Kaka Michuzi pole kwa kazi!
Mimi ni kijana wa umri wa miaka 35,nna mpenzi wangu ambaye ameachika mara mbili,yaani ameshaolewa mara mbili na kuachwa.Hivi sasa nnae mimi natarajia pia kumuowa,mimi nnae mke,pindi nikibahatika kumuowa atakua mke wa pili au mke mdogo.Jambo linaloniumiza kichwa ni kwamba hajatulia,yaani ana wanaume wengine nje.
Mara ya mwanzo tulipokutana alinambia yeye ameachika na muda huu hana mwanaume yeyote,nilimuamini kwani ilikua naenda nyumbani kwani bila ya wasiwasi wala woga.Kwa muda wote huo sikuona ishara yoyote mbaya ilikua ananipa penzi motomto.
Baada ya kupita kama kipindi cha mwezi mmoja niliona mabadiliko,mpaka akanambia nikitaka kuonana na yeye nisifika nyumbani kwake kwani wako mama zake wadogo kwa hiyo ilikua tunakutana mbali kidogo na yeye,hata ile tabia ya kunipigia simu kila mara ilikatika kabisa na nikimpigia mimi ilikua hapokei au anakata kabisa inaweza hata zikapita siku mbili hatujawasiliana.
Pindi akiwa na safari zake ndo ananipigia nende nikampakie kwenye gari langu nimpeleke,nilijaribu kumdadisi kwa nini amebadilika,alinambia ameamua tu nanisiwe na shaka kwani yeye bado ananipenda kwa udhati wa moyo wake.
Hali ilizidi kunitia wasiwasi nikaamua kupeleleza ndipo nilipogundua kwamba kumbe kaja bwana wake ambae anaishi UK.Niliumia sana lakini ilibidi nivumilie nilijua iko siku ataondoka tu na nitamueleza duku duku langu.
Siku moja akaniaga kua anakwenda Kenya kwa ajili ya kuwasindikiza mama zake wadogo ambao wanatoka UK wamekuja Zanzibar kwa msiba,Nilimkubalia kwani huko nyuma aliniaga anakwenda Kenya kwa matibabu kumbe ilikua ndio amekwenda kumpokea huyo bwana wake wa UK na pesa ya nauli na matibabu nilimpatia.
Siku ilipofika aliondoka na kuwasindikiza wageni lakini nilijua kika kitu kwamba anamsindikiza huyo bwana wake,ruhusa nikatoa.Alikaa kwa kipindi cha wiki moja Kenya baadae akarejea Zanzibar nilikwenda kumpokea bandarini nikamrejesha nyumbani kwani,lakini kwa kipindi chote hicho hakufahamu kwamba mimi naelewa kila kitu kuhusu yeye..
Zikapita siku mbili ndipo nilipoamua kumueleza kila kitu mwanzo alikataa baadae akakiri kua ni kweli akaomba msamaha nikamsamehe kwa vile ilikua bado nampenda.Tuliendelea kuishi vizuri baada ya kupita mda kama wiki tatu akaniaga tena kua anakwenda tena Kenya kwa ajili ya kumtafutia mdogo wake chuo niliingiwa na wasiwasi kidogo ingawa nilimruhusu baadae nikagundua kua sio kweli.
Niliamua kufanya utafiti wangu tena baada ya kurejea Zanzibar ndipo nilipogungua kwamba ana mwanamme mwengine huko kenya ambae ni kigogo wa KRA.Kama kawaida yake alikataa.Siku moja niliamua kuchukua cm yake nikaona msg za mapenzi kutoka Kenya,moyo uliniuma sana kwa huna moyo huwezi hata kumaliza kusoma msg moja.
Nilimuonesha msg zake akanambia kua huyo jamaa yeye hana mahusiano nae kimapenzi ila amamdanganya tu kwa vile alimuahidi kumtafutia kazi,isitoshe huyo ni kaka wa shoga yake kwa hiyo na yeye ni kama kaka yake.
Na hivi sasa huyu kigogo wameagana anakuja Zanzibar karibuni ingawa yeye ananificha lakini nimeona msg kwenye cm yake ingawa yeye hajui kama mimi najua.Mpaka hivi sasa bado wanaendelea kutumiana msg za mapenzi na huyu bibie kila siku safari za Kenya hazimwishi.
Kaka michuzi naomba wadau wanishauri nifanyeje na mimi bado huyu dada nampenda.
Ahsante,
Mdau Zanzibar


mh!~umri huo unataka nyumba ndogo? si bure umerogwa wewe!
ReplyDeleteyaghe huyu malaya mpige chini atakupa ukimwi hafai hata kidogo ndo sababu kaachika ati hio sumu babake
ReplyDeleteDuh, una miaka 35 na mke juu, halafu jinga namna hiyo??? Hahahha, unaomba ushauri vitu obvious wewe jinga la kutupwa??
ReplyDeleteyou better call it quits, the chick will kill you with the latest desease. too many partners. WATCH OUT!
ReplyDeleteSIKILIZA BWANA, KUNA WASICHANA WENGINE WANA SURA YA BINADAMU LAKINI NI MASHETANI.UELEWE HIVYO.MAJIBU UNAYO MWENYEWE KWA HISTORIA YA MAISHA YAKE, ulimkuta kaachika, na sasa anaendelea na mambo ambayo yanaonyesha kuwa ndiyo yanayo mfanya wanaume wamuache, na wewe pia utamuacha.Majibu unayo mwenyewe kutokana na vituko anavyokufanyia.Hajawa mke wako bado, na anakufanyia hayo na bado unajiuliza watu wakusaidie uamuzi.Bwana mpende akupendaye asiyekupenda achana naye.Utapoteza muda wako bure na utampoteza na huyo uliye naye. Ningeshauri ukae na huyo mmoja tu kwa ndoa za kikristu.MMOJA huwa ni ngumu, ukielewana naye unashukuru mungu, sasa wewe unataka wa pili wa nini?
ReplyDeleteNaitisha mgomo wa comments kwa huyu jamaa manake hana jipya zaidi ya kuanika ulofa wake.Wadau tumkaukie.
ReplyDeleteWewe unapenda bado kuishi? Utaondoka sasa hivi ohoooo, achana na huyo kicheche.
ReplyDeleteMkubwa hapo hamna mapenzi ya kweli na hata kama ni uvumilivu basi wewe ni field marshal, hapo unachosubiri ni kupata maradhi yasiyo na tiba ujifie ACHANA NAYE
ReplyDeleteHii imenifurahisha sana, siwezi amini nimeisoma habari yote ya jamaa mpaka mwisho. Ushauri... acha ujinga - endelea na maisha yako!!! Mdau Geneva
ReplyDeleteunaambiwa usiikurumie zinaa sasa wewe zinaa imekunogea utakoma kuringa.
ReplyDeletemtie pilipili huko chini ili atulie maana anawashwa atii
WEWE NI BUZI WAKE MDOGO MDOGO TU UMESHINDWA KUTURIA NA MKEO SASA WA HANGAIKA UTAKOMA
ReplyDeleteNYINYI MNAOTAKA NIMUACHE MMEIONA SURA YAKE??????
ReplyDeleteJE SAUTI YAKE MMEISIKIA????
KAMA KUFA BASI NIACHENI ANIUE NI MZURI ANTI
Watu ambao hawajatulia kama wewe ndo wanaosambaza ukimwi kila kukicha Tanzania. Una mke tayari, mwingine wa nini? Huyo uliye naye hakutoshi? Tafuta shughuli za kufanya muda wako wa ziada mbali na kupepeta pepeta nanihhii yako kwa wanawake! Nenda michezoni, nenda kimbia, hata anzisha vibustani vya mboga vitakusaidia nyumbani na familia yako.
ReplyDeleteTulia mwanaume, jilinde na ulinde familia yako, wewe mwenyewe umeshashuhudia watu wanavyopuputika mmoja baada ya mwingine, au wewe ni mmoja wa wale wanaojidanganya kifo cha wengi harusi? Kama hujui hakuna cha harusi, na usituchoshe na watoto yatima mitaani. Ukome kabisa na ushindwe!!!
Mwee umeniudhi!!!
Ushauri gani unaoutaka wakati tayari majibu unayo?mke wa pili wa nini yakhe zaidi ya kuongeza matatizo.Au unafata mapenzi?inaonyesha umeshapigwa juju na huyo mwanamke. kwani umeshajua ana wanaume wengine bado tu unamngangania.ukisikia zoba basi ndio wewe.
ReplyDeleteMICHU HUYU BWANA KAOMBA MWENYEWE USHAURI, HUTOMTENDEA HAKI KAMA UTABANIA MAONI YA MTU.
ReplyDeleteMAONI YANGU NI KWAMBA ILI NA WEWE UMKOMOE BASI TAFUTA BWANA NA WEWE AKUOE
Unauliza wapi mbuzi anaendea haja kubwa wakati mkia unauona? pole!
ReplyDeletekaka, poa na mke wako kwani yeye ana miaka mingapi?? mie naishi huku (UK) na bibi wa nguvu Bongo
ReplyDeletenaona watu wanaipiga mabao kwa nguvu zaho lakini nampenda sana nimekubali, tuambiane isiwe ni bibi wangu na nilikuwa TZ karibuni kila la kheri.
HIVI WEWE MDAU WA ZENJI UNATAKA UFANYIWE NINI NDIYO UJUWE KUWA HICHO NI KIMEO ? KWA MAELEZO YAKO TU HAIITAJI KUJIULIZA MARA 2,CHAGUA 1 EITHER UKICHUKUE HICHO KIMEO CHAKO KILICHOKUBUHU AU UKITUMIE LAKINI UKIJUA UKO NA WABIA KIBAO, NAJUA UMEPENDA KWA SAAANA HIVYO SIWEZI KUKUSHAURI UKIACHE HICHIO KIMEO INGAWA NINGEKUWA MIMI UAMUZI UKO WAZI, ILA PIA SIWEZI KUJUA SANA MAANA MTU MZIMA KAMA WEWE KUNG`ANG`ANIA KIMEO SIWEZI KUJUA UNAPEWA NINI UKIZINGATIA HIYO NI ZENJI, BUT PANGA PANGUA VIRUSI HAPO HAVIKOSEKANI NA KAMA HAVIPO BASI VINAKUJA !!! POLE SANA NDUGU YANGU, MAANA MTU KATOKA U.K NA MWINGINE KATOKA KENYA TENA KRA ! LAZIMA KUNA MAMBO HUYO DADA ANAYO AU ANATOA YANAYOWACHANGANYA NINYI WOTE WATATU NA WENGINE AMBAO HUKUWATAJA, POLE SANA SANA NDUGU YANGU ILA USIMSAHAU MKEO KWA HAYO MAMBO YA HUYO MTAALAM WA MAPENZI, BYE BABAA !!!
ReplyDeletewewe una umri wa miaka 35 una mke na kwa dunia ya sasa achilia mbali kwamba huenda dini yako inaruhusu kuoa zaidi ya mke mmoja,lakini una shangaza kweli yaani huoni maisha yasikuhizi kwanza ni hatari kuwa na ndoa zaidi ya moja,na pili unategemea utazaa watoto wangapi na utaweza kuwapa maisha ya quality inayostahili kwa sasa?kwa ufupi wewe ni kijana lakini unamawazo ya kijima na ume dumaa!!!huna muelekeo na kama tanzania itaendelea kuwa na watu wenye mtizamo wa maisha kama wewe nchi itazidi kuwa maskini maana una macho unaona lakini hunauwezo wa kutambua,nakushauri utafute watu wa kukufundisha maisha maana hujui hata unachohitaji maishani kwa sasa.
ReplyDeletefocus kwa mkeo uliye naye na kama una watoto watengenezee mipango ya maisha ilikama itatokea bahati mbaya hauko hai unawaacha wakiwa na msingi wa maisha bora.nawachukia watu wenye kuongea utumbo kama wewe kwa dunia ya sasa ,na ungekuwa karibu yangu ukaongea kinyesi hiki ningekupinga ngumi ya mdomo ubaki na diastema kama la ng'ombe,na ungezimia ukizinduka unaamka na akili mpya ya kisasa.kama una watoto wanadhani wana baba basi wameula wa chuya maana ni useless father hatakama una vijipesa visikupe kiburi chodo wee!
wewe unamuendea kinyume mke wako, jee huyo mke wako akielewa kama unamundea kinyume atafurahi. Huyo malaya wako anatembea na wanaume wengine umeona wivu. mimi nakushauri utulie na mke wako , pia ukapime ukimwi.
ReplyDeletesiamini kama naandika hapo kwa ulichopost..kama unataka kuishi KIMBIA HARAKA SANA NA USIANGALIE NYUMA!
ReplyDeleteunaona hivi hivi maji yana sumu, halafu unauliza eti ninywe au nisinywe! unatuchezea akili zetu sio! kunywa sasa, ndo ushauri wangu, ufilie mbali, maana roho ya kufa utaijua tuu! ahh, watu wengine bwana!
ReplyDeletenana
czech rep
Mh! My friend kula kona, Wanawake kibao, isitoshe wanatamani kuolewa vile vile wanatabia nzuri.
ReplyDeleteIla pia nashangaa una wake wawili inaonyesha huyo mwingine katulia kwa nini usibaki nae alie tulia?
Mimi binafsi nilishawahi kupata tatizo dogo kama lako nikamkimbia msichana mapepe akanipigia simu we mpaka akachoka, na nikampata msichna mwingine amabye sio mzuri wa sura ila tabia imetulia sio Malaya nimemwoa na mambo mswano kwenda mbele nafanya kazi vizuri, makampuni yangu mawili, kabiashara ka mafuta, mke katulia.
Achana na mademu mapepe watakupoteza, mawazo yao sio maendeleo bali kukutumia kwa sana na ukiishiwa watakukimbia,
demu mzuri ni yule mnaanza nae kwenye shida mpaka kwenye raha.
Thanks.
Nyie wote mafala - wewe na malaya wako. Wewe una mke halafu unazini. Na huyo mwenzio kazi yake kuhesabu vichwa. Wewe na huyo malaya mnastahili UKIMWI lkn bi mkubwa na watoto utawaingiza katika matatizo wasiyostahili.
ReplyDeleteHII SI MADA YA KUJADILIWA NA JAMII NZIMA BALI JAMII INAYOKUBALIANA NA MITALA KAMA WAISLAMU NA WAPAGANI/JADI.
ReplyDeleteMAANA KOMENTI HASI NA UOSHA VINYWA VINAHISIWA KUTOKA UPANDE UPI KWA KUUMIZA IMANI ZA WASIO WAVUMILIVU.
SIKU NYENGINE FIKIRIA HILO KABLA YA KUPOSTI AU NENDA MSIKITINI.
USHAURI WA NINI TENA HUMU, WAKATI MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA...
ReplyDeleteHUYU JAMAA ANAHITAJI KUPELEKWA KWA MSHAURI NASAHA ILI APIMWE VVU KWANZA KABLA YA YOTE.PIA INAWEZEKANA YAKHE ANA MICHEZO MICHAFU NDO MANA ANAMGANDA HUYO MZINZI MWENZIYE.LET'S BE SERIOUS SOMETIMES BWANA!THIS IS STUPID FOR A MAN OF 35YRS JAMANI!TENA MARRIED, HAMTENDEI HAKI MKEWE!KWA MGANDO HUO WA MAWAZO JAMAA ANAWADHALILISHA WAZENJ WENZIE ATII.
ReplyDeleteunampendea nini mtu kama huyo??isijekuwa una mambo ya kizenj kwa huyo mzinzi mwenzio halafu unatuzuga.inawezekana mnafanana tabia, subirini NGOMA mtuachie dunia yetu kwa amani.
ReplyDeleteTatizo unalo wewe ndugu yangu. Umesema una mke. Halafu huyo mwanamke unayetaka kumwoa anakupa penzi motomoto. Ina maana unamwibia bi mkubwa maana bado hujafunga ndoa na huyu anayekupelekesha. Kwa ufupi hakuna tofauti kati yako na huyo mwanamke anayekupeleka mbio. Unavyojisikia ndivyo mkeo anavyojisikia. Nenda katubu kwa mkeo utulie naye.
ReplyDeleteWeeeeeee utakufa na ukimwi wewe, huu ni ujinga wa mtanzania, usifikiri kuwa na wake wengi ni sifa nyakati hizi za gonjwa hili la ukimwi, mke mmoja anakutosha wewe acha tabia hii chafu imepitwa na wakati unatakiwa kuelimika wewe kijana mdogo wa miaka 35 utakufa wewe kabla ya wakati wako!
ReplyDeletewewe unampenda lakini wewe hakupendi huyo.Pia inawezekana nawewe ni ktk kundi hilo.
ReplyDeleteSASA WEWE UNATAKA USHAURI GANI MTU MZIMA UMESHAO ,UMESHAPITIA MAMBO MENGI.ANYWAY INAONEKANA ANVYOWATUMIA HAO WANAUME WENGINE NA WEWE ANAKUTUMIA TUUU
ReplyDeletehili jamaa fala kweli, yaani zuzu kuliko niliowahi kusikia duniani, kah!
ReplyDeleteSeriouslyyyyyyyyyy? Are u for real? cumon man! Una mke bado wahangaika na huyo mwanamke kicheche utadhani umeambiwa sijui mwali hajaguswa.You should know better than that .Inawezekana una enjoy second hand goods eeh?
ReplyDelete..nafikiri wa-kongo(zaire) wana jina la mtu aina yako: 'zoba'..sijui ni maana moja na kinyamwezi: 'kazoba' ama 'kadata'..poooleeee, mwakwetu!..
ReplyDeleteYaani Michuzi kama kungekuwa na zawadi ya majitu majinga (ashakum si matusi), basi huyu jamaa angeitwa. Yani sikuamini nimesoma mpaka mwisho, halafu anamalizia na signature phrase "na bado nampenda". kweli duniani kuna watu wanaofikiri, na wengine wanasindikiza wenzao kufikiri. Nimemaliza.
ReplyDeletekama duniani kuna mabwege basi ww namba moja kaka..........
ReplyDeleteWEWE MUULIZA SWALI NIMEKUPELEKEA HILI SWALI LAKO KWENYE WEBSITE YA HARUSI YANGU ILI WAMAMA WAKUCHAMBUE KISAWASAWA MAANA WAMAMA KWENYE HIYO WEBSITE HAWATAKI USHENZI, WANAWEZA WAKAKUVUA NGUO JAPO NI MTANDAONI.
ReplyDeleteAcha upumbavu wewe! una mke tayari, tulia na mke wako ndani,utakufa na utamuua huyo mkeo ukiendelea na huyo malaya wako, kwanza kapime ukumwi au unao tayari nini? ndio maana hutaki kumuacha?
ReplyDeleteWacha akucheze...You deserve it. Mke wa pili...mnaweka huku habari za wake wa pili....jamani Tanzania bado kama commodities vile...Inasikitisha sana...
ReplyDeleteNa wewe michuzi tutatia mgomo wanawake kusoma blog yako....unatembea kila siku nchi za nje wala huelimiki...
bradha mithupu hii ngoma umeitengeneza mwenyewe ili uchangamshe wadau. good job!!!!!!
ReplyDeleteJE MFUPA ULIOMSHINDA FISI WEWE UTAWEZAJE KUULA?mdau usa
ReplyDeletekwa kuwa imani yetu inaruhusu kuoa wake 4 mimi nashayri muoe tu kama hataacha ujinga wake mpe talaka yake kama mtume wetu alivyotufundisha ok
ReplyDeleteWewe ni shetani na unasubiri kufa, pambaf
ReplyDeletewewe chiziiiiiiiiii.....utaukwaa umeme.....
ReplyDeleteBWEGE MKUBWA TOA UZOBA WAKO UNAKUWA KAMA MGENI WA MAPENZI!!SAFI SANA DADA ENDELEA NA UKICHECHE UMLETEE NA LILE GONJWA KUBWA YANI NDUGU
ReplyDeleteMhhhhhh siamini kweli kama bado kuna kubwa jinga, miaka 35! Duuuuuu pole inaonekana kichwani hamna kitu
ReplyDeleteKwanza kapime afya yako na mke wako kama mmeshaathirika na UKIMWI au laa,namsikitikia sana mkeo wa kwanza kama atakua ametulia utakua umemletea balaa manake hana hatia.Ushauri ni uachane na huyo kicheche na ukome.
ReplyDeletehivi wewe una akili kweli? hapo uanomba ushauri watu wakuambie nini sasa wakati majibu unayo? MIMI NINACHOKUAMBIA, UNAYOMFANYIA MKEO NDIYO HAYO YANAKURUDIA NA KAMA HUJUI MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI, ANGALIA TU USIJE UKAMUUA MKEO NA HUO UBWEGE WAKO.
ReplyDeletehivi wewe una akili kweli? hapo uanomba ushauri watu wakuambie nini sasa wakati majibu unayo? MIMI NINACHOKUAMBIA, UNAYOMFANYIA MKEO NDIYO HAYO YANAKURUDIA NA KAMA HUJUI MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI, ANGALIA TU USIJE UKAMUUA MKEO NA HUO UBWEGE WAKO.
ReplyDeletehivi wewe una akili kweli? hapo uanomba ushauri watu wakuambie nini sasa wakati majibu unayo? MIMI NINACHOKUAMBIA, UNAYOMFANYIA MKEO NDIYO HAYO YANAKURUDIA NA KAMA HUJUI MALIPO NI HAPAHAPA DUNIANI, ANGALIA TU USIJE UKAMUUA MKEO NA HUO UBWEGE WAKO.
ReplyDeleteJamani wadau sio kila topc 2changie 2taonekana wote wehu,cha msiingi kama anony 06:54;pm hapo juu alivyosema,TUMGOMEENIkwn hawa nda waoeneza ukimwi TZ
ReplyDeleteKaka yangu Mrudie mke wako mpigie magoti hiyo ni laana kutoka kwa mkeo nakuhakikishia...acha kuhangaika ishi na mkeo kwa amani... AMA KWELI DUNIA INA MAMBO YANI HAUONI SOME THING IS WRONG WITH YOUR HEAD!!!!!
ReplyDeleteJAMANI MMEONA JAMAA AMEJIBU HAPO KATIKATI KUWA "MNATAKA NIMUACHE MMEONA SURA YAKE? NI MZURI..." .. KWELI JAMAA NADHANI KALISHWA LIMBWATA HAFIKIRI VIZURI.. YAANI UZURI NDIYO UKUSABABISHE UFE KIJINGA?
ReplyDeletePIA KUNA JAMAA ALIYESEMA KUWA MADA HII IJADILIWE NA WANAOKUBALI MITALA.. KWA ISSUE HII HAPA HATA JAMII INAYOKUBALI MITALA HAIWEZI KUKUBALI UWE NA MWANAMKE MALAYA..
MI NAOMUOMBEA JAMAA YAMKUTE ANAYOYATAKA...
kaka michu, huyu jamaa hajui matumizi ya hii globu. aeleweshwe vizuri ni ya kutoa ushauri wa maana kwa watu wa maana, na wanaojua maana ya maisha na maendeleo, si kwa watu wanaotaka ku-promote ufuska na UKIMWI!Hatujali sura,wala sauti...Tabia ni muhimu zaidi. Mtu una mke unahangaika na malaya wa nini? Unataka kuacha wanao yatima jamani? Kutokana na tabia kama hizi kuna sababu ya dini zetu kufanya review ya kuhusu mambo ya kuoa,oa ovyo.
ReplyDeletewewe ni full mdebwedo ndo walewale mguu pande mguu rejesha
ReplyDeleteby the way kunguru hafugiki
PUMBAVU WE! UNADHANI HAO WALIOMUACHA WALIKUWA WAJINGA? USITULETEE UJINGA WAKO HAPA! PUMBAVU ZAKO!
ReplyDeletebadala ukajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura wewe umekaria vicheche tu ndio nyie badae munaleta fujo, acha zinaa.
ReplyDeleteKAMA HIZO FINDINGS ZA 'UCHUNGUZI' ULIOFANYA NI ZA KWELI, MAJIBU UNAYO MWENYEWE... ACHA KUPOTEZEA WATU MUDA KWA KUOMBA USHAURI KWA SWALA AMBALO LIKO OBVIOUS..ACHA UJINGA, HILO JIKE LITAMPELEKEA NGOMA MKEO
ReplyDeletemdau chiggs, deslam
NYINYI MNAOTAKA NIMUACHE MMEIONA SURA YAKE??????
ReplyDeleteJE SAUTI YAKE MMEISIKIA????
KAMA KUFA BASI NIACHENI ANIUE NI MZURI ANTI
WED;SEP 30.07.24PM
Kaka michuzi ili blog yetu iweze kuheshimika nakuomba tena sana Ujinga wa namna hii usiwe unapost plz. Huyu jamaa anatuchora au kutupima akili sisi wachangiaji wa mada. umeona maneno yake hapo juu. Eti nimuache umeona sura yake; sauti yake ni mzuri. sikuachi muache aniuwe. Sasa kama anajajua yote na anamaamudhi kama mtu mzima 35 age. Si anatuchora;ushauri gani? Anataka kwetu kama sio matusi anataka. Eti anamke tayari halafu anataka mwingine aliyaachika mara mbili na bado anafanyiwa vituko live akiona ,jibu bado nampenda ;Sikalogwa huyu au kama hajalogwa anatochora tukitoa comments anacheka. Mie ukijakwangu kuomba ushauri na maelezo kama hayo uliyotoa juu nakupiga tena sana .na matusi juu ; Kutufanya wajinga kamuombe ushauri Mama yake.Msenge wee
Hahahaha!! This is real crazy. Man I wish I could get a chance of meeting you. Majibu unayo mwenyewe.
ReplyDeletendugu yangu huyo malaya achana nae atakuja kukupa msiba mkubwa katika familya yako kumbuka wewe una mke na watoto sasa unatafuta nini kwa huyo shangingi kama unataka mke wa pili hapo zanzibar wapo mabinti wazuri wenye heshima zao
ReplyDeletewewe acha ujinga huo una mke tayari halafu unaenda kuzini nje unasema mnampenda huyo malaya sasa kwanza nenda kapime ukimwi tena tafadhali usije ukamuua mtoto wawatu mkeo umemkosea sana kwa huyo mayala miaka 35 bado una ujinga kichwa tele usituletee ujinga wako goja utaona karibu
ReplyDeleteNibebeeeshe Nibebeeeeeshe Nibebeeeshe UKimwi nihangaike nao !!
ReplyDeleteYaani hapa VICTIM ni MKE Wako wa Ndoa alietulia NDani wewe unahangaika na Viruka njia zobe wee na Tafadhali naomba uwe ulikuwa unatumia condom na huyo mke wako wakati unafanya huu uasherati wako na kabla hujamuingilia bila ya soksi pls huyo dada wa watu NENDA UKAPIME !!! MUASHERATI , BUZI na ZOBE MAKUBWA weee !!
............Sasa unamchunguzia nini trip zake za kenya n.k. na wakati umeshasema utamwoa, na kama ni kufa tukuache ufe tu.......KUFA hata leo,...nyama, kenge mkubwa wewe, malaya wa kiume, tunaomba sheria ya kukatwa nyeti hadharani kwa wanaume fuska kama wewe....mnaoona hatari na kuikimbilia. Hufai hata kupewa kitambulisho cha m-zanzibar mkaazi wewe!!!
ReplyDeletebooss kimeo hicho achan nacho,tulia na mkeo,kama hakurihishi basi mwambie mkeo kuwa aongeze ujuzi,ila ila hicho kimeo kitakuua tena kinasafirisha hadi kenya du?huyo kiboko,then anakurudishia ungonga tena,then anakipeleka tena nairobi,na jamaa nae kanogewa nairobi nae anakifuata huko huko zanzibar dah,kimeo kinaonekana kitau kweli kweli..
ReplyDeleteJAMANI JUENI PENZI NI KIFO JAMAA HAPO LZIMA AFE,..LAKINI MIMI NAMSHANGAA MBONA WA AFRIKA JINSI TULIVYO TUNAWIVU AMBAYO HUWEZI KUJUA MPENZI WANGU ANATEMBEA NA MTU MWINGINE ETI BADO UNAENDEREA KUWASILIANA NAE TUU.yAANI HAPO NDO PALE WANASEMA PENZI LINAUWA,HAPO JAMAA NAHISI MPAKA SASA SIO MZIMA,MAANA HUYO MWANAMKE YAWEZEKENA KUNA WENGINE HAPO BONGO USIOWAJUA.WEWE UNAENDEKEZA KUNOGEWA TUU,,HAYO YOOTE UTAYAKUMBUKA UKIWA UNAKOLOMEA NDANI YA SHUKA PALE MUHIMBILI.KINACHOUMIZA NI BIMKUBWA AMBAE NAYE ATARETEWA AU AMERETEWA BILA YEYE KUTAFUTA.hAPO BONGO AU HUKO AFRIKA NI VIGUMU KURARA NA MWANAMKE ZAIDI YA 1, 2, 3,4 UKIWA BADO HUJAPATA ZILE NYAYA ZA UMEME.kWA UFUPI HUNA AKILI NDANI YA HILO LIFURUSHI.
ReplyDeleteSASA KAKA UNACHO NG'ANG'ANIA NINI?UYO KWANI UMEZALIWA NAE AU UMEMTOA BIKRA WEWE AU WEWE NDO AMEKUTO A BIKRA?MBONA UNATAKA USHAURI NA USHAURI UNAO MWENYEWE????????CHAPA MWENDO WANAWAKE WAPO WENGI.ZAIDI YA YOTE UNAJICHIMBIA KABURI MDAU.
ReplyDeleteKAKA GABEY.
Bro Michuzi huyu jamaa asitupotezee muda. Akili yake inaonekana ina maji kama si bangi. Yaani unakuwa bwege halafu unawaeleza watu wengine kuwa wewe ni taahira?? shenz type, pumbaf, mkojo wewe.
ReplyDeleteYakhe atakutoa roho huyo....pengine anataka kuliwa ugonjwa na wewe ni ustaadh huli nyama ....heheee u made ma day bro!
ReplyDeleteWadau na watu wenye busara,msishangae bado tunao watu wengi wa aina hii katika jamii yetu.washaurini lakini mjue kuwa jamii pia ina watu wanayoiona dunia differently.we exteremely perceive this world differently.hata si kweli haya lakini tujue wapo watu wa aina hii.
ReplyDeletehuyo malaya wa kesha namjua fika yeye kabila lake ni mkamba,yaani jamaa ni hatari kwa watoto wa watu anawarubuni eti atawatafutia kazi kumbe haja yake awafunue tu,kwa vile anaringia chapaa yake.hata wake za rafiki zake yeye anachukua tu,kuna kipindi hata watu walimvumishia kwamba ana ukimwi,hivi sasa ana maskendo kibao na hwenda kibaki akamfukuza kazi kwani kaibia sana serikali yetu
ReplyDeleteBwana michuzi huyu jamaa ametupotezea muda wetu maana ametoa maelezo marefu ambayo hayana hata mantiki yoyote. Ushauri wangu kwako michuzi jaribu kusoma kwa makini mada wanazokutumia kwa ajili ya kuweka kwenye Blog yako. la sivyo utaichafua blog yako ambayo inatupa habari makini.
ReplyDeleteHuoni kichefuchefu wewe? unajua huyo kicheche wako anavyogawa nawe unaingiza kichwa chako hapo hapo! Naona kichefuchefu mie. Uzuri wa mtu sio sura ni Tabia.
ReplyDeleteKWANZA NAANZA NA WEWE MICHUZI,HII UMETOA TUSOME ZETU TUKITUMA UNACHUNA,HUYU MJINGA NA HATA WEWE MWENYEWE KUTOA HII NI UPUUZI,HUYU PUMBAVU ANTAKA USHAULI GANI???KESHAJUA MKE ANAMABASHA KIBAO...SIKUSOMA UPUUZI WOTE SEMA HADI UTUMIWE VIJISENTI NDIYO UNATOA HABARI NINI...CIOA.
ReplyDeleteUshauri wa nini wakati wewe mwenyewe kiruka njia. Mola amsitiri mke wako kama unaye na maradhi.
ReplyDeleteUshauri Mzuri mi nakushauri ukamuulize mke wako,nafikiri atakujibu vizuri kabisa!!'Kila la kheri.
ReplyDelete