KAKA MICHUZI,
POLE SANA KWA KAZI NGUMU YA KUTUPASHA HABARI ZA KILA SIKU NA KILA MARA. MIE KAKA NNA JAMBO AMBALO LINANITATIZA HASA KWA WATOTO WETU PALE SHULE YA MSINGI TEMEKE. PALE KUNA VITU VYA AJABU SANA WATOTO WANAVIONA NA KUVISIKIA KILA KUKICHA. WENGINE WANAZIMIA KABISAAAA.
INASEMEKANA KUNA VITU VYA KISHIRIKINA SASANAOMBA UIPOST HII INSHU KWENYE GLOBU YA JAMII ILIMRADI HATA MANYAUNYAU AJE KUTUSAIDIA JAMANI WATOTO WETU WANATESEKA KWA KWELI.
ABDALLAH
MDAU TEMEKE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Sasa si uwahamishie watoto wako shule nyingine?? Hujalazimishwa watoto wako waende hiyo shule

    ReplyDelete
  2. nilishaacha kutuma comment coz michu sijui huwa anatumia vigezo vipi kuchuja comment au post, mwanzoni nilihisi labda hataki mambo ya politics lkn si kweli hata comment au post za kijamii ni 50% 50% kutundikwa na nimeshamtega mara kadhaa kwa kutuma comment hasi na chanya huwa anaamua kuwa biased japokuwa si mara zote. naanza kuamini maneno ya wadau wa matawi ya chama ughaibuni, haiwezekani comment 20 zote ziwe na ukandiaji

    wengi huwa tunapenda kusoma comment kujua mawazo ya watu na wengine huwa ndio wahusika wakuu lkn wewe unaweka kapuni

    Wanaokutukana siwalaumu sana coz najua wanatumia akili na muda wao mwingi kuleta habari za maana wewe unawaweka kapuni,it's ok blog ni yako na wewe ndio mwenye maamuzi yote endelea kuleta post kama hii ni nzuri sana kwa uhai wa blog,,,itadumu...daima

    na kuna post muhimu ya kijamii kbs ya watoto mara kufungwa jela nimeona malalamishi ya mtumaji kwa michuzijr yeye kaweka wewe umeweka kapuni. IDUMU...

    hata hii usiweke lkn ujumbe umefika

    ReplyDelete
  3. Saidi MbondeSeptember 02, 2009

    HAKUNA CHOCHOTE, MIMI NIMESOMA HAPO MIAKA 7 NA SIJAONA WALA KUSIKIA MAMBO HAYO, WATU WANATISHANA NA KUTIANA HOFU, HICHO NDIO KINACHOTOKEA NOTHING ELSE.
    PUNGUZA USHIRIKINA DULLA

    ReplyDelete
  4. EBU NA WEWE ACHANA NA MAMBO YAKO YA KISHIRIKINA. UNAONEKANA UNAAMINI USHIRIKINA. KAMA KUNA WATOTO WANA UGUA INATAKIWA WAPELEKWE HOSPITAL. JINGINE WATAALAM WAJE KUCHUNGUZA HIYO SEHEMU KAMA KUNA CHEMICALS AU VITU VINGINE VINAVYO WADHURU HAO WATOTO.

    ReplyDelete
  5. salama kaka abdalla.
    jibu hapo ni maombi tu,
    ungekuwa mkristu ninge
    kushauri uombe kwa jina
    la yesu maana hatashindwa
    na hayo mauza uza.nakuachia
    uhuru wa dini yako ila mwenyezi
    mungu ataweka yote sawa kwa maombi.

    ReplyDelete
  6. tutsfika kweli kama tutakua na akili za kuamini ushirikina.

    ReplyDelete
  7. seeing is believing, Jamaa ameona nyie mna-mbishia, nendeni nanyi mkaone na ndipo muamini.

    Ni Hayo tu.

    ReplyDelete
  8. Wapo Wazee(Masheikhe) hapo Temeke toka Twariqatul Qadiria, wanaweza kuweka kikao hapo kufanya Ruqyah na Dhikr Mujarrabu hayo mambo yote yataondoka na kuteketea!Fanya mpango Bwana Abdallah uwasiliane na Masheikhe.Hiyo kazi ndogo sana.Iliwahi kutokea Mombasa wakaja wa-Jina la Yesu(kama alivyodai mmoja wa waosha vinywa hapo juu) wakachemka.Wakaja Maqadiria toka Makadara inshu ikasovika kilaini...!Gonga hapa uonehttp://www.youtube.com/watch?v=iVX2tpc5YRc&feature=related
    Polisi Mwitu

    ReplyDelete
  9. napenda kukupa shule kidogo mtoa mada. kwakweli pamoja na ukweli kwamba nguvu za giza zipo duniani na zinaathiri watu,lakini sio matukio yote ambayo wahusika huona au kusikia au kuhisi hali tofauti huwa yanasababishwa na nguvu za giza.
    kitaalam ni hivi:baadhi ya maeneo huwa yanakuwa na magnetic field(nguvu ya usumaku) kuliko maeneo mengine,na kutokana pia na mzunguko wa dunia kwa mwaka au kipindi fulani inatokea kuwa nguvu hiyo inakuwa kubwa sana ktk eneo husika. sasa binadamu wameumbika tofauti na wengine wanaweza kuathiriwa(nikimaanisha kuwa wanahisia za juu sana )kirahisi kuliko wengine,na pia inategemeana na hali ya afya ya muhusika,wengine wanakuwa na matatizo ya moyo ila siyo makubwa sana na hawajifahamu,nao pia inakuwa ni rahisi kuathirika na nguvu hiyo. sasa ikitokea mtu akawa ktk uelekeo wa nguvu hiyo kwa wakati muafaka na yeye anahisia za juu sana atahisi hali isiyo ya kawaida na hata anaweza kuanguka na kwakuwa kunakuwa na mvurugiko wa mzunguko wa damu hasa kwenda ktk ubongo,basi ni dhahiri mtu anaweza kuona maluweluwe kwakuwa ubongo unakuwa haufanyi kazi vizuri. sasa hilo likishatokea, wengine kwakuwa ni watoto na sio watoto tu,hupata hofu na kupata hali ya kuathirika inayoitwa hysteria,ktk hali hiyo nao wanaweza kuona vitu ambavyo kiuhalisi havipo ila nivya kufikirika tu. kwa mfano mtu anayetembea usiku na akahisi kunamtu anamfuata nyuma na anasikia kishindo chake mwenyewe anaweza kukimbia wakati kumbe hakuna kitu. au anaona kitu kwa mbali akiinama nacho kinaonekana kuinama lakini kumbe hakiinami ila ni kisiki tu!
    kwa misingi hiyo basi ukienda kwa mganga wa kienyeji hatakosa la kukuambia zaidi ya kukuchanganya na kula pesa yako,zaidi ya kukufanyia mazingaombwe na kukuwekea nguvu zake za giza kama anazo kisha anakuwa anakufanya kama roboti inayoendeshwa kwa remote control, anakuvuta akihitaji pesa unakwenda anakutibia na kupata mlo.
    ila kweli nguvu za giza zipo lakini sio mara zote!!!!

    mdau**********

    ReplyDelete
  10. a total waste of energy and time to believe such kokomanga stories.

    ReplyDelete
  11. Hao watoto wapimwe afya, inawezekana ni lishe duni au kemikali au ugonjwa mwingine tu unaosababisha akili kuruka kwa muda na kukumbwa na hallucination (samahani sijui kiswahili chake). Kwa maelezo zaidi tembelea link hizi: http://www.answers.com/topic/hallucination

    na

    http://en.wikipedia.org/wiki/Hallucination

    Please, hakuna cha majini wala mashetani, hivyo vitu havipo dunia hii jamani, tuachwe kudanganywa kijinga jinga hivi. Hao watoto watakuwa vichaa sasa hivi kama hamuwapeleki hospitali wakachunguzwe ni nini kinawafanya wawe hallucinated. Wabongo tuache longolongo, zingatieni elimu jamani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...