Kaka Michu!
Basi bwana siku ya Idd ili kuwa taabu kidogo ya usafari hapa London. Nilipanda bus hili maeneo ya East Ham kuelekea Walthamstow, na tulivyofika mitaa green street abiria kibao wakapanda. Dereva akanuna na kususa kuendesha Bus eti sababu ya health and safety risk. Ebo fikiria hapo ingekuwa Kibongo- bongo ingelikuwaje. Ajabu na kweli ni kwamba hadi naondoka abiria ambao wengi wao walikuwa ni wa asili ya Asia walikataa katakata kuteremka. Sijui kwa bongo mambi yangekuwaje hapo??

Mdau Diaspora writer

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Jamani habari ntingine siyo Habari, sasa cha ajabu ni kipi hapo, suala la Afya na Usalama ni muhimu sana katika dunia ya sasa.....

    ReplyDelete
  2. asee nakubaliana kabisa na wewe anon hapo juu huyu jamaa alioleta hiyo habari nadhani atakuwa na matatizo kidogo sasa cha ajabu nini hapo? kila kitu bongo bongo bongo bongo, bongo poa tu sio kila kitu kutaka kufananisha na ulaya acha ulimbukeni wewe

    ReplyDelete
  3. Aacheni majungu nyie...public transport ULAYA ni za ukweli kushinda BONGO hivyo mi naamini hii ingetokea bongo dereva angeendesha gari tu asingejari.ukiangalia vizuri hiyo picha kwa juu pameandikwa NOT IN SERVISE kumaanisha kwamba hilo basi halitatembea tena mpaka abilia wapungue kiasi fulani ndo dereva aendeleshe gari.kwa kifupi usafiri wa ulaya uko poa zaidi kushinda hapo bongo.ni hayo tu!!!!
    Mdau-Ukerewe!!!!

    ReplyDelete
  4. Acheni hizo, dereva anaonyesha alikua racist, hiyo inaeleweka, hizo sababu za kiafya na usalama ni sababu tu.

    ReplyDelete
  5. Hii habari inatufundisha nini wana jamii! habari zingine wala hazisaidii jamii ni basi tu Mathupu angezitema ila kakuonea huruma kwa kulalamika kwa habari zisizozamaana kwa jamii. Think hard before you write something my friend!

    ReplyDelete
  6. LOO!tulivyofika "mitaa ya green steet"?

    ReplyDelete
  7. Mbona Marekani kuna mpaka mikanda ya kusimamia na watu wanashona kama kawa! Nyomi likiliwa linaliwa kama kawa lakini kwa sababu ya Mafua ya Nguruwe uamuzi mzuri!

    ReplyDelete
  8. Dereva hakuwa mbaguzi na ana haki ya kukataa kuendesha gari iwapo watu waiokuwa na ustaraabu wamejaza gari na kukataa kuteremka. Lolote likitokea dreva atakuwa reprimanded na hao waliokataa kuteremka watakuwa wa mwanzo kudai fidia. Aidha si aghlabu kuona jambo kama hilo likitokea katika nchi zilizoendelea japo hata kwetu si tu ni kosa la barabarani bali katika hali ya hatari laweza kumfikisha dreva pabaya kwa "kuhatarisha maisha ya wananchi".

    ReplyDelete
  9. Sasa hapo wengi wao wangekuwa Wazungu, moja kati ya haya yangetokea.

    1. Wengi wasingepanda hilo basi na wangesubiri lingine.

    2. Wengi wangekuwa tayari kushuka ili wasubiri basi lingine

    Sisi wengine tuna matatizo. Mniite mbaguzi mkipenda, ila ukweli ni kuwa tuna MATATIZO SANA.

    ReplyDelete
  10. mabasi ya abiria ya ulaya yanajaza abiria kuzidi hata ya bongo si utani ni ukweli mtupu, basi 58, 69, 257 zote ziendazo huko anakosema walthamstow zote hujaza abiria kibao.

    Ukiangalia kwenye tube zenyewe sana sana 'Central line' abiria wanajaa kibao sio mchezo. Utabakia kunusu vikwapa vya watu tu. Siku nilihesabia watu katika kibehewa kimoja sikuamini kabisa.

    Mdau msemakwelii

    ReplyDelete
  11. wewe acha hizo, ati racist, racist gani hiyo? Abiria kama kibao mara nyingi huwa ni kawaida ya dereva kugoma kuendesha basi. Akiendesha tu amepoteza kazi yake. Na mara nyingi kama unaingia kupanda basi, na unaingilia mlango wa kutokea. mara nyingi huwa unaamrishwa utoke nje, usipotoka dereva haondoi bus.
    habari ndo hiyo.

    Mkulima

    ReplyDelete
  12. huyo aliye ituma hii newz mashamba alikua anataka kutufanya hatuna macho na hatuelewi kitu,huoni limeandikwa not in servici,afu uko state kimombo promblem

    ReplyDelete
  13. HII HABARI NI MUHIMU SANA, NA ANAYESEMA MICHUZI ASINGEIANDIKA ANA UPEO MDOGO SANA

    GARI LIKIJAA SANA UWEZEKANO WA AJALI UNAONGEZEKA...NDIO MAANA BONGO KUNA AJALI NYINGI SANA. HAKUNA DREVA ANAYEWEZA KU-REASON KAMA HUYU HAPA, NDIYO MAANA YANAANGUKA OVYO BONGO! TUJIFUNZE

    MDAU BONGO.

    ReplyDelete
  14. Hilo basi ni la gharofa ni dhahiri likijaza mno ni laweza yumba na kupoteza mwelekeo na kusababisha ajali, dereva ni mahiri kwa kazi yake na ana vigezo vya kazi yake.
    Mabasi unayosema yanajaza sana abiria ni yale ambayo si ya ghorofa.

    London yaelekea hakuna madaraja mengi kama marekani hivyo rahisi kutumia basi la ghorofa, lakini Maekani huwezi enda zaidi ya maili mbili bila kukumbana na barabara kuu maana yake kukumbana na madaraja ambayo kimo ni 13-14 feet, je basi hilo lipita?

    ReplyDelete
  15. afu upo state kimombo promblem......................hahhah ama kweli nyani aoni kundule ,sasa wewe unamnanga mwenzako kuwa yupo state halafu kimombo hakipandi wakati wewe upo tanzania hata hicho kiswahili hakipandi vilevile nani alikuambia kuna neno afu dogo siyo afu sema halafu ..sasa bahati mbaya kabisa wewe hujui vyote hakuna neno promblem ..ni problem dogo nenda shule acha kunanga watu wewe

    ReplyDelete
  16. hilo lilikuwa liko kwenye huduma kama kawaida na ndio unaona watu ndan lakin baada ya hao abiria kuzidi ndio hiyo NOT IN SERVICE akaiweka(imeprogramiwa)tatizo la london watu kila aina wapo hapo na unajua sis weusi na waasia mitimti sana

    ReplyDelete
  17. Dereva kajiogopea shuzi la dengu mwaya, wala sio mjazano.

    ReplyDelete
  18. HAINGII AKILI, KWA SISI TUNAOISHI LONDON NIJUWAVYO MIMI NI DEREVA HUSIMAMA KITUONI NA KUFUNGUA MLANGO AUTOMATICALY AMA KURUHUSU ABIRIA KUTOKA AU KUINGIA SASA ILIKUWAJE YEYE ASIMAME KITUONI NA KUINGIZA WATU WAKATI BUS LIMEJAA? NI UPUUZI WAKE YEYE MWENYEWE KWANI ANARUHUSIWA KUTO KUCHUKUWA WATU KITUONI KAMA BUS LIMEJAA ATASHUSHA TU SI KUCHUKUWA KWA VILE MLANGO WA KUSHUSHA NA KUINGIA NI MIWILI TOFAUTI

    ReplyDelete
  19. EBOOOO, WATU WAMEINGIAJE HUMO WAKATI HAPO MBELE LIMEANDIKWA NOT IN SERVICE!!!!!!!!!!!!!! NDO MAANA ALIKATA KUENDESHA. HUO NI USHENZI WA NYINYI WATU WA KUJA MLOZOWEA DALADALA NA UBABE WA KIMBUZI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...