how is this sitting?
(hii imekaaje?)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. michuzi , katika hili watani wa jadi wametupiga bao. hata ukiwapeleka THE HAGUE bado watashinda maana wao hawajasema mlima upo kwao wamesema uko Bongo lakini best view ipo kenya.
    hii ni challennge kwa wizara ya maliasili kufanya matangazo ya kutosha kuhusu mlima huu.

    ReplyDelete
  2. Kwa sasa kidogo Tanzania inajulikana,kwani u.k kuna advertise kwenye t.v ya British airways ambayo inakwenda moja kwa moja tz,na katika hilo tangazo wameonyesha mbuga za wanyama Tanzania.Itasaidia kwa upande fulani kuitangazia Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Imekaa sawa kabisa, maana hata ukiwa ESAMI Njiro Hill Arusha unauona Kilimanjaro, ukikaa Upareni unauona, ukikaa Loitoktok unauona Kilimanjaro, ukikaa Amboseli unauona Kilimanjaro.

    Ukitumia Google Unauona Kilimanjaro pia. Ukiwa kwenye Space Shuttle MIR unaonekana, Ukiwa kwenye SPACE STATION (satellite)tunauona pia.

    Mdau
    Globalvillager.

    ReplyDelete
  4. Mmesahau ule usemi...Kila muwamba ngoma ngozi huvutia kwake? Endeleeni kujiuliza wakati wenzenu wanatangulia

    ReplyDelete
  5. GOLD DIGGERS

    ReplyDelete
  6. Wako sawa kabisa...kunawa utanawa lakini kula hauli...utaona mlima ukiwa Kenya ila huwezi kuupanda, itabidi uende Tanzania ndo upande...wako sahihi.

    Ila kikubwa hapa ni kuwa wenzetu wametumia tu nafasi ya mlima kuonekana kutoka kwao kuvutia watalii katika mbuga zao na hoteli zao...."Mjasiriamali by definition ni yule anayeona / identify opportunity na kuitumia"

    ReplyDelete
  7. HAKUNA TATIZO, KWANI USHIRIKIANO USIISHIE KWENYE POLITIKI TUU, SISI WOTE NI WA IST AFRIKA.

    ReplyDelete
  8. Tayari washawatangazia Tanzania, Ukiwa Arusha unauona. Wangejiuliza Wenyewe au Wataulizwa Je Nikitaka Kuupanda Huo MLima Kilimanjaro Nitapandia wapi? Jibu watawapa Tanzania wamejifunga wenyewe hapo Ukiwa tanzania unapata Yote View na Kuupanda huo mlima. Pazi.

    Nakubaliana na Aliyesema ndio kwanza kawatangazia Tanzania watajiuliza Kumbe umetega Tanzania.

    ReplyDelete
  9. washajisemesha wenyewe uko Tz basi washatutangaza
    lakin since ni mlima mrefu africa basi lazima uonekane hata ukiwa kenya ila wanajua uko Tz

    watani wa jadi wanatutangaza kistyle aha aha ha ha

    ReplyDelete
  10. mimi sina lakusema, wadau hapo juu wamemaliza.

    ReplyDelete
  11. Globalvillager,

    Umeelewa lakini hii post?Naona wewe unaongea vingine kabisa!!!!Kazi kweli kweli!

    ReplyDelete
  12. how long shall they keep using (abusing) mt kilimanjaro while we stand aside and look.

    hawa jamaa kweli ni watani lakini wanatumia 'utani' huu kutupiga bao.

    kenyans are second investors in our country. walipolikosa soko la sadc kijografia wakaamua kuleta tuviwanda twao twa colgate na pipi ili wauze zambia na kwingineko.

    wananunua ardhi kwa kupitia watanzania kama hawana akili nzuri.

    sasa wanataka kununua serengeti breweries kwa minajili hiyohiyo

    sie tunawabung'alia mimacho tu.
    wakenya wana akili ya kutafuta jamani, tuwaige!

    ReplyDelete
  13. Eeenhe don worry bado shirikisho linakuja we know you kelele mingiiiiiii!

    ReplyDelete
  14. Nafikiri Globalvillager amejumuisha njia mbalimbali za kuuona Mlima Kilimanjaro.

    Kazi sasa ni kuwashawishi watalii watue moja kwa moja eapoti ya uwanja wa Kilimanjaro, uwanja wa JK Nyerere au Zanzibar kabla ya kuelekea Kenya.

    Maanake hivi sasa watalii hushukia Nairobi au Mombasa na kutumia siku kibao Kenya kwa utalii kabla hawajafikiria kuupanda Mlima Kilimanjaro.

    Watalii wengine hujikuta wameshamaliza mapesa yao wakiwa Kenya na hivyo huamua kuuangalia Mlima Kilimanjaro kutokea upande wa Kenya.

    Kazi kubwa kwa wadau wote ni jinsi ya 'kunadi' the whole package, yaani fukwe safi za Zanzibar, Mafia, mbuga za Selous, Katavi, Serengeti n.k pamoja na Mlima Kilimanjaro.

    Tusibakie kungangania kivutio kimoja, bali the "whole package' mpaka watalii wachanganyikiwe wamalize mapesa bila kwenda Kenya.

    Iwe watalii wakifikiria kuja Afrika badala ya kufikiria Afrika ya Kusini, Namibia, Mauritius, Seycheles au Kenya basi wajue 'mambo yote utalii' Afrika ni Tanzania Kwanza, kwingineko ni 'utani'

    Ndio Ya Wezekana Tanzania Kwanza.

    Mdau
    Ma-Visheni

    ReplyDelete
  15. Wana haki ya kuzungumzia kuwa pia unaonekana kutokea Kenya lakini si suala la "upo TZ but the best view inaonekana toka Kenya",huu ni upuuzi wa kuonyesha kuwa haina haja ya kuja TZ,Vutia watalii waje kwako si kwa kuharibu kwa wenzio,pumbavu.
    Na nyinyi wizara ya utalii ongeeni official na wizara ya utalii kenya jinsi ya kutumia ustaarabu katika kutangazia kilimanjaro,si kukaa na kupakata mikono kwa hivyo vijitangazo vyenu vichache vya Europe

    ReplyDelete
  16. Sijui Watz tukoje. Zambia na Zimbabwe wanapakana na mto Zambezi kwenye eneo la maporomoko ambayo ncho zote mbili wanashindana kuvutia watalii tena kwa mafanikio. Upande wa Zambia kuna mji unaoitwa Livingstone na upande wa Zimbabwe unaitwa Victoria Falls Town. Wakati wa Zambia maporomoko hayo wanayaita Mosi O Tunya wazimbabwe wanayaita Victoria Falls. Na nchi zote mbili wanavutia watalii kila mmoja kwa nfasi yake.

    Na sisi tupende tusipende Wakenya hawataacha kuutangaza mlima Kilimanjaro. Tunachotakiwa sisi ni kuwa wabunifu. Halafu historia inasema wakati waingereza hawajaja kuitawala Tanzania mlima huo ulikuwa sehemu ya Kenya kama vile Mombasa ilivyokuwa sehemu ya Tanzania (Zanzibar). Of course Malkia Victoria akautoa zawadi kwa binamu yake ambaye alikuwa mfalme wa Ujerumani. Wakati huo Tanzania ilikuwa ikitawaliwa na Wajerumani.

    Of Course Kenyans are damn smart. Hata South Africans wanautangaza kwa kusema "njoo Joburg tutakupeleka Kilimanjaro ambako ni only three hours from Joburg". That is being smart. Tuache kulia kulia. Sisi si wabongo? Fine tutumie mbongo zetu basi.

    ReplyDelete
  17. Iam dreaming of a day when a mountain which is just one of a natural geographical feature, among the many, won't be a source of enmity and hatred between AFRICANS. Iam dreaming of a day when a WHITE man's coming to the country of Tanzania and Africa in general won't be a source of pride and income. Amen

    ReplyDelete
  18. wameona wa tanzania wamekua waki lalamika kwa wao kusema mlima kilimanjaro uko kwao kwahiyo wakaja na ujanja mwingine wa kusema best view iko kwao. kwakweli view ya upande wa kenya si mzuri kama upande wa tanzania. upande wa kenya una snow ndogo sana. snow nyingi inaonekana upande wa tz na mlima unavutia sana upande wa tz.

    ReplyDelete
  19. Tusilaumu tu ooooh,wamesema hivi,Ooooh,jamaa wamesema hivi.Hata sisi (watz) tungekua ndo wakenya,tungetumia hiyo opportunity ya view ya huo mlima.Kuna swala la sheria hapo,kwamba ni kuona,hawajasema kwamba upo kwao.
    Tatizo letu ni bla bla nyingi badala ya kuja na strategy nzuri za kuinua uchumi wa Tanzania yetu.
    Wiki ilopita,nimezunguka kwenye karibu ma-underground yote ya LONDON,sijaona hayo matangazo tulioambiwa yametumia mabilion ya shilingi.WIZI M2PU!!

    mKuLiMa-kIjIjInI gEzAuLoLe

    ReplyDelete
  20. Wahenga walinena na mapema kuwa:

    ''Usimpe Maskini Mnofu wa Nyama, Itamwozea Mkononi''

    Kwa maana atashinda anazunguka nayo mkononi Wiki nzima kwa Kutoamini Kama Kweli Ameangukiwa na Bahati ya Kupata Mnofu.

    Mdau Ma-Visheni kesha tupa changamoto ya "Whole Package', Mlima tunao, Mbuga tunazo, Mkonga wa Optic Fibre(TeknoHAMA)upo, www. youtube.com ya bureee ipo, Bahari ipo, Fukwe zipo, Hotel/Inns kibao, Eapoti kubwa, Wizara Mama tunayo, Tanzania Tourist Board/ Tanapa nawaona, Charter aeroplane zipo, 4X4 Vehicles, Nguvukazi n.k

    Vipi Watanzania Mnofu Unatuozea Mkononi!?!

    Mdau
    Wahengawalinena

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...