steve kanumba aongea na wenzie juu ya filamu mpya ya village pastor pamoja na sababu kwa nini filamu za kimatumbi zina majina ya kiinglishi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Kanumba is very smart! I like the way he can arrange and present his his points.

    ReplyDelete
  2. Ebwana kanumba kaongea point hapo ya kua yule bwan thabeet kaalikwa mpaka ikulu wakati hawa wasanii wa bongo hata hawapi kipaumbele kwa kweli mr president angalia hili swala usipagawe wa tz waliopo nje ya bongo

    ReplyDelete
  3. Nice interview, huyo kijana ana upeo na nadhani fani itaendelea kumkubali!

    ReplyDelete
  4. KANUMBA UPO JUU MWANANGU,KAZA BUTI

    ReplyDelete
  5. Tatizo ni ulimbukeni wa lugha. Kwani kuna tatizo gani kwa hiyo filamu kuitwa MCHUNGAJI WA KIJIJINI kisha kwenye mabano iandikwe Village Pastor kama suala ni kuvutia soko la nje? Nadhani walengwa wakubwa ni watu wanaoelewa kiswahili (wamatumbi wa kawaida) hivyo wasanii waondokane na dhana nzima ya kukitukuza kiingereza kwa filamu za kiswahili. Picha ya kiingereza iwe na jina la kiingereza, picha ya kiha iwe na jina la kiha, ya kiswahili iwe na jina la kiswahili...acheni visingizio visivyo na kichwa wala miguu.

    ReplyDelete
  6. Ila Kanumba, Ray na wengine wa filamu za KIMATUMBI inabidi kuzingatia:
    -mila za mwaafrika
    -tamaduni za kiafrika
    -maadili ya kiafrika
    -lugha sahihi
    -washiriki wa filamu wazingatie madili hata kama mchezaji wa filamu atapewa mfano uonekano wa 'playboy' , basi pamoja na hiyo 'role' utamaduni na maadili ya mtanzania yazingatiwe.
    - yaani kwa kifupi filamu zetu ziwe zenye maadili ya 'heshima' kama ktk filamu za Kihindi na Kiarabu, tusitie u-Hollywood.

    Mwisho Kanumba na sekta ya filamu Tanzania mjue Tanzania Tv huangaliwa na familia nzima na jirani zao, sio kama huko Ulaya ambapo nyumba nzima inakuwa na 'mtu mmoja na 'pet' wake'

    Mdau
    WaKunyoosha Maadili
    Mbezi Juu.

    ReplyDelete
  7. MJOMBA MICHU HABARI ZA LEO. NDUGU YANGU KAMA INAWEZEKANA UWE UNATUWEKEA MATOKEO YA LIGI YA VODA YA TAANZANIA ILI TUWEZE KUJUA KWANI KUNA TIMU AMBAZO ZINATUPA MOYO WA MAENDELEO NAZO NI AFRIKAN LYON. AZAM,MTIBWA NA MORO UNITED
    WAKO
    JAMES PHILLIP
    POLAND

    ReplyDelete
  8. Bunch of booooooooooooo...Yaani wabongo tunamdharau President kiasi cha kumuomba atukutanishe na hollywood superstar.Eti kanumba anasema C.T hakumshika mkono.none sense nonsense. Instead ya kuoma baraza la sanaa au minister of Sports anamuomba Rais.Shame on us. na anachoomba eti ashikwe mkono.Jamani huu ulimbukeni utatufikisha pabaya.
    Ni hayo tu. Ila Misupuu your tone kwenye hii dialogue inaonekana kabisa hukubaliani na huyu jamaa.
    naomba namba ya aunt ezekieli maana ni msupuu haswa

    ReplyDelete
  9. hapo mwisho mwisho kanumba umeongea point...big up....

    ReplyDelete
  10. Hii tabia ya kubeba mashuka naona imeenea mpaka wanaume sasa hivi wameshanza kuvaa kama kijana huyu hapa.
    kazi kwoko michuzi na wewe sijui utaanza kuvaa lini.

    ReplyDelete
  11. Siasa tupu kwenye Uigizaji. Sasa raisi awazungumzie nini? Lini Raisi alimzungumzia Hasheem? Mbona yeye ametoka kivyake? Fanyeni mambo mkiwa poa Raisi atawazungumzia tuu na kuwakaribisha ikulu, lakini sio sasa hivi ni hovyo kabisa. Mnapiga siasa tu

    ReplyDelete
  12. Mpemba 100%August 23, 2009

    Daah kweli nakubalina na maneno ya Allah (SWT) aliposema "Hawawi sawa wenye elimu na wasio na elimu.." Hapa ndo pana dhihirisha umuhimu wakukaa madarasani! Sipati picha mugazaji nyota Tanzania anajibu MAKAPI kiasi hicho....!Eti kiswahili hakijitoshelezi...! Ha ha ha sasa hiyo "title" ya kiengereza ndo imetosheleza nini ikiwa ndani mnazungmza kiswahili??Huyu kweli mshamba! Anafananisha majina ya vyama vya siasa na title za movie! Aibu kweli hawezi ku reason hata kidogo! Na huyo Anti ezekiel nae ndo wale wale...! Sanaa ya uigizaji Tanzania ni akina King Majuto, mzee small, bichau , mtanga na bambo. Hawa wengine vurugu mechi tu!

    ReplyDelete
  13. kumbe thats how jokate looks..photoshop zasaidia

    ReplyDelete
  14. Hivi wewe bwana kanumba kwanini sasa hivi unaonekana saana ukiwa na hicho kijitambaa shingoni?au na Dar sasa hivi balidi ni kama Sweeden?mbona sasa hivi hushilikiani na Kigosi? yani mala nyingi mkiwa wewe na Kigosi mkanda unakua super saana ..jitahidi ushilikiane naye mtafika mbali.

    ReplyDelete
  15. Jina la filamu kuwa kwa kiingereza linasaidia hata yule asiejua Kiswahili kuifuatilia filamu hio na kuielewa (kupitia vitendo mbalimbali vinavyoonyeshwa) ili mradi anakuwa ameshajua itakuwa inahusu nini. Watengenezaji hawalengi Tanzania pekee lakini wanapenda kutumia lugha ambayo wataongea kwa ufasaha zaidi.

    Kwetu sisi wa Tanzania inajulikana tuna lugha mbili kuu na kwa jinsi inavyoelekea imeshazoeleka kuzichanganya hata ukienda kwenye ofisi mbalimbali utakuta lugha zote zinatumika. Kurekebisha itakuwa ni jambo la kitaifa na si mtu mmoja mmoja.

    ReplyDelete
  16. Kakamichuzi unazidi kutouch kwenye moyo wangu.
    jamani mi naomba nitoke nje ya kijitopic kidogo. Ni kwamba mimi ninampenda sana huyu dada aliyetokea mwanzoni mwa hii script huyo anayeitwa Jokate Mwegelo. kwakweli nampenda sana huyu dada jokate baada ya kumfuatilia kwa muda. yani huwa nikiona picha yake kwenye magazeti mtandaoni au hapa michuzi huwa mwili unasisimka sana, kama hapa nimemuona nikasikia nimesizi kabisa. kwakweli kila napofikiria kutafuta mwenzangu wa kuishi naye huwa namfikiria huyu dada. tatizo niko nje na sijui jinsi ya kuwasiliana naye. nimejaribu kuomba namba yake kutoka kwa mwandishi fulani wa globo publishers akaniyeyusha. jamani naomba mwenye kuweza kuniunganisha na huyu dada hata kwa email yake au sim namba nitashukuru sana na nitatoa zawadi nono. kwa kweli niko serious sana katika hili. ni jinsi tu ya kupata mawasiliano naye. naomba kama kuna ambaye yuko tayari aniambie hapa kwenye hii post ili tubadilishane mawasiliano tuwasiliane kwa siri. nitashukuru sasa na ninaahidi zawadi. kaka michuzi i'm pretty sure that you always read these comments before posting them up, please if you come across this one and think that there is a way to help me, please do the needful brother. i really need to be put in touch with this girl. she's a girl of my dream and i'm really happy and deeply touched by her appearence in here today. i promise a very handsome prize for the one who's gonna ease my communication with her.
    Nitashukuru sana
    Mdau, PhD candidate, Southampton Uni.

    ReplyDelete
  17. Hicho kitambaa kina Maana Gani?
    Mbona Wengi wanavaa sielewi.

    ReplyDelete
  18. kwa mdau uliyeulizia ligi ya nyumbani matokeo ni kama haya
    African lyon vs timu ya wananchi yanga lyon 1 yanga 1
    simba 2 majimaji 0

    ReplyDelete
  19. KIINGEREZA CHAO KIGUMU, SASA HATA TITLE TUSHINDWE KUANDIKA? UKWELI UTABAKI KUWA UKWELI KIINGEREZA KINATUSHINDA HATUKIJUI, ILA UBISHI MWINGIiiii KAMA TULIVYOLONGA ZAIN AFRICA CHALLENGE, WAKATI ILIPO TANGAZWA TULIDAI KUWA KUMEJIANDAA VIZURI LAKINI KUMBE TULIJIANDAA KUSHIRIKI TU.WATANZANIA TUKO JUU ZAIDI YA NCHI NYINGINE.

    ReplyDelete
  20. Kanumba umesahau maneno nilyokuambia pale Reading(UK)usiku ule,wewe ukiendekeza kulalamika utasahau kuigiza waachie watu wengine wafanye kazi hiyo.we ongeza ufanisi katika kazi yako ili uzidi kuimarisha soko lako(market share) na kadri unavyofanya vizuri zaidi watu wanaona sasa unataka serikali ifanye nini?tatizo hapo sio serikali bali soko limezungukwa na watu masikini angalia kwenye nyumba zetu jinsi watu wanavyojazani kwenye TV moja kuangalia mchezo hii ni dalili tosha uchumi ukiimarika watu watanunua kazi zenu.hivyo jitihada zako ni changamoto kwa vijana wengine kujiajiri kwa kutumia vipaji vyao na kutoa ajira kwa wengine hivyo kujenga uwezo(capacity)kwenye soko la sanaa.

    ReplyDelete
  21. kanumba hacha ushamba na wivu presdaa hapangiwi kwanza hasheem yuko kimataifa zaidi kuliko kigosi na wewe mnajulikana wapi tz tu halafu film ya the director hamna kiwango hata chembe jitahidini,mambo mazuri ujitangaza yenyewe.

    ReplyDelete
  22. Kwa faida ya watengenezaji, waigizaji na watazamaji wa hizo mnazoziia filamu(movie za tanzania),

    ever since nimeanza kuangalia, nabaki naumia roho, a friend of mine(from holland) once asked about one movie(something like village pastor), ilibidi nisingizie ni movie ya wa kwenya kwa aibu, kwa kweli mnakera, scripts haziendani na uhasilia, watu wanaonekana wamemeza maneno kabisa,lightings mbovu, hamna cinematographers, screen plays are not scripted, hmna professionalism in any field,wahusika atleast muwe mnaangalia movie za nje na mjifunze acheni kuangalia movie za kinaijeria, scene moja inaweza ikachukua zaidi ya dak 5 na inarudia mara kwa mara hadi unaboreka, unakuta movie ina masaa matatu hamna lolote ndani,

    ReplyDelete
  23. Kwa kweli kuna improvements kubwa katika sinema zinazotengenezwa Bongo. Lakini bado hazijafikia standard ya Hollywood. Nendedni mkasome Filmmaking 101 kwanza.

    ReplyDelete
  24. Kanumba unajitahidi, ingawaje unamengi mno kujifunza, ujitahidi kuangalia filamu za nje kuboresha ufanisi wako. Tatizo kubwa nililo nalo ni vile mnavyopandisha sauti zenu na muda wote kufokea ambao mnawaita wake zenu hii inaleta picha mbaya sana kwa watu wanaoangalia movie zenu, mimi nilikuwa naangalia movie moja na rafiki yangu hapa USA nilikuwa namtafsiria mnachoigiza akaniuliza huko kwenu wanaume kazi nikofekea wake zao? kwani kila movie tunayoangalia wote ndio anachoona, kwa hiyo msitudhalilishe jamani. Kingine vp siku hizi Tz kumekuwa na winter? mbona Kanumba unacover shingo isipigwe na baridi?? Utapata mapele ya joto weeeee!! koma kuiga kuiga mambo ya Ulaya ambayo hayanamsingi, iga vitu vitakavyokusaidia katika fani yako.

    ReplyDelete
  25. Nawapongeza watoa maoni waliotangulia hapo juu hasa anonymous wa Mon Aug 24, 10:27:00 PM, kweli filamu zetu bado zipo katika viwango vya chini sana na inasikitisha ukizingatia dosari nyengine ni nyepesi na rahisi sana kurekebishwa lakini bado zinajirudia karibu kila filamu.

    Matatizo ninayoyaona, ni kama alivosema mdau godfather hapo juu watengeneza filamu wetu bado ni amateurs sana wengi wanahitaji angalau hiyo filmmaking 101. Wanachojua ni kuiga vitu vya kinaijeria tu, sijui labda vile wanalenga soko la uswahilini zaidi.

    Wanashindwa hadi na vitu very basic kama lighting set up, jinsi ya kucompose shots, au kuadjust exposure ya camera kulingana na mwanga uliopo pia ni ngumu kwao, wakati kila mpiga picha anapaswa kujua hayo. Filamu hazina viwango kabisa, yani kuna filamu za kibongo nimejaribu kuwatch nashindwa kuendelea baada ya dakika 10 za mwanzo tena nyengine zimefika kupewa tunzo. Scripts ndio mbovu, yani hakuna uhalisia kabisa, poor dialogue ukichanganya na uingizaji wenyewe mgogoro tu, wenyewe wanasema "Acting is acting like you are not acting" yani igiza kwa hisia kama vile hiyo nafasi unayocheza ni mtu halisi kwenye jamii. Wanachojua wao ni kuweka annoying soundtracks hata zisizoendana.

    ReplyDelete
  26. mambo vp mzee wa bwawa la maini?pole nakazi kwanza.
    kaka kanumba anajitahidi sana ila bado nayeye anakale kaugonjwa kakuiga mtu fulani kutoka nigeria hiyo haija kaa sawa,pili mandalizi ya filamu zetu ni dumu haiwezekani mtu kwa mwezi anatoa filam mbili lazima zinakua hazina uwezo tutaishia kuza hapa hapa bongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...