
Kampuni ya Bia Tanzania kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original inatangaza rasmi kuwa, ‘Redd’s Original’ itakuwa kinywaji rasmi cha shindano la kumtafuta mlimbwende wa Tanzania lijulikanalo kama Vodacom Miss Tanzania 2009 linalotegemea kufanyika mapema mwezi Octoba.
Akizungumza kwa niaba ya TBL katika ukumbi wa Savannah Lounge, Meneja wa kinywaji cha Redd’s Original, Bi Kabula Nshimo alisema, “Ninafuraha kutangaza kuwa Redd’s Original ambacho ni kinywaji cha kimataifa ndio kitakuwa kinywaji rasmi cha shindano hilo na kwamba tutaweza kujitangaza zaidi katika tasnia ya urembo Tanzania ’’ Bi Kabula aliongeza kuwa kwa zaidi ya miaka minne sasa Redd’s Original imekuwa ikidhamini shindano hili la urembo.
Tofauti na fikira za hivi karibuni kuhusiana na Redd’s kujitoa katika udhamini wa Miss Tanzania, kinywaji hiki kimekuwa kikidhamini shindalo hili kuanzia ngazi za chini hadi ngazi za kanda na kimekuwa mdhamini mkuu wa kanda za Dar es Salaam, Ilala, Kinondoni na Temeke.
Aidha, mwaka huu Redd’s Original inashirikiana na Blogu ya Issa Michuzi kwa kudhamini shindano la Miss Photogenic ambalo ni moja ya mashindano mengine madogo ndani ya shindano hili la kitaifa la ulimbwende.
Vikiwa vinathibitishwa na Bodi ya Viwango ya Miss Tanzania, vigezo vitakavyozingatiwa katika shindano hili la Miss Photogenic ni sura yenye haiba, mpangilio mzuri wa meno, siha yenye kufurahisha, ngozi laini na angavu na uwezo wa kujieleza.
Mshindi atapokea zawadi ya pesa taslimu ila hatokuwa na nafasi yeyote ya kushika ya ubalozi wa Redd’s. pamoja na kuzawadiwa, mshindi pia atatengenezewa kabrasha la picha zake ambalo anaweza kulitumia endapo ataamua kujiendeleza katika fani ya uanamitindo.
Akitoa maoni yake juu ya udhamini huu, Mkurugenzi Mkuu wa Lino Agency, Hashim Lundenga alisema,“Kila mwaka tunajionea maendeleo katika shindano hili la Miss Tanzania na mwaka huu tunayo furaha kubwa kabisa kushirikiana na kinywaji cha Redd’s katika kulifanya liwe bora na kubwa zaidi. Wasichana wote ni wazuri wa sura na wachangamfu vilivyo.
Katika kushirikiana kuwasaidia katika fani yao ya urembo, mimi pamoja na kinywaji cha Redd’s Original tunayo hamasa kubwa juu ya shindano hili na tunaamini kuwa tutakuwa tumecheza nafasi kubwa katika kumsaidia mmoja wa warembo hawa kwa kumpa fursa ya kufanikisha ndoto yao.”
Kwa mwaka huu Redd’s Original imetumia zaidi ya Shilingi Milioni 200 kwenye mashindano haya ya Vodacom Miss Tanzania 2009 kwenye mashindano ya vitongoji, kanda mpaka fainali.
Umaarufu wa shindano la kutafuta mlimbwende wa Tanzania umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka tangu lilipoanza rasmi mnamo mwaka 1996 na Redd’s Original imekuwa mstari wa mbele katika kudhamini shughuli mbalimbali zinazohusiana na urembo likiwemo shindano hili.
Redd’s pia imekuwa ikijihusisha na maonyesho ya mitindo yanayosaidia kukuza wabunifu chipukizi na waliobobea wa mitindo nchini na wengi wa wanamitindo wa maonyesho haya wameshiriki katika shindano la Miss Tanzania na wamepata mafanikio makubwa katika fani hii ya urembo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...