Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odingawakitazama ngoma baada ya Waziri Mkuu, Pinda kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta eapoti kwa ziara ya siku mbili.
WAZIRI MKUU ATAKA NCHI ZA EAC
ZIUNGANISHE NGUVU KIUCHUMI
Na Irene Bwire, Nairobi
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kuna haja ya nchi wanachamawa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuunganisha nguvu za kiuchumi ili kuweza kukamatasoko la pamoja kwa ajili ya bidhaa zinazozalishwa na nchi hizo.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Septemba 2, 2009) wakati akifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Kenya Bw. Raila Odinga kwenye ofisi zake zilizoko jengo la Hazina, Mjini Nairobi, Kenya.
Waziri Mkuu ambaye yuko nchini Kenya kwa ziara ya sikumbili ya kikazi amesema kuna haja ya kuunganisha nguvu za jumuiya za sasa zaCOMESA na SADC ili kuweeza kukamata soko soko kubwa ambalo litahudumia bidhaa zinazozalishwa na nchi hizi.
Akizungumzia kuhusu biashara kati ya Tanzania na Kenya,waziri Mkuu amesema Watanzania hawana budi kuamka na kuchangamkia fursazilizopo ili waweze kuuza zaidi upande wa pili kama ambavyo wenzao wa Kenya wamekuwa wakifanya.
Mapema akizungumza katika kikao hicho, Waziri Mkuu wa Kenya, Bw. Odinga alisema Kenya hivi sasa inakabiliwa na hali mbaya ya ukamepamoja na njaa kwa sababu imekumbwa na matatizo makubwa matatu tangu waingie madarakani mwaka huu.
Alisema machafuko ya kisiasa yaliyoikumba nchi hiyo yalikuwa ni pigo la kwanza ambalo lilisababisha watu washindwe kufanya kazi za uzalishaji kwa kuhofia usalama wa maisha yao.
Wakati wakitatua tatizo hilo walipwatwa na ukame na pigo la mwisho lilikuwa ni mtikisiko wa kiuchumi ambaoumezikumba nchi nyingi.
Alisema mvua zinazotarajiwa kunyesha mwezi huu huenda zikasadia kuikoanchi hiyo na janga la ukame na njaa ambalo limeikumba nchi hiyo.
Mchana huu Mh. Pinda ametembelea kituo cha utafiti cha Kilimo cha Kenya (Kenya Agricultural Research Institute -KARI) na baadaye jioni amekutana na Watanzania wapatao 200 ambao wanaishi hapa Kenya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Wakulu wa Kunyumba wote ziarani nje ya Tanzania!

    Mh. Raisi Kikwete, Tripoli Libya maadhimisho ya mapinduzi ya September 1.

    Mh Makamu wa Raisi Dr. Shein, Geneva Uswisi masuala ya hewa.

    Mh. Waziri Mkuu Pinda, Nairobi Kenya.

    Kwa hiyo kikatiba Mkulu wa Nyumba ni Spika wa Bunge Mh. Sitta? au Jaji Mkuu Ramadhani?, tukumbushane somo la uraia/siasa.

    Mdau
    Kivukoni

    ReplyDelete
  2. ..mdau hapo juu umenchekesha uliposema 'kunyumb' ukan'kumbusha watani zangu wa bomb'bili..saa nna-imagine mmoja akistaajabu anazungumza peke yake: "iv' kumwachi' six uyu uy', six uyu'uyu kunyumb' ii? na uku majuz' juz' tu kumwek' kit mot' six uyu'uyu, six uyu'uyu six!?..

    ReplyDelete
  3. Nina sababu za kuamini kuwa JK ameisharudi. Kwa hiyo ondoa hofu Anon wa sa 06:39. Kesho atafungua benki ya wanawsake asubuhi.

    ReplyDelete
  4. SASA HII IMEKUWA KICHEKESHO. YAANI VIONGOZI WETU HAWAKAI OFISINI. SIKUBALI KUWA KAZI WAZIFANYAZO WAKIWA SAFARINI NI SAWA NA KUZIFANYA KWA UTULIVU WAKIWA OFISINI. DUNIA NZIMA SIZANI KUNA KIONGOZI ANA SAFIRI MARA NYINGI KAMA HUYU WETU. KWANI NI LAZIMA AENDE KILA ANAPO ALIKWA. RAISI WETU ANA ACT KAMA VILE YEYE NI CELEBRITY NA ANASAHAU KUWA YEYE NI KIONGOZI WA NCHI.

    ReplyDelete
  5. NCHI IMEWEKWA REHANI, LAST TIME NILICHEKI MZEE SITTA ALIKUWA KAJICHIMBIA URAMBO NA MH. RAMADHANI ALIKUWA ARUSHA, WACHENI PANYA WAFANYE MAMBOZ PAKA HAWAPO.

    ReplyDelete
  6. Jaji Mkuu anachukua hapo. Spika si walimwengua kwenye hii kitu kwani CCM wajanja wanajua siku moja Spika anaweza toka Upinzani kwa hiyo Spika ameenguliwa na Waziri Mkuu ndio akapewa nafasi yake.

    CCM kweli inaona mbali manake sasa hivi ingekuwa songombinde, Mzee Six angechukua halafu anaitisha lile file lake aone nani anasema nini kuhusu yeye

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...