wachezaji wa timu ya taifa ya chini ya umri wa miaka 17 a.k.a serengeti boys wakirejea leo toka kahrtoum, sudan, ambako walishiriki kombe la challenji ambapo waliibuka washindi wa tatu baada ya kuifunga sudan bao 2-0 katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu. kabla ya hapo walitolewa kwa shida kwenye nusu fainali kwa mabao ya penati. eritrea ndio waliobeba ubingwa kwa kuilaza uganda kwenye fainali.
waziri wa habari, utamaduni na michezo, mh. george mkuchika, na maofisa wa michezo na wa kampuni ya serengeti wakiwapokea serengeti boys leo.
kocha wa serengeti boys rodrigo stockler akiongea na wanahabari
serengeti boys wakielekea kwenye gari maalum
serengeti boys wakifurahia kurudi nyumbani baada ya kufanya vyema kwenye michuano ya chalenji yaliyoshirikisha nchi 11.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Ati kuwa Mshindi wa tatu tumefanya vizuri.... huu ni ukenge

    ReplyDelete
  2. Wewe mchangiaji wa kwanza ndio kenge, fedhuli mwanaharamu usie na shukrani. Je wangekuwa washindi wa kumi na moja ungesemaje? ungejisikia raha? au unadhani hao waloshika nafasi ya nne mpaka ya kumi na moja sio watu wenye akili zao timamu, mandondocha? you people sometimes you have to appreciate other people's efforts. mnakera kama pilipili kichaa

    ReplyDelete
  3. mejitahidi hongereni sana

    ReplyDelete
  4. kisiju.
    Natoa hongera zangu za dhati kwa mafanikio hayo. Cha muhimu na cha kusikitisha ni mfumo ambao upo chini ya TFF. Tujiulize. hivi wale vijana waliochukuaa kombe la Coca Cola Brazil asilimia 90% wako wapi? Je TFF wanachukua hatua gani katika kulinda kizazi kijacho cha soka letu la Tanzani? Ama mpaka aje mzungu awe Raisi wa TFF ndio ufanisi uonekane?
    Ni ujinga mtu na inasikitisha sana.

    Watu kua washindi wa tatu kwenye mashindano ya kimataifa ni hatu ya kujivunia hata ikiwa ni mashindano ya kucheka tu.

    Swali, serikali na wizara yake ya michezo inachukulia vipi swala la kukuza na kudumisha hivi vizazi vya baadae vya Taifa letu. Tukiwa kama wananchi tunasikitishwa sana na mifumo ya kijinga ambayo ipo na watu wanajivunia.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa kwanza sijui namna gani. Mashindano yaliyopita tulishika nafasi ya ngapi? Mashindano haya tumeshika nafasi ya ngapi? Huoni kwamba tumepiga hatua mbele? Ukumbuke kwamba moja ya timu tulizozifunga ni Malawi ambayo itashiriki katika fainali za mashindano ya vijana afrika au duniani sijui.
    Mdau unayehoji vijana wa Copa Coca Brazil nk kama umefuatilia utagundua Maximo amekuwa akichanganyia vijana kwenye timu ya wakubwa. TFF timu zao ni za taifa lakini klabu zilipaswa kuwanyakua wachezaji hao kwa ajili ya ligi. Yawezekana wengine wameamua kutoendelea na mpira kwa maamuzi binafsi. Lakini changamoto ni kwa klabu zetu kulea chipukizi, hasa TFF wanapowarahisishia kwa kuwaweka mbele ya macho ya watu.

    ReplyDelete
  6. Kisiju

    Mjomba kama uneelewa kuhusu mifumo ilioko hapa kwetu Tanzania usingejaribu kunijibu. Hawa jamaa wa TFF na wizara yao ya michezo ni bure na waste of space. Wale watoto walioshinda Brazil ni watatu tu ambao Maximo anawatumia na haukuna hata mmoja anechezea timu yoyote. Kama mtu anauwezo kama ya wale vijana na hawa basi tusingekua wasindikizaji kwenye mashindano makubwa. Generation ya akina Njiti Geremi Wome na kazalika wa timu ya taifa ya Cameroon walilelewa na matunda yameonekana.
    Sisi wajuba wa kibongo tubakie hivyohivyo. Hatuendelei kamwe chini ya uongozi huu wa TFF.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...