Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya nakala za misahafu kutoka kwa Dr. Abdel – Baqi (kushoto) wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur’an tukufu yaliyofanyika katika Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam huku Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkullo (kulia) akishuhudia. Mashindano hayo yaliandaliwa na ubalozi wa Misri kupitia kituo chake cha utamaduni kiitwacho Egyptian Islamic Center na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) mkoa wa Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. samahani lakini hilo baibui si saizi yake hiyo dizaini inatakiwa iwe chini kabisa ya nido na si katikati wala juu.

    ReplyDelete
  2. KUNA MDAU MMOJA ALINIFUMBUA KUWA KIARABU NI LUGHA KAMA KISWAHILI PIA WAKRISTU WAARABU HUWA WANA MASHINDANO YA KUSOMA BIBLIA ZA KIARABU.

    ReplyDelete
  3. sasa wanaolalamikia kwamba ubalozi wa Vatican uko kwa ajili ya wakristo peke yao wanasema nini kwa kitendo hiki cha ubalozi wa Misri kuwa na kituo cha utamaduni kinachoandaa mashindano ya kusoma Koran?

    pia wamefuatilia mwenendo wa ubalozi wa Iran?

    ReplyDelete
  4. huyo alokufumbua anaonesha ni kalulu kama wewe,kwa kukuelimishia ni wamba kiarabu na quran ni ligha mbili tofauti kabisa,na ingeuwa quran ni kiarbu basi hata wewe ungeielewa kwa kiasi kikubwa kwa sababu kiswahili asilimia 75 ni kiarabu,kwa mfano mchache ni maneno kama tafadhali,shukrani,yatima,masikini,rais,na mengine kibao,na hata miji na mitaa mingi ya tz ni majina ya iarabu,kama dar es salaam,zanzibar,ilala na mengineyo.

    ReplyDelete
  5. Mkuu, Kiswahili asilimia 75 ni Kiarabu? Una hakika? Kama una hakika hebu tuhakikishie hapa kwa data. Zanzibar na Ilala ni maneno ya Kiarabu? Nini maana ya maneno Zanzibar na Ilala kwa Kiswahili? Halafu naomba ututajie majina ya Kiarabu ya mitaa.

    ReplyDelete
  6. anony wa tarehe 14 sept.04:06:00
    naomba utuambie rais/mfalme wa Vatican,mawaziri,wabunge,jeshi nk.

    ReplyDelete
  7. zanzibr asili yake ni zenjbar na maana yake ni kisiwa cha watu weusi,sema muingereza akashindwa uitamka na ikaitwa zanzibar,ilala imetokana jina la mwenyzi mungu y laila hailalah,lakini wazee wa pale walifupisha kuita ilalah,walivyokuja watu wasioweza kutamka na kulipelekea kuwa ilala,kwa kiswahili ni mchangnyiko ya lugha tatu,kibantu,kiarabu na kiingereza,kihindi pia kiliingizwa kidogo kwenye vitu kama chai,ukiangalia maneno mengi ya kiswahili sahihi kwenye kamusi utagundua kinatokana na kiarabu,kwa uongeza kuna vitu ama hakimu,yatima,fukara.na hata hesabu,kama sita,saba,arobaini,.majina ama mola,mungu.fikra,hesabu.tunaweza kuijaza blog mzee.kwa ushauri tafuta kamusi ya kiswshili ili ujijibu.

    ReplyDelete
  8. Anon Tue Sep 15, 12:42:00 PM,

    Naomba tafsiri ya maneno yafuatayo toka Kiarabu kwenda Kiswahili;

    Kisiwa =

    Watu =

    Weusi =

    Mimi si mwanataaluma wa lugha wala historia naomba unifahamishe umepata wapi maelezo ya neno Ilala yametokana na kama ninavyokunukuu hapa "lala imetokana jina la mwenyzi mungu y laila hailalah,"

    Halafu una hakika maneno Mola na Mungu ni maneno ya Kiarabu?

    Umeshawahi kuwasikia WaFulani toka Afrika Magharibi wakihesabu. Kama umewahi kuwasikia naomba utupe maelezo yako. Na kama hujawahi kuwasikia naomba utafiti halafu utuambie.

    Ninazo kamusi tatu za Kiswahili. Mbili ni za zamani sana zilizoandikwa na kina Bwana Krapf, Madan, Steere na Johnson. Kamusi nyingine niliyonayo ni ile iliyotolewa na Baraza la Kiswahili Tanzania. Sasa naomba unielekeze nizitumie vipi ili nijijibu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...