Je, umesimamishwa na polisi wakati ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?

zijue haki na wajibu wako !

Bila kufuata sheria na kanuni za usalama
barabarani kutakuwa na vurugu katikabarabara zetu.

Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za Barabara – iwapo kila mmojaatazifuata sote tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao,isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.


Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya kisheria na kukueleza ni wakati ganianakusimamisha uwapo barabarani.


Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na kuyaweka kwenye gari lako – lakini kumbukakwamba ni mwongozo tu.


Mamlaka ya kusimamisha gari lako:

Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari lako – kamaatakupa ishara ya kusimama, punguza mwendo kwa usalama na utoke barabarani – piaanaweza kukuuliza jina na anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya Usalama Barabarani (RTA),s.78).


Leseni ya kuendesha gari:

Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni yako yakuendesha gari – anaweza kukataa fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua kupelekaleseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha polisi kilichochaguliwa na ofisa.Ili kuepukamatatizo, wakati wote tembea na leseni yako kwenye gari (RTA s.77).

Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko cha usajili – gari lazima liendane na maelezo yakwenye kibandiko, lakini vitu vidogokama rangi iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).

Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama umebandika leseni halali ya barabarani nakibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo cha gari lako (kioo cha mbele).

Kunyang’anywa:
Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko na kuchukua leseni
isipokuwa kwa mujibu wa sheria.

Mikanda ya kiti ya usalama:
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima mfunge mikanda ya kiti ya usalama unapoendesha (gari iwe inatembea au imesimama) – unatendakosa kama unaendesha wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa abiria wote wafunge mikanda.

Kuendesha baada ya kunywa pombe:
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa pombe na huwezi kulidhibiti gari ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi chapombekwenye damu yako ni zaidi ya kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa na hatiaya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).

Kutumia simu ya mkononi wakatiunaendesha:
ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la “kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).

Mwendo kasi:
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi, (ikiwa ni pamoja na km 50kwa saa katika maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na alama) – ofisa wa polisianaweza kupima mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata hivyo, unawezakupinga ushahidi wake mahakamani (RTA s.51, s.73(2)).

Kustahili kuwepo barabarani:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama gari lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi, breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe vinafanya kazi vizuri –unawezakutakiwa kupeleka gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1, s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako limekaguliwa.

KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU KWAMBA UMEFANYA KOSA:
Mara nyingi utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa faini ya sh. 20,000 kwaofisa wa polisi, au kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa ataandika maelezokwenye Fomu ya Polisi ya PF 101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu iliyotiwa saini. Unaweza kwenda na ofisa kwenye kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda wake wa eneo (RTA, s.95).

KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA NJIAYOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO: muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na anwani ya kituo cha polisianakofanyia kazi (unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka malalamiko ya maandishikwa Ofisa Msimamizi Mkuu – ambaye atachunguza na kujibu.

Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa waaminifu –
usitoe rushwa na usipokeerushwa.
Said A. Mwema
Inspekta Jenerali wa Polisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Asante IGP Mwema. Asante na ubarikiwe. Nimekipenda kipengele cha kutuma malipo kwa kamanda wa eneo.

    ReplyDelete
  2. Kitu kimoja ambacho ningetaka kufahamu ni kwamba je tumefikia uamuzi Mimi na polisi wa kwenda kupelekeshana Kituoni, polisi huwa wanaingia kwenye gari yako na kudandia raidi. Je nnahaki ya kumkatalia kupanda gari langu? Yeye atembee Mimi niendeshe tukutane kituoni.

    ReplyDelete
  3. Obwatasyo OmpokocholeSeptember 23, 2009

    1.Kamanda Mwema asante sana kwa kutumbusha hayo muhimu. Tunakukubali sana na tunakutakia utendaji mwema wewe na jeshi lote la Polisi.

    2.Isipokuwa katika hisabati ambapo hasi zidisha hasi hubadilika na kuzaa chanya; tunakiri kuwa makosa mawili hayabadiliki yakawa si makosa (halali). Hata hivyo bado utawala wa sheria unatuhitaji kuhukumu na kutoa adhabu kwa HAKI. Je ni HAKI kuwatoza madereva raia faini eti kwa sababu hawana 'fire extinguishers' na 'Triangles 2' wakati tunajua kuwa madereva wa magari madogo na makarandinga ya Polisi / Magereza yanatembea sio tu bila hivyo vitu bali mengine yana makosa kibao ya kiufundi?

    Tunaomba tuwatendee raia kama ambavyo maaskari tungependa pia tutendewe hii ni pamoja na suala la kufunga mikanda na kuvaa Helmet tuwapo na pikipiki zetu maana ' We don't have any special immunity to accidents'. Aidha kero hii inaweza kukaribisha 'mahakama za umma barabarani (zitakazosimamiwa na sheria ya kukosa uvumilivu ya miaka yote tangu kuumbwa ulimwengu)kutuhukumu vibaya!

    ReplyDelete
  4. SWALI LANGU NI KWAMBA SIHITAJIKI KULIPA FAINI PALE PALE KWA POLISI BARABARANI? ANATAKIWA ANIPE KIPANDE CHA KARATASI KITAKACHONIELEKEZA WAPI NATAKIWA NIKALIPE HIYO FAINI, KAMA NI SAWA NA KA SI HIVYO MIMI SIAFIKI KUMPA POLISI BARABARANI FAINI YANGU NATAKA NIKAITOLEE OFISI NA NIPATIWE RISITI YA SERIKALI, NA NDIVYO ILIVYOKUWA SIKU ZOTE HII MPYA YA KUMPA POLISI PESA BARABARANI NI MPYA. MOJA YA SABABU YA POLISI KUTOLIPA PESA KATIKA DALADALA TULIAMBIWA NA MREMA WAKATI HUO AKIWA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KUWA POLISI HARUHUSIWI KUTEMBEA NA PESA AKIWA KAZI NDO MAANA ATASHINWA KULIPA NAULI YA DALADALA, PIA SI BUSARA KWA ASKARI KUPOKEA FAINI SUPPOSE THAT DAY AMEKUSANYA FAINI ZA WATU MIA PESA ZOTE HIZO ATATEMBEA NAZO TU, PIA NI LOOPE HOLE YA WIZI KWANI WANAWEZA KUCHONGAA RISITI FAKE NA NI KITU KINAWEZEKANA SANA. TU TANZANIA YA LEO. NAKUOMBA SAID MWEMA KAMA KUNA UTARATIBU HUO WA KUTOA FAINI BARABARANI UTAZAMWE UPYA NA UFUTWE.

    ReplyDelete
  5. BLOG YA JAMII INASAIDIA SI UNAONA SAID MWEMA AMECHUKUWA MUDA WAKE NA KUTOA MONGOZO KWA JAMII, SO WE BEG OTHER GOVERNMENT LEADERS TO VISIT THIS BLOG AS IT WILL HELP THEM TO SEE WHAT WE HOI POLLOI WHAT WE WANNA THEM TO DO FOR US, THIS IS OUR COUNTRY, IT IS NOT THEIRS ALONE, THEY MUST REMEMBER THAT, IT IS US WE EMPLOYED THEM SO THEY HAVE TO WORK FOR US NOT FOR THEMSELVES. TIME WILL COME AND WE WILL RENEW THEIR CONTRACT VIA BALLOT BOXES - KUPITIA KURA.

    ReplyDelete
  6. wadau kesi ya mzee wavijisenti na bajaji inaendeleaje. (huyu mzee namkubali sana alisema vijisenti akimaaanishe wengine wamekula pakubwa) lakini waandishi habari wetu wako shalo sana kwenye kuanalaizi mambo wakakurupukuka ikawa ukweli wake ni kasha kumbe wala tuupende na kuukumbatia yukweli ili tuwe huru.

    ReplyDelete
  7. ungetuuliza maswala ya TRA na Julius Nyerere International Airport-JNIA pia tungekupa tano, ila dawa yao iko jikoni, Naona kama wanacheleweshwa, Ajila siko nje nje hapo atolewe mtu anaingizwa mtu damu mpya.

    Thanks.

    ReplyDelete
  8. Tunakushukuru sana Bwana Michuzi na pia tunamshukuru SAID MWEMA kwa kutoa ufafanuzi kwa masuala ambayo tunakumbana nayo.na hayo ndiyo yalikuwa mategemeo yetu tunapoleta issue kwenye blog tunategemea kupata ushauri na maelekezo. Tunaosoma Michuzi tumeelewa. naomba kumshauri SAID MWEMA kuchukua hatua zaidi za kuelezea haya labda kwa njia ya redio na magazeti. Kidogo itapunguza tunayokumbana nayo ili raia na polisi tuweze kuelewana

    ReplyDelete
  9. WEWE INSPECTOR,NAKUOMBA TAFUTA MTU UNAYEMWAMINI MWAMBIE AENDESHE GARI KUTOKA DAR MPAKA MOSHI. NAKUHAKIKISHIA UTAFUKUZA KAZI POLISI SI CHINI YA ISHIRINI.JARIBU KAMA UAMINI.

    ReplyDelete
  10. Said Mwema, hayo yote yaloandikwa yangekuwa kweli yanafuatwa ajali zingepungua au kuisha kabisa.

    ZIJUE HAKI NA WAJIBU WAKO! HAPA VIPI KWA WAENDA KWA MIGUU? MAANA TUNAJUA HAKI YETU YAKUVUKA ZEBRA LAKINI MADEREVA WANATUUA NA KUTUWEKA VILEMA HII IMEKAAJE?

    TUNA WATOTO, WAZEE, VILEMA NA PIA WATU WA KAWAIDA INATUWIA VIGUMU KUVUKA BARABARA, MTU UNASALI SALA ZOTE KABLA YAKUVUKA LAKINI WAPI.

    HAYA UYAANDIKAYO HAKIKISHA YANAFUATWA ILI KUPUNGUZA AJALI.

    ReplyDelete
  11. Hii imvizuri sana, toka mwanzo nilijuwa utakuwa tofauti na waliopita kiongozi yoyote asiye kuwa mbunifu katika kuwasiliana na wananchi huyo hafai, endele kutembelea libeneke mzee utang'amua mengi sana na utajua nini kinaendelea kwa urahisi kabisa. Big Up Mkuu

    ReplyDelete
  12. Katika nchi iliyojaa watu wenye tamaa ya utajiri wa harakaharaka kuwa na sheria kama hizi, hasa ya kumruhusu Polisi kupokea faini ni mwanya mkubwa sana wa rushwa.

    Ushauri wangu.

    Nafikiri suala la kukusanya fine liwe chini ya TRA, Polisi iwe ina account maalum TRA ijukanayo kama
    "Road traffics misconducts fines and safety defficiencies penalties collections"

    Hii iwe inalipiwa TRA na mtuhumiwa na kisha kupewa risiti mbili, moja yake na moja anaiacha polisi kwa kumbukumbu

    Hili linawezekana tu kama fine itatozwa kwa gari bila kujali dereva ni nani, yaani mwenye gari ndiyo anakuwa respinsible na kulipia account hiyo badala ya kuangalia dereva. Hili linafanyika sana huku ulaya na gari likivunja sheria lipigwa picha kesho unaona barua toka polisi ya kukutaka ukalipie kiasi fulani.

    Kazi kubwa ya polisi iwe kukamata mhalifu, kurekodi namba ya gari na kumtaka dereva asaini kisha ndani ya siku saba awe amepeleka risiti ya TRA kwa record.

    Yaani ichukuliwe kuwa kila gari katika daftari ya usajili wa gari ni sawa na account ya bank ya mwenye gari, ukipigwa fine account yako inawekewa negative na TRA.

    Hili lifanyike kwa kuwa na kitengo maalum cha computer Polisi na mtu anaingiza data kila siku zilizounganishwa na account yake TRA.

    Pili fine isiwe kubwa yaani kama elfu moja (Tshs 1,000) hivi kila ukikamatwa na haijalisi umekamatwa saa ngapi na lini, ili mradi upo barabarani na kosa basi polisi wanaweza kukuandikia hata mara mia kwa siku kama hujarekebisha kosa.

    Hili litapunguza rushwa na kuwafanya wenye magari kuwa makini kwani akikamatwa mara moja itabidi akarekebishe ili asikamtwe tena baadaye.

    ReplyDelete
  13. Nadhani siyo good IDEA kuwapa CASH POLICE wa barabarani kwani inavutia sana ulaji wa RUSHWA, Akikwambia umpe elf kumi au ukalipe elfu 20 serikalini ofcourse utatoa nusu hasara, DISCOUNT IS ALWAYZ GOOD.
    Sasa utakuta kwamba SERIKALI NDO INAYOPOTEZA PESA TENA NYINGI SANA. Siamini kwamba serikali haiwezi kutafutia ufumbuzi suala kama hili.
    Jaribuni kuweka (Kwanza) sehemu za kulipia ziwe nyingi na HURU kama Posta, Police,Iwe Police station yeyote(na wala isitegemee kamanda kwani hiyo ni pesa ya police wa mkoa na wala si vinginevyo),malipo yawe kwa njia tofauti kama Cash,credit/debit card na hata checki. PILI watu wapewe muda wa kulipa siyo papo kwa papo(wapewe 7days up to one month) MUSIWAWEKEE UGUMU KTK KULIPA ILA WAWEKEENI UGUMU WALE WASIOTAKA KULIPA.MSIWAKOMOE ETI KWA VILE WANAMAGARI, KUWA NA GARI HAIMAANISHI KWAMBA NI UTAJIRI AU KUWA NA PESA ZA KULIPA FAINI. MAAMUZI YETU YAZINGATIE UPENDO NA USALAMA.
    thanx
    mdau

    ReplyDelete
  14. Yaani na wish Tanzania ingekuwa na viongozi wabunifu kama Said Mwema! Tumejaza Mawaziri, Makatibu wakuu na hata wakurugenzi 'YALEYALE" YAANI UBUNIFI ZERO KABISA!! TUTAENDELEAJE??!!!JK ANGALIA WATENDAJI WABUNIFU UWAREJESHE KAZINI 2ND PHASE HAO WANAOFANYIA KAZI MAZOEA PIGA CHINI!!!!

    ReplyDelete
  15. Ngugu Yetu IGP Saidi Mwema, kwanza kabisa napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa kazi nzuri uifanyayo, kwa kweli thamani ya jeshi letu adhim inaaza kurudi, japo kuna baadhi ya maaskari bado wanakungusha. kwa mfano pale darajani malalakua karibu na makao makuu ya JWTZ, kwa kweli ni aibu jamaa ( maaskari ) wamegeuza mardi siku za wikendi na usiku kama saa mbili na kuendelea, jamaa wanasanya pesa kama biashara flani hivi, gari zenye number za chasiss yaani amabazo bado kusajiiwa jamaaa wanapiga bao na kudaka kidogodogo, na hata wenye gari zenye taa moja au insuarance imeesha pale ni pesa tu,kuanzia elfu mbili mpaka kumi yaani inatengemea na kuchachawa kwako, mkwala ni uleule unatajiwa makosa kibao ukijumlisha inafika kama laki hivi, alafu anakuuliza twende kituoni ukalipe??? au ulete buku tano, wewe mwenyewe na uzalendo wako dhaifu unabidi utoe kitu kidogo yaishe, kwa kweli hali ndo hiyo kama huamini mzee chukua gari isio sajiliwa alafu pita pale uonne. wanavyofanya vijana wako, japo kutoa na kuokea yote ni kosa, kwa kifupi pale kunatoke makosa yote mawili. Kazi kwako mheshimiwa. Ila hata hivyo tumetyoka mbali sana hongera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...