skwadi zima la the kilimanjaro band 'wana njenje' tayari kuduarisha salender bridge club jijini siku ya iddi mosi na kisha kila jumamosi watakuwa hapo na si new msasani tena
nyota na waziri wakipongezwa kwa kuduarisha
wapennzi wao kwenye moja ya shoo zao
wadau wakiburudika kwa raha zao na njenje. hapo unapigwa 'boko'
kiongozi wa the kilimanjaro band 'wana njenje' waziri ally akisimamia ujenzi wa jukwaa katika viwanja vya salender bridge club (zamani italian club na pia pink coconut) karibu na kituo cha polisi na daraja la salender jijini dar tayari kwa mduara wa kwanza siku ya iddi mosi na baadaye kila jumamosi. hawatokuwa new msasani tena
maandalizi ya kukaribisha njenje salender bridge club yakiendelea kwa kasi sana
taswira ya salender bridge club usiku. parking ya kumwaga,
ulinzi kama nanihii na maraha kama ya enzi za ambassador plaza. ukikosa mi simo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ni kweli patakuwa bomba ila jamani sehemu nyingi sana za burudani bongo msalani kunakuwa ovyo sanna mara ukute hakuna maji mara hakuna tishu kama kuna maji ni lindoo lichafuuu ndo lina maji na mkikombe wa kunywea mbege umo ndani yani ni full fungus hakuna sabuni mimaji chini plus kojo unaanza kukutana nalo mlangoni yani starehe za bongo karaha wanakazana kuwauzia manywaji maulaji sasa pakwenda kuvishushia is not richabo inakera sana jamani jitahidini na humo chooni mtu ni afya ikitokea umedondosha kiselula chako ndo basi tena manake mh! starehe inakuwa adhabu muweke vyoo viwe safi sio ombi ni amri mtu ni afya!
    miss michuzi

    ReplyDelete
  2. Hello Mtoa Maoni: Anonymous Sat Sep 19, 02:30:00 PM

    Napenda kuungana nawe na yote uliyo yasema hapo juu..sehemu zetu nyingi za starehe kule nyumbani TZ hata iwe inavutia vingi kwa huduma na vilaji na chakula, wanashindwa kabisa kutunza mazingira ya chooni...na hilo tatizo nimeliona pia kwenye clubs nyingi za Ki-Afrika huku ughaibuni...Naamini Wa- Afrika tuna nature ya kutojali kanuni za afya.

    ReplyDelete
  3. Hongereni Wananjenje mmependeza kwenye mavazi yenu ya nyeusi na nyeupe hasa mjomba Kitime... na dada Nyota ndiyo zaidi!
    Pia ninawasifu kwa mafanikio mliyo nayo na kutunza viwango vya utendaji kazi. Kwa takwimu za harakaharaka bendi nyingi za Bongo hazidumu na pia viwango hushuka kadiri siku zinavyozidi kwenda.

    ReplyDelete
  4. Naungana nanyi sio club tu hata katika migahawa yetu hali ndiyo hiyo hiyo.Pia wateja/watumiaji tunakuwa ovyo vile vile hatujali wapi tunashushia kojo ili mradi kojo litoke mwilini.

    ReplyDelete
  5. na sie kina dada ndio tumezidi kwa uchafu. mtu anatoika chooni na kuja kuitupa toilet paper kwenye sink. ukimwangalia alivyojisiliba na mipoda, miwanja, mi-lipstick na uchafu aliouacha unatamani ukamuumbue mbele ya mpenziwe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...