akiwa ni mmoja wa wanamuziki wakongwe waliokuwa wa mwanzo kuingia bongo toka kongo enzi za mwalimu, mzee makassy anabaki kuheshimika sana katika tasnia ya burudani nchini. hivi sasa ameokoka na anaimba nyimbo za gospo. wenye data zaidi msaada tutani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. MAKASI SIO MCHEZO MZEE MAKASI NAKUMBUKA ZAMANI WAKATI NDIO NAANZA KUPATA AKILI YA KISIKIA MUSIC KWENYE RADIO TANZANIA DAR ES SALAAM RTD MAMBO YALIKUWA MAKASI REMMY KWA KWELI GOD BLESS MAKASI ANAFAA KUKUMBUKWA SANA. HONGERA MAKASI

    ReplyDelete
  2. Kweli nasikitika mtoto anapozaliwa,
    Anakuja pata tabu za duniani,
    Njaa nyingi magonjwa mengi
    Surua, kuhara, homakali eeeeaaahh ohoooo eeeeiih eeeahhhh!!!
    Ukimzungumzia makasi nakumbuka enzi za kipindi cha "ombi lako" cha RTD ilikuwa miziki inayosikika ndio hii tu ukitaka ya kizungu lazima usubirie jioni kwenye "idhaa ya biashara au jumapili at 1330 hrs external service!!!!!
    Mweee enzi za mwalimu wote tulikuwa tunasikiliza kitu kimoja tu!!

    ReplyDelete
  3. "Mambo bado mambo bado, mambo bado.
    Makasi toka toka Kinondoni ee, mambo bado
    Makasi toka toka Daisalame, mambo bado....yabisose malembe mambo bado".

    Wacha bwana mambo yanakwenda yanabadirika. Siku hizi tuko upande mwingineeeee! tunainjoi mambo kwa Yesu

    ReplyDelete
  4. MZEE MAKASSY !SIO MWANAMZIKI WA MWANZO WA KIKONGO KUINGIA NCHINI ENZI ZA UTAWALA WA MWALIMU!
    MWANAMZIKI WA MWANZO ALIKUWA "Cosmass Papa Micky" (kalonda Lunganga) aliyekuwa mmiliki wa bendi ya Orch.Nova Sucess enzi zile katika makao yake ktk Bar ya TOP LIFE.
    Papa Micky ndiye alikuja na mwanamziki Marehem Joseph Lusungu,ambaye aliwapa NUTA JAZZ kama zawadi hili mziki wa dansi nchini uendelee.
    Baadaye bendi za Orch.Nkashama Nkoy,Santa fe,zote zilipita njia,baadaye ndio bendi za Orch.Baba Gaston hiliyoukuwa inamilikiwa na mwanamziki Baba Gaston Ilunga wa Ilunga hilikuja,na wakati huo huo Mzee Makassy nae alikuja,na bendi yake akitokea Uganda sio moja kwa moja Kongo.lakini wakati hule kulikuwa na ushindani katika fani ya mziki.
    Lakini MZEE MAKASSY anaheshimika katika mziki adi leo na ni GWIJI.
    Mzee Makassy enzi ya ujana wake alikuwa mwanamziki wa JOHN BOKELO ISENGE

    ReplyDelete
  5. kwa wale wapenzi wa muziki wa dansi kama mimi huyu bwana tulikuwa tuanmuita profesa.....profesa makassy upo wapi???ingawa sijapata kusikiliza gospel muda ila nitatafuta nyimbo zako za gospel profesa...maana ukiwepo wewe hakiharibiki kitu.

    ReplyDelete
  6. Ni wachache waliopata Neema kama ya huyu Mzee ya kujikana nafsi na kumrudia Mungu wao na kumuabudu kabla hawajaurudia udongo walimotwaliwa. Uzidi kubarikiwa Mzee wetu mpaka siku Mungu atakapokutwaa. Utaimaliza safari salama Mtumishi na wala usikate tamaa. Ingawa ni wengi watajaribu kukukatisha tamaa wakisema ooh umefulia n.k. Kufulia ni duniani tu lakini Mbinguni utakuwa ni mkubwa zaidi ya Bilionea.

    ReplyDelete
  7. JAMANI KULIKUWA NA BENDI MOJA IKIITWA BANA NGENGE NA MWIIMBAJI MTOTO KIJANA ENZI HIZI AKIITWA FATAKI, KUNA MTU YOYOTE ANAJUWA FATAKI YUKO WAPI NI WA-KONGO WALIKUWA

    ReplyDelete
  8. ..kintozegwu..jina lake la biblia limekua nani?..

    ReplyDelete
  9. kwa Anony: sept 16, 10:56PM

    MWANAMZIKI FATAKI WA BENDI YA BANANGENGE ALIKUFA 11/12/2006 NA KUZIKWA 13/12/2006 MJINI Dar-es-salaam.
    Kweli ilikuwapo bendi za Orch.Banangenge na marehemu Fataki Lokassa aka Fataki "Masumbuko mingi ya dunia" alikuwa anaongoza safu ya mbele ya waimbaji,na unenguaji wake akiwa na kibatali kichwani!1976 mpaka 1978,Banange ikafia Kena na Fataki akajiunga na Les Kinois mjini Nairobi akiwa pamoja na Samba Mapangala,baadaye 1981 Samba na Fataki na wengineo wakaizaa Virunga Band.
    Lakini Fataki alifia Dar 11/12/2006 hizo ndizo taarifa za uhakika.
    wadau
    FFU

    ReplyDelete
  10. Leo mzee Makasi amepewa udaktari wa heshima...ni Dr Makasi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...