kufuatia maombi ya wadau kibao toka kila pembe ya dunia, globu ya jamii imepiga mbizi na kuibuka na ile sehemu inayotafutwa kwa udi na uvumba na kila mtu ambaye hakubahatika kuiona ya wakati steven kanumba alipokuwa anahojiwa kwenye chumba cha faragha ya Big Brother Africa IV.

Kunradhi clip hii imerekodiwa kwa kamera ya simu, tena nyumbani,kwaliti sio nzuri kiiivyo ila maongezi yanasikika vyema tu, inagwa kuna sauti za wadau.

--------------------------------------

Mithupu ebu wape wadau hii link ili waone kuwa kiingrish siyo lazima ile kwa saaana. Usitoe mail yangu. Hata ancelotti mwenyewe kiingereza ndo amejifunza uzeeni leo hii.

http://www.youtube.com/watch?v=r7FUBduIaOw&feature=related

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 69 mpaka sasa

  1. KABLA SIJAIFUNGUA NAKUPA SALUTI MWANA NIMEKUKUBALI MICHUZI...

    ReplyDelete
  2. Jamani mwacheni Kanumba nyie mnaotuma hizi ndio Wenye chuki wenyewe. Kanumba kama unasoma mie, nipo na wewe Watu wana wivu tu. wanapenda kuwa nafasi yako hawajapata. Miss World tunaona wangapi wanaenda hawaongei Kiengereza na wanashinda na Kupendwa? Kanumba number 1. Pazi.

    Tunajuwa kwamba vengine hajaelewa ila USA mbona wengi wamezaliwa na Muda mwengine hawaelewi wanachoambiwa. Amekuaibisha hakuna alichoaibisha. GAE TANO alienda Big Brother UNITED KINGDOM walimpenda na English yake haikuwa nzuri muda mwengine alikuwa hawaelewi Waengereza sababu wengine wana Scouser Accent ila wamependana hawajapondana Yule jamaa wa Uganda. Pazi.

    ReplyDelete
  3. Na wewe Uliyoweka Usijifanye wewe lugha inapanda sasa Kwaliti ndio nini? mwacheni kanumba. Kanumba usijali tunakupenda.

    ReplyDelete
  4. Nyinyi Sasa ndio mtaiaibisha Taifa yaandikwa Nje huko Sijui mkoje Vichwa kama Kokwa za ubuyu.

    ReplyDelete
  5. Kha!!! ametaja i like zaidi ya mara 21! Kanumba hamna ubishi inabidi uende shule baba Holywood au Bollywood hawaendi hivihivi mzee! unatakiwa uteme yai! sio kumung'unya utomvu namna hiyo sira ikiwa imekunjamana kisa maswali relax baba!

    ReplyDelete
  6. hapo sasa mm sina chakumtetea ingawa ni shabiki wangu sana huyu jamaa

    ReplyDelete
  7. Ufisadi mpaka Big Brother! hii kweli Bongo! Takururu inabidi wapite office za Mnet Tanzania kuna harufu ya fweza watu walidakishwa! Kuanzia mwaka kwesho Mnet mnatakiwa mfanye Interviews kwa uwazi la sivyo nitaacha kununua kadi zenu! huku kuliabisha taifa!

    ReplyDelete
  8. this is too much..the guy cant understand english and thats that..enough already..move on people. michuzi whats next..

    ReplyDelete
  9. The Problem with US tanzanian's
    Ulimbukeni,majungu na mambo yasiyo na maendeleo tumeyapa kipaumbele

    Suala muhimu ni kujadili mambo yanayojenga na yasiyojenga
    kanumba kama kioo cha jamii hajakosea
    lugha yake imekuwa ya kueleweka isipokuwa ni wahuni wachache ndio wanaleta upinzani na unafiki

    Umuhimu tuwe na positive views na maono endelevu..

    KANUMBA STEVEN dont feel ashamed with your speech...unaeleweka na kama unahisi pasipo na uelewa basi huna budi ya kujiendeleza lakini si kwa kusudi la kuwafurahisha watu

    hapa wengi wanaoweka comments ni waosha vinywa wengi maisha yamewashinda...
    Uingereza- 90%(wengi maisha yashawashida na ni wapiga boksi)
    Us & Canada- 5%(wasomi)
    Malaysia,China,India- 2%(ufuska)
    Rest of Africa - 2% hawana Internet hivyo wengi wanakosa muda wa kutembelea michuzi)

    Prof. Mwaigobeko
    University of East London
    woolwich Arsenal

    ReplyDelete
  10. Plzzzzz naomba blog ya jamii ilimlipie ada ya inglish kozi kabla mambo hajaharibika, yaani hapa kama kichaa ndio kinaanza bora tuanze kumtibu. hawa jamaa kwajita majina makubwa etii Kanumba THE GREAT....

    najitahidi kutafuta pedeshee wa kumlipia kozi aanze mchango wa daftari na pen.

    ReplyDelete
  11. Mimi nasimama kidedea kumhamasisha huyu Kanumba na hao wengine akina Teddy Kalonga waende shule wakajifunze lugha na pia wajifunze skills nyingine mbalimbali. Lugha nikimaanisha kusoma na kuandika. Ni muhimu sana katika dunia ya leo kwa mtu kuweza kujieleza kwa lugha kama kiingereza. Mimi sina shida wala sina hila ya kumuonea wivu huyo Kanumba kama watu wengine ambavyo wanapenda kufikiri( kwamba ukimponda mtu, unamuonea donge!)hapana, mimi nasisitiza aende shule kwa sababu hii kwa kweli ni AIBU kwa MISINGI YA ELIMU YA TANZANIA.Kama kiingereza kinakushinda, nadhani angeomba ushauri na ingekuwa busara kwake yeye kuomba afanyiwe hiyo interview kwa kiswahili. I am sure wangeweza kufanya "SUBTITLES" kwenye kideo kutafsiri hicho kiswahili kwenda kiingereza. Pole sana Bw. Kanumba. Nakuonea huruma sana na tena uchukue mawazo na wosia wa watu kwa msisitizo sana. NENDA KAJIENDELEZE. WEWE NI MFANO MZURI WA WATU WASIOWEKA ELIMU KIPAUMBELE. EVENTUALLY IT IS CATCHING UP ON YOU. USITUAIBISHE TENA. GO TO SCHOOL. Samahani kama roho imekuuma lakini, sikubali kukaa kimya na kuachia uwaaibishe watanzania wenzio walioelimika, wote tubaki tunaonekana mazoba kwa sababu ya mtu mmoja. Tena uwe na busara next time kama huwezi kufanya kitu, ni vema kukubali udhaifu wako na kusema, mimi kwa sasa sina uwezo huu na nitahitaji muda kujifunza na kujiandaa. Na nyie watu wa MNET, kwanini hamfanyi entry level English qualifications kwenye mambo kama hayo. Celebrities kina Jokate mmewaacha mnaenda kumchukua huyu kweli akaaibishe TZ nzima. What the hell?? Standards zenu watanzania ziko wapi? I am very disappointed, embarrassed, ashamed, sad that this had to turn out the way it did.Ngoja niishie hapa. Michuzi, asante sana kwa hichi kipisi cha video, na wewe michuzi tafadhali usitetee udhaifu, kwa kweli hautakuwa unamsaidia huyu kijana hata kidogo. Lazima aambiwe ukweli na ukweli wa mambo ni kwamba this does not look good especially if he is representing the Country. Msimtetee kabisa, he needs to be told, part of learning is accepting your weakness and taking time to learn how to get better. Nimemaliza!

    ReplyDelete
  12. inabidi bwana kanumba ujifunze kusikiliza na kuelewa maswali ya kiingereza first time.

    si mbaya kuchukua a moment kujibu swali kwani inaonesha unafikiria jibu sahihi.

    usitafakari na kutranslate kiswahili into english,ninamaanisha mtiririko wa maneno na tone ya sauti.

    kama upo katika public eye na kama ulivyosema unairepresent Tanzania,lazima uiprotray katika kiwango ambacho kinaleta mtazamo mzuri na sio kudhalilika.

    nimeshindwa kusikiliza mpaka mwisho kwani najisikia naanguka pia nipo na watu hapa wa mataifa mbalimbali hapa najisikia down kwani nchi yetu bado iko nyuma sana kimaendeleo na perception ya watu huku hutafurahi kusikia.

    kujua kiingereza ni muhimu kwani ni lugha iliyoendelea,inatumika ulimwenguni kote,pia inaenrich knowledge.na kwa fani yako mzee,ndipo utaweza kuinfluence african audience na kukua commercially.

    naipenda nchi yangu na naitakia maendeleo pia kwa wawakilishi kama wewe juu ya social issues,lazima uraise your standard.

    mwingereza asingekuuliza several times kama bigbrother alivyokuuliza repetatively,yani angefanya bidii amalize mahojiano basi tu akuache.

    ni hayo tu mzee,usikasirike,bali kwa ushauri tuu naomba uniprove wrong next time uhojiwe kwa kiingereza kwani utakuwa umefanyia kazi maoni ya watu.

    ReplyDelete
  13. nilijaribu kukutetea katika ile clip ya Michuzi, lakini kwa hapa basi, nibatilisha utetezi wangu wote na kukutaka uangalie udhaifu ulionao. Pamoja na kwamba una kipaji lakini elimu ndugu yangu ni muhimu na ndiyo iliyokutenganisha na ukweli katika ile interview. Maswali yote pamoja na kuongea kiingereza cha kubabaisha, lakini pia hukuwa unajibu maswali kikamilifu, umeonesha kupata taabu sana kukusanya fahamu zako na kujua swali ni nini? Hii ya kujua swali ni nini haihusiani kabisa na kuongea kiingereza kibovu, inaonesha unatatizo katika kuelewa mambo kwa ujumla na ndiyo maana ulishindwa KABISA kujibu swali la mwisho kwa hukujua BBA ameongea nini na pamoja na kurudia swali mara kadhaa aligundua kuwa huna unachokielewa.
    AIBU TUPU!!!

    ReplyDelete
  14. Ahsante sana Bro Michu kwa kuweka japo haka ka-clip, sina la kusema zaidi ya fedheha au zahamaimetukuta watanzania mbele ya macho ya dunia.
    Huyu bwana anaweza akatumiwa kama kielelezo cha kuonesha kuwa huyu ndiyo the best Mbongo.

    ReplyDelete
  15. hivi nyie mnaomsema kanumba hajuwi kiingereza, ina maana mtoto wa miaka mitano wa kiingereza ana akili kuliko maprofesa wetu?

    ReplyDelete
  16. Kwanza kaka michu nakupa hongera sana kwa kuweza fatilia hayo mahojiano ya huyu celb wetu. Ukweli ni kwamba Watanzania tumejaaaliwa majungu fitina na midomo na chuki binafsi. Kwanza ingekuwa mi ni Kanumba ningefurahia sana manake hivyo ndo unapanda chati. Otherwise usidanganyike oh kiswahili ndo lugha yetu or sijui nini, English Lugha muhimu kuna maali ukishindwa kujieleza utakosa dili hivi hivi. kunawatu hapo wanakupa moyo oh tunakupenda oh, wao wanaongea lugha zote mbili vizuri wanakutia tu moyo. kajiendeleze kaka na pia jua wewe ni celeb na watu wataongea sana ukikosea.

    ReplyDelete
  17. Big up Kanumba!Never mind wana wivu hao.....eti hajui kingereza!!!what!!unafikiri ni rahisi kuwa interviewed na mtu ambae humuoni??especially kama mtu hujazoea mambo ya slang?????

    Jamani hebu tujifunze kuwapa masuperstar wetu moyo maana thats not our monther toungue especially we all know shule alizopita kanumba wetu...sasa kwanini tusimpongeze???

    Msipende kukosoa tu wenzenu.....Kanumba unaweza, what you need is more practice but you all most there!

    Big up!

    Mdau from Kambarage!

    ReplyDelete
  18. kaka KaNUMBA wewe endelea mambo yako achana na hao mahasidi kwani wao wana juu kiingishi.maana yale maswali ni magumu pia huko bongo lugha kubwa ni kiswahili.huna watu wa kuongea nao kiingilishi mara kwa mara ili uwe na uzoefu.ukijifanya sana unaongea kiingilishi huko bongo watasema unaringa hawana jema hataki kidogo.wewe nenda mbele jifunze kutokana na makosa.waache wafungue vinywa vyao watachoka wanachuki binafsi hawana lolote la kukusaidia zaidi ya kukutisha tamaa.

    ReplyDelete
  19. I don't know where to start but Kanumba please please do something about your LINGO. confidence unayo ila vaery simple plain english inakupiga chenga. Mimi sio mtaalam wa Lingo but maswali uliyoulizwa yalikua straight foward.
    ushauri wa bure usikate tamaa take this as a learning opportunity.ucelebrity wa kibongo usikuvimbishe kichwa.you have a long way to go bro
    God bless Tz and it's people

    ReplyDelete
  20. MSITUZUGE TOENI UJINGA BWANA, HAKA KACLIP SIO HII TU, IPO NYINGINE SISI HUKU INDIA TUTAITOA YOTE TUNAYO TOKA SATELITE KWA HIYO MSITUZUGE NA HICHO KITIVII AMBACHO HATA HAKISIKIKI VIZURI, THE GUY WAS AN EMBARASSMENT PERIOD, HATA MKITUTOLEA FINGER PRINTS ZAKE HAZITAONDOA THE FACT KWAMBA KANUMBA NI MWEUPE, FANYENI YOTE HE NEEDS TO GET HIMSELF BACK TO SCHOOL KWA SABABU KUANZIA CLIPS TULIZOONA SISI NA HIYO BLOG YAKE ALIYOIFUNGA NI WAZI HE IS SO IGNORANT NA MAMBO MENGI, ACHENI KUFAGILIA UZEMBE NA UVIVU, HATUTAFIKA WATANZANIA, WOTE MPAKA WALIOSHIRIKI KUMPELEKA KANUMBA HILI LIWE FUNDISHO, HATUTAKI TENA MJADALA WA KUMTETEA HAPA, KITAKACHOMKOMBOA NI KURUDI SHULE NA KUJIENDELEZA HASA KWENYE LUGHA ZA KIMATAIFA, HE NEEDS ENGLISH JAMAA NI MCHOVU PERIOD.

    ReplyDelete
  21. Huu ni utoto sasa, Kanumba nilitegemea angetoa interview na waandishi wa habari ili ajielezee na kumaliza hizi shutuma na longolongo, angetumia nafasi hiyo kuwashukuru watu kwa maoni yao na kukubali kuwa atayafanyia kazi, hiyo ndio kazi ya usupastaa,msukuma vipi mjomba, wote kina multichoice na yeye wangeliona hili suala kama challenge sio kutuwekea vijiclip ambavyo sivyo halafu mnatusokomezea kooni tumeze tu, kiburi chake hakitamfikisha popote na hao wapambe wake wanaompa kichwa badala ya kumshauri watamcheka kesho tena akienda kutuwakilisha. Grow up Kanumba!!

    ReplyDelete
  22. ANAJIFANYA HASIKII KUMBE HAELEWI MASWALI, HOVYO KABISA HUYU, HUYO NDIO CELEBRITY WETU BONGO, KWELI TUMEKWISHA.

    ReplyDelete
  23. We,Prof Mwaigobeko,Umejishushia heshima sana kutoa maoni yako mchanganyiko na vichaa.Jiulize mpo ma-prof wangapi mnaochangia ujinga kwenye glob hii.Hawa wabeba box wamesafiri na wanaishi nje kivyao,hawajaomba msaada serikalini,ni wao na familia zao.Kama hawajasoma ama ni mafuska wewe kipi kinachokuwasha?Utaongea nini siku utakapogundua mwanao wa kiume amekuwa gay.Nilidhani ungekuwa msaada mkubwa katika mjadala huu nini kifanyike ili kupunguza matatizo miongoni mwa watanzania.Kama wewe uliyesoma kwa kusomeshwa unakuwa mstari wa mbele kubeza wanaojisomesha kwa jasho lao basi nchi yetu bado haijaingia karne ya 21.Tumia elimu yako kwa kuleta maendeleo na kuondoa umaskini Tanzania ili utakapokufa kizazi kijacho kijifunze kutokana na japo kile kidogo utakachokiacha duniani.
    Toto tundu-Upper Marlboro.

    ReplyDelete
  24. hapo wadau wa north america hatuna ubishi!! jamaa yaani angelichuna tuu baada ya kuharibu, yaani wazalendo ninoma juu ya noma!
    representative!

    ReplyDelete
  25. OH MY GOD!JOB IS COTTON FIRE.

    ReplyDelete
  26. MImi nakubaliana na msomi mwenzangu Prof Mwaigobeko. Mimi nimesoma bongo na hapa UK. Wanaochonga sana ni wabongo wenzetu wa hapa UK, ambao wengi wao ni form IV na VI faluires ila shauri ya kukaa sana huKu nakubeba mabox wameona kama wamefika kwa english. Ukweli Kanumba na English yake ni bora mara tatu kuliko wengi wao. They can try to talk queen english but kichwani pumba tupu. Na ndiyo maana wanaacha ku adress issues nakupoteza muda talking negative about others`

    ReplyDelete
  27. Dah nilikuwa naangalia kwenye SKY News sasa hivi jinsi Coach ANCELLOTI wa Chelsea anvyoongelea match ya leo ya Chelsea. Jamani mbona Kanumba wetu anaongea english iliyonyooka kuliko huyu mtalianao na wala waingereza wenyewe hawamshangai. Iweje nyie wa bongo na english yenu ya kikabila na kigugumizi mum judge Kanumba hajui wakati na imani waingereza wenyewe wakimsikia wataona kawaida tuu. Acheni hizo

    ReplyDelete
  28. MDAU JUU UMENIKUMBUSHA KUHUSU GAITANO WA BIG BROTER AFRICA 1. Ni kweli Gaitano alivyoenda Big brother UK alisema kuna wakti alikuwa hawaelewi kabisa waingereza na slang zao, ikabidi wakati mwingine anaitika mmmh!, mmmh, angalau topic ipite. So Kanumba kuuliza uliza kurudiwa kwa swali ni jambo la kawaida ili aweze kuelewa. Na pale alipoona hajaelewa au hana jibu lililonyooka ilikuwa ni sawa kufunika kombe mwana haramu apite. Wengi wetu hafanya hivyo hivyo

    ReplyDelete
  29. Basiiii...Kanumba kasikia teyari...thats too much for him.

    Si vizuri kumsema sana, hana kosa kabisa. He has been invited, did people wanted him to turn down that invitation?

    Kanumba endelea kufanya kazi yako, Mungu atakusaidia. Mimi niliona makosa ya lugha, but lugha wengi hukosea esp ukiwa mbele ya watu.
    soma tu na tafuta editor wa website zako, movie zako pia.
    Ur smart and hawa watu hawatakushusha.

    Watu wa ajabu sana...Michael Jackson alipokuwepo alikuwa hana umuhimu, kaondoka ndio wanamuona mtu.
    R . Kelly sasa wanamuona si mtu, akiukata lazma itabadilika.
    Banadamu tuna akili za ajabu, bt kama ulivyosema Kanumba...siku umekufa watu ndio wanaanza kukutukuza...fitina mkubwa.

    kuna critisms za positive na nyingine za kukejeli. take it as a man, take it as a challenge. English si big deal sana, naona haikufai ktk maswala ya kuandika.

    ReplyDelete
  30. jack chain movie actor yuko hollywood au yuko wapi? naomba unisaidie Anonymous: Tarehe Sat Sep 12, 02:53:00 AM,

    ReplyDelete
  31. mimi nina Degree yangu ya University ya hapa france nina kazi kubwa TRA ukiniita kwenye Innterview, nachanganyikiwa na panic.
    ila jamani nauliza Jack chain yuko Hollywood au .... yupo Temeke?

    ReplyDelete
  32. Ohhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh the guy tried.Si lazima sana uongee kiingereza kizuri wakati hujazaliwa nacho.Je wazungu tunachekwa kuongea kiswahili ambacho si kizuri????Mwacheni bwana.Acheni majungu wabongo wachache wenye wivu.Kumbukeni Kanumba alikuja Holywood,na pia alikuwa London majuzi,kufikia u hizo hatua ni jambo lakujisifu.Wengine wanapiga kelele hata ndege hawajawahi panda,hata hawajui dunia inaendaje,je simaajabu sasa!!!lol.Anyway,K'numba,mwizukulu,jitahidi kaka utawashinda na utayashinda majalibu kufikia kilele cha mafanikio
    Mdauuu

    ReplyDelete
  33. AY NAE HUYOOOOOOOOOOO KALA NDONDO LA KUTUMBUIZA BBR,C JUI WAOSHA VINYWA MMEJIANDAA VP KUALIBU.

    ReplyDelete
  34. Kuna kina Ally Retumlla the young design,Lady Jadee - Musician,Nancy Sumari -Miss World Africa nadhani Furaha wa DSTV kam ulitaka Celevrity wa TZ hao hapo wangeenda kuwakilisha but not Kanumba koz Exposure ilikuwa bado haoni kina Teddy Kalonga wanaenda Xkul koz wanataka kujua jamani UMETUAIBISHA Ona hiyo Clip kanumba ujue ulichokosea sio unalalalama kam unaona Watanzania ni Wana WIvu ila tunataka UELIMIKA SAWA mbona Movie zako ni KIngereza

    ReplyDelete
  35. To Annon Sat Sep 12,9:44:00 AM:
    Yes, he should have rejected the invitation kama alikuwa anajua uwezo wake na kama walimueleza kuwa atakuwa interviewed kwa kiingereza, na kwa kuwa alikuwa anajua uwezo wake ni mdogo ingempasa kuweka request aseme, je kuna uwezekano wowote kuwa niwe interviewed in Kiswahili? Hapo alikubali invitation na kuchukua challenge kubwa kuliko uwezo wake. Kwa kweli kuna umuhimu sana wa kujijua, kama nilivyosema hapo awali, he needed to show responsibility. Na kuwa responsible some times means having to say NO to certain things! yeye aah! kapata dili na ticket ya ndege basi kaona ngoja nizame bondeni, ili nipate props! Hakuonyesha busara na kajiaibisha. Tena kama kuna watu wengine huko wana dili za kurepresent taifa, tunawasihi mjiandae.kama practice inaonekana kuwashinda, kaeni nyumbani!!
    -mdada

    ReplyDelete
  36. WEWE UNAEMLINGANISHA KOCHA WA CHELSEA NA KANUMBA HAZIKUTOSHI!!!
    kANUMBA ANTOKEA COMMON WEALTH COUNTRY WAKATI KOCHA WA CHELSEA ANATOKEA ITALY AMBAYO SIO COMMON WEALTH COUNTRY.YEYE NI KAMA MTOTO ALIYEZALIWA JANA.LAKINI ANAJITAHIDI KULIKO HUYU KICHECHE AMBAYE ALIKUWA MSTARI WA MBELE KUMDHALILISHA WEMA SEPETU!!

    ReplyDelete
  37. BORA WEMA SEPETU ULIENDA KWA JUMBE.
    HUO MUDA ULIOKUWA UNAUTUMIA KUMSHITAKI WEMA MAHAKAMANI KAMA UNGEUTUMIA KWA ENGLISH CLASSES HAYA YOTE YASINGEKUKUTA! YAANI MWENDO WA KU SMILE NA I LIKE TU,ZE A GOOD!

    ReplyDelete
  38. KWANZA NINGEOMBA WATU WOOOOOOOOOOOOTE WANAOMPONDA KANUMBA WAWEKE COMMENT KWA KINGEREZA, PILI TANZANIA TUNATABIA MOJA MNAFIKIRI UKIMPONDA MTU MWINGINE WEWE UNAONEKANA UNAJUA, KUMBE UNAJIDANGANYA MWENYEWE, KABLA HUJAMPONDA MTU, ANGALIA WHAT DO HAVE? UNAMPONDA MTU HAJUI KINGEREZA, WEWE UNAJUA? NA UNAJUA, UNAJUA KIPI, CHA KUOMBEA MAJI, OR ARE GOOD ENOUGH KUREPRESENT NCHI YAKO, SIELEWI KWANINI TZ TUNAPONDANA SISI KWASISI, ETI KANUMBA ALITOA MFANO WA ANTONIO BENDERA NA KOFI OLOMIDE, WATU WAKASEMA ANAJICOMPARE NAO, KWANI WAO SI WATU TU, THE DIFFERENCE NI KWAMBA WAO WANAJULIKANA ZAIDI YA KANUMBA, NA HUYO DADA ALIYESEMA HAPO KWENYE CLIP KUWA KANUMBA AMEENDA VIPI WAKATI HAJUI KIZUNGU, TUNAOMBA AONGEE LIVE TUMUONE, WATANZANIA WENGI SISI NI WASHAMBA, WAJINGA, HATUNA LOLOTE NDO MAANA TUNAONGEA SANA ILI TUJISKIE VIZURI, kANUMBA BIG UP BROTHER, U R LIVING UR DREAM, U R LIVING LARGE, HAO WANAOKUPONDA SI LOLOTE SO CHOCHOTE, WATAKUFA HAWAJAFIKA HATA UKO SA, NA PROBABLY HAWAJAACHIVE ANYTHING KATIKA MAISHA YAO, WATU WANAJUA TZ TUNAONGEA KISWAHILI, SASA NALUMBANA NA LUGHA ZA WATU KWANINI? BALIDIKENI WATANZANIA MNATIA AIBU. KANUMBA LIVE UR LIFE, LIFE IS TOO SHORT, KUSIKILIZA HATERS, PEOPLE DONT HATE A PLAYER HATE THE GAME. FIKIRIENI KABLA HAMJAONGEA. BIG UP KANUMBA

    ReplyDelete
  39. NIMEFIKA "POINT" YA KUWADHARAU WOTE MNAOENDESHA MJADALA KUMZODOA KANUMBA KWA MADAI YA KUTUAIBISHA KWENYE BBA.

    Nauliza hivi, hapa nchini kuna mambo mangapi ambayo Viongozi wetu wa juu wametuaibisha na kufanya Taifa liwe katika hali ngumu na tumeshindwa kuwajadili na kuleta suluhisho badala yake tunamkomalia mtoto wa watu ambaye ndio kwaaanza anaibuka katika sanaa ya Tanzania? Hivi hamoni aibu shirika la reli kupewa wahindi na wanashindwa kuliendesha kiasi kwamba watanzania wanaohitaji treni sasa wanateseka kwa kutokuwa na usafiri huo? Viongozi walioingia mikataba ya kijinga na kuliletea taifa hasara kubwa je si hao ndio wanaotutia aibu kubwa? Hivi wangapi Tanzania wanakiingereza kizuri na hatujaona faida zao, Hivi Miss Tanzania Nasra kiingereza si yuko fit? Alikuwa wangapi Miss world je Ile si aibu? Je mlimzodoa kiasi cha Kanumba?

    Ok hata kama ni Ukweli Kanumba hakuongea vizuri lakini kueleweka alieleweka kwa kiasi, na interview sio maana yake ujibu maswali yote kwa ufasaha! For What? Kuna maksi? Mbona zile zilikuwa ni Opinions tu? Je unataka kumdhalilisha mtu kwa simply opinions? Acheni dharau jamani. Wakati wa Mkutano wa Sullivan kuna Waziri fulani (Sitamtaja) Alizungumza broken mpaka nikazima TV, huyo ni waziri Masters holder, sembuse Kanumba form Six. Watanzania tutabaki nyuma milele kwa chuki zisizo na msingi kwa kweli, na wote wanaomzodoa Kanumba mbona hawaandiki kwa Kiingereza tuone cha kwao kama kimenyoka.

    Nilitegemea sisi wote tumpe support mtu wetu kwanza ndipo tumshauri tunayoweza kumshauri. Hapa ni sawa na mgonjwa aliyepata UKIMWI huwezi kumshambulia kwa madai kwa nini ulikuwa hutumii CONDOM? Kuna utaratibu wa kumshauri mtu wa ili asikate tamaa. Kanumba ni kijana mdogo Kiumri na kiakili anahitaji kukuzwa, usidhani umaarufu wake unamfanya awe mkomavu kwenye kila kitu THAT IS NOT POSSIBLE huyu anahitaji msaada wa ushauri, lakini sio ushauri wa kimajungu. Tatizo la watanzania ROHO ZA KOROSHO zisizo na sababu.

    Hebu tujifunze kuheshimu kazi anayoifanya na tusikimbilie kulalamika tu bila utatuzi.

    bro Michuzi uwe unaweka Clip za Viongozi wetu wakizungumza kizungu ili kuweka usawa wa tatizo hili kama huna chuki na Kanumba, tafuta mahali fulani kiongozi anaongea au profesa au First Lady au yeyote mwenye jina kubwa na elimu kubwa tuone, maana Kanumba ni form six tu tena sio ST. Marys.

    Kanumba wewe ni kijana bado una nafasi ya kuendelea kukua kisanaa na hata lugha pia, mi naamini just time will tell usihangaike na pressure za wanablog fanya vile ulivyojipanga maishani mwako na nakutakia mafanikio zaidi, wanaolalamika mafanikio yao huyajui yanatokana na nini, tena ukute wengine wanaopiga boksi walipata huruma tu kwa sababu hawajui Kizungu, sasa ivi wame"interact" wanakijua kidogo tabu. Kanumba kadiri utakavyokuwa na interaction zaidi utakijua vizuri na Mungu atakuwa upande wako, usijikweze tafadhali.

    Mdau HSL Nginja. Netherlands

    ReplyDelete
  40. LoH!! Bwana Kanumba naomba ujitahidi kusoma vitabu mbali mbali ili uongeze uwezo na upeo wa kufikiri na kukuelewa mambo mbali mbali. hii itakusaidia kuweza kupambanua maswali mbalimbali utakayokuwa ukikumbana nayo kwenye interview kama hizi za BBA, maana naamini there is more to come!! Usiwe mbishi wala arrogant ukijifanya hutaki kukubaliana na ukweli kuwa ulichemka mbovu yani!! naungana na mdau mmoja hapo juu alishauri kwamba maoni haya yawe kama changamoto kwako na Multichoice waliokupeleka huko au hata kampuni nyingine zenye utaratibu wa kuchagua wawakilishi wa TZ nchi za nje!! wewe Kanumba umetuwakilisha sisi kama mambumbu tusioelewa tunachoulizwa ama tunachoongea! mi sikulaumu sana kwa kutoongea kwako kingereza cha kunyooka bali nakulaumu kwa kujibu maswali nje ya topic yani kinyume kabisaaaa na ulichoulizwa, sijui ulikuwa unawaza nini!! were you nervous?? you were supposed to concentrate na wala si kupeleka misifa yako ya huku bongo huko duniani!! mi nakupa fact kwamba ULICHEMKA, na ULITUBOA. Naomba nikupe ushauri: siku nyingine kama unaona swali hujalielewa vyema au jibu ulilokuwa nalo linakushinda kuliexpress jaribu kujibu kwa kifupi zaidi, usijibu kwa ureeeeeeeefu matokeo yake unaenda nje ya swali!! we ni kijana bado una muda wa kujirekebisha nenda kapige kozi ya kizungu na uwe unasoma vitabu, majarida mbalimbali na magazeti pia. ukiwa kama celebrity au mwana jamii kwa ujumla unatakiwa uwe na habari ya matukio yanayoendelea kila situ. Usione noma coz umejitahidi kwa kiwango chako mwana..ila fatilia sana ushauri wa watu ili Usije kutuaibisha tena siku nyingine. Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  41. Oyoooooooooooo, Kanumba u really made my day!! hahahaa!!

    ReplyDelete
  42. I LIKE IT, I LIKE IT, JOKING JOKING!!! HAHAHAAAAHAAAAAA UUUWIIII!! .Umejitahidi though.

    ReplyDelete
  43. IASEEEE KUMBE KANUMBA YUKO FITI KWA KINGEREZA!!! KANUMBA ANATATIZO MOJA TU...INAONEKANA HANA MAZOEA YA KUONGEA LUGHA HIYO MARA KWA MARA NDIO MAANA UWEZO WAKE WA KUSIKIA MATAMSHI YAKE VIZURI NI MDOGO!! LKN AKIPIGA MSASA KIDOGO TU AAAAAAH ATAKUA JUU....KANUMBA, UNATAKIWA KUFANYA MAZOEZI TU...SANA SANA KWAKUWA WEWE NI CELEBRITY BASI MIALIKO KAMA HIYO NI MINGI JENGA TABIA YA KUONGEA KIMOMBO MARA KWA MARA....UKO JUUU

    ReplyDelete
  44. This is tuu machiiii,ayi no endestend ingilishiiii wajamenii,,soorry

    ReplyDelete
  45. bado kidogo ila umejitahidi bwana!!

    ReplyDelete
  46. hata mumtee vipi huyo kanumba ni maimuna tuu huo ndo ukweli halisi ati kuna mdau mmoja anadai watoa mada woote waandike kiinglish ile iweje wakati anatakiwa ujumbe umfikie wewe unayemtetea kwa bidii huna lolote kawaida sana huna upeo kama huyo nunda yani kitu kinajieleza bado mnakuwa matomaso eboh! hapa watu wana hasira ni kwa nini huyu maimuna alienda south wakati lugha is no richabo?? mbona miaka yoote watu wanauchuna tuu hata ile movie yake ya this food is too much pilipili mbona watu tuliminya pia?? mle kwa ile movie kuna madudu washa balaa full aibu na hakunangwa kwa vile haikuwa laivu kama hii ya big bro ambayo africa yooote walikuwa wanatizama je angekaa kule mwezi si ndo ingekuwa kitimtim nyumba ya big broo maimuna amefikaje? acheni kutetea ujinga hata shule ukikosea mwalimu anakusahihisha ili ujue umekosea wapi nyinyi mnamvimbisha kichwa kwa kipi haswa acheni unafiki ewe kanumba jiendeleze kwa faida yako BETTER LATE THAN NEVER!!
    miss michuzi

    ReplyDelete
  47. HAHAHAHAH ETI MAISHA YAMEWASHINDA BOX, SIZANI MTU AMBAYE MAISHA YANAMSHINDA ANAFANYA KAZI. ANAYEUZA UNGA NA UMALAYA NDIO MAISHA MIE NAONA YAMEMSHINDA NA ANAYEJIUWA. NDUGU YANGU WEWE ENDELEA CHUO HIKO MPAKA MVI ZIKUTOKE SUBIRI SIKU YAKO BASI. KUHUSU KANUMBA MWACHENI HURU.

    JAMAA ANASEMA WATU MAISHA YAMEWASHINDWA YEYE PIA HAPO HAPO ANAPONDA WATU KAMA SIO UNAFIKI NA MAJUNGU SASA NI NINI? MAANA YA MAONI NAFIKIRI WATU HAWAELEWI PENGINE. UPO CHUO OVYOOOOOOOOO. JAMES. NY,QUEENS

    ReplyDelete
  48. Kanumba ni mirror yetu sisi watanzania wengi tulipata elimu ya bure..yaani watoto wa wakulima....Kuna mtu alisema English ni janga la taifa letu.. ni kweli..Kumbuka kama utaendelea kumshambulia Kanumba ni sawa unajishambulia wewe mwenyewe kwani hata wewe kama ulisoma elimu ya bure kwa ajili ya baba yako mkulima kama mimi, basi English yako inaweza kuwa mbovu kuliko ya Kanumba.. Juu ya upeo wa kufikiri..nadhani kwa watanzania wengi upeo wetu bado ni mdogo kwani hatuna utamaduni wa kusoma vitabu na kufuatilia issue za maana. Mauzo ya magazeti ya udaku ni makubwa kuliko magazeti yenye issues..Mimi binafsi na familia yangu tumechulia suala la umaimuna wa kanumba kama changamoto ya kuenda shule na tutasoma vitabu na kufuatilia masuala ya maana badala ya majungu, gossips na takataka zingine..Thank Kanumba kwa kutukumbusha kuwa watanzania wengi bado tuna safari ndefu ya kushindana na Globalization!..

    ReplyDelete
  49. LEt me tell u somethng Kanumba he was tried for his level best to speak because even u if u know that ur in the interview and the camera is all over the place wht can u do? im sure u can start to find the good point to speak and as u know that people from all countries their watching it. So for me i can say big up Kanumba u tryed for ur level best and mabye ths is ur first interview in english.bye lv u all ..

    ReplyDelete
  50. SIJAISIKILIZA HIYO CLIP ILA NINA SWALI KWA WADAU WOTE NYIE KISWAHILI CHENYEWE MNAKIJUA? MLIPATA NINI LA SABA,FORM FOUR? WENGI KISWAHILI D KAMA SIO F, ENGLISH D/F. LEAVE THE GUY ALONE

    ReplyDelete
  51. hebu tumuongelee na kocha wetu wa timu ya Taifa, MAXIMO vp English yake?

    ReplyDelete
  52. Huyo jamaa anayejiita ati PR0FFESSOR mbona naye anaonekana MAZABE tu, hizo data alizoweka kazipata wapi? uzushi mtupu! huyo jamaa unaye mtetea (Kanumba) katia aibu bana, english yake bomu tu sasa kitu kinachonitia wasiwasi zaidi ni hasa wewe unayejiita Proffessor kuunga mkono udhaifu ambao upo dhahiri, au na wewe ndio kati ya wale mnaopata shahada za kwenye internet?

    ReplyDelete
  53. Nimeipenda comment yako Miss Michuzi. Ndio maana Tanzania haitaendelea mpaka Masihi arudi tena. Mtu akikosolewa unasikia eti mna wivu. Mkapa alisema hayahaya lakini leo nchi iko pabaya. Wengine wanakuja na mifano ati mara Ancelloti mar Jack Chan upuuzi mtupu. Dalili ya ujuha kuwa kama kuna mtu anafanya vibaya hivyo na wewe ni sawa ukifanya vibaya. Wanasahau kuwa lugha za hawa ni za kimataifa. Na nyie manaomtolea mfano Gaetano eleweni mnacho shabikia. Tatizo la Gaetano halikuwa kiingereza cha kuungaunga kama cha Kanumba wenu bali ilikuwa lafudhi(accent) Watetezi wengi wanaonekana kudhani hoja zinajengwa juu ya lfudhi ya Kanumba, la hasha suala ni kuwa hajui kiingereza PERIOD.

    ReplyDelete
  54. Hao multichoice mazabe tu! I doubt their credibility, si ndio haohao walompeleka Flaviana kwenye miss na kumvalisha kigauni cheusi kilichoshonwa na mangi kariakoo kikampunguzia points? Kama ndo wao they need to find something else to do..MAZABE yamedizi very incompetent and the sad thing is there is nobody to hold them responsible! They should never get this contracts again kwani hakuna agency nyingine? wajasiriamali mko wapi?
    NOT ONLY ENGLISH IS THE PROBLEM THE GUY SOUNDS VERY ILLITERATE AND MOST OF THE THINGS HE SAYS ARE VAGUE..
    He seems to desire taking the elevator rather than taking the stairs!

    ReplyDelete
  55. englishie ni KIMO CHA NYOKA mwacheni wajameni kha!

    ReplyDelete
  56. we kanumba umemwona mwenzako kocha wa chelsea hana noma amesema ukweli kuwa yeye anajutahidi kujifunza kughahakuwa mbishi kama wewe unayelalamika lalamika kubali ukweli usaidiwe dogo acha kuleta ubishilolo

    ReplyDelete
  57. Mimi nasema kuingia tu mjengoni BBA hafai. Programu yote ya BBA ni kuiga ujinga usiotusaidia Afrika. Je Afrika tunaongezewa nini kwa kushuhudia eti house-mates wakilana denda hadharani au kuonyesha ushapu wa kutongoza / kutongozwa bila kujali kama umeoa au umeolewa huko unakotoka?

    Big Brother ya Afrika ingekuwa kuonyesha nani anaweza kubuni kitu cha kumtoa / kututoa katika umaskini uliokithiri.
    Vinginevyo tutaiga hata ile programu ya vijana wa mtaa (USA) kutukanana matusi ya nguoni juu ya dada au mama na baba zao mpaka anapopatikana mshindi na kuzawadiwa!

    Kaka Michuzi nakushauri ufunge huu mjadala maana hauna tija kwetu wala hata kusaidia kumsafisha au kuwashawishi watu ambao wanamchambua Kanumba juu ya uwezo wake katika lugha ya Kiingereza au hata katika mambo mengine kwa ujumla.

    ReplyDelete
  58. Wee anony wa Sat Sep 12, 05:07:00 PM,

    Huyu profesa, uprofesa wake ni kama ule wa profesa Vulata tuu.

    ReplyDelete
  59. kaka michuzi ahsante kwa unafanya ili kutuletea taarifa sie tuliombali na nyumbani. ila kuhusu comments watu tunaupeo tofauti mi ningekuwa kanumba ningechukulia huku kusemwa au kupakwa na binadamu wenzangu kama CHALLENGE ili aweze kujifunza zaidi na kujiendeleza zaidi ni muigizaji mzuri lakini kama anataka kufika level za hollywood au bollywood he need to improve his english!!!

    ReplyDelete
  60. Ha ha haaaa,duuuuh dogo alipopata upenyo wa kutimua,katoka nduuuuuki huo,kwenye kona speed 120 shaaaa!!!,kudadadadadedededekiiii!!,pole sana bro ndo ukubwa huo.

    ReplyDelete
  61. kaka michuzi naomba usinibanie maana nilisha jaribu sana lkn comments zangu sizione,kwa kanumba kweli lugha inahitajika na ni muhimu sana kwa hiyo fania yako ya tansia,usisikie watu wanasema eti mbona china wanaongea kichina ua korea au ujerumani hilo wanakudanganya wale wenzetu wameendelea huwezi kufana nisha na bongo hata kidogo mbona south africa wanaongea kizulu na kikosa na kiinglish kipo mbele,usisikie maneno ya hao wa2 kanumba lugha muhimu ooh china wanaongea kichina sijui ujerumani wanaongea kijerumani hao ndugu zetu wabongo hatupo nao kari wala hatuwezi kuwa nao karibu....mdau wa holland

    ReplyDelete
  62. Prof. hapo juu, nenda kachimbe mizizi umsaidie ndugu yetu kayumba alainishe ulimi yai limwagike kama kazaliwa London
    sidhani kama Prof wa kufungua vitabu anaweza kuja na statistic za uongo on public where is your source for you to conclude with that percentages? did you do any survey/pass out questionnaires? Let's see it..provide a link please! mi naona umepiga ramli.. endelea kuongeza matunguri
    no disrespect, I am disgusted by your post there is merely no truth in it! I am in US and 90% of my friends have bachelor degrees and you're telling me only 5% of wabongo in US ni wasomi? shut the F up man!

    ReplyDelete
  63. Michu!

    Hii kitu inaitwa "lack of exposure". Nafikiri Kanumba anapaswa afahamu kuwa kelele zinazopigwa na wana jamii ni "changamoto kwake". Na sio kung'ang'ania kuwa aliongea au kufanya vizuri.

    Tunamtakia heri katika fani yake, lakini aelewe kuwa dunia si lele mama.

    Kanali MIZAMBWA
    durban nankoya

    ReplyDelete
  64. PROFESSOR MWAIGEBOKO sijui nani,duh!
    Mimi nafikiri wewe ni professor Ndumilakuwili,unaweza kutuambia source ya hizo data?au ulitumia emperical evidence?I doubt huo u-prof wako na hata hicho chuo chenyewe.

    wanza wadau huko EAST LONDON kwenyewe mnakujua lakini,yaani kumejaa wabongo,wazanzibari,wanigeria,kenyas kibao.Yaani mimi nilifika nikashangaa,watu mitaani wanasalimiana "habari za saahizi mzeeeeee!"utafikiri hawapo UK.Yaani pale nikama TANDIKA tu,no wonder hata ma-prof wanaotoka huko wanakua wa aina hizo.East London hamna chuo ambacho ipo serious,na wewe ni KAYUMBA tu,ukirudi Dar,nenda ukajiandikishe Open University ili urudie huo u-prof wako wa EAST LONDON aka TANDIKA.

    mKulImA-kIjIjInI gEzAuLoLe

    ReplyDelete
  65. kama kikwete alitia aibu kwenye africa forums meeting iliyofanyika dar last year kama sikosei. kanumba ni cha mtoto. acha wafu wazikane.

    ReplyDelete
  66. Huyo professor plastic hapo juu mwenye statistics fake sijui umeoteshwa usiku wa kuamkia hiyo siku au, hivi karne hii unaweza kucompare UK na Canada kweli, yaani hata mshipa wa aibu huna, UK story zenu tunazo sana si wapo wanaokuja huku kutueleza yaani mna ziki kama kunguni, Canada ni miongoni mwa nchi 10 ambazo hazijaathirika sana na recession unasubutu kuilinganisha na hiyo UK yenu ambako wabongo wamebakiza tu kuweka vigoda nje waanze kuchoma samaki na mihogo we vipi wewe, tembea uone, tunapeta, hatuna shida,health coverage yetu ni bure mpaka kesho halafu unaongea nini wewe, watu wameenda shule huku na ni wastaarabu si kama huko sijui ndio east london uswahili mpaka basi, acha hizo wewe fanya research iliyoenda shule sio unaongea kama kibogoyo hapa.
    Mdau Canada.

    ReplyDelete
  67. Muda Kanumba uliotumia kumzalilisha Wema na kumpeleka mahakamani ungetumia huo muda kwenda British council kusoma mana mwenzio anajua kiingereza vizuri tu bora ungekua nae ata angekufundisha ha ha ha nenda kasome kaka tena Uganda au kenya mana British council ya hapa ni noma

    ReplyDelete
  68. ndiyo mdau hapo juu waambie waspime mziki wa canada kabisa huku kuko swari kwa kwenda mbele hakuna foleni ya wabongo njaa kutwa wamebakia majungu yani nilikwenda london nlilichoka ni wambea jamani kitu kinafanyika bongo hata bongo watu hawajui wao zamaniii ni umbea majungu kwa sana nyiee wadanganyeni watu mko ulaya nyumba zenu zinatia aibuuuuuuuuuuuu mavitu yamepandiana jamani mh! wenye british passport njooni huku mle bata ila umbeya ufuska marufuku
    mdau toronto

    ReplyDelete
  69. Ndugu Kanumba,kuchemsha ulichemsha lakini si kosa lako ni uelewa mdogo wa kiingereza tulionao wengi wabongo. Hata wenye degree pia huchemsha kama hawana mazoea ya kuongea mara kwa mara lugha hiyo. Fuata ushauri mzuri wa Anonymous Sat.Sept.12,11:26:00 utakusaidia. Achana na wasiokutakia mema - wenye wivu. Mafanikio yanakuja mbele yako ukifuata maelekezo mazuri badala ya kupuuzia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...