sanamu ya baba wa taifa iliyokuwa katika bustani
ya mnara wa saa jijini mwanza enzi hizo
sehemu iliyokuwepo sanamu ya baba wa taifa hivi sasa iko tupu. haijulikani imeenda wapi, ingawa redio mbao zinadatisha data mbali mbali. moja inasema sura ya sanamu hiyo ilikosewa hivyo imeenda kurekebishwa, ingine inadai kwamba wakuu wameiondoa sanamu hiyo baada ya kukaa bila matunzo kwa muda mrefu kiasi kwamba vinyesi vya ndege viliiharibu na kuleta taswira mbaya. wengine wanasema dili halijakaa sawa. ni matumaini wadau wa mwanza mtatupa jibu muafaka. lakini wadau watembeleao jiji hilo wanalalamika kwa kukosa kumuona mwalimu
mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
hakika wakuu wa mwanza wanajitahidi kuitunza sehemu hii muhimu
kijani cha pahala hapa kinamwagiwa na kutunzwa vyema
mandhari ni ya kuvutia ila pangenoga zaidi endapo kama baba wa taifa angerejeshwa pahala pake. wadau mnasemaje??




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Kwa kweli hiyo sanamu haikuwa na sura ya Mwl. Hongera kwa kuiondoa. Wakuu wa Mwanza, tafuteni msanii wa ukweli atengeneze sanamu la maana, sio ilimuradi!!

    ReplyDelete
  2. Hata ingekuwa na sura yake ni vyema kuiondoa. Tuache hizi tabia za kuweka masanamu huwatumbukiza watu katika ushirikina

    ReplyDelete
  3. Acheni uongo hapo sio Mwanza ni Thailand

    ReplyDelete
  4. Mwanza hapo, hivi huoni hilo tangazo la Zain?

    ReplyDelete
  5. hapo mpiga picha hajachukua picha yote ya mandhari ya hiyo bustani ni nzuri zaidi ya uionavyo kwenye picha. mwanza ni safi,hongera viongozi na sasa mmempata mkuu wa mkoa kandoro a.k.a man of actions na siyo yule mpayukaji wa chama sipati picha baada ya miaka miwili itakuwaje, Ameondoka dar sasa hivi tunaiona kazi ya lukuvi

    SANAMU ZA MWL ZILIZOPO ZINATOSHA JAMANI...

    ReplyDelete
  6. Hatuna la kusema

    ReplyDelete
  7. SASA MASANAMU YA NINI?

    ReplyDelete
  8. hakuna maana kusimika masanamu mijini

    ReplyDelete
  9. Hilo Sanamu linatusaidia nini?Mbona kina Kinjekitile Ngwale hakuna masanamu yao?Hao ndio mababa wa Taifa walimwaga damu zao.Nyerere katugawa Watanzania kwa udini na ukabila(ingawa nitaonekana nisiyejua historia) leo hii Wazanzibari hawatupendi kabisaa kwa sababu ya Nyerere(Zamani wazee wetu walipelekwa Zanzibar kulelewa na kupata akhlaq njema) leo hakuna kutokana na huyu Nyerere.Haina haja ya kuwa na sanamu lake

    ReplyDelete
  10. huyu ndo alotumaskinisha akatufanya maimuna!
    kanumba uongooo?!

    ReplyDelete
  11. i wish ningekujua anony hapo juu kama hujui historia bora unyamaze kama ulivyosema, wazanzibar hawatupendi kwa ujinga wao kama wewe usiojuo kwanini husome na kuuliza

    ReplyDelete
  12. Sat Sep 12, 06:00:00 PM, sijui mpewe nini ndugu zangu mje mridhike.au labda wakristo wakristo wahamishiwe nchi nyingine mbaki peke yenu TZ?

    sanamu na majina ya barabara,mitaa,vyuo,hospitali,organizations,majengo,viwanja vya michezo&biashara vinatosha mpk sasa hivi ukimwambia mtu mkutane kwa mwl nyerere maswali lukuki kichwani maana hakuelewi

    ReplyDelete
  13. Kandoro kaikuta Mwanza ikiwa safi tayari, kuna mtu mmoja watu hawamtaji, huyu ni Wilson Mbonea Kabwe ambaye niMkurugenzi wa jiji la Mwanza, kaenda huko akitokea mbeya ambako alifanya kazi kubwa sana tu, na baada ya kuondoka mbeya ikaanza kunuka vibaya!
    Nadhani wakuu wetu wangempeleka DAR baada ya mwaka tofauti ingeonekana kwani jamaa ana uwezo sio hawa wakurugenzi wengine wanaoteuliwa kimitandao tu.
    Mdau wa libeneke la misupu.

    ReplyDelete
  14. Mwanza ina madhari manzuri sana siyo mDar bwana nyamazeni kabisaaa sukumaland lazima tujifunie the land of opportunity ha ha ha Dar mpo basi mtaka yote kwa pupa hukosa yote.

    ReplyDelete
  15. Tusiwe watu wa kuliziki kiasi hiki hiki ni kijisehemu kidogo sana wala sio jiji zima la mwanza, chakufurahiya ni nini?au tnaamini hatuwezi kitu chochote?kuhusu sanabu la Nyerere hatulihitaji sisi,halitusaidii na wala halimsaidii aliko..kwani yeye ndio aliotengeneza kina Kanumba leo hii usiku mmoja ameuona kama miaka kumi kwene jumba LA BIG BRO!!halina faida kwa mnayomuita babaenu wa taifa.

    ReplyDelete
  16. Mh, jamani watoa maoni, wengine mnaponda vitu hata msivyovijua, kama huyo aliyesema hapo Sio Mwanza namshangaa!! Hapo ni Mwanza Babu, mji wa watu huo, na mandhari yake ndiyo hayo na kwa taarifa yako na hali ya hewa inalipa. Mi niko Dar ila niliwahi kuishi Mwanza na ninapafagilia hadi basi. Asante kwa picha nzuri ya bustani. SANAMU HAINA MAANA!!

    ReplyDelete
  17. PUT BABA WA TAIFA BACK IMMEDIATELY PLEASE.GO TO NEW YORK AND SEE THE STATUAL OF THE LIBERTY, EVERY WHERE ALIYEWAPA MWANGA HUKUMBUKWA DAIMA NYIE VIPI??? MSIWE KAMA WENZETU WALIEMCHAGUA MTU MWEUSI KUWA RAISI WAO NA SASA HAWAONI KWA NINI AWAONGOZE, WATANZANIA ACHANE ZA KULETA BABA WA TAIFA ANASTAHILI KUWEKWA KILA MKOA TENA KWA SANAMU KUBWA KABISAAAAAAAAAAA???NDIYE ALIYEWAWEKA MLIPO TODAY HALAAAAAAAAAA!!!

    ReplyDelete
  18. Baba wa taifa arudishwe hapo sio vizuri,kwanza nani kamtoa hapo? No 1 z perfect so MWL alitenda mema kaenda zake...WAREJESHE SANAMU PALE BEFORE 14thOct...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...