
Matokeo ya mauaji ya kimbari yaliongeza chuki zaidi kati ya Wahutu na Watutsi. Katika hali ya kawaida, wengi tungetegemea Rwanda ingesuasua na ingedidimia zaidi. Lakini ukienda Rwanda utaona maendeleo makubwa mno; wafanyakazi kuanza kazi saa moja asubuhi, ujenzi, barabara nzuri nk.
Badala ya kuona na kukaa kimya au kuanza kulalamika nimeonelea ni busara kuandika na kushare huku nikitarajia tutaweza kujifunza kwa majirani, ambao kasi yao wengine wanasema wameshatuacha au watatuacha mbali.Haya ni machache; Uongozi bora, Uthubutu wa Wanyarwanda, Usafi na utii wa Sheria, Nyumbani ni Nyumbani na Mipango miji.
Uongozi bora wa Rais Paul Kagame umechangia kwa kiasi kikubwa sana kuifikisha Rwanda hapa ilipo. Wiki iliyopita Rwanda imetajwa na ripoti ya Benki ya dunia kama nchi iliyoboresha zaidi mazingira ya uwekezaji. Tofauti kubwa na nchi nyingi za kiafrika, Mawaziri wanaendesha magari na tena sio mashangingi kama TZ.
Tulishuhudia Rais Kagame mwenyewe akiendesha gari !. Ikiwa Rais anaonyesha mfano mara nyingi viongozi wengine watafata. Kagame amesimamia utawala bora, ukiwa Rwanda na ukafanya kosa hakuna cha wewe nani, jamaa hawapokei rushwa!. Jarida la TIME lilimtaja Rais Paul Kagame kati ya watu 100 wenye ushawishi duniani. Najua kwa kutambua uwezo wa Kagame, Tony Blair hakusita kuwa mshauri wake binafsi!.
Uthubutu wa Wanyarwanda:
Tukifuata historia Wanyarwanda huzungumza kinyarwanda na kifaransa. Hili sasa limebadilika Wanyarwanda wanazungumza kiingereza na Kiswahili vizuri!. Kwa wale wafuatiliaji wa BBC idhaa ya kiwahili, siku chache zilizopita ilizungumzia uanzishwaji wa ufundishaji wa Kichina kwenye chuo kikuu cha Kigali!.  Tayari wanafunzi wengi wanasoma na wanaongea Kichina, hii ni ishara tosha ya uthubutu wa Wanyarwanda, wanatambua umuhimu wa kujifunza lugha nyingine muhimu. Jambo kuu zaidi ni Warwanda kuyapa kisogo yaliyotokea na kuangalia mbele. Dereva wa texi aliyeniendesha alipoteza wanafamilia wote kwenye mauaji yale, lakini anaangalia mbele.
Jambo la kwanza kugundua ufikapo Rwanda ni usafi wa hali ya juu wa jiji la Kigali. Hairuhusiwi kutupa takataka ovyo bali sehemu maalum zilizotengwa. Kusisitiza suala la usafi kila Jumamosi ya mwisho ya mwenzi ni siku ya usafi kila mtu anashiriki katika kufanya kazi za usafi, hili pamoja na sheria zimefanya tabia ya usafi ijengeke. Sheria za usalama barabarani ni msumeno, kila anaendesha pikipiki ni lazima avae kofia pamoja na abiria. Waendesha pikipiki za kukodi wana namba na mavazi maalum ya kazi, hili linafanya kutambulika kwa rahisi. Usalama wa Rwanda ni jambo jingine ambalo ni thahiri, hapa napata swali lisilo na jibu; polisi huwianisha uhalifu wa silaha na nchi zenye au zilizokuwa na machafuko. Iweje Rwanda iliyotoka kwenye machafuko, iko jiranio zaidi na nchi zenye machafuko hadi leo za Burundi na Congo iwe salama hadi mabenki yanafungwa saa nne usiku!.
From Rwanda with lessons – Part II itafuata.
Mdau IK.
Machafuko yanaweza yakatoa mchango fulani katika kustawisha utawala wa sheria. Tunaona mazingaombwe yanayofanyika mahakamani kwa wahalifu wakubwa, mafisadi nk. Ni wazi kwamba kwa mtaji huo ambao tumerithi toka utawala wa Mwalimu hautatufikisha popote.
ReplyDeleteKila kitu ni uongozi bora. Pia nchi yetu nikubwa kuliko Rwanda na tuna makabila mengi mno.Tukitaka kuendela ni lazima turudishe madaraka mikoani na Wakuu wa mikoa wawe wna chaguliwa siyo kuteuliwa. Hii inakuwa mfano wa Marekani kwa magavana au premier kwa Canada. Kila mkoa utunge sheria kabambe za kumiliki resources kwa manufaa ya wananchi wake, na sheria kama usafi, usalama barabarani na barabara kwa ujumla. yaani majukumu ya serikali kuu na serikali za mikoani yajulikane. Hii ku centralize kila kitu kunakuwa hakuna uiano sawa wa kimaendeleo
ReplyDeletewanaelekea wamejitahidi ila jamaa nae mnazi sana huyu...
ReplyDeleteWanyarwanda inabidi wajifunze kutoka kwetu. Ukiharibu sehemu moja unahamishiwa sehemu nyingine.
ReplyDeleteKAMA KLINTONI ALIKUWA RAIS BORA KWA WAKATI HUO HAPA NDIPO ALIPOTOKOTA. INAWEZEKANA YALIYOTOKEA SOMALIA YALIMKATISHA TAMAA. LAKINI SIO KISINGIZIO
ReplyDeleteVIONGOZI WETU NI WACHOYO NA WABINAFSI HAWATAKI WATU WENGINE WAFAIDI MATUNDA YA NCHI, WANAFANYA NCHI NI MRADI WAO NI WACHO NA WEZI, MPAKA TUPIGANE VITA YA SISI KWA SISI NA TUUWANE NDO UCHOYO WAO NA UBINAFSI WATAACHA, NASI TUMEZIDI KUWA KAMA KONDOO, TUNAPELEKWA MAJINJIONI TUKO KIMYA TU HATFURUKUTI KAMA MBUZI, SOMETIMES WE NEED TO MBUZI, VIONGOZI NI AIBU HIYO WACHANE UCHOYO NA UBINAFSI NA WIZI WA MALI YA UUMA KWA MANUFAA YENU NA WAKE ZENU
ReplyDeletewatanzania tumekalia kusema sisi tuna amani bwana!amani my FOOT!tanzania lazima damu imwagike hapo ili heshima iwepo kwa viongozi na watu wa chini.
ReplyDeleteNINI TOFAUTI YA MKIMBIZI MASKINI NA TAJIRI. UTAJIRI NA UMASIKINI SI CHOCHOTE BALI NI KURIDHIKA NA ULICHONACHO NA KUTOKURIDHIKA NA ULICHONACHO.KOSOVO 1992 KILIKUWA NA WAKIMBIZI , VIVYO HIVYO AFRIKA IMEKUWA NA WAKIMBIZI LABDA MILELE HADI KUFIKIA WAKATI WA VITA YA MFEKANE. TOFAUTI YA WAKIMBIZI WA KOSOVO NA WAAFRICA NI KWAMBA WAZUNGU WANAKIMBIA NA MIGUU YAO ILI MRADI WASALIMIKE. WAAFRICA WENGI WAMEJIKUTA WAKIRUDI KWENYE NYUMBA ZAO KUCHUKUA THAMANI ZAO MAGODORO, REDIO NA VINGINE MAANA YAKE WAKO TAYARI WAFE ILI MRADI WAOKOE NA KUONDOKA NA THAMANI ZAO. TULIZALIWA BILA KITU KWA HIYO KUTOKUWA NA KITU NDIO KUZALIWA UPYA.
ReplyDeleteNAJUA WENGI MNAUCHUNGU NA WATAMANI KAMA WANGEISHI RWANDA KWANI MAMBO MAZURI, HAKUNA MATATIZO KAMA YA HUKU YA TRA YA KUTAFUTIANA UBAYA, HAKUNA MATATIZO YA WIZI KAMA UWANJA WA NDEGE WA JNIA,
ReplyDeleteILA NATAKA NIWAAMBIE KITU KIMOJA KIKWETE ANATAKA KUTUMIA SYSTEM YA ROMA HAKIJENGWA KWA SIKU MOJA YA KUWANYOOSHA MAFISADI,KWA JINA LINGINE TUNAITA STEP BY STEP (bureaucracy ) UTAWALA WA SHERIA, LAKINI SISI TUNATAKA KU-DEAL NA HAWA WATU WA TRA NA JNIA HARAKA (FASTA BILA KUCHELWESHA) KAMA TUKIPEWA RUNGU,TUTASHUGHULIKA KWANI TUNAJUA KILA KITU KINACHOFANYIKA TRA KUANZIA WANAVYOJITENGENEZEA CHEQUE, PIA WANAVYOWAKANDAMIZA WANYABIASHARA KWA KUWATOZA KODI KUBWA NA KUWATISHA KUWA INVOICE FAKE, PIA MARA NYINGINE KUWAAMBIA ANAYETAYARISHA DOCUMENT HAYUPO LETA PESA TUKUSAIDIA FASTA BADALA KUSUBIRI KESHO ULIPE STORAGE CHARGE,NJIA YA KUMTISHA MTEJA , HII KITU INASABABISHA WAFANYABIASHARA WAINGIZE VITU FEKI ANGALAU WARUDISHE NA FAIDA BAADA YA KUHONGA, SASA KAMA JUKUMU HILI TUKIPEWA USALAMA WA TAIFA TUTALIMALIZA MARA MOJA TUTAWAIBUIA HAWA WOTE KUWAONDOA KWENYE NYADHIFA, NA WENGINE KUAJILIWA KUZIBA MAPENGO HAYO, TATIZO LIKO HAPA CHINI, ILA NGUVU INABIDI ITOKE JUU, ILA MSIHOFU KILIO CHA MNYONGE KITASIKIKA, SIKU ZA ZINA HESABIKA WATAHAHA KUFUTA USHAHIDI HAWA TRA, VILE VILE 9uWANJA WA NDEGE) JNIA DAWA YAO IPO TU, MUDA SI MREFU TUWASHUGULIKIA.
THANKS
MDAU
USALAMA WA TAIFA.
Mdau wa kwanza kwa hiyo Tanzania nayo inabidi iingie katika machafuko ya kivita ili wabongo tupate mwamko wa kudai haki zetu,au ?
ReplyDeleteKagame ni mfano wa kuigwa Afrika.Kama yote ni somayo kwenye vyombo vya habari kuhusu Rwanda ni kweli watakuwa in a good track
ReplyDeleteNa ndio nchi ya kwanza duniani kufanya vyema baada ya mtikisiko wa uchumi duniani.
ReplyDeleteJamaa walionyeshwa juzi kwenye CNN
Hio title hakuna nchi yoyote duniani itakayolichukua.
BIG up Rwanda.
MNAELEWA PESA NGAPI RWANDA WAMEPEWA NA BELGIAM KWA HASARA WALIZOWACHIA?
ReplyDeleteNA PESA NGAPI ZIMETOKA UN KWA HASARA WALIZOWASALITI?
NA PESA NGAPI WAMEPATA TOKA MAREKANI ?
KIASI WAWE HAPO WALIPO NA PIA BIDII ZAO HUWEZI KUFANANISHA NA SOMALIA AU NIGER AMBAO MAREKANI HAWATAKI HATA WAENDELEE.
UNAFIKIRI BILA MISAADA YA NJE RWANDA WANGEKUWA HAPO?
CHA KUSIFU NI RWANDA KUTUMIA PESA ZA MSAADA ILIVYOTAKIWA NA KUSHUKURU MWENYEZIMUNGU WAPO HAPO KATIKA HALI NZURI. TUWAOMBEE WENGINE WAFIKIE HAPO AMBAO WAPO KWENYE MATATIZO. PAZI.
NCHI YETU YA TANZANIA SASA HIVI HATA VIONGOZI HAWAJUI SHIDA HATA WAPEWE NINI HAIWEZEKANI.
RWANDA VIONGOZI NAO WALIONJA SHIDA NDOMANA PESA WAMEZITUMIA VIZURI HAWATAKI KUONJA SHIDA NA MATESO WALIYOYAPATA. HIYO NDIO TOFAUTI YA RWANDA NA TANZANIA SIO KUSEMA TUMESHINDWA NA RWANDA.
Well, nadhani wanatia chunvi haya maendeleo ya Rwanda. Nchi haina umeme asilimia 90, how can it develop? Universities zake are ranked out of the best in africa, Kigali is small but still has slums, poor salaries of civil servants. Ok, with genocide, we can say they are trying, but it should not get into Kagame's head. Do more major general!
ReplyDeleteHistoria inaonyesha mara nyingi ni lazima zipigwe kwanza ndio heshima ipatikane.
ReplyDeleteinawezekana mafisadi wa Rwanda walikufa wote mwaka 1994.
ReplyDeleteHalafu ww anon uliyejiita usalama wa taifa mbona unaimaindisha kazi ya watu wakati wenyewe hua hawajitaji.....ooh shauri yako angalia wasije wakakutoa nishai hao.
Anayesema wanatia chumvi na asome hapa:
ReplyDeleteAfrica: Rwanda Named World's Top Business Reformer
9 September 2009
--------------------------------------------------------------------------------
Email|Print|Comment(4)
Share:
Cape Town — Rwanda was named today as the world's top business reformer, measured by the changes the country has made over the past year to make doing business there easier. And Mauritius retained its top ranking as the African country in which it is easiest to do business.
The two countries are named as top performers in the annual report on the ease of doing business published by the International Finance Corporation (IFC) and the World Bank.
"It now takes a Rwandan entrepreneur just two procedures and three days to start a business," said a statement issued by the IFC and the World Bank.
"Imports and exports are more efficient, and transferring property takes less time thanks to a reorganized registry and statutory time limits. Investors have more protection, insolvency reorganization has been streamlined, and a wider range of assets can be used as collateral to access credit."
Rwanda's ranking was based on the number and impact of reforms introduced in the year to May 2009.
Business Reforms
Document: Doing Business 2010: Reforming through Difficult Times - An Overview
Mauritius held its position as Africa's easiest place to do business by passing a new insolvency law, setting up a specialized commercial court, easing property transfers and expediting trade processes, the statement said.
The IFC and the World Bank also named Liberia and Egypt as being among the world's top 10 reformers.
"Liberia... eased procedures for business start-up, reduced fees for construction permits, and sped trade with a new one-stop centre," the statement said. "Sierra Leone introduced a company law that strengthened investor protections, enhanced access to credit, and provided for the reorganization of troubled firms. It also established a one-stop centre for business registration."
Other African countries cited for their reform efforts included Burkina Faso, Angola, Cameroon, Ethiopia and South Africa.
http://article.wn.com/view/2009/09/09/Rwanda_Named_Worlds_Top_Business_Reformer/
Vigogo 17 kuwakaanga Mramba, Yona, Mgonja
ReplyDeleteNa Hellen Mwango
23rd September 2009
Mawaziri wa zamani, Basil Mramba ( kulia), Daniel Yona (katikati) na aliyekuwa Katibu Mkuu, Gray Mgonja (wa pili kulia) wakiwasiliana na mawakili wao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana.
Upande wa mashitaka katika kesi ya kutumia madaraka vibaya na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7 inayowakabili waliokuwa Mawaziri waandamizi, Basil Mramba, Daniel Yona na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, unatarajia kuita mashahidi 17.
Kati ya mashahidi hao wa upande wa mashitaka, yumo aliyewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Abdisalam Issa Khatib.
Shahidi mwingine ni aliyekuwa Kamishna wa Madini katika Wizara ya Nishati na Madini, Gray Mwakalukwa, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Madini Tanzania (Stamico) na maofisa wengine kutoka serikalini.
Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la mahakimu watatu, John Utamwa, Saul Kinemela na Deo Rumanyika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Wakili wa Serikali Mkuu, Boniface Stanslaus, alidai kuwa upande wa Jamhuri unatarajia kuita mashahidi 17 katika kuthibitisha tuhuma dhidi ya washitakiwa hao.
Stanslaus aliwataja mashahidi wengine kuwa ni Maria Kejo, Nakuwera Senzia, Kesisia Mbatia, Betha Kisoka, George Kaindoa, Nyelo Godwin, George Tigiti na Aggrey Temba.
Kaindoa alikuwa Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Alex Stewart ( Assayers) Government Business Corporation iliyopewa jukumu la kufanya ukaguzi wa madini.
Wengine ni Bashiri Mrindoko J. Mrindoko (Kamishna wa Nishati), Rehema Kitambi, Mustapha Ismail, Ludovick Kandege, Saddy Kambona, P.M. Kasera na Christin Shekidele.
Wakili huyo alidai kuwa hiyo ndiyo orodha ya mashahidi wa Jamhuri na kwamba wataitwa kupitia ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru).
Baada ya Jamhuri kutoa orodha na majina ya mashahidi wao, wakili huyo aliiomba Mahakama kuuamuru upande wa utetezi kutoa orodha ya mashahidi wa washtakiwa hao.
Hata hivyo, wakili wa Mramba, Hubert Nyange, alidai kuwa washtakiwa hawawezi kutoa orodha ya mashahidi hadi pale mahakama hiyo itakapowaona wana kesi ya kujibu.
Nyange alidai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kifungu namba 231 kidogo cha (1) (a), Mahakama inamtaka mshtakiwa atoe ushahidi ama kwa njia ya kiapo na aite mashahidi wake na si vinginevyo.
Aidha, upande wa mashitaka ulidai kuwa kwa mujibu wa waraka uliotolewa na aliyekuwa Jaji Mkuu wa zamani, marehemu Francis Nyalali, ni lazima upande wa utetezi utoe orodha ya mashahidi dhidi ya washtakiwa.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo ambapo upande wa utetezi umeomba muda wa kupitia waraka huo.
Awali mahakamani hapo, upande wa mashitaka ulidai kwamba Mramba alimuelekeza Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), marehemu Daudi Ballali na kampuni tanzu ya Alex Stewart ( Assayers) Government Business Corporation kuusaini mkataba unaoruhusu kampuni hiyo kupata msamaha wa kodi pasipo kuthibitishwa na Baraza la Mawaziri au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Pia ilidaiwa kuwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alibariki kampuni Assayers kuteuliwa kufanya ukaguzi huru wa madini ya dhahabu baada ya kuandikiwa barua na mshitakiwa wa pili, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa walipohojiwa na Takukuru walikiri kuhusika na tuhuma zinazowakabili.
Hata hivyo, washtakiwa kwa nyakati tofauti walikana kukiri tuhuma hizo walipohojiwa na Takukuru.
Katika kesi hiyo, washitakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14, mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka yao.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao walitoa msamaha wa kodi bila kusikiliza ushauri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha.
Waziri wa Afrika Mashariki alia na wingi wa bidhaa feki
ReplyDeleteNa Dominic Nkolimwa
23rd September 2009B-pepeChapaMaoni
Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Diodorus Kamala.
Waziri wa Afrika Mashariki, Bw. Diodorus Kamala, amesema Serikali haitakubali kuona viwanda vya ndani vikifa kutokana na soko kutekwa na bidhaa feki zilizozagaa kila mahala nchini.
Ameyasema hayo wakati akikagua kiwanda kimoja cha kutengeneza vifaa vya umeme Jijini, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kujifunza bidhaa na aina ya viwanda vilivyopo nchini kwa ajili ya kutafuta soko katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema kuwa hivi sasa, soko lote la Afrika Mashariki limetawaliwa na bidhaa feki kutoka nchi za nje, jambo linalosababisha hasara kubwa kwa wananchi na kuathiri viwanda vya ndani kutokana na bidhaa hizo kuuzwa kwa bei ya chini ukilinganisha na bidhaa halisi.
Aidha, akasema si bidhaa feki pekeetu zinazoweza kuua viwanda vya ndani, bali hata bidhaa zinazozalishwa kwa ruzuku, kwani zenyewe pia huuzwa kwa bei za chini.
"Ni lazima tuendelee kudhibiti soko hili ili wajanja wachache wasiliharibu na kuua viwanda vya ndani," akasema.
Akaongeza kuwa sasa ni wakati muafaka kwa wazalishaji wa ndani kuisaidia Serikali katika vita hiyo kwa kupendekeza njia bora ya kumaliza tatizo hilo.
Akiendelea, akasema ofisi yake itakuwa wazi kutoa msaada wowote katika kuimaRisha soko la bidhaa za Tanzania katika soko la Jumuiya hiyo inayoundwa pia na nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.
Kamala ameongeza kusema kuwa sasa Tanzania inafanya vizuri katika soko la Afrika Mashariki kwa bidhaa za viwandani, ukilinganisha na bidhaa zitokanazo na kilimo eneo ambalo imekuwa ikifanya vibaya katika soko hilo.
"Muungano huu lazima uwe na tija kwa nchi yetu kwa Watanzania kuzalisha sana na kuuza katika soko hilo ambalo linahitaji sana bidhaa kutoka Tanzania kutokana na ubora wake," akasema Kamala.
Akaongeza kuwa hivi sasa, soko zuri katika Jumuiya hiyo ni nchi za Burundi na Rwanda, kutokana ukweli kuwa gharama za kusafirisha bidhaa kwenda katika nchi hizo ni nafuu zaidi kulinganisha na sehemu nyinginezo.
Hakuna chumvi katika lisemwalo hapo Rwanda imepiga hatua kubwa sana ya maendeleo miaka 15 baada ya mauaji.Umeme kukatika ni nadra sana, rushwa imetokomezwa hali ya usalama iko juu sana katika kitongoji chochote cha nchi. Badala ya kushabikia hii ni chumvi ama vipi tuangalie ni jinsi gani nchi hii imeweza kujitoa kwenye hali iliokua nayo na sasa inasonga mbele.Tena nchi isiokua na maliasili yoyote.
ReplyDeleteUkitaka kujua wenzetu wanajiamini vipi ndio nchi ya kwanza Jumuia ya Afrika Mashariki kufungua milango kwa raia wote wa Afrika Mashariki kufanya kazi na kuishi bila kuhitaji vibali vya aina yoyote. Sisi bado tunaogopa wakenya na waganda kuja Tanzania maana ni waoga wa kushindana.
Mdau IK na wote waliochangia Maoni ya Mdau IK kutokana na trip yake huko Rwanda nawapongeza. Napenda pia nitoe yangu:
ReplyDeleteNimefika Rwanda kabla ya 1994 na pia mara mbili baada ya hapo mara ya mwisho ikiwa ni wiki tatu zilizopita. Observations (partial ones) of anyone visiting Rwanda for the first time will be the same as IK's. But, I am afraid that things are not as they seem to be particularly katika hili la utawala bora!! Njia iliyoamuwa kutumiwa na serikali, the Honorable Kagame, inakula zaidi kwa walio wengi ili kuendelea kuipa nguvu serikali yake na hasa nje. Swala la haki na usawa bado ni ndoto kwa raia walio wengi. Nenda vijijini ona raia wengi wasivyoweza kupata huduma muhimu, wanavyohofia usalama wa maisha yao. Kila kukicha wanashukuru Mungu. Wanaishi na kufanya wafanyayo kwasababu hakuna a way out!!! Lakini pia naungana na mdau aliyezungumzia swala la mishahara ya watumishi wa umma....ni midogo mno na hasa kwa maisha ya mijini!!
Kwa kulinganisha kabla ya 1994 na baada ya hapo Rwanda bado iko juu kwetu. Lakini naomba wadau wasiipe serikali sifa isizostahili. Sifa hizo ni za wanyarwanda wote...ndivyo walivyo kabla na hata milele...wachapakazi, wasiohitaji kusukumwa sana kuamua hatima ya maisha yao.
Mdau K Jr.
rwanda waruhusu wakimbizi wa kihutu kurudi nyumbani kwao. waachane na PR stunt za kudai wanaruhusu kila raia wa afrika mashariki kuweka makazi rwanda. watanzania mkiingia mkenge wa kuruhusu wahamiaji mtaona jinsi wanyarwanda na wakenya watakavyomiminika huku kwetu.
ReplyDelete