Vodacom Tanzania imeboresha zawadi zake MPYA na BOMBA za Tuzo Pointi mahususi kwa wateja wote Vodacom wa Malipo ya Kabla, VodaJaza na Malipo ya Baada.
Kujikusanyia Tuzo Pointi
Wateja wa Vodacom Tanzania wanaweza kupata pointi kwenye matumizi yote ya Vodacom – inajumuisha kupiga simu, kutumia Internet, SMS, MMS, gharama za kujiunga na malipo ya kila mwezi.
Kwa wateja wa Malipo ya Kabla & VodaJaza:
Kwa kila Tsh 100 inayotumika (Bila ya Kodi: VAT & Excise) kwenye kupiga simu, SMS, MMS na kutumia Internet = 1 Tuzo Pointi.
Kwa wateja wa Malipi ya Baada:
Kwa kila Tsh 500 inayotumika (Bila ya Kodi: VAT & Excise) kwenye kupiga simu, SMS, MMS, Kutumia Internet, gharama za kujiunga na malipo ya kila mwezi = 1 Tuzo Pointi
Kwa kila dakika MOJA unayoongea na simu kutoka kwenye mtandao mwingine wa Kitaifa = 1 Tuzo Pointi
Kwa kila wiki MOJA unayoendelea kuungwanishwa na kutumia mtandao wa Vodacom = 1 Tuzo Pointi
Kuangalia Tuzo Pointi zako BURE!
Wateja wanaweza kuangalia idadi ya Tuzo Pointi zao BURE kwa kuandika maneno TUZO POINTI kwenda 123.
Jipatie zawadi zako za Tuzo Pointi BURE!
Wakati wowote mteja anapokuwa na pointi za kutosha, anaweza kubadilisha na kupata zawadi MPYA na BOMBA za Tuzo Pointi.
· Ofa za Simu: Simu za Kisasa
· Ofa za Internet: USB Modem, Simu za Kisasa, Laptop & BlackBerry smart phone
· Ofa za Vifurushi: Vifurushi vya SMS, Vocha za Internet & Punguzo la kupiga simu

Wateja wanaochagua kujipatia simu, Vocha ya Internet, USB Modem na Laptop watapokea SMS itakayokuwa na neon la siri.
Mfano: Umeamua kuchagua kujipatia simu yenye pointi sawa na XXXX. Salio la Pointi zako ni XXXX. Neno lako la siri ni XXXX. Tembelea Vodashop au Depot yeyote iliyo karibu na wewe ujipatie zawadi yako. Neno hili la siri lazima liwasilishwe wakati wa kuchukua zawadi.
Kujipatia zawadi yako ya BURE (Simu, Vocha ya Internet, USB Modem au Laptop), wateja watatakiwa kujaza fomu kwenye Vodashop au Depot. Hakuna kujaza fomu wakati wa kupata zawadi za Vifurushi vya SMS au punguzo la kupiga simu za Vodacom kwenda Vodacom.
Wateja wanatakiwa waandike vitu vifuatavyo wakati wa kujaza fomu:
Namba ya simu (MSISDN),
Majina kamili (Cheo, Jina la Ukoo na vifupi),
namba ya kitambulisho chako (Kitambulisho cha kupigia kura, Leseni ya Udereva, Pasipoti, Kadi ya Matibabu n.k.),
Anuani ya Posta & Mahali unapoishi na Kazi unayoifanya.
Kwa maelezo zaidi, piga BURE
0753 300006 (Swahili)
au
0753 300007 (Kiingereza)
*Vigezo na Masharti kuzingatiwa
Pamoja daima
Vodacom Tanzania
nimeipenda hii!!
ReplyDeleteHii kidogoafadhali, manakemwanzoni ilikuwa ili ubahatike kupata kitu kizuri inabidi upate pointi zaidi ya 10,000. ni sawa na kununua vocha za shilingi 500*10,000 au?
ReplyDelete