Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kesho, Jumatano, Septemba 9, 2009, atazungumza moja kwa moja na wananchi kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na vyombo vingine vya utangazaji nchini kuanzia saa mbili na nusu usiku.
Mbali na TBC, televisheni nyingine za ITV, TVZ, Mlimani TV, Tumaini TV na Channel Ten zinatarajia kuonyesha mazungumzo hayo.
Rais atatumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao, kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, Serikali yetu na maendeleo yetu.
Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.
Mazungumzo hayo yatakayochukua muda wa dakika 90 kuanzia saa mbili unusu usiku (saa 2:30 usiku) hadi saa nne kamili usiku.
Aidha mazungumzo hayo yatatangazwa kwenye redio za TBC-Taifa, Sauti ya Tanzania, Zanzibar, Radio Mlimani, Radio Clouds, Radio Tumaini, na Radio Uhuru.
Maswali, maoni, hoja, ushauri utapokelewa moja kwa moja na TBC kupitia simu nambari
Rais atatumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao, kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, Serikali yetu na maendeleo yetu.
Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.
Mazungumzo hayo yatakayochukua muda wa dakika 90 kuanzia saa mbili unusu usiku (saa 2:30 usiku) hadi saa nne kamili usiku.
Aidha mazungumzo hayo yatatangazwa kwenye redio za TBC-Taifa, Sauti ya Tanzania, Zanzibar, Radio Mlimani, Radio Clouds, Radio Tumaini, na Radio Uhuru.
Maswali, maoni, hoja, ushauri utapokelewa moja kwa moja na TBC kupitia simu nambari
+255-22-2772448,
+255-22-2772452
na
+255-22-2772454.
Aidha, maswali, maoni, hoja ama ushauri unaweza kutumwa moja kwa moja TBC kupitia ujumbe mfupi wa SMS kwenye nambari
Aidha, maswali, maoni, hoja ama ushauri unaweza kutumwa moja kwa moja TBC kupitia ujumbe mfupi wa SMS kwenye nambari
0788-500019,
0714-591589
na
0764-807683
ama kupitia kwenye barua pepe
kuanzia leo.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inawashauri wananchi kutumia kikamilifu nafasi hiyo ya kuwasiliana moja kwa moja na Rais wao.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
08 Septemba, 2009
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inawashauri wananchi kutumia kikamilifu nafasi hiyo ya kuwasiliana moja kwa moja na Rais wao.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
08 Septemba, 2009
anko nakuomba sana fanya yote hila sisi tulikuwa huku maboksini tunatamani sana kusikia mazungunzo hayo ya rais wetu
ReplyDeletepili naomba watanzania watakaopiga simu waende direct to the point
pia naomba km kunauwezekano mwambie mkurungenzi wa habari ikulu kuwa rais akiulizwa maswali apunguze majibu marefu maana dakika 90 kwa ninavyomjua mimi rais wangu anaweza kujibu maswali 4 tu atakuwa ajawatendea haki watanzania maana wanamaswali mengi sana na wangependa kupata majibu ya kiualisia na si siasa sana mdau mbeba mabox
INGAWA TUNAMPAKA MATOPE JK KWAMBA HAONGOZI NCHI IPASAVYO ILA HUKO MBELENI TUTAMKUMBUKA KWA KUFUNGUA UHURU WA KWELI WA VYOMBO VYA HABARI NA WANANCHI AU WATU KUWEZA KWELI KUONGEA, JE NANI WAKATI WA MKAPA ALITHUBUTU KUPIGA KELELE ZA UFISADI? THUBUTU.. MNGEWEZA KUPIGA HIZO KELELE ENZI YA MKAPA NYIE CHADEMA AU CCM WENYEWE WA KWA WAO?
ReplyDeleteLEO HII MZEE WA PWANI (JK) ANAWARUHUSU MFUNGUE KINYWA MNAANZA KUMLETEA LONGOLONGO!
HILO KANISA KATOLIKI AU HAO WAISLAMU HAWAKUWAPO WAKATI WA MKAPA? MBONA HAWAKUWA NA UCHUNGU HIVI? ACHENI USANII BWANA..
TUONE AKIONDOKA JK ATAKAECHUKUA ZAMU YAKE KAMA ATAKUBALI WABONGO MPIGE MAKELELE. WATANZANIA BWANA.. KISA.. ETI TUMESOMA SASA TUNAJUA HAKI ZETU.. AH! YAANI KWELI MIAKA 10 ILIYOPITA KWELI WATANZANIA MBUMBUMBU MSIONE WEZI AU MAFISADI?
ACHENI FITINA WATANZANIA NA MUWE NA SHUKRANI. ANGALAU JK AMEWAFUNGUENI MACHO.. HATA KAMA JK ALIKUWA HATAKI KUWAFUNGUA MACHO (KALAZIMISHWA NA HALI YA MAMBO) BASI MPENI HONGERA YAKE, SIO FITNA.
NAKWAMBIENI NYIE WATANZANIA SUBIRINI, AKIONDOKA JK,RAISI ANAEFATA HATATAKA MAMBO YA KULETEWA LONGOLONGO, MTAPIGWA BAKORA NA MIKANDA, NA HIYO NYODO YENU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI
ITAPUNGUZWA, MTARUDISHIWA UHURU WA MKAPA, HALAFU TUONE NYIE WANASIASA WENYE UCHUNGU AU WANADINI WENYE UCHUNGU KAMA MTAPIGA MAKELELE YENU. TUNAJUA JK ANA KASORO ZAKE NYINGI NA ZA MSINGI, LAKINI KACHAGULIWA NA NANI? HAKUCHAGULIWA NA WAKONGO WALA WAGANDA? NI NYIE WENYEWE WATANZANIA MLIOSOMA MLIMPIGIA KULA ZA NDIO, HALAFU LEO HII MNALETA ZA KULETA.
MPENI SIFA ANAZOSTAHILI JK. ACHENI FITNA NA UZUSHI WATANZANIA. TATIZO SIE WATANZANIA TUNA SIASA ZA KUSHIBISHA MATUMBO.. BLAH BLAH BLAH NYINGI...
maswali ya kagoda,richmond,dowans,kiwira yananitatiza sana.lkn waangalie sana maana hawakawii kupanga wauliza maswali
ReplyDeletewasipange watu wakuuliza maswali,kagoda,kiwira,dowans zinaniumiza sana kichwa
ReplyDeleteThis is trash.. are we using yahoo? Anyone can crack and read from here. What security do we have? I am disappointed.. really really disappointed with this
ReplyDeleteMichuzi hili litafanyika kweli? Au? Ninaogopa wapuuzi wengine wasije wakaitumia vibaya fursa hii kumdhalilisha Rais wetu jamani. Otherwise ni style nzuri. I hope watu watamuuliza maswali ya maana na siyo ya kipuuzi.
ReplyDeletewhat the hecks is that? mheshimiwa rais hajui kero za wananchi? hivi huyu rais anawashauri au they try to destroy him. huwezi ukamwanika rais ajibu maswali wakati kuna kero hazijapatiwa ufumbuzi.mfano namba ufisadi, sheria tata(zombe), BOT( Maumba),yona and basil....and bunch of s*** kila la kheri watanzania
ReplyDeleteKUSEMA KWELI NI WAZO ZURI SANA KUSIKILIZA SHIDA ZA WANANCHI ILA IKUMBUKWE KUWA KUNAWENGINE HAWANA HIYO HELA YA KUPIGA SIMU SIJUWI WAO WATATOA VIPI SHIDA ZAO
ReplyDeleteAU WAENDE KWA MJUMBE WA NYUMBA KUMI NA WAKACHANGE MAONI YAO KISHA MJUMBE AYATUME
blaza Michu,kwa heshma na taadhima naomba urekodi hiyo clip yoote kisha ui-upload ili wadau wa huku Gezaulole nao tuweze kuona.
ReplyDeleteMkulima-Kijijini Gezaulole
Jamani mbona TZ bado hatujafunguka macho ... Hivi kweli kabisa watu wamekaa wakaamua kufungua hiyo account "swalikwarais@yahoo.com" eti maswali yatumwe hapo ... Hivi ni nani Manager wa IT wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, naomba km anasoma bs naomba aweke e-mail yake then nimpe ideas kdogo ... kwa ufupi, unajua unapotuma e-mail bs e-mail yako huifadhiwa ktk Mail Server ya kampuni unayotumia, aftr smtime ndio huwa wanazifuta n still they have archives so hata km itaitajika baadae for reference inaweza kupatikana. Sasa leo e-mail zetu kwa rais ziende kukaa ktk mail server ya Yahoo, kuna usalama munadhani? Wat if someone hack that e-mail address and misuse, who is to be blamed? you knw it is very easy to hack Yahoo, hotmail address, atleast Gmail they have much protection ... Pls lets change, tubadirike jamani tutazame usalama pia ...
ReplyDeleteTown Hall Meeting?
ReplyDeleteUnaona? Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi sasa J.K anataka kutuchorea picha ya kuwa yeye yuko karibu na wananchi na anasikiliza kero zao.
Eti yeye si mmoja wa wanaoifilisi nchi kwa mikataba mibovu, rushwa na ufisadi.
Eti ni mawaziri ambao amewateua yeye tu, na makatibu wakuu, na mwakurugenzi, wakuu wa mikoa na wilaya ambao ndio wa kulaumiwa!
Eti anaachia vyombo vya sheria ambavyo practically vyote viko chini yake vifanye kazi ya kuwachukulia hatua za kisheria rafiki zake waliomfinance kuingia madarakani.
Ni juzi tu alikuwa anawasikiliza waroho ndani ya chama chake wakimshambulia spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu mwenye guts za kuleta demokrasia ya kweli ndani ya bunge.
Kila swali gumu atasema, vyombo husika vinashughulikia!
Danganya toto karibu na uchaguzi!
Hivi kwanini Ikulu haina website? mbona hii haibu?
ReplyDeleteHakuna lolote hapo itakuwa ni longolongo tu. Kama angekuwa na ubavu wa kutatua kero angeshachukua hatua kwa mafisadi. Ikulu imeanzisha usanii mwingine.
ReplyDeletetunashukuru rais kwa uamuzi wako wa busara hata barack obama hufanya hivyo mara kwa mara,NINA SHAKA UTAJIBU MASWALI YA AKINA PONDA WANAODAI SERIKALI YA CCM 70%NI WAKATOLIKI,20%WAPROTESTANT NA 5% NI WAISILAMU mimi nakuonea huruma ngoja nikabebe box nipate euro nitume bongo
ReplyDeleteNi uamuzi mzuri aliouchukuwa mheshimiwa Rais.
ReplyDeleteLakini naamini kuwa wananchi wengi wa nchi hii wataikosa nafasi hii muhimu.
maana kama inafahamika kuwa huu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani,na maelfu kwa maelfu ya raia wa nchi hii walio waislamu muda huo watakuwa wanatekeleza ibada ya Ramadhani.hivyo kukosa nafasi hii .
Ingependeza hao waratibu wakatafuta muda muafaka zaidi ili kila mwananchi akapata nafasi ya kushiriki.
NAWASIWASI HUENDA ZIKAPOKELEWA SIMU ZA WATU WA CCM TU.NINGEPENDA KUONA INDEPENDET TV IKIONGOZA HICHO KIPINDI NASIO TV YA TAIFA KWA SIKU ZIJAZO.
ReplyDeletekwani tuna hamu ya kum shoot muheshimiwa maswali live.ILA NI MWANZO WA DALILI NZURI.
NA HUYO HAPO JUU ANAEJIONGELESHA KUHUSU MAFISADI.JIBU BILA DR.SLAA/ZITO KUJITOA MWANGA WALA USINGEJUA NENO FISADI WEYE!
MICHUZI hongera sana bwana!Naona umeamua kubadilika,yaani umekuwa kama SPIKA WA BUNGE.Ukweli unauachia,hubanii tena maoni.
ReplyDeleteMakamba bado tu hajakuita ofisini kwake???
Mheshimiwa Rais, hongera kwa kuamua kuongea na sisi wananchi wako kupitia njia hii ya vyombo vya habari.
ReplyDeleteKwanza nina swali hivi unafahamu kwa nini kauli mbiu yako na ya CCM ya maisha bora kwa kila Mtanzania inabezwa? Siyo kwa sababu wananchi wanaona hujafanya kitu. Ila ni kwa sababu CCM kupitia Watendaji wake wakuu kuanzia Katibu Mkuu Makamba hadi ngazi ya Wilaya wameshindwa kuelewa kuwa maana ya kauli mbiu hiyo kimatendo ni yale ambayo Serikali imekuwa ikifanya ndani ya miaka minne iliyopita ambayo ni kuibua mipango na miradi mbalimbali na kueleza jinsi miradi hiyo inavyochangia kuboresha maisha ya Mtanzania. Kwa mfano barabara za lami ambazo zimejengwa sehemu mbali mbali zinachangiaje kuboresha maisha ya Mtanzania. Au zahanati mashule, mbolea, huduma za kibenki, mikopo kama vile mamilioni ya JK n,k hayo yote ni mafanikio ya CCM.
Ushauri: Uwe na ujasiri wa kumwondoa Katibu Mkuu wa CCM na ile safu ya watendaji pale makao makuu ya CCM na uweke timu mpya ambayo itainadi CCM kisayansi. Uongozi wa sasa umezeeka, umechoka, umejaa kiburi ubabe na hauna jipya. Nilitegemea wangekuwa waelewa wakajiondoa na kwenda kupumzika. La sivyo mwakani unaweza ukajikuta wewe ni Rais wa CCM na wabunge wengi kutoka upinzani. Asante Mheshimiwa Rais.
Namna gani globu ya jamii haikupewa nafasi ya kukusanya maswali!!!
ReplyDeleteSasa jamani na mkongo wa mawasiliano tunao vipi maswali yakusanywe kwa njia ya e-mail za yahoo? Hatuna wataalamu wa IT?
Swali langu kwa Mh. Rais ni: “ijapokuwa TZ haina dini, je ofisi yako imeshindwa kuwafikiria/kuwaenzi sehemu ya wananchi wake ambao kwa mujibu wa imani yao (Waislamu) watakuwa kwenye ibada na hivyo kushindwa kusikiliza live hotuba yako na pia kukukabili live na yanayowatatiza, isitoshe kunyong’onyezwa kutambua kuwa wenziwao ‘wanafaidi’ fursa hiyo adhimu”.
ReplyDeleteIfikapo hapa ndipo ninapotanabahi kuwa aidha ni vigumu kuwaelewa waTZ waumini wa kiislamu ama pana ‘kusudi ya makusudi’. TZ/serikali haina dini ila wananchi ndio wanadini (waweza kuigeuza na kusema serikali haina udini ila wananchi wanao). Na wala hili si jambo la kushangaza, ni sawa sawa kabisa na 'nadharia' ama kanuni ya 'mali ya umma' ama 'SU'..na pia nadharia ya madaraka/utawala (kwa mihimili ya Bunge/Serikali-urais na Mahakama-sheria) kama chombo umajumui wa raia bila ya kuwa mali binafsi ya raia mmoja-mmoja. masuala kama mahakama ya Kadhi kwa waislamu) inakuwa si tatizo. Sababu inaibidi serikali/nchi isiyo na dini ihudumie raia wake (ambao ni waumini na hivyo kutatizwa, pamoja na mambo mengine, na masuala ya imani ambayo mengine yanatoka nje ya milki mahususi ya vyombo vinavyosimamia imani zao). Sivyo, basi wanapogombana ma-askofu/masheikh ingebidi waambiwe rudini hukohuko dini-ni mwenu mkatatue sababu tu kwa kuwa chanzo cha ugomvi wenu si mambo ya ‘secular’. Ninachotaka kusema ni kuwa ni busara kuona (kukubali yaishe) kuwa nchi kuwa ‘secular’ haimaanishi kutekeleza mambo ‘nje ya dini’ zote husika ila ina maana kusimamia masuala bila kujikita katika mashiko ya dini yoyote kati ya hizo (mfano kwa kuanzia kwenye ‘shahada ya waislamu’ ama ‘canonical law’ ya kanisa mojawapo ama Veda za ki-sankrist ) – ndo maana Marekani ni secular lakini Mluo (Museveni angesema Jaluo!) alipeleka salaam za Ramadhan Karyim na kufuturisha (kama sikosei), na hapa kwetu tumeona mifano hiyo kwa viongozi wa serikali. Ni vizuri kukiri kuwa kuna ugumu mkubwa katika kupambanua haya na kuwafanya waumini waelewe hivyo. Ila pia ni kiongozi shujaa na makini ambaye atajitahidi kufanya hivyo (katika issue ya ‘waraka/muongozo’ labda ni vigumu kumpa Kingunge sifa zote hizi ila anastahiki hii ya ushujaa). Waoga ni kama Nyalandu ambaye anafikiri kuna ‘jawabu mujarabu’ la matatizo haya, nalo ni kupiga marufuku mijadala ya anachoita ‘udini’ bungeni (hiyo hasa ni suluhu ya kidini, ambayo ni ‘exclusive’ huwakilisha kundi-imani moja tu ambapo muumini huambiwa ‘ingia kwenye mstari ama tunakutoa kundini’!). Kwenye nchi yenye makundi ya imani, huo ni upotofu. Katika nchi kama ya kwetu dawa ni kurudi katika mizizi ya uvumilivu kwa ‘kuvaa viatu vya wengine’ ili kutambua vinafinya wapi – na hii ni kwa dini zoote!. Kurudi katika utamaduni ambao kwa mfano unatambua kuwa ukiweka arusi ama mnuso katika mwezi kama huu unakuwa umelibagua kundi moja (ikiwa hayo si makusudio yako vinginevyo ‘rukhsaa’!) ama ukimwalika mkristo nyama choma wakati wa kwaresma unakusudia kumfikishia ujumbe mahsusi..........
..............Kwa kuhitimisha, je washauri wa Rais wameshindwa kumtanabahishia kuwa ‘prime time’ ya hotuba yake ya leo inagongana na salatul ‘isha ya waislamu. Isitoshe, kwa kuwa ni mwezi wa Mfungo, inagongana pia na salatul Taraweeh, inayohimizwa kusaliwa misikitini, ambayo hupatikana mwezi huu adhimu tuu na mtihani mkubwa kuwaambia waumini hawa (haidhuru kama ni 30%, zaidi ama ndo kundi moja kubwa zaidi la kiimani nchini). Ama washauri wake wengi hawana habari na hili kwa kuwa si Waislamu (hata kama ndivyo basi, haingii akilini kuwa na wataalamu wasoweza soma alama za nyakati!). Ama labda ujumbe wa Rais wetu si wa muhimu kwa kundi hili? Dhamira inanikataza kukubali kuwa haya nayo ni makusudi? Maswali ni mengi kuliko majibu na nalazimika kuishia hapa nikitarajia kuwa wenye kuelewa wataelewa na kujitahidi kuwa na uangalifu zaidi siku zijazo..Aidha kwa hotuba hio ya leo, wengi wetu haidhuru tutazama marudio yake ama aghalabu tutaisoma kwenye blogu am magazetini kesho.
ReplyDeleteswali: ile miezi sita aliyoitoa kwa epa, richmond, bot na kwingineko inaisha lini? je, rais wetu hakufahamu kwamba kuna vyombo vya sheria yaani mahakama wakati anatumia mrema-publicity-style?
ReplyDeleteMlioko ughaibuni...fuatilieni 'mazungumzo' hayo kwa kupitia RADIO MARIA
ReplyDeletehttp://radiotime.com/station/s_6424/Radio_Maria_Tanzania_891.aspx