
sanamu ya baba wa taifa iliyokuwa katika bustani
ya mnara wa saa jijini mwanza enzi hizo

sehemu iliyokuwepo sanamu ya baba wa taifa hivi sasa iko tupu. haijulikani imeenda wapi, ingawa redio mbao zinadatisha data mbali mbali. moja inasema sura ya sanamu hiyo ilikosewa hivyo imeenda kurekebishwa, ingine inadai kwamba wakuu wameiondoa sanamu hiyo baada ya kukaa bila matunzo kwa muda mrefu kiasi kwamba vinyesi vya ndege viliiharibu na kuleta taswira mbaya. wengine wanasema dili halijakaa sawa. ni matumaini wadau wa mwanza mtatupa jibu muafaka. lakini wadau watembeleao jiji hilo wanalalamika kwa kukosa kumuona mwalimu

mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.
hakika wakuu wa mwanza wanajitahidi kuitunza sehemu hii muhimu

kijani cha pahala hapa kinamwagiwa na kutunzwa vyema

mandhari ni ya kuvutia ila pangenoga zaidi endapo kama baba wa taifa angerejeshwa pahala pake. wadau mnasemaje??
Kwa kweli hiyo sanamu haikuwa na sura ya Mwl. Hongera kwa kuiondoa. Wakuu wa Mwanza, tafuteni msanii wa ukweli atengeneze sanamu la maana, sio ilimuradi!!
ReplyDeleteHata ingekuwa na sura yake ni vyema kuiondoa. Tuache hizi tabia za kuweka masanamu huwatumbukiza watu katika ushirikina
ReplyDeleteAcheni uongo hapo sio Mwanza ni Thailand
ReplyDeleteMwanza hapo, hivi huoni hilo tangazo la Zain?
ReplyDeletehapo mpiga picha hajachukua picha yote ya mandhari ya hiyo bustani ni nzuri zaidi ya uionavyo kwenye picha. mwanza ni safi,hongera viongozi na sasa mmempata mkuu wa mkoa kandoro a.k.a man of actions na siyo yule mpayukaji wa chama sipati picha baada ya miaka miwili itakuwaje, Ameondoka dar sasa hivi tunaiona kazi ya lukuvi
ReplyDeleteSANAMU ZA MWL ZILIZOPO ZINATOSHA JAMANI...
Hatuna la kusema
ReplyDeleteSASA MASANAMU YA NINI?
ReplyDeletehakuna maana kusimika masanamu mijini
ReplyDeleteHilo Sanamu linatusaidia nini?Mbona kina Kinjekitile Ngwale hakuna masanamu yao?Hao ndio mababa wa Taifa walimwaga damu zao.Nyerere katugawa Watanzania kwa udini na ukabila(ingawa nitaonekana nisiyejua historia) leo hii Wazanzibari hawatupendi kabisaa kwa sababu ya Nyerere(Zamani wazee wetu walipelekwa Zanzibar kulelewa na kupata akhlaq njema) leo hakuna kutokana na huyu Nyerere.Haina haja ya kuwa na sanamu lake
ReplyDeletehuyu ndo alotumaskinisha akatufanya maimuna!
ReplyDeletekanumba uongooo?!
i wish ningekujua anony hapo juu kama hujui historia bora unyamaze kama ulivyosema, wazanzibar hawatupendi kwa ujinga wao kama wewe usiojuo kwanini husome na kuuliza
ReplyDeleteSat Sep 12, 06:00:00 PM, sijui mpewe nini ndugu zangu mje mridhike.au labda wakristo wakristo wahamishiwe nchi nyingine mbaki peke yenu TZ?
ReplyDeletesanamu na majina ya barabara,mitaa,vyuo,hospitali,organizations,majengo,viwanja vya michezo&biashara vinatosha mpk sasa hivi ukimwambia mtu mkutane kwa mwl nyerere maswali lukuki kichwani maana hakuelewi
Kandoro kaikuta Mwanza ikiwa safi tayari, kuna mtu mmoja watu hawamtaji, huyu ni Wilson Mbonea Kabwe ambaye niMkurugenzi wa jiji la Mwanza, kaenda huko akitokea mbeya ambako alifanya kazi kubwa sana tu, na baada ya kuondoka mbeya ikaanza kunuka vibaya!
ReplyDeleteNadhani wakuu wetu wangempeleka DAR baada ya mwaka tofauti ingeonekana kwani jamaa ana uwezo sio hawa wakurugenzi wengine wanaoteuliwa kimitandao tu.
Mdau wa libeneke la misupu.
Mwanza ina madhari manzuri sana siyo mDar bwana nyamazeni kabisaaa sukumaland lazima tujifunie the land of opportunity ha ha ha Dar mpo basi mtaka yote kwa pupa hukosa yote.
ReplyDeleteTusiwe watu wa kuliziki kiasi hiki hiki ni kijisehemu kidogo sana wala sio jiji zima la mwanza, chakufurahiya ni nini?au tnaamini hatuwezi kitu chochote?kuhusu sanabu la Nyerere hatulihitaji sisi,halitusaidii na wala halimsaidii aliko..kwani yeye ndio aliotengeneza kina Kanumba leo hii usiku mmoja ameuona kama miaka kumi kwene jumba LA BIG BRO!!halina faida kwa mnayomuita babaenu wa taifa.
ReplyDeleteMh, jamani watoa maoni, wengine mnaponda vitu hata msivyovijua, kama huyo aliyesema hapo Sio Mwanza namshangaa!! Hapo ni Mwanza Babu, mji wa watu huo, na mandhari yake ndiyo hayo na kwa taarifa yako na hali ya hewa inalipa. Mi niko Dar ila niliwahi kuishi Mwanza na ninapafagilia hadi basi. Asante kwa picha nzuri ya bustani. SANAMU HAINA MAANA!!
ReplyDeletePUT BABA WA TAIFA BACK IMMEDIATELY PLEASE.GO TO NEW YORK AND SEE THE STATUAL OF THE LIBERTY, EVERY WHERE ALIYEWAPA MWANGA HUKUMBUKWA DAIMA NYIE VIPI??? MSIWE KAMA WENZETU WALIEMCHAGUA MTU MWEUSI KUWA RAISI WAO NA SASA HAWAONI KWA NINI AWAONGOZE, WATANZANIA ACHANE ZA KULETA BABA WA TAIFA ANASTAHILI KUWEKWA KILA MKOA TENA KWA SANAMU KUBWA KABISAAAAAAAAAAA???NDIYE ALIYEWAWEKA MLIPO TODAY HALAAAAAAAAAA!!!
ReplyDeleteBaba wa taifa arudishwe hapo sio vizuri,kwanza nani kamtoa hapo? No 1 z perfect so MWL alitenda mema kaenda zake...WAREJESHE SANAMU PALE BEFORE 14thOct...
ReplyDelete