
HAYATI MARY J. MWAIBULA
Familia ya Mary J. Mwaibula inasikitika kutangaza kifo cha Mama yao mpendwa Mary J. Mwaibula (Mama Gladys) kilichotokea tarehe 30/8/2009 katika hospitali ya Hindu Mandal dar-es-salaam baada ya kuugua akiwa nchini Marekani.
Ibada ya kumuombea marehemu itafanyika kesho Alhamis tarehe 3/9/2009 saa nane mchana katika kanisa la Lutheran (KKKT-usharika wa Kijitonyama) ikiambatana na kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu.
Mazishi yatafanyika siku hiyohiyo ya
alhamisi saa 10 jioni katika makaburi ya Kinondoni.
Mola ailaze Roho yake mahali pema peponi
AMINA
Pole kwa wote waliofiwa,kaka michu tafadhali jaribu kupata details zaidi,Mzee MAJI amefariki jioni hii,Tumaini hospital,anaishi Mbezi beach,yule aliyewahi kuwa mkuu jeshi la polisi DSM,enzi za Mzee Ruksa,na waziri wa mambo ya ndani -Mrema
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi. kKwa wale akina dada (sasa hivi mama) waliosoma Meta Girls school, huyu ni yule yule Mary Mwaibula mliyesoma naye miaka ya 1970, 1971;jamani tumuombee mwenzetu katutangulia.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa wote. Gladys Pole sana dadangu. Mungu ailaze roho ya mama mahali pema peponi. AMEN
ReplyDeletemungu ailaze roho ya marehemu mahali peme peponi,gladys,puli,doreen na mwesi mungu awatie nguvu katika wakati huu mgumu.tumuombee na ametukumbusha kujiandaa kwa safari kila mmoja wetu,
ReplyDeletepoleni wafiwa kwa msiba huu, mboa maelezo naona yananichanganya, huyu ni mama yao kina carlson na skeeter mwaibula au mama yao kina gradys? Maana wote kina mwaibula, samahani kama nitakuwa nimewakwaza lkn hao wote ni majirani zangu...
ReplyDeletekwako04.23.00 huyu ni Mary J Mwaibula Ni mama ya Gladys, Doreen Prisca Na victor Rweyendela. Dada ya Dick, David etc. mdogo wa dada Ester Muro wa Atlanta Ga.
ReplyDeleteMary ni mpenzi na shahidi mzuri sana wa bwana wa mabwana Yesu Kristo.
Mungu amulaze pema peponi. Pole sana Adam Mwaibura, Glady, Maria Adam Mwaibura. Familia ya Kichwabuta inawapa pole sana.
ReplyDeleteAzizi, Nebraska USA