Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia Airlines imekwama uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar ilikotua jioni ya leo milango ya saa kumi hivi ikitokea Addis Ababa na abiria kibao wa Dar.
Habari za uhakika kutoka visiwani humo zinasema ndege hiyo yenye namba ya mruko ET 805 ilikuwa imechelewa kiasi cha masaa manne kutua Dar na kwa vile ina kawaida ya kupitia Zenji kutoka Dar kubeba abiria, ikaonelewa kwamba heri ipite kwanza Zanzibar na kubeba abiria ili isisumbuke tena kwenda visiwani wakati wa kuondoka.
Ilipotua Zenji ndege hiyo ilipata matatizo ya kiufundi na kulazimika kutafuta ufumbuzi kwa masaa kadhaa na kushindikana, ikiwa ni kutoka saa kumi jioni hadi saa nne usiku. Hivyo abiria zaidi ya 45 waliotakiwa kushuka Dar leo wamejikuta wakipelekwa mahotelini ili kusubiri safari kesho asubuhi ambapo inasemekana zimekodishwa ndege za Precision Air kuwavusha bahari.
Wenye mizigo mingi wameahidiwa kuletewa mizigo yao kesho na ndege kubwa itayofika mchana.
Zogo kubwa liliumuka uwanjani hapo, hasa toka kwa abiria wanaounganisha ndege kuelekea kwingineko, na pia wafanyabishara ambao walikuwa wametoka mashariki ya mbali wakiwa na bidhaa kadhaa mahususi kwa Idd el Fitr inayotarajiwa wikiendi hii ama Jumatatu kutegemea na kuandama kwa mwezi.
Globu ya Jamii inafuatilia sakata hili
na itatoa taarifa za hatma ya safari hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. ikizingatiwa JNIA-dar airport kuna wizi wawe makini. safari hii lazima nimkabe mtu hapo.

    ReplyDelete
  2. He! Hilo zogo lilitokana na nini? Yaani baadhi ya abiria walitaka ndege iwarushe hivyohivyo ingali ikiwa na matatizo? Kipi hasa kinachowakimbiza Dar? Biashara? Connection kwa ndege zingine? Itakuwaje wasipofika huko Dar na kuishia kilindini mwa bahari ya Hindi? Jamani tumieni ubongo mliopewa na Mungu kufikiria! Hiyo ndege imetengenezwa kwa mikono ya binadamu, hupata matatizo. Cha muhimu kufika salama na si kuwahi hayo mambo, maisha ni ya thamani sana kupita hivyo vitu vinavyowapandisha hasira. Come down, Mungu amewaepusha kifo - who knows?

    That was a good decision from Ethiopian Airlines! Dont just rush with an air craft with some technical problems which are known. I am pleased!

    ReplyDelete
  3. Zogo la nini as it is beyond anybody control around there, plane too do get breakdown, but don't forget that ETHIOPIAN AIRLINE has a reputation of the safest and reliable airline in the world.

    ReplyDelete
  4. ndugu zetu mbona atupenda kuna nini kwani kuna ubaya gani kufika kwetu mapema watu walikuwa Airport wanatusubiri atujanaona kwa miaka mingi??

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...