Habari za kazi Anko Misupu
a.k.a anko Nanilii kama anavyojiita mwenyewe,

Uwanja wetu mpya wa taifa ulishakamilika muda mrefu na kufnguliwa lakini kama taswira inavyoonekana yale mabati yanawekwa na kuzungushiwa kama uzio wakati wa ujenzi mpaka leo hayajaondolewa yapo yapo tu kama yanavyoonekana yanaleta picha mbaya na kuharibu taswira ya uwanja hapo

Mdau mwanaharakati

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hayo mabati watu wanayachorea dili usiwe na wasi utaamka kesho kutwa utakuta hayapo! na mathalani ushatangaza humu sisi watu wa scrap metal tunandaa nyenzo zetu ili tukautoe uchafu ule. Huu ndo mwendo wa maisha katika shamba la bibi!

    ReplyDelete
  2. Tizo la watanzania akuna anaye jiamini na kazi yake,Hapo anasubiriwa JK kutoa tamko la kuyatoa,akyamwungu vile.

    ReplyDelete
  3. wanawasubiri wachina waliojenga uwanja waje wayatoe

    ReplyDelete
  4. Wananchi msiwe na shaka. Mchakato unaendelea. Kila kitu kina utaratibu

    ReplyDelete
  5. Tunasubiri warrant period ya uwanja iishe tutatoa, msilete ngebe zenu hapa.

    By Management
    National stadium

    ReplyDelete
  6. hahahaha kaka umesahau kuwa hii ni bongo land???????????? ukute pesa ya ukuta ilishaliwa cku mingi sana. sasa wafanyaje wakati wanaendelea kusaka mahela huo ndio ukuta 4 the tym being. usiwamaindi sana kijana

    ReplyDelete
  7. Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa utawala wa sheria. faili la hayo mabati limepelekwa OFISI ya DPP Mr. Feleshi. sasa mafaili yamekuwa mengi hata mafaili ya Rada na kagoda bado yako kwa feleshi. wadanganyika kuweni na subiri.

    ReplyDelete
  8. Hii imenigusa. kwa kawaida watu huingia mpirani katika muda unaopishana kabla ya mpambano na baadya ya mpambano kuanza (waliochelewa nk). Lakini watu wote hutoka kwa wakati mmoja punde mpira unapoisha.

    naanisha uwepo wa mabati hayo utaleta maafa kama sio hivi karibuni basi baadaye. wakati wa kuingia hakuna msongamano na hivyo milango inayotumika inatosha. wakati wa kutoka huwa kuna msongamano wa watu usiomithilika. ukiongezea na mdundiko (yanga ikimfunga hayawani, mathalani(not vice versa)). watu watakuja kukanyagana (stampede)halafu tukatafuta mchawi kumbe wachawi sie wenyewe.

    Post zako michu za leo hasa ya pancha zote kali sana.

    ReplyDelete
  9. nchi inaongozwa tu kama mifugo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...