Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Anga la Afrika ya Kusini Luteni Generali Carlo Gagiano wakati wa kufunga wiki ya maadhimisho ya miaka 45 ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya jeshi hilo Airwing, Ukonga leo jijini Dar es salaam. Picha na Aron Msigwa (MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. kaka Michuzi! haya ni mageuzi halisi katika nyanja yaulinzi.Ndani ya miaka 45 jeshi limekamilika na haya ni mapindizi halisi. jeshi karibu na jamii na kwa mara ya kwanza wananchi wamewezi kuifikia na hata kuigisa "bakora" inayowalinda. Inahamasisha jamii kuweza kupata wanajeshi makini wakati ujao. tazama General wakisasa na msomi afande Davis Adolf mwamunyange alivyo funika. "Changamoto kwako" anza kutengeneza mrithi

    ReplyDelete
  2. Jamani tuwekAne sawa hapa. Generali Davis Mwamnyange sie Mkuu wa MAJESHI, ni Mkuu wa MAJESHI YA ULINZI.

    Mdau USA.

    ReplyDelete
  3. Umenena kweli Anony wa pili hapo juu, Tanzania ina majeshi mengi kwa mfano jeshi la polisi mkuu wake ni Said Mwema na jeshi la Magereza lina mkuu wake. Kwahiyo Mwamunyange ni mkuu wa JWTZ.

    ReplyDelete
  4. SHERIA YA ULINZI WA TAIFA NAMBA 24 YA MWAKA 1966 INAELEZA KUWA KUTAKUWA NA MKUU WA MAJESHI YA ULIZNI (CHIEF OF DEFENCE FORCES - CDF). HII NI KUTOKANA NA KWAMBA WAKATI NCHI IKIWA VITANI, MAJESHI YOTE KWA MAANA YA JWTZ, POLISI, USALAMA WA TAIFA, MAGEREZA, UHAMIAJI, JKU, KMKM VALANTIA N.K. HUSHIRIKI KULINDA NCHI NA CDF AMBAYE PIA NI MKUU WA JWTZ NDIYE ATAKAYEYAONGOZA KIMAPIGANO. NDIYO MAANA AKAITWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI.

    Mtanzania Mzalendo

    ReplyDelete
  5. Nafikili sahihi ni kuwa yeye ni mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama. majeshi yote kwa maana fulani yanakuwa chini yake.
    Nchi inapokuwa vitani ama kupata majanga makubwa mkuu wa jeshi ndio utawala opersheni yote inayohusisha majeshi yote nchini. hata kwa mtazamo wa kawaida tu, utaona jeshi kama JKT ni kama ni mtoto wa jeshi la ulinzi. msitishike na wakuu wao waliopo, mambo yanapoalibika tunabakiwa na mkuu mmoja tu wa kutuongoza.

    ReplyDelete
  6. Ni mkuu wa majeshi na ndiyo siku za kitaifa utaona Amirishejeshi mkuu uambatana na Mkuu wa majeshi kuingia uwanjani na kukagua gwarinde la vikosi vyote vya majeshi. Hujawahi kuona Mkuu wa Mkuu wa Police au Mageraza wanauhusika, hata wakuu wa majeshi mengine wanasalute kwa mkuu wa majeshi, tunaye amirijeshi mkuu na baada ya hapo anafuata mkuu wa majeshi, na kama kama mlivyoelzwa sheria ya ulinzi inaeleza bayana kuhusu ilo.

    ReplyDelete
  7. asanteni kuniweka bayana...kumbe mume wangu uyu ni kibosile ivo?unajua huwa haongeagi saana

    yan uyu jamaa niko hoi tu utafikili picha za mabinti wa mfalme mswati

    a wanna lavu yuuu beibeeee

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...