Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa (kulia) akitangaza zawadi za sh.M 17 kwa waandishi wa habari kuhusiana na shindano la mbia za baiskeli. litakalofanyika Oktoba mwaka huu mkoani Mwanza.( katikati ) katibu Mkuu wa chama cha baiskeli Lado Haule(kushoto)Meneja Matukio wa pepsi Carolyn Clement.
Vodacom yatenga zawadi za 17m/-
kwa washindi wa mashindano ya baskeli
Vodacom Tanzania imetangaza kuandaa mashindano ya mbio za baiskeli yanayotarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao Jijini Mwanza na imetenga Sh.milioni 17 kama zawadi kwa washindi mbalimbali.
Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania, Rukia Mtingwa, aliwaambia Waandishi wa Habari Jijini jana kwamba ili kufanikisha mashindano hayo Vodacom imetenga Shilingi milioni 16,540,000 za zawadi kwa washindi wa mbio hizo.
Alisema kwa mwaka wa 4 sasa Vodacom imekuwa ikiandaa mashindano haya ya baiskeli na kwamba mwaka huu wameongeza hamasa na ubora wa mashindano hayo.
“Lengo la Vodacom Tanzania kuandaa mashindano haya ambayo yatafanyika mwezi Oktoba mwaka huu Jijini Mwanza ni utekelezaji wa mkakati wetu tuliojiwekea wa kukuza michezo mbalimbali hapa nchini kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa michezo mingine,” alisema.
Alisema mashindano ya mwaka huu yamegawanyika katika makundi matatu, kundi la kwanza ni la mbio za km 150, kundi la pili ni la mbio za km 80 kundi la mwisho ni la kilomita 10 ambazo hizi ni maalum kwa walemavu.
Alisema mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 150 atapata Sh.1200,000, wakati mshindi wa pili atazawadiwa Sh.900,000 mshindi wa tatu atapokea Sh.600,000.
Alisema katika kundi hili mshindi wa nne hadi wa kumi atazawadiwa Sh. 450,000, mshindi wa 11 hadi wa 20 atapokea Sh.200,000 kila mmoja na wakati mshindi wa 21 hadi wa 30 ataondoka na kitita cha Sh. 100,000.
Kwa upande wa Kilomita 80, alisema mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh.1000,000, mshindi wa pili atapewa Sh.750,000, mshindi wa tatu atazawadiwa Sh.500,000, mshindi wa nne hadi wa kumi atapewa Sh.320,000, mshindi wa 11 hadi wa 20 atazawadiwa Sh. 120,000 wakati mshindi wa 21 hadi wa 30 atapewa Sh. 60,000.
Alisema kwa upande wa mbio za walemavu, mshindi wa kwanza wa kiume na wa kike kila mmoja atapokea Sh.300,000, washindi wa pili watazawadiwa Sh.200,000, na washindi wa tatu kila mmoja atapokea Sh. 100,000.Kuanzia mshindi wa nne hadi wa kumi atapokea Sh.50,000.
“Vodacom inatoa zawadi hizi kama motisha kwa mashindano haya ambayo yana lenga katika kuuboresha mchezo huu hapa Tanzania, ni matumani yangu kwamba motisha hii ndiyo itakayoleta ushindani na hivyo kutupatia washindi wenye kiwango cha juu,” alifafanua.
Aliwaomba wakazi wa Jiji la Mwanza kujitokeza kwa wingi kuwashangilia wanamichezo hawa ili kuwapa motisha na hivyo kuyapa mashindano msisimuko.
Pamoja na mchezo huo, kutakuwepo na burudani mbali mbali kutoka kwa wanamuziki wa bongo fleva TMK wanaume Family na Tiptop Connections.
dadaangu rukia tadhali sana niandikie mdogoako janetjesse51@yahoo.com muhimu
ReplyDeletelasttime kuonana tangia unakaa sinza madukani pale
ReplyDeleteNaomba kaka michu waulize hawa jamaa wa voda hivi msemaji wa kampuni (pr officer) ni nani? inakuwaje kampuni hii kila mtu anafanya press conference? yaani kila idara ikiwa na jambo inaita press conference yake. leo tunamuona ansi mmasi, kesho rwehumbiza, keshokutwa mtinga, juzi mwamvita makamba, jana mafuru, na wengineo kedekede. hebu watuambie. mnaharibu brand tafuteni mtu mmoja ndio awe face of the company. sio kila mtu anataka publicity.
ReplyDeleteMBIO ZA BAISKELI.....ONLY HAPPEN IN MWANZA!!!
ReplyDeletehongera, Voda tunaomba tubadilishe mipango sasa tuende kwenye kusaidia mambo ya mji kama kupanda miti mjini kushilikia na serekali kujenga barabara hata kama ni kipande kidogo tutashukuru au taa za barabara vituo vya polisi.
ReplyDelete