baadhi ya mastaa wa simba sc wakiwa kambini. hiki ndicho kikosi kinachosemekana ndiyo kilikuwa bora kuliko wakati wowote ule kutokea mtaa wa msimbazi. wenye data msaada tutani tafadhali. mie hapo naanza na wa kwanza kushoto kaka yusuf kaungu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Simba hii kweli sio mchezo niliowatambua mimi niwa3 toka shoto ni Nico Demas Njohole wa5 toka shoto ni Mohamed Bakari Tall wa6 toka shoto ni Adam Sabu garincha wa8 toka shoto Mohamed Kajole Mchella
    Mdau
    Kisiju Pwani

    ReplyDelete
  2. Huyo wa pili kushoto mwenye afro siyo Martin Kikwa huyo?yuko wapi siku hizi?

    ReplyDelete
  3. naona jamaa wako na MP3 players za enzi hizo......na ndiyo walikuwa wajanja wa nyakati hizo.

    ReplyDelete
  4. nimezipenda suruali zao hii fashion ikirudi wanume mtakuwa mko juu sana

    ReplyDelete
  5. haki ya nani ze fulanaz itanoga zaidi ukivaa na suruali mtindo huu kama ya huyo jamaa aliyekunja nne tu
    miss michuzi

    ReplyDelete
  6. Nami naongezea Martin Kikwa, Mohamed Bakari Tall, Adam Sabu, Mohammed Kajole 'Machela'.

    ReplyDelete
  7. Namuona marehemu Martin Kikwa hapo, (RP brother)

    ReplyDelete
  8. Yusuf Kaungu,Martin Kikwa,Aluu Ali dynamo,Ismail Mwarabu,Mohamed Bakari Tall,Athuman Juma,Herman Kiseka,Mohamed Machela Kajole na Lucas Nkondola...wasiomo hapo ni Omar Mahadhi,Athuman Mambosasa,Daudi Salum,Aloo Mwitu,Filbert Rubibira,George Kulagwa,Dan Mwalusamba,Adam Sabu,Jumanne Hassam Masimenti,Thuwein Ali na Abdallah king Kibaden mputa.

    ReplyDelete
  9. Aliyesema Mp3 za siku hizo hajakosea hata mie kichwa changu ndio kilifikiria hivyo Mp3 mwanangu. wametoka pina Tizama Afro zina AFYA sio Drogba na kalikiti.

    ReplyDelete
  10. wengi watakimbilia kusema ‘kibadeni’, hayupo hapo! martin kikwa; aluu ally; yusuf kaungu; mohamed kajole; mohamed bakari tall; alloo mwitu; abdallah hussein; usiniulize yupi ni yupi, mdau..go figure!..

    ReplyDelete
  11. KIKWA, MACHELA KAMA SIKOSEI NA SABU NI MAREHEMU, PIA KUNA KAKA YAKE OMARY HUSSEIN, ALIKUWA ANAITWA KAMA SIKOSEI NI ABDALAH HUSSEIN ALITOKEA MSETO NI WA MWISHO KUSHOTO, MSETO ILIKUWA YA MOROGORO ILIWAHI KUWA BINGWA WA TANZANIA NA MWAKA ULIOFUATIA WACHEZAJI WENGI WALIIBIWA NA SIMBA NA YANGA

    ReplyDelete
  12. SURUALI ZILIKUWA ZINAITWA PEKOSI/PECOS ZILIKUWA PANA CHINI JUU KWEMBAMBA UKITAKA UTOKE UNAVAA NA AMA SHATI AU T-SHIRT YA KUBANA MBAVU NA UNACHANA AFRO YAKO NA LAIZONI/RISE-ON VIATU VYENYE SOLE NDEFU SANA HII YOTE ILIKUWA NI MITINDO TOKA MAJUU KUWAIGA AKINA THE BEATLES (UNITED KINGDOM MUSIC LEGENDS AKINA PAUL MACCA, RINGO STAR - MTALAM U WA TUMBA - DRUMMER, JOHN LENON) NA COOL AND THE GANG) AMERICAN LEGENDS OF THE TIME

    ReplyDelete
  13. zitto kiaratuSeptember 14, 2009

    yussuf kaungu,martin kikwa,aluu ally, nadhani nicodemus njohole,mohamed bakar tall,athman juma,hamisi askari,mohamed kajole na lucas nkondola. hapa wako fresh baada ya kuichabanga nyota afrika (yanga raizoni) takriban june 1976 kule arusha. mambosasa mwaka huo alichezea nyota afrika kwa muda kidogo, akarudi tena msimbazi.

    ReplyDelete
  14. Michuzi kwa kukupa listi ya kamili ya waliomo kwenye picha hiyo ni
    Kutoka kushoto Yusuf Kaungu,Martin Kikwa, Aluu Ally,Ismail Mwarabu,
    Mohamed Tall,Athuman Juma,Hamis Askari,Mohamed Kajole (Machela) na Abdallah Hussein (Kaka yake Omari Hussein ) na hicho kilikuwa kikosi cha 76 na 77 baadae wengi wao wakaondoka kwenda Arabuni (Dubai,Abuu dhabi nk) kucheza mpira wa kulipwa . mfano Kaungu, Aluu Ally na wengine . Mdau Kikopo Leicester UK.

    ReplyDelete
  15. hebu acheni ushabiki wa uongo...hamis askari yuko wapi hapo?...next to kajole ni mganda herman kiseka!

    ReplyDelete
  16. Martin Kikwa ni m'jomba wangu. Maskini ame kufa but I shall never forget him; he was hilarious and generous. M'ungu ata m'saidiia. Sorry for my bad swahili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...