kaka michu, heshima mbele mkuu!
Jumatatu ya tarehe 7 kuna mdau alituma post kulalamika kuhusu ndugu zetu wa usalama barabarani.
Napenda kutoa pongezi kwa mengi mazuri ambayo kikosi hiki kinaonekana kuyafanya katika barabara nyingi kwa siku za karibuni,Ni wazi kuwa hawa jamaa wameonyesha uwepo na uhai katika siku za karibuni kwani wanaonekana kwenye kila pembe.

PAMOJA na pongezi hizi pia kuna wengine wanaolitia doa jeshi hili! JANA (13/09/2009) nikiwa nasafiri kuelekea Iringa nilisimamishwana wanausalama barabarani maeneo ya Sanga Sanga nje kidogo na mji wa Morogoro karibu na Mzumbe, kama kawaida aliyenisimamisha alikagua kila kitu stahili katika gari ikiwemo leseni yangu, matairi,taa, insurance, m.v licence, triangle, fire extinguisher n.k,

kila kitu kilionekana kuwa safi! Askari huyu alidai chai ambayo sikuwa tayari kumpatia, ndipo akaniambia ataanza kukagua mfumo mzima wa kwenye gari , kwangu nilimwambia aendelee, katika kukagua weiper zilikuwa zinafanya kazi ila maji ndio yalikuwa hayatoki (MAJI YA WEIPER!!) jamaa akashangilia na kudai ni mojawapo ya makosa 39 yaliyoko katika NOTIFICATION TRAFIC OFFENCES hivyo akadai nimpatie nusu ya fine ambayo ni 10,000/=yaishe au nilipe fine 20,000/=,

kidogo tulishindwana lugha hapa. baada ya mabishano jamaa alingangania nilipe fine pamoja na kuwa wenzie walimsihi kuniachia na kunipa onyo!Sikuwa na jinsi ila kulipa fine ambayo ni 20,000/=.

Naomba kuuliza hivi hii ni sawa??????

je magari yote huwa yanakaguliwa hivi au ni njaa tu ya huyu jamaa?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Ndugu pole, hawa jamaa ni njaa tu inawasumbua, kuna magari mangapi hayana m.v licence au insurance imeisha au hata fire extinguisher imeisha lakini hayakamatwi na yapo town daily? Ni kama story ya yule bwana aliyekaguliwa kiiiiiila kit wakakosa kosa wakamwambia aende zake, nae akamwita yule trafiki polisi akamwambia 'Afande umesahau kukagua mziki' akamuwashia muzik system kwa sauti halafu huyooooo1

    ReplyDelete
  2. WATER SYSTEM MBOVU.... I LIKE THAT.

    ReplyDelete
  3. Kama kosa hilo limeorodheshwa ktk trafic offence adhabu aliyokutoza ni sahihi kabisa. Suala la kukagua gari kwa kiasi kikubwa sio hoja kwa kuwa ukaguzi hauna mipaka, ila ninakupongeza kwa kutokubali kumaliza kosa hilo kinyume cha taratibu nadhani madreva wote tungefanya kama wewe hao askari wangeacha tabia mbaya waliyo nayo.

    ReplyDelete
  4. Ulimukomesha,, pole sana wamezoea lakini ndugu hayo maneno ni ya ukweli au, kama ya kweli hayo ndo mambo

    ReplyDelete
  5. Haaaa,, water system mbovu. Kubwa kuliko ndo mapongo wa kibongo walivyo, changanya lugha

    ReplyDelete
  6. Hivi ninyi mnaolalamika kuhusu maaskari mnashindwa hata kusoma number zao? Kitu cha kwanza unaposimamishwa na askari ni kuhakikisha unasoma number yake na unaandika hata katika simu yako. Kama hana namba na hakuna mwengine mwenye nayo basi una haki ya kuomba kitambulisho chake. Akikataa yote hayo ni muhimu kuwa na number ya IGP ambayo ni public na huwa anarespond ASAP ama msaidizi wake na utume sms kumuelezea tukio hilo. Baada ya hapo unachukua risiti ya faini na kuondoka apende asipende kwa ajili ya kulipia katika kitua cha mkoa ama wilayani.

    Yote hayo yanahitaji utayari wa kupoteza muda ama kupewa faini zaidi lakini mwisho wa siku unakuwa umeshughulikia haki yako na kupunguza udhia kama huo.

    Again, bila ya number ya huyo askari ama details za kitambulisho chake ni kupoteza muda kulalamika kwa michuzi.

    ReplyDelete
  7. Mimi nadhani adhabu uliyopewa sio kubwa kulingana na tatizo lenyewe. Wakati mwingine inabidi kuwaeleza wazi hawa askari wa usalama kuwa mimi hongo sitoi ila tu nitafuata sheria.

    Ukiangalia upande wa pili wa hili tatizo, ni kuwa kama maji ya wiper hayamo au system yake haifanyi kazi basi kioo cha mbele kikichafuka kinaweza kusaidia kupata ajali kwani huwezi kuona uendako. Na vile vile maisha yako yanakuwa hatarini pamajo na ya watu wengine.

    Vizuri uligoma kutoa hongo lakini faini uliyopewa ni sahihi. Na kama tunataka kutokomeza hizi ajali barabarani basi nilazima kila kitu kikaguliwe kwa hali ya juu

    ni hayo tu.

    P.E.D

    ReplyDelete
  8. Je hiyo pesa ulimpatia yeye mkononi? kama ulifanya hivyo basi utakuwa uliruka majivu ukakanyaga moto. Maana nadhani ulitakiwa urudi Morogoro mjini ukalipe hiyo fine kwenye office za polisi na upewe risiti. Otherwise hiyo hela watakuwa wamelamba. Maana kwa Nchi zetu hata hiyo notification book inaweza kuwa feki. Au imekaaje hii wakuu?

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  9. TUNGEWAFANYIA HIVYO TRA WASINGETUNYONGA TENA, TUNATAKIWA KUBANANA NAO KUWAAMBIA INVOICE SIO FEKI, VILE VILE UWANJA WANDEGE TUNATAKIWA KUBANANA NAO ILI KUMALIZA WIZI.
    NAOMBENI KAMPENI ZENU WANANCHI MIMI MBUNGE WA UPINZANI NITAKAPO PATA UBUNGE NIPEWE UWAZIRI KWENYE MOJA WAPO YA WIZARA HIZO NIWATENGENEZE KWANI NITAONYESHA UMAHIRI WA KUWAMINYA MANYANG'AU KWA VITENDO BADALA YA KUENDELEA KUWAPIGIA KELELE BUNGENI TU THANKS.

    ReplyDelete
  10. Pole sana ndugu yangu lakini bwana kumpa chai tu jamaa ilikushinda na ukaona ulipe faini elfu ishirini nadhani listi utapeleka ofisini kwako ili urudishiwe hiyo pesa yako kama ni gari la kazini, lakini kama ni lako naona unazo pesa sana maaana ungempa buku moja tu jamaa angeachana na wewe lakini si mbaya kwa ubishi wako umesaidia kutunisha mfuko wa faini za makosa ya barabani, swali umemkomesha nani, au umetufundisha nini ubishi na huku gari lina kosa au kutoa chai na unaokoa muda wako.

    ReplyDelete
  11. JAMANI UNAJUA WABONGO WANAKERA...ETI WATER SYSTEM MBOVU....

    ReplyDelete
  12. Kaka, napenda nikuambie kuwa hiyo ni sawa ulivyolipishwa kama imeanishwa kwenye orodha ya makosa. Ni wazi kuwa magari yetu yanakuwa na makosa mengi na ni mara chache sana utakwosa na kosa. Lugha nzuri wakati mwingine inasaidia kumalisa matatizo bila hata ya kutoa chochote kwa makosa ambayo sio criticle. Kwa msg hii nasisitiza kuwa askari waendelee kuwa waadilifu kwani ndio njia pekee ya kuokoa taifa letu katika majanga kwenye sekta hiyo.

    ReplyDelete
  13. Kwa safari ndefu lazima wiper zifanye kazi vizuri,Na kama huna maji ya wiper haziwezi kufanya kazi vizuri na kuweza kusababisha ajali kutokana na poor visibility.
    Ungempa chai nawewe ungekuwa una makosa ya rushwa,Lipa hiyo fine na usifikiri kakuonea!!

    ReplyDelete
  14. Mimi najua baadhi ya taasisi watumishi wake siyo waaminifu.

    Hivyo hata hivyo ERV/NOTICE/Fee form n.k inaweza kuwa feki.

    Pamoja na kukataa sana inawezekana bado hiyo faini imekwenda mitaani badala ya kwenda katika mfuko wa serikali.

    Mdau
    Mkaguzi wa Bloguni

    ReplyDelete
  15. lol, hiyo ndio bongo. angalia kwamba the traffic act ni ya mwaka 1973. miaka mingapi imepita bado haijawa updated. kuna mabadiliko mangapi ya meshatokea?

    ReplyDelete
  16. kuna aliyeuliza namba ya huyu askari, pale naona kuna namba D9968nadhani hiyo inaweza kuwa namba yenyewe. Hongera na pole mdau kwa kutokutoa hongo kwani kufanya hivyo tunazidi kujiharibia wenyewe!

    ReplyDelete
  17. Sikia, hiyo Sh.20,000 umewapa bure, kwa sababu hukupewa risiti (zile risiti za serikali za rangi ya njano).

    Ila kwa sababu una ushahidi, namba ya polisi, ambayo ni unique, unaweza kumshitaki kwenye vyombo vya sheria.

    ReplyDelete
  18. NDUGU MTANZANIA UMEFANYA LA MAANA SANA KWA KULIPA ADHABU.

    HONGERA KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA.

    HERI KULIPA ADHABU, UKA REKEBISHE GARI KULIKO KUTOA HONGO.

    MAINA OWINO

    ReplyDelete
  19. Pole ndugu. Huo ndio utaratibu unaopaswa kufuata. Unakosa kisheria tumikia adhabu ipasavyo, sio kimkatomkato!!

    ReplyDelete
  20. Wadau nina swali: baada ya kubainika kwamba gari la mdau lina water system mbovu na mdau kulipa faini, mdau alilazimishwa kuita gari la break-down kukokota gari lake kwenda kwenye sehemu ya matengenezo? Kama alilipa faini na kuondoka akiliendesha gari si ina maana amerudia tena kosa papo hapo?

    ReplyDelete
  21. Umemlipa elf 20 amekupa notification, na sio risiti! We huoni kuwa umeibiwa na huyo askari?

    Ukiisoma hiyo notification, inakwambia kama unakubali kosa basi saini kipengele fulani B au A i think, kisha uchukue hiyo form pamoja na faini yako ukalipe kwenye mamlaka husika katika kipindi cha siku kadhaa zimetajwa kwenye hiyo notification.

    Notification ni kuwa unataarifiwa juu ya kosa ulilotenda, na sio uthibitisho kuwa umelipa faini, hata kama ameandika received!

    Sasa hawa askari wana lazimisha ulipe hapohapo, na kisha hawakupi risiti. Lengo la kutajwa siku kadhaa, ni kuwa inawezekana msafiri asiwe na hiyo faini pale alipokamatwa.

    Mimi nimeshagombana nao sana juu ya hilo, ndio nakubali kosa lakini kama wanataka pesa hapohapo basi wawe na risit za serikali hapohapo, huwa wanaishia kuniachia tu.

    Hizo notification sio uthibitisho wa kupokea pesa, hivyo hatujui huko ofisini wanaingizaje mahesabu kwenye vitabu!

    Asante

    ReplyDelete
  22. NI UTARATIBU MBOVU KAMA UNAMPA PESA ASKARI UNATAKIWA AKUPE HIYO NOTIFICATION NA PESA UNAKWENDA KULIPA AMA MAHAKAMA AU TRA SI POLISI NA WALA SI KWA WAO HUO NI WIZI, NENDA UHAKIKISHE KAMA PESA YAKO IMEINGIA KATIKA MFUKO WA SERIKALI, KWANI UNAWEZA KUDAIWA TENA, HAO NI WEZI TU.

    ReplyDelete
  23. Mimi najua hizo check up zinatakiwa kufanywa kila mwaka wakati ukienda kurenew registration na unatakiwa upeleke gari ikafanyiwe inspection.

    Na kuna gari zingine mpya unafanyiwa inspection kila miaka mitatu.Sasa hizo za njia na kucheck maji kali sana. sasa ukienda mbele kidogo kuna road cheak point nyingine na askari wengine wataanza nao inspection yao tena. Hiyo safari utafika kweli.

    ReplyDelete
  24. Tungeyajua wapi yote haya kama siyo kwa mifano kama hii. Tunawashukuru sana wadau.Tuombe mwongozo kutoka Polisi kuhusu ukaguzi wa magari. kaka Michuzi kama ungeweza kuwafikishia wahusika. Tunaomba watuelimishe na kutuelekeza taratibu tuzielewe na siyo kuendeshwa kama treni mbovu

    ReplyDelete
  25. maaskari wa bongo waache njaa zao,kosa lahuyo askari ni kuwa alimwambia huyo dereva ampe 10,000 amwachie au amtoze 20,000.hayo ni makosa.Gari likiwa halina maji huo sio ubovu wa gari.JESHI LA USALAMA WA BARARANI LIICHE KULA RUSHWA HIVYO SIO VIZURI...

    ReplyDelete
  26. me hapa ndo nachoooka kabisaa,
    dah,ila umeibiwa jamaa RISITI IKO WAPI?maskini weeee

    ila mmenifungua jicho yan ni kukomaa na mtu nipe ilo notification pesa naenda lipia ofisi za serikali nk

    naombeni simu ya IGP au msaidizi wa maswala aya apa ya askari "barabara"

    nione sasa

    ReplyDelete
  27. Ulifanya vyema kutokutoa hongo. Bali pia si busara wewe kusafiri safari ndefu hivyo bila ya maji ya kioo kwani hii ingeweza kuleta ajali pindi mvua ingenyesha au vumbi vingekutaka kioo kishafishwe. Hata kama sheria haiitaji uwe na maji hayo usalama wako na wengine barabarani vinabusarisha uwe nayo. Matatizo haya yanaepukika tukifuata sheria. Tusipofuata tunatowa mianya ya hongo sisi wenyewe.

    ReplyDelete
  28. Hivi jamani hii imekaaje? Kwamba baada ya jamaa kulipishwa faini kwa ajili ya WATER SYSTEM MBOVU (LOL) anaruhusiwa kuendelea na safari ndefu? Si wadau wengi wamesema kwamba hilo ni kosa na linaweza kusababisha ajali? Sasa ukishalipa hiyo faini ni kwamba huwezi kupata ajali tena? Nilidhani kwamba gari ambayo haifai kuendeshwa barabarani basi ingeegeshwa kabisa mpaka itengenezwe!
    Otherwise the purpose of fining the culprit(s) is just to raise money for the govt and NOT to serve lives!

    ReplyDelete
  29. NEXT TIME, Gne, IT IS SAVE NOT SERVE, SERVE means many things, among them are 1. to perform duties, 2. to attend a customer in a shop or at whatever, these are just few. BUT YOU WERE SUPPOSED TO USE "SAVE" SAVE MEANS AMONG OTHERS TO rescue or to deliver from danger or harm, or to prevent somebody from dying or to guard from injury or loss. There you are! You know the word and its meaning but not the spelling

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...