Waziri wa Afrika Mashariki Dkt. Diodorus Kamala (aliyevaa koti yeupe) akiangalia power cable ambayo inatumika katika shughuli za kuingiza umeme mkubwa viwandani wakati alipotembelea kiwanda cha East African Cable kilichopo jijini Dar huku Charles Ngachwelwa Meneja ubora wa Kiwanda akimuangalia .Waziri Dkt. Kamala alitembelea kiwanda hicho leo kwa lengo la kuona bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ili aweze kuzitangaza kwa wanachama wa Afrika Mashariki
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI imetoa changamoto kwa wenye viwanda kutoa taarifa za wanaouza na kutegeneza bidhaa feki ili iweze kuchukukua hatua, huku ikisisitiza kwamba utoaji wa elimu ndio dawa ya kupambana na tatizo hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala wakati alipotembelea kiwanda cha East African Cables Tanzania Limited.
Alisema ziara hiyo ni ya kwanza kuifanya katika kiwanda hicho kwa lengo la kujifunza kinazalisha bidhaa zipi, ambazo ataweza kuzitangza katika nchi uwanachama, pia ana mpango wakuvitembelea viwanda vyote nchini. “ili kuweza kukabiliana na na tatizo la nyumba kuugua kutokana na utumiaji wa nyaya zisizona ubora ninantoa changamoto kwa wenye viwanda kutoa taarifa za watu wanaouza na kutengeneza bidhaa feki ili serikali iweze kuchukua hatua.
“Hatuwezi kukaa kimnya kwani bidhaa feki zinatuulia viwanda na ajira. Dawa ya kupambana na bidhaa zisizo na ubora ni utoaji wa elimu kwa umma ili wananchi waweze kuzielewa na kuzitofautisha,” alisema Waziri Kamala.
Waziri Kamala alisema wizara husika na wenye viwanda wakikaa pamoja na kuweka mikakati ya utoaji wa elimu hiyo ili kuweza kuondoa tatizo hilo si kuachia kwa taasisi zinazohusika.
Alisema Tanzania uwanchama wa Jumuia ya Afrika Mashariki inaongoza kwa kuuza bidhaa zaidi kuliko nchi za Kenya,Uganda,Rwanda na Burundi,hivyo katika kipindi cha mwaka 2007/2008 imeuuza bidhaa dola za Marekani milioni 272 na kununua bidhaa za dola za Marekani milioni 201.
Waziri Kamala alisema zamani Tanzania ilikuwa ikiuuza bidhaa za kilimo zaidi lakini sasa za viwanda ndizo zinauzwa zaidi kwa asilimia 25 ni chumvi wakati mafuta ya kula ni asilimia 12.
Alisema ujumbe wa wafanyabiashara wa Tanzania unatarajia kutembelea nchi za Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda, Novemba 22 hadi 30 mwaka huu ili kuangalia sehemuza kuwekeza na kuzishawishi nazo nije kuwekeza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Muriithi Ndegwa alisema wameweza kuongeza mapato ya Serikali kutoka sh.milioni 62 hadi kufikia sh, bilioni 1.5 katika kipindi cha nusu ya mwaka huu.
Pia kuongeza Kodi ya Ongezeko la Thamani(VAT) kutoka sh. milioni 766 mwaka 2001 mpaka sh.bilioni mbili katika kipindi cha nusu ya mwaka huu.
Alisema changamoto inaikabili kiwanda hicho ni kuwepo kwa watu wanauuza na kutengeneza nyaya feki zilizochini ya kiwango au kuchanganya mali ghafi ya copper na Aliminiam na kuuza bidhaa hizo bila risiti.
Ndegwa aliitaja changamoto nyingine ni nchi zinazotoa ruzuku zinafanya bidhaa zao kuuza kwa bei ndogo. Akizungumzia suala hilo Waziri Kamala alisema Serikali italingalia tatizo hilo.
Najua John mashaka anatabasamu kweli, kwani yeye ndo anapigaga kelele kuhusu bidhaa za kichina feki
ReplyDeleteMimi kinachoniuzi hawa wanasiasa ni kelele tu juu ya hizi bidhaa feki, lakini wala hawachukui hatua yeyote!
ReplyDeleteSasa nani adhibiti? hizo mamlaka za kudhibiti ziko chini ya nani? sisi wananchi au wao mawaziri?
KABLA YA BWANA YESU WA UCHUMI KUSHUKA DUNIANI(CHINA) NANI ANGEWEZA KUNUNUA HATA CD YA MUSIC. CD ZIKO TANGU MIAKA YA 1980 LAKINI TZ ZIMEFIKA 1995 LABDA. SASA HAO WANAOTENGENEZA BIDHAA FEKI WANA UBUNIFU WA HALI YA JUU KUFIKIA KWAMBA UNAWEZA UKASEMA NI KITU HALISI. TUKIPATA BAHATI YA KUWA NA WABONGO WENYE UWEZO HUO TUWAPE MTAJI TUWAJENGEE VIWANDA NA TUINGIZE BIDHAA ZAO KATIKA USHINDANI MWA SOKO. HIKI NDIO CHAZO CHA KUWASAIDIA WALALAHOI KWA BIDHAA NAFUU.
ReplyDelete