

Nondozzz za Bongo ni bora - Mrisho
Imeelezwa kuwa pamoja na kuwepo kwa mapungufu kadhaa katika utekelezaji wa mtaala wa Elimu Tanzania, mtaala huo umefanikiwa kwa kiasi kukubwa kuifanya Tanzania kuwa ni moja ya nchi zinazotoa wahitimu bora wanaothaminika kwenye medani za kimataifa.
Hayo yameelewa na Katibu Mkuu mstaafu, Vincent Mrisho, wakati akiwasilisha rasimu ya Mtaala mpya wa Elimu Tanzania kwenye warsha ya Azaki ya kuchangia maoni juu ya sera ya Elimu na Mafunzo iliandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania, TENMET, kwenye ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Bwana Mrisho alisema kuwa Elimu iliyotolewa na Mkoloni, ilikuwa ni elimu bora kukidhi matakwa ya wakoloni, na baada ya uhuru, tukaanzisha elimu ya kujitegemea iliyoleta mafanikio makubwa.
Bwana Vincent Mrisho amesema ni kutokana na ubora wa Elimu ya Tanzania ndio maana wasomi wa Kitanzania waliosemea Tanzania toka awali mpaka vyuo vikuu, wanashinda nafasi mbalimbali za ajira za kimataifa na kutolea mfano Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rose Migiro.
Nae Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, TENMENT, Dr. Joseph Kisanji, amekiri kuwepo kwa mapungufu katika mtaala uliopo hivyo kuhalalisha hitaji la mtaala mpya wa elimu Tanzania utaokakidhi mahitaji ya sasa likiwemo suala zima la utandawazi.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Elimu Tanzania, Pascal Mdemu, amesema maoni ya wadau ni muhimu sana katika mchakato wa uundwajwi wa mtaala mpya ndio maana serikali umeiweka wazi rasimu hiyo ili ijadiliwe kwa kina na uwazi na hatimaye kupatikana kwa mtaala huo mpya wa elimu Tanzania.
Akifungua majadiliano hayo ya siku moja, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo, Prof. Hamisi Dihenga, aliwahakikishia wadau hao kuwa serikali itazingatia kwa makini maoni yao ili kuzidi kuuboresha mtaala huo mpya unaotarajiwa kukamilika hivi karibuni. Jumla ya Asasi za Kiraia zaidi ya 50 zinazojihusisha na masuala ya elimu nchini zimeshiriki.
huyo Mrisho kachemka hajui hata anachosifia ndo maana wenzake wanaona mapungufu na wanajadili ili yaboreshwe ye anasema iko bomba,hao ndo Makatibu wakuu wetu maadam ye alikuwa hapo kachota zake kaondoka hivyo hana sababu ya kutaka mfumo uboreshwe!!!?
ReplyDeleteHiyo elimu bora tuliyo nayo imewezesha watu wetu kuvumbua chochote? Kuna mbongo kakanyaga mwezi? Tunapata elimu ya kuajiriwa, sio kujitegemea. Huyo Dk Migiro naye ameajiriwa, sio kujitegemea. Siasa za nafasi za juu za UN ni nzito, muulize Dk Boutros Boutros Ghali kilichomnyima ulaji.
ReplyDeleteSijui anasifia nini, vyuoni vitabu ni vya miaka ya 80. Anaingiza siasa na hapo, maana leo hii msomi wa chuo kikuu haajiriki si Tz tu ambapo Katibu wa wizara ya utalii last week alisema kazi nyingi zinachukuliwa na majirani zetu sababu ya elimu yetu duni na mapungufu ya lugha. Tatizo journalists na WEWE ANKO mnakaa tu mtu huyo ungemuuliza elimu yetu ni bora ukilinganisha na miaka ya 60 au elimu ya nchi gani? Mambo yaleyale kama ya televised Q & A last wk.
ReplyDeleteMlowezi.
Wa-tz huwa tunasifia tu hata vitu ambavyo si kweli. Enzi ya mkoloni watu walikaa chini? Elimu yetu bado ya chini na ifike kipindi tukubali English nayo iwe kipimo cha kukua elimu maana mambo hayaendi bila English, BBA mmeona, Interview ya mkuu wa nchi kwenye CNN nayo mliona the, the nyingi. Tusijifanye oo mbona Japan, French, German hayo ni mataifa makubwa!!!! ELIMU HAIJAKUA USITUDANGANYE.
ReplyDeleteUS.
Katika picha ya 1. Katibu mkuu Prof. Dihenga ni aliyekaa kushoto na sio Katikati. Aliyekaa katikati ndie Nd. Pascal Mdemu
ReplyDeleteANNON O4:30 JUU YA ALAMA MAONI YAKO YANAFUNGA NA KUFUNGUA MJADALA. NIMGEKUFAHAMU NINGEKUMWWAGIA KAKA DOLA KUMI ZA MUDA WA MAONGEZI KWA SIMU YAKO. ASANTE SANA
ReplyDeleteunatupotosha, kama hujui watu kaa kimya, eti dihenda (kati, Dihenag ni huoyo wa mwisho kushoko.........
ReplyDeleteDR GHALI ALINYIMWA ULAJI KWA KUWA MKWELI NA WA HAKI KUKATA KUBURUZWA KAMA MWANASESERE.
ReplyDeletewasifa wake huu
http://www.notablebiographies.com/Be-Br/Boutros-Ghali-Boutros.html
Nimefarijika sana kusikia kuwa muda si mrefu nasi elimu yetu ya msingi itaanza kutolewa kwa Kiingereza. Tulikuwa tunawekwa kati sana, maana ukiingia shule ya msingi unaambiwa usiongee kikabila,bali ongea kitaifa (Kiswahili) na ukifika upili/sekondari unaambiwa usiongee kitaifa (Kiswahili) bali ongea kimataifa (kiingereza)
ReplyDeleteNi hayo tu... najua, ndiyo! Kwani vipi
jamaniii huyo anaitwa PROF DIHENGA na sio vingenevyo
ReplyDeleteMichu, msimamo wa vyuo bora ktk afrika, UDSM ni chuo kikuu bora cha 15 Afrika, namba ktk mabano ni msimamo Duniani. Tuendelee kukata mzizi wa fitna bin fitina
ReplyDeleteThe InternetLab Ranking of 30 Top African Universities
Rank University Country World Rank
1 University of Cape Town South Africa (398)
2 Universiteit Stellenbosch South Africa (566)
3 Universiteit van Pretoria - University of Pretoria South Africa (718)
4 University of the Witwatersrand South Africa (720)
5 Rhodes University South Africa (738)
6 University of South Africa South Africa (1,449)
7 University of the Western Cape South Africa (1,553)
8 American University in Cairo Egypt (1,826)
9 Noordwes Universiteit - North West University South Africa (1,857)
10 University of KwaZulu-Natal South Africa (2,214)
11 University of Johannesburg South Africa (2,3230
12 University of the Free State South Africa (2,369)
13 Université de La Reunion France (2,387)
14 Nelson Mandela Metropolitan University South Africa (2,542)
15 University of Dar Es Salam Tanzania (2,819)
16 University of Zimbabwe Zimbabwe (3,072)
17 Al Akhawayn University in
Ifrane Morocco (3,174)
18 Cape Technikon South Africa (3,414 )
19 University of Mauritius Mauritius (3,682)
20 University of Zululand South Africa (3,724)
Source: InternetLab (Observatorio de Ciencia y Tecnologia en Internet)
http://www.socialcapitalgateway.org/eng-rankingafrica.htm---------------------------------------------
Mdau
Mlimani
Kwa wakaanga mbuyu:
ReplyDeleteTop 100 Universities and Colleges in Africa by 4icu.org Web Popularity Ranking
1 Cairo University Egypt
2 University of Cape Town South Africa
3 University of Pretoria South Africa
4 Mansoura University Egypt
5 Helwan University Egypt
6 University of KwaZulu-Natal South Africa
7 University of the Witwatersrand South Africa
8 The American University in Cairo Egypt
9 German University in Cairo Egypt
10 Zagazig University Egypt
11 Tanta University Egypt
12 University of Ghana Ghana
13 University of Dar es Salaam Tanzania
14 Assiut University Egypt
15 Alexandria University Egypt
16 Minufiya University Egypt
17 South Valley University Egypt
18 Benha University Egypt
19 Al Azhar University Egypt
Last update: 12/09/2009
print share link send
4 International Colleges & Universities • About us • Link to us • Site map • www.4icu.org
wadau hizo rank zenu mbona zipo outdated Mon Sep 14, 02:05:00 PM hiyo ranking ni ya kwako au ni org ya egypt?udsm inaelekea 30 africa,univ of capetown ipo top 200 sasa hivi
ReplyDeleteelimu yetu kila siku inazidi kushuka
Hizo ranking zenu hazionyeshi ubora wa elimu ya UDSM, zinaonyesha ubovu wa elimu ya Afrika.
ReplyDeleteHivi kiwango cha elimu kinapimwaje?
ReplyDeleteKama kweli elimu yetu ni nzuri hivi, kwanini kwenye University zetu kuna wanafunzi wanajisaidia lakini hawa-flush choo baada ya kukitumia?
Kwanini wanafunzi wetu wanaingilia dirishani wakipanda basi?
Kwanini kitanda cha kulala mtu mmoja kinalaliwa na watu wawili bwenini?
Kwanini "Computer room" inafungwa eti kwa sababu kuna wanafunzi wataiba "mouse"?
Kwanini mwanafunzi wa University anakosha chungu alichopikia na kumwaga maji yenye ukoko kwenye "flower beds" na kukaribisha mbu?
Naomba mnifahamishe hivi kiwango cha elimu kinapimwaje hapa kwetu?
Chifu Matangalu,
ReplyDeleteUtamaduni wa mtu na mazingira atokayo mtu hayajifichi. Hivyo usishangae sana, ndo maana India wanatambua hayo, choo lazima kiwe cha kuchuchumaa ndiyo mambo yanaenda vizuri.
Kuhusu hizo flower bed kutupiwa ukoko ni yaleyale, maana tumezoea bustani za maharage na mchicha kuzipatia mbolea na siyo flower beds za Roses kwa urembo..
Hizo Ranking za Vyuo Afrika toka kwa wadau zinaonyesha TZ ni namba 13 na 15, pia vyuo ni vile vile Afrika Ya Kusini, Egypt , Tanzania.
Hivyo kwa Tanzania ni sahihi kitakwimu kuwa hapo, ila Egypt na Afrika ya Kusini labda wanajipendelea, kwa sources hizo mbili zinaangukia Nchi moja hivyo utafiti zaidi unatakiwa.
Hivyo UDSM kuwa ya 13 au 14 source tofauti, inaonyesha tupo juu.
Mlimani juu juu zaidi.
Mdau
Prof. wa Kijiweni.
WABONGO TUMEZIDI SANA SIASA NA POROJO.
ReplyDeleteMHESHIMIWA MICHUZI NAOMBA UMTAFUTE HUYU JAMAA ANAYEDAI ELIMU YETU NI BORA AJE AFAFANUE ALIKUWA ANAMAANISHA NINI, NA HIVYO ALIVYO VITAJA HAPO NDIVYO VIGEZO VINAVYOTUMIWA KUELEZEA KUWA ELIMU YETU NI BORA AU NI BORA ELIMU?
NAOMBA UMUOJI NA UMREKODI ALAFU TUWEKEE HIZO VIDEO. NAAMAINI TUNA MENGI YAKUCHANGIA
duu..hata mimi nisiyewajua viongozi leo nitachangia..jamani ukiangalia picha ya pili kutoka juu Dihenga ni huyo aliyekaa kushoto na amekunja mikono kwa pamoja..
ReplyDeleteKuhusu issue ya rank za vyuo vyetu nafikiri lazima tuelewe ya kwamba chuo kama chuo mpk kuwa kwenye nafasi fulani kuna mambo mengi sana yanazingatiwa sasa sioni haja ya watu kuanza kutoana macho. Mfano ikiwepo na masuala mazima ya Ada, number ya wanafunzi wanao anza na kumaliza shule bila ya kuacha, idadi ya maprofesa na madaktari, uwingi wa wanafunzi, research zinazofanyika na mengineyo
hivi nyie mnaotoa sifa zote hizi kwa udsm mmewahi kutembelea vyuo vikuu na taasisi za uchunguzi za nchi nyingine?
ReplyDeletemmefika ujerumani,uingereza,japan,finland,australia,usa, na mkaona jinsi wanavyoendesha vyuo vyao vikuu? nazungumzia vile vyuo vinavyoitwa 1st tier university.
elimu ya tanzania inazidi kushuka viwango. mtu mwenye akili zake timamu hawezi kudai kwamba mazingira ya udsm miaka ya 70/80 wakati wa kina dr.migiro ni sawa na ya miaka hii.
UDSM ni chuo kikuu kwa hapa bongo lakina hakina hadhi ya University kimataifa. Kilikuwa University zamani lakini sasa hivi yamebakia mauzauza tuu.
ReplyDeleteMungu amlaze mahali pema peponi mwenyekiti wa Tenment ndg Pascal Mdemu aliyefariki dunia siku ya jumamosi tarehe 19/09/09 huko Mwanza alipokuwa amekwenda kikazi. Mungu awape nguvu wafiwa wote na namuomba amlaze marehemu mahali peme peponi, Amina
ReplyDelete