HABARI TOKA A-TAUN ZINASEMA KWAMBA MWANAMUZIKI NYOTA TOKA MAREKANI KANYE WEST AMETUA A-TAUN TAYARI KUUKWEA MLIMA KILIMANJARO WAKATI WOWOTE KUANZIA SASA.
KANYE ANAKUWA MTU MASHUHURI WA PILI KWA MWEZI HUU KUJA KUKWEA KILELE CHA AFRIKA. JUZI MMILIKI WA CHELSEA FC ROMAN ABRAMOVICH ALIKUWA HUKO JAPO HAKUFIKA KILELENI.
MASTAA KIBAO, IKIWA NI PAMOJA NA DAVID BECKHAM, INASEMEKANA WAMEPANGA KUJA KUKWEA KILIMANJARO. NI MATUMAINI YA GLOBU YA JAMII NA WADAU KWAMBA WAHUSIKA WA UTALII HAWATOLAZA DAMU KWA PROMO HII YA DEZO. ILA USISHANGAE MAMBO YAKIWA YALE YALEEEEE..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Michuzi hivi Tanzania sisi tumelogwa na nani? Hivi kweli kaja Abrahamovich viongozi wakubwa wa Serikali wameshindwa hata kujipendekeza kwa ukaribu maana naamini watu kama hawa wanauwezo mkubwa sana wa kuitangaza Tanzania kwenye nyanja ya Utaliii sanaa na upo uwezekano wa dunia sasa kutambua kwamba KILIMANJARO ipo Tanzania na sio Kenya.

    Haya sasa anakuja muimbaji ambaye dunia nzima inamjua KANYE WEST bado utaona ujinga ujinga tuuu

    Yaani kweli kwenye miti hapana wajenzi..mijitu inawaza kupitisha MADOKEZO tuuu na invoice kwenye maofisi. Hivi wanafikiri kuutangaza utalii ni kuweka mabandiko tuu kwenye Tax za London na kwenye vituo vya Treni na isitoshe wakisikia vitu kama hivyo ndio kila mtu analilia safari ya kwenda UK wakati njia za kutangaza utalii wetu zipo nyingi jamani

    Mdau Davey

    ReplyDelete
  2. nimefurahi sana watu sasa kuijua tanzania ilivyo nzuri ila bado tunahitaji promo kwa wingi na europe pia matangazo tuna hitaji na wateja wa huku waelewe na maanisha sweede,finland,denmark nk matangazo kwa wingi yanaitajika hata kuwe na website ambazo zipo update kila wakati mtu akitaka kuja anaingia on line hizi nchi nilizo taja huku tunaona matangazo ya wa thailand india,vietnam tunaomba watangaze na huku kwenye mabasi au kokote nayo itasaidia kwa wateja wa huku.wanablog wengine wameweka wanyama inapendeza sana kuifill nchi yako.

    ReplyDelete
  3. samahani kwakwenda nje ya topic email iliyowekwa ya raisi mbona ukituma email haziendi au ni ya uongo nisaidieni.imeandikwa swalikwarais@hotmail.com ukituma haziendi kweli ni kampeni za uchaguzi

    ReplyDelete
  4. Kanye west kafika lini Bongo jmn? Huyu alikuwepo kwenye mtv awards jana usiku, leo kashatua Bongo!

    ReplyDelete
  5. Huyu jamaa alishawahi kudai jina lake limechanganya Kiswahili na Kiingereza. Nadhani hakujua alichokisema = Kajisaidie haja kubwa Magharibi!

    ReplyDelete
  6. Babu ametua bongo lini wakati masaa 8 tu aliyopita alikuwa kwenye MTV music wards hapa Marekani. Wabongo tuache uzushi jamani. Labda useme atakuja, sio ameshatua, come on!!!!!!

    ReplyDelete
  7. Wabongo wazushi kweli, Kanye alikuwa anachafua mazingira katika MTV VMAs jana huko marekani pia hakuna news network duniani inayoongelea jamaa kupanda mlima wetu...acheni kutuzuga jamani

    ReplyDelete
  8. Samahani Michuzi,

    Ila uwe unacheki kidogo habari kabla ya kuzituma.
    Maana kwenye news,jamaa usiku wa jana amefanya vituko kwenye VMAs, sasa itafikaje fikaje Arusha tayari???maana ukumbukue tuko mbele masaa kadhaa!!

    Mngeweka source ya taarifa zenu,labda!!

    ReplyDelete
  9. Baada ya kufanya vituko jana kwenye MTV video Awards.... Jamaa anabidi apunguze matani yake... watu wanaanza kumchukia....Taylor swift anapendwa na watu.....

    ReplyDelete
  10. Duh! Huyu jamaa si alikuwa MTV awards loe na kudhalilisha demu wa watu hivi? Sasa anakuwaje a-town pia?

    mtoto

    ReplyDelete
  11. itakuwa ngumu hili jamaa limeharibu vilivyo kwenye mtv music awards limeacha watu hoi na kuzomewa juu yote hiyo ni sababu ya keroro kaazi kwelikweli kama kaja huko kweli atakuwa anakimbia aibu tu na hatfuka kileleni
    miss michuzi ukerewe

    ReplyDelete
  12. KUTANGAZA UTALLII NI KITU RAHISI SANA. HUYO TAJIRI ALIYEPANDA JUZI NI TOSHA TANGAZO NA HUYU ANAEKUJA TUSILAZE DAMU. TATIZO LA BODI YA UTALII NI SEMINA TU WANAKULA HAWAJUI WANALOTAKIWA KULIFANYA PIA MABALOZI YETU NDIO YAMELALA SANA

    ReplyDelete
  13. ebwana uzushi acheni.hivi punde jamaa katoka kushikiwa bango kwa kumdhalilisha Taylor swify,saa hz mnadai yupo A-town.Acheni hizo jamani.Au mnazungumzia kanye west yupi?wa pale mtoni mtongani nini!

    ReplyDelete
  14. ACHENI UONGO KANYE BADO HAJAFIKA A-TOWN USIKU WA KUAMKIA LEO ALIKUWA KWENYE MTV AWARDS.LABDA ANA MPANGO WA KUJA LAKINI BADO YUPO LA.NANI KASEMA AMEFIKA HUKO?

    ReplyDelete
  15. ebwana uzushi acheni.hivi punde jamaa katoka kushikiwa bango kwa kumdhalilisha Taylor swify,saa hz mnadai yupo A-town.Acheni hizo jamani.Au mnazungumzia kanye west yupi?wa pale mtoni mtongani nini!

    ReplyDelete
  16. huu mlima wa Kenya kweli unapendwa na wadau mashuhuri wanaokuja kuukwea ;-)

    ReplyDelete
  17. Jamani KANYE WEST anakuja na sio kwamba ameshafika jaribuni kusoma vizuri makala zinapowekwa

    ReplyDelete
  18. Imekuwa ni vizuri sana kutembelewa na watu mamarufu kwa ajili ya kukuza utalii wetu.
    Kwa kweli inabidi watanzania tuamke, na tujipange. Hakuna sector nyingine itakayotupatia ajira nyingi kama utalii,( wa ndani na wa nje)
    Pia kuinua pato la taifa na kuliingizia fedha za kigeni.

    Mdau. Oscott Garden

    ReplyDelete
  19. kanye ameharibu vibaya sana mtv na sasa anaelekea LA kwenye ufunguzi wa jay leno show with jay z and rehhanna sasa katua bongo duh sielewi.

    ReplyDelete
  20. KANYE WEST = GO TAKE A DUMP ON THE WEST!

    ReplyDelete
  21. Angekuwa Kobe Bryant nisingempa ushauri huu lakini kwa huyu mwanamuziki atumie jina tofauti akiwa nchini. Ushauri huu nawapa vilevile Wajapani watakaotutembelea wenye majina ya K'moto, Takau'hi nk

    ReplyDelete
  22. Please people don just comment kwa kushambulia michuzi. kwani kanye hawaze kufanya viroja MTV and few weeks later akaenda Bongo.kweli malimbukeni utawajua. Mtv blunder inahusiana nini na his future plans???
    and unayetaka viongozi wamshadadea billionaire wa watu we hujui kama trip yake ni private???
    btw RIP Medi Mpakanjia

    ReplyDelete
  23. I like this Kanye !
    http://entertainment.timesonline.co.uk/tol/arts_and_entertainment/music/article6833664.ece

    London for life !

    ReplyDelete
  24. naomba nimshambulie huyo jamaa aliyoongea kuhusu ulimbekeni wakati yeye ndio namba one,watu wanaangalia ukweli wa Kanye kutua bongo kwa muda aliotoa vioja uku marekani,kutoka uku kuja bongo ni masaa 21 kwa ndege sasa sijui huo ukweli wa hiyo habari uko wapi kama sio ulimbukeni.

    ReplyDelete
  25. WACHENI KUDANGANYA WATU JAMANI KAINGIA BONGO LINI WAKATI HATA SIKU HAIJAPITA, JANA USIKU ALIKUWA AMEHARIBU(JAMAA NI CHIZI) KWENYE MUCH MUSIC AWARD HAPA TORONTO.

    ReplyDelete
  26. JAMANI MSALIE MTUME!!!! NAFIKIRI TATIZO LIPO KWENYE KUANDIKA ---------"AMETUWA"----- HAPO HAPO KUMEANDIKWA ANATEGEMEWA KUWA MLIMA KILIMANJARO WAKATI WOWOTE,
    INAONEKANA BAADAE SIO SASAHIVI.

    HABARI IMEJIGONGA KIDOGO.

    MSIMLAUMU SANA MICHUZI.

    KANYE WEST KAJIZALILISHA KWENYE MTV AWARD POMBE MBAYA HATA KAMA KWELI AWARD ANASTAHILI BEYONCE! KANYE WEST KAJIZALILISHA ILA YOTE NDIO UBINADAMU WOTE TUNAKOSEA DUNIANI. PAZI.

    ReplyDelete
  27. Kaharibu huyo ktk VMA..wamemzomea na kesho yake kaomba msamaha.jamaa akiwa ktk "mwezi mchanga" huwa kizaazaa sana..

    ReplyDelete
  28. MTV AWARD HAIKUWA LIVE ILIKUWA "PREVIOUSLY RECORDED", PEOPLE MUWE MNASOMA FINE PRINTS. SO POSSIBILITY ILIREKODIWA LAST WEEK NA KWAMBA YUKO A-TAUN. ILA ALIBOA KINOMA KWENYE MTV. SIJUI SIKU HIZI ANAVUTA BANGI GANI! YAANI ANA MI-JAZBA ISIYO NA KICHWA WALA MIGUU

    ReplyDelete
  29. Ok , hata mimi nilishangazwa kuwa Kanye West ameshafika Arusha wakati tumemuona live kwenye MTV Awards akiharibu live kwa yule teenager.

    Lakini ina wezekana kuwa yuko Bongo ukipiga mahesabu ya muda .

    Ukizingatia haswa macelebrity wengi huwa wanaonekana kwenye Premmere wakipita kwenye reb carpet halafu wakisha ingia ndani kwenye shrehe , huwa hawakai huwa wanapitia milango ya jikoni kutoka na kwenda kwenye shughuli nyingine ambazo ziko kwenye ratiba

    Tuseme kafika Arusha kwa kupanda KLM ambayo inaingia kama saa tatu au saa nne huku TZ.

    Haya tuseme , immediate afer kuharibu alikua ana plan kusafiri, alipo haribu pale kwenye Award show ilikua ni kama saa Saa kumi usiku huku Bongo (04:-- .am )huku Bongo.

    Kwa kua ilikua ni New York City , baada da tuu ya kuaharibu akaondoka kwenda Aiport ambapo sio mbali na hapo tuseme ni Laguardia Airport . Hapo akapanda Private jet mbaka Amsterdam ni ma saa kama 7 or 6 , hapo aka ichukua KLM kuja nayo Bongo ambapo ni masaa kama 9

    Kumbuka Atakua kafika Amsterdam saa nne asubuhi na kuondoka na KLM na kufika Bongo saa tatu or mbili usiku , hilo lina wezekana kabisa.

    Nakumbuka siku za Nyuma nilipo kua LOndon, Naomi campbell Cloudia Schiffer na yule model mwingine nimemsahau jina, walikua wana fungua restourant yao inaitwa Fashion cafee hapo Leceister Sq. LOndon.

    Kukaa na R umor kuwa Naomi hawezi kuwepo sababu jana yake alionekana yuko Washington.DC kwenye Dinner kwenye White House kama mgeni mwalikwa wakati huo Raisi ni Clinton na pia asubuhi ameonekana NY city , lakini walisahau kuwa kulikua na Concord fight from NY to LOndon na Naomi alitokea kweney ufunguzi watu wakashanga ina wezekanaje awe London ana ameonekana kweney TV akiwa Washington .DC?

    ReplyDelete
  30. An. wa sept 14, 11.00pm, Kabla ya kuita watu limbukeni inabidi ujue kusoma kiswahili, habari inasema AMETUA, asasa labda kama unaongea kikwenu ila hiyo maaana yake AMESHAWASILI, Ila sasa hivi tunawatch Jay Leno, show na anasema Kanye West ataongelea zangazanga la kwenye awards jana New York..Limbukeni nani sasa!

    ReplyDelete
  31. eti sasa hivi tunawatch Jay Leno show...who cares???nani kakwambia Jay Leno show inarushwa live????na mwingine eti kutoka US kwenda bongo ni 21 hrs...kweli wabongo tunajua kujishebedua...ulimbukeni wa states utawatokea kwa pua mtakapoishia kwenye nursing homes mkiwa vikongwe
    God bless TZ and it's people

    ReplyDelete
  32. kaka Michuzi!
    Naomba niwawekee watu hii link http://www.drum.co.ke/node/2476, ni gazeti la DRUM online. sasa kazi kwenu wale wote wanaojifanya wanajua.

    ReplyDelete
  33. ...aya mbona uyu mazee yenyewe ya fashion uko kavaa ilo tambala ya Yasin??..afu mwamkomalia KANUMBA

    ofkoz mibangi nk inawasumbua saaana "masupastaa" c ajabu kituko

    mkome

    ReplyDelete
  34. Ann.uliotoa mahesabu ya muda vp kuhusu muda alioenda kurekodi Jay leno shoo LA? maana show imerushwa hewani jtatu usiku, so labda imerekodiwa jtatu alfajiri. mahesabu ya muda hapo inakuwaje? kutoka Ny=LA-Tz. NAULIZA TU?

    ReplyDelete
  35. Labda yule aliyekuwa pale kwenye VMA awards alikuwa ni mzuka na ndio maana akafanya kile kituko alichokifanya hadi sasa almost the whole world hates him.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...