The African Stars band wana Twanga Pepeta inarejea tena kupamba usiku wa mwafrika katika kiota cha maraha cha Club Billicanas kuanzia Jumatano ijayo tarehe 23 Septemba, 2009 na kila Jumatano kuanzia hapo. Wapenzi wengi wa bendi hii wanasuuzika na staili yao inayotamba sasa ya 'Sugua Kisigino' pamoja na vibao vipya na vya zamani vinavyorukwa hasa na safu ya unenguaji ya wadada na wakaka chini ya mkongwe super zembwela.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hiyo ni habari njema. Tulikuwa tunawasubiri kwa hamu Twangapepeta maeneo tulivu yenye mandhari kama hayo ya Bils, manake sisi wengine sehemu kama za Mango Gardens na makumbusho zimekaa kulia kidogo japokuwa bendi tumekuwa tukiitamani

    ReplyDelete
  2. da' Asha hongera kwa kukuza mziki wa kibongo, pili tuletee watoto huku Manchester tunatafuta wake wengi tumefuria tuna kazi zuri sana lakini atuna wake tusaidie kwa hilo, Manchester (UK)

    ReplyDelete
  3. mdau unajua maana ya kufulia kweli?. Kama una kazi nzuri huko Manchester si ndiyo umeukata tena. Au umefulia kwa uhanga wa
    mademu?

    ReplyDelete
  4. Mango yetu huwa tunalipa elfu tano kiingilio. Huko Bilicana ndiyo itakuwa maelfu mangapi sasa ili tujiandae, tusije rudishiwa mlangoni

    ReplyDelete
  5. Duuh Mjomba Michu umechapia Mimi naona ni Super Nyamwela sio Super Zembwela.
    Mdau
    Kisiju Pwani

    ReplyDelete
  6. Hivi Aisha Madinda amerudia kuwa fit tena kumbe na shape ya kuvutia naona.Lazima nikamdeku kimwana huyu

    ReplyDelete
  7. jamaa ndugu zangu mie nimeishi huko Man kwa miaka mitatu nilikiuwa nasoma Manchester kwa sasa nimerudi Bongo ni kweri watu wa huko wanawake waho ni wazee ndio wanaowa na wengine wanasimama babarani dada zetu, mdau kufuria ni kuaribu si lazima umeishiwa pesa, wenu Gitu Mbenzi juu.

    ReplyDelete
  8. Unataka Waluketee stage player kama mke, and you are telling it to those who operate the band or group. Isnt that as much as sexual slavery??? are you that desperate to find a pussy, that you are requesting people to find one for you??? Leave the ladies alone they are just trying to make a living and not being exposed as sex objects or to those horny who are not men enough to find their own lady love.
    Waheshimuni wa dada wa watu, wapo kazini hao. The last time I checked, atakayekuletea mwanamke on the terms I undestand you just said, kwa sheria za TZ ni kosa na unweza kwenda jela. Kama untaka rudi bongo, nenda kamtafute mwenyewe.
    Kwanza huyo mke jiulize atakuwa amefuata nini. Halafu wakiwakimbia, mnaanza kuwaponda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...