Washtakiwa wa wizi katika benki ya NMB tawi la Temeke jijini Dar leo walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi 12 zikiwamo za mauaji, pamoja na wizi wa kutumia silaha.

Kati ya watuhumiwa nane waliopandishwa kizimbani, yumo askari wa Jeshi la kujenga Taifa (JWTZ), MT 55935 Sajent Methew Magunga.

Watuhumiwa wengine ni pamoja na wafanyabiashara Boniface Joseph, Deogratious Masawe, Antony Jeremia, Said Hamisi, Isaac Swai, Jackob Salumu na Yusuph Rajab.

Katika kesi hizo, washitakiwa hao wamehusishwa katika kesi za wizi wa magari kadhaa katika maeneo tofauti, ikiwa ni pamoja na wizi wa vitu mbali mbali.

Aidha watuhumiwa hao, walipandishwa kizimbani kwa awamu tofauti tofauti katika kesi hizo, huku wakisomewa mashtaka na Mawakili wa Serikali pamoja na Mahakimu tofauti tofauti.

Katika kesi ya wizi huo wa benki ya NMB, washitakiwa hao walipandishwa kizimbani wote, mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo na kusomewa mashitaka ambapo wote walikana.
Kesi zao zitatajwa tena Septemba 9 kwenye mahakama hiyo hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. JWTZ ni jeshi la wananchi tanzania..........kfnabo

    ReplyDelete
  2. Haya nayo ni mazingaombwe mengine tu. Jaji atasema hakuna ushahidi wa kutosha kwa vile hakuna mtu aliwaona waki-pull trigger! Hizi sheria jamani, bora tujichukulie mikononi tu.

    ReplyDelete
  3. HAYO MAJINA YA WACHAGGA NI YA UONGO. HAO JAMAA WENYE MAJINA YA KICHAGGA SIO WACHAGGA. UIZI WA NAMNA HII HATA SIKU MOJA HAUFANYWI NA WACHAGGA. WACHAGGA NI WATU WANA MUAMINI YESU. HAO WATU NINAFIKIRI WANATOKA SEHEMU ZINGINE ZA TANZANIA NA SIO KILIMANJARO.

    ReplyDelete
  4. Dr. Michuzi - I have seen them pictures of the victims was horrible and if I were the judge - these people need to be life sentenced without any parole.

    Mdau - Wichita, Kansas.

    ReplyDelete
  5. Waosha vinywa!!!
    Ama Kweli huwezi kumjua jambazi kwa kumuangalia sura, Watuhumuwa jana walionyeshwa katika TV (news) na huwezi kabisa kusema kama wanaweza kushiriki katika uhalifu kwa kuwaangalia sura zao. Wanaharakati wa haki za binaadamu, kuna polisi mmoja jana alimnyanyua kichwa juu kwa nguvu mtuhumiwa mmoja ili apigwe picha pale mahakamani, jee hii ni sheria?
    Ndau, Zenj

    ReplyDelete
  6. Tumeishazoea hakuna jipya litakalotokea zaidi ya kusema hawana atia,,, si mda mrefu watakuwa mitaani kama kawa. Kama ya Zombe yamekosa ushaidi itakuwa hao?

    Mdau toka,, Malaysia,,,,,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...