MKUTANO WA WANAFUNZI WA TANZANIA WAISHIO NEW DELHI

Uongozi wa TASA - NEW DELHI, unapenda kuwatangazia wanachama wake wote, kuwa Jumamosi wiki hii kutakuwa na mkutano wa wanachama wote, Mkutano utakaofanyika nyumbani kwa BENARD RUTA,Maeneo ya JAIPUR karibu na Central Market, SAA kumi za jioni.

Mada zitakazozungumziwa ni pamoja na

- Salam kutoka kwa Mheshimiwa BALOZI KIJAZI.- Upitishwaji wa Katiba ya TASA.

-Maandalizi ya BONANZA la watanzania.

- Kuwakaribisha wanafunzi wapya.

- Na mengineyo.

Tafadhali anayepata taarifa hii amtaarifu na mwingine na yule asiyepafahamu awasiliane na BEN kwa Namba

9910232724.

WOTE MNAKARIBISHWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. "...nyumbani kwa BERNARD RUTA maeneo ya JAIPUR karibu na Central Market"

    Kwa hiyo twende "Central Market" tuanze kuuliza wahindi Bernard Ruta anakaa wapi? Watatwambia Bin who? Who the heck is that?

    Isitoshe shughuli official hazifanywi majumbani mwa watu. Anaweza kutumia influence ya wenyeji wake kuelekeza Katiba imtaje yeye Rais wa kudumu! Au inawezekana Bernard ananidai, au mimi namdai changu hataki kulipa, sitaki kwenda ku hang out kwake mida hii wala kumpigia piga simu. Heri tukutane hapo hapo "central market" ya JAIPUR kieleweke.

    "Kutakuwa na Mkutano Jumamosi wiki hii." Wiki hii wiki gani? Tangazo kwa Michuzi mi najua limebandikwa wiki gani hapa?

    Na tutaendaje kusikiliza "ujumbe wa balozi" at the top of the agenda, umekua ujumbe wa Nabii?

    Kama balozi ana care, angekuja mkutanoni akatoa nasaha akaondoka tukaendelea na yetu, kwani moja ya kazi za balozi si ndo hizi? Balozi hatambui kwamba anatuhitaji tumsaidie kuitangaza Tanzania, sisi wote hapa ni assistant ambassadors wake, lakini balozi Kijazi wala hana habari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...