Na Mohammed Mhina,
wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi nchini limewatahadharisha wananchi katika maeneo mbalimbali kujihadhari na vitendo vya kihalifu na wahalifu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye siku kuu ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Tahadhari hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Kamishna Msaidizi Abdallah Mssika, (pichani kulia) wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.
Kamanda Mssika amesema kuwa uzoefu umeonyesha kuwa mara nyingi wananchi wa dini zote wamekuwa wakisherehekea siku hii kwa shamra shamra mbalimbali ukiwemo unywaji wa pombe kupita kiasi na wengine kuthubutu kuendesha magari kwa mwendo kasi na kupelekea ajali.
Amesema kuwa kutokana na uzoefu huo, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi mbalimbali wakiwemo walezi na wazazi, kutowaacha watoto wadogo pasipo na uwangalizi wa watu wazima ili kuepuka kugongwa na magari ama kuzama majini wakati kwenye fukwe za bahari na maziwa ama mabwawa.
Aidha wazazi na walezi wasiache nyumba zao bila uangalizi wa kutosha na pia kuepuka kuwaruhusu watoto wadogo kwenda kujazana kwenye kumbi za starehe kwa kuhofia kukosa hewa na kufariki dunia.
Kamanda Mssika amewatoa hofu wananchi na kusema kuwa watakuwa salama mwanzo hadi mwisho wa siku kuu hiyo na kwamba Jeshi hilo kwa kushirikiana na vikundi vya ulinzi wataimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mijini na sehemu za kufanyia ibada na burudani na maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu..
Amesema kuwa Jeshi hilo litatumia askari wake wa miguu, magari, Mbwa na Farasi katika kufanya doria kwenye maeneo korofi kwa lengo la kuwahakikishia wananchi usalama wao pamoja na mali.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linawakumbusha wafanyabiashara kuepuka kusafirisha fedha nyingi kwa wakati mmoja kutoka eneo moja hadi lingine lakini ikiwa ni lazima kufanya hivyo wanashauriwa kutoa taarifa kwa wakuu wa Polisi ili kupatiwa askari wa kuwasindikiza ili fedha zao ziwe salama.
Kwa upande wa Walinzi wa majengo ya viwanda, ofisi na maghala ya kuhifadhia mali na bidhaa mbalimbali zikiwemo za madukani wametakiwa kujiepusha na vishawishi vya kufadhiliwa vyakula na vinywaji kutoka kwa watu wasiowafahamu wawapo kwenye malindo yao ili kuepuka kupewa sumu ama madawa ya kulevya na kuibiwa.
Amewataka pia Madereva wa magari ya abiria na madereva wa Taxi kujiepushe na mambo ya ulevi na kwenda mwendo wa kasi ambao unaweza kusababisha ajali za barabarani. Pia abiria wa magari hayo a wanatakiwa kutoa taarifa kwa askari wa usalama barabarani ili waweze kuchukuliwa hatua zinazostahili kwa kukiuka mashariti ya udereva.
Aidha amewakumbusha pia wamiliki na madereva wa magari madogo waepuke kutoa lifti kwa watu wasiowafahamu ili kuepuka kuporwa magari na kusababisha hasara kwa wamiliki wake.
Amesema kuwa pamoja na uchache wa skari wa Jeshi hili hapa nchini, Jeshi hilo limejipanga kuwashirikisha wananchi katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa kuimarisha doria na kufanya kwa pamoja katika kuwahakikishia wananchi usalama wao.
Asante sana kamanda Musika kwani kama mikakati hiyo mmeipanga vizuri at least ajali zitapungua kwa kipindi hiki tunapokaribia sikukuu.
ReplyDeleteMara nyingi wizi, ajali hasa vifo vya watoto vimekua vikitokea sana tena muda mwingine kwa uzembe.
Keep it up
Tunashukuru kwa hilo,ila tunaomba nyanja nyingine na wao watoe ushirikiano kwa wateja wao, kama vile TANESCO NA NUWA. Nyie pia mnaihudumia jamii, tutashangaa sana mkitukatia umeme kama inavyotokea, hasa line ya Kisarawe kuja huku Dar, kuna sintofahamu ya kukatika-katika kwa umeme sijui kwa sababu gani.
ReplyDeleteTunawatakia nyote maandalizi ya Idd njema ingawaje hali ni ngumu,lakini hivyohivyo tutafanyeje.
Na nyie wauza nguo, viatu nk tafuteni thawabu kwa kutoa punguzo,kama mkono wa Idd, hiyo itakuwa akiba yenu ya baadaye, faida utakayoipata sasa kwa kupandisha bei itakusaidia muda mchache tu hapa duniani .
Na nyie matajiri toeni mlichoruzukiwa kwa wasio-nacho, toeni ili mtimize amri ya mungu , hii ni heri kwenu kama mngelijua.
Na nyie waajiri, wapeni chochote kitu wafanyakazi wenu, kwani mshahara mnaowalipa ni hand-to-mouth. Sikukuu kama hizi ni za machumo, toeni kwa wafanyakazi wenu ili mupate baraka toka kwa familia zao.
Na sie tuliofunga, tuchunge mipaka ya mwenyezimungu, tujiandae kwa yale mema, na tuayachukie yale yatakayotuharibia toba yetu ya mwezi mzima. Na tusisahau kuwa kuna suna ya kufunga siku sita baada ya Ramadhani kwenye mwezi wa Shawwal.
M3
HONGERA MZEE MSIKA PIGA KAZI KAMANDA TUNAKUAMINIA VIJANA WAKO WA NHC ARUSHA ROAD MOSHI. ULITULEA VIZURI KAMA FAMILIA MOJA WORLD CUP YA MEXICO 1986 YULIANGALIA KWAKO MAANA TV ZILIKUWA LABDA TATU KWA KOROSSO KOCHA WA USHIRIKA NA KWA MZEE ABDALA KIMAMBI. SASA TUMETAWANYIKA TUKO KILA PEMBE YA DUNIA WEMGINE WAKO ANGANI WANAANGALIA MAZINGIRA YA KUTUA. TUDUMISHIE AMANI YETU TUNAKUTEGEMEA SANA.
ReplyDelete