Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro amezihimiza nchi wanachama wa UN kuongeza kasi ya mchakato wa kusaini, kuridhia na kuutekeleza Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu bila ya kuchelewa.
Alikuwa akifungua mkutano wa pili wa nchi ambazo zimekwisha saini na kuurithia mkataba wa haki za watu wenye ulemavu. Mkutano huo wa siku tatu unafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Ameuelezea mkataba huo ambao utekelezaji wake ulianza mwaka 2008, kuwa ni wa muhimu sana kwa ustawi na maendeleo ya watu wenye ulemavu na kwamba utekelezaji wake ni utekelezaji wa haki za binadamu.
Dkt. Migiro amewaeleza wajumbe wa mkutano huo wakiwamo kutoka vyama vya kijamii vya watu wenye ulemavu, na watu wenye ulemavu wa aina mbalibali, kuwa mkataba huo unatoa mwongozo wa kusimamia haki za wanawake, wanaume na watoto milioni 650 wanaoishi na ulemavu ulimwenguni kote.
“ Mkataba huu unatoa fursa ya uwezeshwaji wa watu wenye ulemavu kushiriki kikamilifu katika mambo mbalimbali pamoja na kujumuika katika jamii. Kwa sababu hiyo nazisihi nchi zote kuendelea na juhudi za kusaini, kuridhia na kuutekeleza kwa vitendo mkataba huu” akasisitiza Naibu Katibu Mkuu.
Hadi kufikia mwisho mwa mwezi Machi 2007, nchi 142 zilikuwa zimeshasaini mkataba huo, huku 66 zikiwa zimeuridhia. Aidha nchi nyingine 85 zimesaini Itifaki ya hiari ya nyongeza ya mkataba , na nchi 44 zikiwa zimeridhia Itifaki hiyo.Tanzania ilisaini Mkataba huo wa haki za watu wenye ulemavu mwezi Machi mwaka 2007, na ikasaini pia itifaki ya hiari mwezi Septemba mwaka 2008.
Aidha migiro ameeleza kwamba katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na changamoto mbalimbali katika suala zima la maendeleo , ustawi na maendeleo ya mamilioni ya watu wenye ulemavu duniani kote unakuwa katika mashaka zaidi.
Pamoja na kuzihimiza nchi ambazo hazijasaini au kuridhia mkataba huo kufanya hivyo, ametumia fursa hiyo kuzishukuru nchi ambazo zimekwisha kufanya hivyo. Na kuwataka washiriki wa mkutano huo kutumia siku tatu hizo kubadilishana uzoefu juu ya utekelezaji wa mkataba huo.
Akaongeza kwa kusema inafurahisha kuona kwamba nchi nyingi tayari zimepitisha sheria na sera mpya au kuzifanyia marekebisho zile zilizopo ili ziende sambamba na mkataba huo.
Naibu Katibu Mkuu huyo amewahakikishia wajumbe wa mkutano huo kwamba Umoja wa mataifa uko tayari kusaidia na kuunga mkono juhudi zinazofanyika katika ngazi ya kimataifa, kikanda na kitaifa katika kukamilisha mpango wa utekelezaji wa mkataba huo.
Mkutano huo ambaoni siku tatu utatoa fursa kwa washiriki kujadiliana na kubadishana uzoefu kuhusu utekelezaji wa mkataba huo, fursa sawa kwa watu wenye ulemavu mbele ya vyombo vya sheria na ushiriki katika utoaji wa maamuzi mbalimbali na hasa yale yanayowahusu.
Aidha wajumbe hao pia watajadili kuhusu wajibu wa mabaraza ya kutunga sheria yanavyoweza kutimiza wajibu wao katika utekelezaji wa mkataba
mhe mama Migiro naona umejisahau kama huu ni mwezi mtukufu, hata ukiwa umoja wa mataifa funika basi hicho kichwa. usisahau kuna umoja wa mataifa wa Allah siku ya kiama.
ReplyDeleteMichuzi usibanie comment.
kama ni kufunika kichwa bora afunike wakati wote na siyo kusubiri MWEZI MTUKUFU.
ReplyDeletesuala la kutenda mema na kumcha MUNGU ni la wakati wote wa maisha yetu siyo MWEZI MTUKUFU tu.