hapa ni La Kairo hotel, Bariadi, mikonozzz kama kawa..
anko nanihii na mwenyeji wake, mtendaji wa kata ya Iseni. huo mwembe pale nyuma una mambo flani hivi...
anko nanihii amebahatika kupiga vekesheni karibu kila pembe ya dunia ila hii vekesheni ya mwanza haitosahau maana pamoja na kutembelea vijijini ndani ndani huko, alibahatika kuzuru boma la mganga maarufu wa jadi anayeishi magu, kata ya iseni, mzee masakumaka lwamongo ambaye alishinda naye na kuona anavyofanya shughuli zake. shukrani ziende kwa HelpAge International waliofanikisha vekesheni hii ya aina yake. chini na juu ni boma la mzee lwamongo. upitapo maeneo hayo na kukuta madishi na ma-anttena ya sampuli hii basi ujue hapo ni nyumbani pa profesa wa mambo fulani....
mzee lwamongo na familia yake


hati ya kumruhusu kufanya uganga wa jadi. hii ni kabla havijafutwa na serikali


sera za hapa asiyefanya kazi, na asile


mpunga ukigeuzwa kuwa mchele


taswirazzzz...









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. misupu umeanza kwenda kwa vigagu basi tena naona ndoa haiendi vizuri au unataka kugombea ubunge, haya sisi yetu macho bana tuone kama hivyo vindumba vitafanya kazi..... lakini umepoteza muda bure ungeenda bagamoyo tu hapo, we uoni rafiki yako maggid mjengwa hakauki bagamoyo sasa hivi kishakua lecturer wa vyuo vya maendeleo.

    ReplyDelete
  2. naona hii vekesheni itakuwa na mafanikio kweli mpaka kanda ya ziwa umekutana nao au ndio nawe ulienda kuangalia km viungo vinafanya kazi vya nduguzetu maana mhmm 2010 karibu na majimbo ndio hayo mafisadi awayataki sasa kazi kwako sera au sangoma anko
    mdau hyderabad india

    ReplyDelete
  3. Michuzi I congratulate you for these photos. Very educational.

    I wish Dar-based journalists could be travelling to remote areas and bring us such interesting pieces. Many of them just go aroung at Maelezo offices, hunt for seminars and workshops, then go home.

    Tanzania Media Fund has enough funds for them to conduct such kinds of researches but alas, they are not aware of that. Poor thinking is barring them from reaching to such places. Let them wake up

    ReplyDelete
  4. kazi nzuri. kitu ambacho wabongo wengi hawajui au hawataki kukiri ni kwamba watanzania takriban asilimia 80 wanapata huduma ya uganga wa jadi. wale wanaoishi kwenye pembezoni kama hizo, hiyo ndio huduma yao kuu. wale wa dar nusu ya tiba muhimbili na nusu kwa sangoma. basi tu watu huwa hawataki kukiri au kuambiwa ukweli. sangomas bado wanatoa mchango mkubwa katika tiba (kisaikolojia) kama maji ya kinjekitile yalivyokfanya kazi wakati wa vita ya majimaji. ninapendekeza warejeshewe usajili wao na wale wanaofanya vitendo vya mauaji waadhibiwe kama wataalamu wengine katika nyanja nyinginezo.

    ReplyDelete
  5. Bro Michuzi nakupa hongera sana.Jamaa wengi(majority) wanaishi katika maisha ya chini kabisa na sisi hatiyaoni hayo maisha, huenda kwa kuchagua kutoyaangalia.Wewe ni kiboko kaka, Yaani sina mfano nawe, we need watu creative with creative thinking na sio tu kuona majipicha ya uwongo na kweli(picha za kijuiandaa) we tend to show the pics which are not really us!!Yaani kaka sijui nikupe nini?Nina Binti labda nikupe uoe mke wa pili...!
    Ramadhan Karim
    Mdau
    Wigan karibu na Ilala

    ReplyDelete
  6. MISUPU HANA LOLOTE ALIKUA TU ANATAKA KUWAONESHA WALE WANAJIFANYA SIO WASWAHILI WAO WAZUNGU AMA WAARABU WEUSI WATUMWA WA KIFIKRA WANAUPONDA USWAHILI NA KUUTUPIA USWAHILI KILA LILOBAYA.ALITAKA KUWAONESHA KUA WATANZANIA WOTE WANAOJIVUNIA USWAHILI NDIO WALIOSTAARABIKA KULIKO WALE WANAOJIFANYA SIO WASWAHILI HUKO MAKWAO WALIPOTOKA NI MASKINI WA KUTUPWA WAKISHAFIKA MJINI WANATUKANA WATU!!
    YANI KILA AINA YA MABAYA NI KWAO UMASKINI ULIOKITHIRI MPAKA WANAKULA MAPANKI YALIOODHA,UCHAWI NA IMANI NYENGINE ZA KISHIRIKINA,KUUA MAZERUZERU,KUCHUNA NGOZI WATU,UPAGANI NA UJAMBAZI,KUPENDA UKABILA NA CHUKI ZA KIKOO NA MENGINE MENGI MACHAFU NI HUKO KWAO
    LKN SISI TUNAJIVUNIA USWAHILI POPOTE TANZANIA HATUNA HAYO TUNAWAKILISHA USTARAABU YANI CIVILISATION TUNAJIVUNIA UMOJA WETU WAKUWA WATANZANIA NA SIO UKABILA

    ReplyDelete
  7. Hapo ni Tanzania mkuu michuzi ?



    Majid abdull karim

    ReplyDelete
  8. Naona mzee wa vacation ameenda kumtembelea bibi katika ku renew mambo yake. Haya baba kwa bibi ni muhimu maana ndiko ulithi wote unatoka. Ila aangalia na ww usije anza kurithi maana hamchelewi. Jamani lakini hawa waganga wa kienyeji mbona mazingila yao ni magumu sana? wao ni kuwapa watu utajili mbona wao hawatajiriki???? Ama ni moja ya masharti ya kuwa mganga? KWA BIBI HOYEEEEE!!!

    ReplyDelete
  9. Abdul Massoud, MikanjuniAugust 24, 2009

    Anko Michuzi, nasikia ulikwenda kuuza viungo vya albino ambavyo ulivitia kwenye huo mkoba wa kubebea kamera. Teh Teh Teh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    Abdul, 5yrs old boy

    ReplyDelete
  10. ...uo mwembe una mambo fulani GANI??...

    fafanua na wewe alaa

    ReplyDelete
  11. Hicho ni kijiji cha brazamen mmoja na masister du kibao ambao ukiwauliza kwenu wapi wanazuga Darrisalama ama Mwanzza mjini.

    NApajua hapo
    Usukumani halisi.

    Bora umetoa fact ya Mwanza kukoje ili wasukuma wapunguze malingo ma uwongo wa kwao wana magorofa na mabenzi na sio mingombe

    ReplyDelete
  12. Eti ulienda kuchajisha! Inafanana na ukweli ama sisi ni wa Bwagamoyo?

    ReplyDelete
  13. Michu,

    Huyo Mganga inabidi afundishwe uzazi wa majira maana asipoangalia ataua huyo mama kwa kumzalisha:-) Duuh hebu tazama watoto walivyopea kwa utapi wa mlo na bado wanahitaji attention ya mama lakini wapendana namna hii.

    ReplyDelete
  14. MICHUZI MIMI NAONA KUNA MTU AMEKUUZI UKAMUA KUMUENDEA KWENYE KATIBA.

    ReplyDelete
  15. Nimekumbuka mbali nilipoona picha ya kinu kina mchele, yaani siku hizi nyumba za dar hakuna hicho kifaa kwa sisi wa enzi za mwalimu yaani mpaka miaka ya 1993 karibu kila nyumba kuna kinu kwaajiri ya mahindi ya kande, mpunga na majani ya muhogo(KISAMVU)

    ReplyDelete
  16. Si useme tu kwamba umekwenda kurekebisha nyota! Wewe siyo wa kwanza, wengine huenda Mlingotini Bagamoyo, wengine Sumbawanga, wengine Pemba n.k. kwa hiyo usione ajabu au aibu. Au umeanza kujiandaa na harakati za uchaguzi wa mwakani!

    ReplyDelete
  17. NYIE MNAOTOA MAONI NA KUSEMA MICHUZI ALITAKA KUONYESHA HALI YA HUKO MWANZA ILI WASUKUMA WASIJIDAI SASA HAPO MMEONA NINI KIBAYA??
    KWA TAARIFA YENU HAO WATOTO WANAPATA MILO MITATU KWA SIKU SIO KAMA NYIE UMBEYA MPAKA KTK BLOG

    PILI WASUKUMA WAKIWAAMBIA SI WAMBEYA NI KWELI MNAONAJE KTK PICHA HII JILANI MMEMUONA????
    MSIWAONEE WIVU WENZENU ARDHI WAMEJARIWA NA NG'OMBE,ZIWA MADINI MUNGU AWAPE NINI PIA WANAJITUMA HAWACHEZI BAO KAMA NYIE

    ReplyDelete
  18. Walahiiiiiiii, Asante sana Michuzi.
    Hii Dunia kubwa leo nimeyaona ya Musa!

    Huyo ni Mjomba wangu nimempoteza miaka mingi sana. Ndiye aliyenipeleka Japan. Wasomaji naomba email na anuani yake nimtumie I-Phone niweze kuwasiliana naye. Nashukru sana ameweka Antena. Tutakuwa kunaongea bure kwa Skype masaa 24. Naona amekuwa Millionaire kijana mdogo. Meno nje muda wote, na anamsaidia mkewe kutwanga pamoja na kazi zingine. Watoto wana afya tele. Nyie Wazaramo kutwa kupigana, kusemana na kupeana Taraka na wake zenu mna matatizo gani?
    Nendeni Sukumaland mkajifunze kuishi na wake zenu! Karibuni sana Sukuma Land. Ardhi tele, Dhahabu tele, Sangala tele ha unasshi bila jirani karibu - Hamna umbeya

    Asema Mabele Masangu. (mabele_masangu@yahoo.com)

    ReplyDelete
  19. ASIYE FANYA KAZI NA ASILE!!!! WAGONJWA JE? MBONA HII NADHARIA HAIPO SPECIFIC! COPY AND PASTE? JAMANI TUWE TUNAFAFANUA MABO AMA LA AKINA SIYE TUTAFANYIA KITU MBAYA KUMBE SIYO.

    ReplyDelete
  20. We Mabele Masangu huyo mjomba wako alikupeleka na Ungo huko Japan? Na huyo mbwa hapo ni mlinzi wa hizo madishi na ma-anttena? Jamani watu bado wanakwenda kwa waganga?

    ReplyDelete
  21. UNAFANYA KAZI NZURI SANA MICHUZI..ENDELEA KUTUBURUDISHA NA KUTUWEKA TUENDA NA RATIBA ZA MICHAPO YOTE. ASANTE BABA MZAZI, WEWE POA SANA..

    ReplyDelete
  22. www.chakachua.blogspot.com
    MDAU HII BLOG INAUHUSIKA NA VITU VIFUATAVYO
    • Kutangaza bidhaa mbali mbali zinazouzwa, zilizotumika na zilizo mpya kwa bei nafuu pia wadau wote wanaruhusiwa kutuma bidhaa zao ili zitangazwe bure.
    • Pia inatangazia raia wenye ujuzi mbalimbali kujitangaza kama wathamini wa majengo(valuers),uchoraji wa ramani(architect),ushauri kuhusu mambo ya ardhi (land consultancy) na matengenezo ya kompyuta

    KUJIARI WENYEWE TANZANIA INA WEZEKANA
    Tupo pamoja mdau respect kwako!

    ReplyDelete
  23. Mabele Masangu hapa, Hasira za nini wataka kuniua bure, kisa nimeenda Japani. Toka lini ungo ukavuka bahari ya Hindi? Naona wewe ni Nshomire siyo Mzaramo. Mjomba analalamika amepata majirani. Kuna Nshomire sita Wamenunua ardhi kumzungka ati wanasubiri mji wa Mwanza upanuke wauze ardhi kwa faida. Msiige Wazaramo. Wazaramo washituka hivi sasa, Miji inapanuka kwenda juu na kwenda chini!

    ReplyDelete
  24. Hello Tanzania. Jamani mimi mtanzania mwenzenu Nina shida naitaji kufika kwa mganga haswa wala sina nia mbaya ni mambo ya maisha na kazi.nimeshapitapita baazi ya sehem lalin sikuona mafanikio

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...