Mchungaji wa kanisa la e Winners' Chapel, Denis Mlazi, akisindikizwa kuingia kwenye chumba cha mahakama ya Temeke leo akikabiliwa na mashtaka ya kumuua mkewe, Rosemary Munseri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Jamani inasikitisha dunia ya leo.

    Pia je hiyo mahakama ya Temeke pia ilifumuliwa na mabomu ya Mbagala, maanake kama ndo uani mwa Mahakama ndivyo kulivyo basi inasikitisha.

    ReplyDelete
  2. Wee unashangaa mahakama!!usiombe utie timu huko ngome(jela)kulala mnalala mchongoma inabidi mtu ulale kiubavu ubavu watu mnalala huku miili yenu imegusana halafu siajabu uliegusana nae wewe ana ukurutu mwili mzima na hamlali na mashati kwaajili ya joto kali ni mambo ya ngozi kwa ngozi saa tisa za alasiri mlango unafungwa taa zinazimwa nyote kulala,kama ulikula ugali wa watu na ukagongewa fegi mchana taa ikishazimwa inabidi ulipe fadhila tu

    ReplyDelete
  3. MTU ANASADIKIWA KUUWA NA ANATEMBEA BILA PINGU! NI AJABU ANATAKIWA ALE PINGU, NCHI ZA WENZETU KOSA LOLOTE LILE UNAKULA PINGU NI SEHEMU YA USALAMA, HATA AJALI YA MAGARI BARABARANI TU UNAKULA PINGU HATA UWE NA WADHIFA GANI PINGU MBELE KWANZA KOSA LOLOTE LILE, SEMBUSE KUTOA ROHO YA MTU, EBU MPIGENI PINGU HUYO.

    ReplyDelete
  4. Inasikitisha kweli kweli. But I think waafrika tuna utamaduni wa kupenda vitu vibaya. Hatuna utamaduni wa kupenda vitu vizuri. Usiniambie hapo tunashindwa hata kusakafia na kuboresha mandhari.

    Mfano mzuri ni kuangalia mahakama wakati wa mkoloni na mahakama zetu baada ya kupata uhuru. Hata barabara na vitu vingenevyo vingi.

    ReplyDelete
  5. Duh wkeli huyo baba achana naye inaonekana ni stress ya maisha. manake mchungaji na kandambili mtaani!!!!!


    Ila hiyo mahakama kwanini wasilete wale watu walio huko jela wakafanya kazi siku mbili tu kuziba hayo mapango...????

    Au hata charity work ....national service....volunteer...do the right things...mpaka waje wajapani watujengee.....Jumamosi moja la mgambo likilia hapo pangekua panapitika....kama watu hawaoni vile...hebu waangalie wameangalia mbele

    ReplyDelete
  6. uncle nanihii, kihabari mbona kifupi? hakijitosharezi bana.

    ReplyDelete
  7. JAMANI JIHADHARINI NA WACHUNGAJI WA SIKU ZA MWISHO KAMA HUYU. MCHUNGAJI KWELI UTAUWA. PILI HALI YA MAHAKAMA INATISHA NAKUTUA AIBU, WAFUNGWA WAFANYE HIYO KAZI.

    ReplyDelete
  8. Kama vipi niachie contact za huyo wa kike nataka nimpatie scholarship aje state, nimemzia mtoto huyo, mtoto macho ka amekula kungu!!

    ReplyDelete
  9. Kwa wale ambao hawajui hii habari naomba niwasimulie kidogo, huyu baba anaejiita mchungaji ni mnyama, marehemu nilikuwa nafanya nae kazi,alimfungia chumbani, akafunga madirisha na milango yote kisha akamimina petrol chini ya kitanda akafunga mlango kwa nje kisha yeye akaenda kukaa sitting room kufanya kazi zake kwenye laptop, majirani ndo walimuokoa marehemu ila kwa kuwa aliungua sana alifariki maskini.Kisa cha kumuua mama wa watu ni kwamba alitaka kuoa mke mwingine wakati tayari alikuwa ana mke, so kitendo cha marehemu kukataa ndo kikawa kifo chake. Kweli dunia imekwisha, binadamu tumekuwa wanyama tena hata wanyama hawajafikia hivi kusema ukweli. mbaya zaidi mama mkwe wa marehemu na mawifi waligoma kuja msibani eti mpaka kaka yao atoke gerezani, Its a long story siwezi kuhadithia yote ila angalau mmeweza kupata picha kidogo ya unyama wa huyu anaejiita mchungaji.

    ReplyDelete
  10. Haya! Mchungaji huyo. Mke anae lakini bado macho mia mia na eti waumini wake wanamtegemea kuhubiri upendo na amani!

    Iko siku ukweli na uongo utajulikana tu, kuhusu hawa wachungaji na mambo yao! Ana sura kama mhutu vile!

    ReplyDelete
  11. Hawa kina Denis wako wengi. Mweingine yupo Belgium kamtwanga mke wake Bongo kakimbilia eti kusoma. Hivi wanaume mnawapiga wake Zenu kwa infereiority complex ya kushindwa kuongea nao hadi mkaelewana? Why treat other people like shit mngepigwa nyie ingekuwaje?
    Huyu simuonei huruma hata!
    Wanawake msikubali kupigwa-Run and never look back LIFE is SWEET UNBEATEN!

    ReplyDelete
  12. Kwa kuongezea anoy 10;43,watoto wao mara zote walikuwa wanalala jirani na chumba chao lakini siku ya tukio aliwaamuru wakalale mbali ili afanye unyama wake.Wakati majirani wanataka kumwokoa mkewe yeye akawa hataki na hata wampeleke hospitali kwa sababu zake binafsi,hadi mkewe akafa njiani.Kisa ni kumtaka mke wa pili Rosemary.Sijui atampatia wapi sasa.Na uchungaji gani huu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...