasisitiza si majambazi bali ni hujuma, ichunguzwe vizuri.

    Kipindi cha uchaguzi karibu, kila mmoja anatafuta kumchafulia mwenzake jina na yeye kujisafisha ili achaguliwe.

    Wananchi tuweni makini katika mambo, tutafakari kwa kina.

    Mfano kama hicho kifaa chakufungulia kisingepatikana ingesemekana miundombinu mobovu, Ingeanza kulaumiwa Serikali. Wangechonga wee lakini Mungu hamtupi mja wake wamelaaniwa wakasahau spanner chini.

    Mungu aibariki na aiokoe Tanzania katika uchaguzi ujao wapo baadhi wanataka kuharibu jina la Tanzania na amani yake Bara na Visiwani. Wazidi kuumbuliwa

    ReplyDelete
  6. Si majambazi jamani waliofanya hivyo kwani Sio kama nadharau ila tufikiri huku na kule Majambazi Wafanye hivyo wakiwa wanataka nini hasa kutoka kwa abiria hao wa Treni? Abiria hao hawana hela saana wala vitu vya maana sanaana hadi majambazi wafanye hivyo. Abiria kama wangekuwa na hela nahisi mtu asingekubali kupata mateso na kero ambazo zipo katika treni kukaa siku nyingi njiani wakati Mabasi, Ndege zipo.

    Hiyo ni hujuma za baadhi ya watu wa serikali.

    ReplyDelete
  7. Sio staff wa TRA wamekata. Staff wakate ili wafaidi nini? Wakishaua wananchi wenzao ndio watapata malipo yao?

    Labda kuna jamaa alikuwa anataka atoe kafara hapo lakini Mungu kamlaani hajafanikiwa sababu hakuna aliyekufa.

    ReplyDelete
  8. Kama sio dili la skrepa basi wadosi wamehujumu ili wawasingizie wafanyakazi wazalendo wasiwalipe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...