SHEIKH MKUU WA
MKOA TABORA AFARIKI DUNIA
MSANII MPYA WA KIZAZI KIPYA AMBAYE ANAYEISHI NA KUFANYA KAZI ZAKE NCHINI ITALY , RAMADHANI MAVUMBI, ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA BABAYAKE MZAZI SHEIKH ALLY MAVUMB, KILICHOTOKEA TAREHE 08/09/2009, SAA 09:50 ASUBUHI, NA KUZIKWA TAREHE 09/09/2009 SAA 04:30 JIONI.
KWA NIABA YA FAMILIA MSANII MAVUMBI ANAPENDA KUWAFAHAMISHA WOTE AMBAO BADO HAWAJAPATA TAARIFA HIZO ZA MSIBA, KUPITIA GLOBU YETU HII YA JAMII.
MSANII MAVUMBI HIVI SASA YUPO NJIANI KUELEKEA TANZANIA KWA AJILI YA MSIBA WA BABAYAKE. KWA SALAAM ZA RAMBIRAMBI NA KUTOA POLE WA NDUGU YETU MAVUMBI.
contact;
+393468413470
Italy.
MOLA AIPUMZISHE KWA AMANI
ROHO YA MAREHEMU PEPONI
-AMIN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ina lilahi waina ilaihi Rajiun.

    Mungu amlaze mahali pema sheikh Mavumbi, alikuwa jirani yangu pale Mwanza road karibu na kwa Mzee Hamisi Ibrahim, pia alikuwa Imamu wa msikiti wa Mabatini na Laziz Ijumaa, aligoma kabisa kwenda msikiti mkuu wa Gongoni na kuwaachia vijana, japo inasemekana baadaye alianza kuwachapa bakora za tarasimu walioanza kumdharau.

    Masheikh wa Tabora wameisha sasa, walikuwepo masheikh vijana wengi walimtangulia mbele ya haki. Hakuna la kusema zaidi ya kumtakia makazi mema. Poleni sana Sheikh Shabani na wanafunzi wake wote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...