Ndugu yangu Michuzi naomba niwaulize Watanzania wenzangu hasa wale wanaoongea english.
Hivi lugha yetu ni swahili au kiswahili? Jana nilipokuwa naangalia Big Brother Africa, mwakilishi kutoka Tanzania alikuwa anamuelimisha mwakilishi kutoka Angola akamwambia "You see we in Tanzania our national language we call it Kiswahili but in Kenya they call it Swahili.
Sasa mimi ninachoelewa Kiswahili ni lugha na watu wake ni Waswahili. Ukiongea English unasema "our national language is Kiswahili and our people are Swahili (Mswahili/Waswahili kwa lugha ya Kiswahili).
Naomba mchango wenu ndugu zangu juu ya hili. Imekaeje hii?
Naitwa Petro,
mswahili.
Ndugu petro nadhani hata wewe mwenyewe bado hujaelewa kabsaa pamoja na kujaribu kufafanua....Hakuna watu wanaoitwa waswahili...kuna Lugha ya kiswahili....na waafrica...
ReplyDeleteSwahilli - in English
Kiswahili - in Swahili
Na ndio maana ukiwa nje ya africa ukiulizwa unatoka wapi unasema from Africa..which country?..Tanzania...tunaongea Swahili language....swahili ni LUGHA na sio watu...KISWAHILI kama unaongea ukiwa unaongewa in swahili language...nadhani utakuwa umenipata.
kutokama na elimu yamgu nikwamba , kiswahili ni kiswakili ila lugha yenyewe inaitwa swahili ukiwa umaongea lugha nyingine kwamfano, kihaya,kipare au kichaga ukiomgea kiiingereza utasema chaga tribe na si kichaga soo ukisema we speak kiswahili hapo utakua umekosea unapaswa kusema we speak SWAHILI... bila shaka tuko pamaja, utakua umeelewa .
ReplyDeletesalaaaam.
ReplyDeletekwa jinsi nijuavyo mimi 'kiswahili' ni wakati unapoongea lugha ya kiswahili na'swahili' ni wakati unatumia kiinglish.
mfano; lugha ya taifa letu ni kiswahili.
'our national language is swhili' NI HAYO TUUUUU
Kwa mtazamo wangu Swahili ndio mzizi wa neno lenyewe. So you have to say "Our language is swahili". Unapo weka 'ki' unakuwa umeongea kiswahili zaidi kuliko english. mara nyingi 'ki' inakuwa imetumika kama 'adjective'. Ni neno tunaloongezea kabla ya neno lenyewe (sijui kisifa au kivumishi....sikumbuki, mi najua kuongea tu)kama ambavyo unaweza kuongezea neno 'u' ukasema 'uswahili' au 'wa' na kusema 'waswahili'.Maana kwa mtazamo mwingine "swahili" is a region, from "Swahili land", eneo la pwani ya Afrika mashariki na visiwa vyake. Kwa mfano mtu hawezi sema "naongea Sukuma", atasema "naongea Kisukuma" au "I speak English" and not "I speak England". Au mtu husema "nakula kisukuma" (ugali mkubwaaaa....lol)akimaanisha namna watu wa "Sukuma land" wanavyokula. Vivyo hivyo kwa Kiswahili tunasema "naongea Kiswahili" kwa maana ya 'kwamba' naongea kawa watu wa swahili land waongeavyo.
ReplyDeleteNadhani nimejitahidi kidogo kujieleza ingawa mambo ya nomino na vitenzi nilishasahau tangu form one mwaka 47.Mdau mwingine ataongezea
Mdau
Cardiff
ukweli ni kuwa lugha ya tanzania ni SWAHILI, lakini unaposema KISWAHILI inamaana umeunganisha na ngeli "KI-VI" ambapo "KI" inasimamia umoja na "VI" inasimamia wingi. na kwa vile lugha ya SWAHIKI ni moja ndio inaanza na ngeli ya "KI" ukiunganisha unapata KI-SWAHILI, na ndio maana wengine utawasikia wakisema VISWAHILI wakimaanisha lugha ya SWAHILI kwenye wingi. kwa kumakizia ni kuwa kila neno la kiswahiki lina mzizi wake ambao haubadiliki hata hila neno ukilibadilisha kwa namna tofauti mfano neno "ANACHEZA" mzizi wake ni "CHEZ" kwa hio unaweza kusema CHEZEANA,CHEZESHA,ANACHEZWA,ANACHEZEA nk lakini juu ya kubalidilisha kote huko mzizi unabaki pale pale " "CHEZ", na ndivo ilivyo kiswahili mzizi ni SWAHILI ndio lugha lakini kwenye umoja unaweka ngeli ya "KI" kwa hio inakuwa KI-SWAHILI.
ReplyDeleteMWISHO NAPENDA KUKWAMBIA KUWA WATANZANIA NDIO WANAJUA LUGHA YA KISWAHILI SANIFU KULIKO WA KENYA.
MH NAONA NA WE NA HUYO BIG BROTHER WOTE MNACHEMKA, LUGHA YETU KISWAHILI UKIONGEA KINGEREZA UNAITA "I AM SPEAKING SWAHILI" UKIANZA NA KI NI SAWA NA "KIINGEREZA" "KISWEDESH" "KIGERUMANI" LAKINI UKIONGEA KISWAHILI UNASEMA i AM SPEAKING "SWEDESH, "GERMANY ETC. sO KISWAHILI IT TIPICALLY UNAONGEA KISWAHILI NOT IN ENGLISH.
ReplyDeleteBWana petro kweli we mswahili na huyo mshiriki wako mswahili vile vile.
ReplyDeleteEnglish = English
Kiswahili= Kiingereza
Swahili = English
Kiswahili = Kiswahili
Sambaa = English
Kisambaa = kiswahili
Haya = English
Kihaya = kiswahili
kiswahili ni kwa kiswahili, swahili ni kwa kizungu, upo hapo!
Mdau No 5 !
KAKA HILI SWALI LA KIZUSHI MPLEKEE KAMUSI YA WEBSTER YAANI SHAKESPERE MTAKATIFU, NABII MTEULE MESIAH YOHANNA MASHAKA. YEYE NDIYE ANAYEELEWAGA MANENO KAMA HAYA KWA MAANA AMESOMA MUZUMBE CHUO CHA UNIVESITY YA ECONOMICS NDIO MAANA ANA AKILI NYINGI KULIKO NYWELE. WATU WOTE WA MUZUMBE MARA NYINGI NI WATU MAKINI SANA WENYE HEKIMA NA BUSARAMKAYA YOHANNA MASHAKA AMBAYE YUKO KWENYE VEKESHENI DARISALAMA. LAKINI KWA MKENYA KUSEMA KWAMBA KISWAHII NI SWAHILI NDO YALE YALE YA KANUMBA
ReplyDeleteKaka michuzi lugha inaitwa Kiswahili na wanaozungumza ni waswahili.Umenipata
ReplyDeleteHaya lete swali jengine???
Michango imeenda shule kweli...nimeelimika.
ReplyDeleteAhsante Wadau.
Mdau No 5..naafikiana na wewe
ReplyDelete"English = English
Kiswahili= Kiingereza
Swahili = English
Kiswahili = Kiswahili
Sambaa = English
Kisambaa = kiswahili
Haya = English
Kihaya = kiswahili"
very clear and imple!!!!
Kwa uelewa wangu naomba na mimi nichangie hapa. KISWAHILI na SWAHILI ni maneno yenye maana sawa kabisa ila yanaonekana ni tofauti kutokana na lugha ambazo zinatumika kutamka maneneo hayo.
ReplyDeleteMfano.
1.- Nimejifunza kuzungumza KISWAHILI
- I learn to speak SWAHILI
2.- Lugha ya KISWAHILI
- SWAHILI Language
Ahante!!
Habari zenu,
ReplyDeleteLugha yetu jin lake ni SWAHILI, ambalo ndio asili ya Kiswahili yaani Ki- ni kiunganishi cha mwanzo tu kuonyesha ni lugha, kwa mfano China, wachina wanaongea lugha gani, KIchina, waingereza KIingereza, wamatumbi, kimatumbi, ki- ni kuonyesha ni lugha tu.
Hata katika lugha zingine ni hivyo hivyo,England wanaongea English, Poland Polish -sh mwishoni ni kuonyesha ni lugha, ktika kiingereza ipo mwisho si lugha yetu inaweza mwanzo.
Swali linauliza alivyo sema Watanzania tunaongea Kiswahili na wakenya wanaonge Swahili..ni sawa....?Nahisi angesema wote tunaongea Swahili. kenya na Tanzania...
ReplyDeleteNaomba nitofautuane na wengi mliokuwa mnaounga mkono kwamba lugha yetu ni Swahili kwa kiinglishi.Watu wa pwani wanaitwa Waswahili kwa kiswahili na Swahili people kwa Kiinglish.Lugha ya Kiswahili inaitwa Kiswahili kwa kiswahili na Kiinglish hakuna tofauti
ReplyDeleteWako Mpemba
Nitoe mfano wa lugha mbili kufafanua.
ReplyDeleteEndapo unaongea Kiingereza, lugha yetu ya taifa ni "Swahili". Endapo unaongea Kiswahili basi lugha yetu ya taifa inaitwa "Kiswahili".
Ni sawa na ambavyo kama unaongea Kiswahili basi yai huitwa "Kiingereza" lakini kama unatema yai basi yai huitwa "English".
Huyo mwakilishi wetu BBA ni yaleyale ya kina KANUMBA!!!!!tutafika tuu hamna shida.
ReplyDeleteHAPA NI NGELI TENA KWA WALE WALIOSOMA KISWAHILI HATA CHA DARASA LA SABA, LUGHA YETU NI SWAHILI UNAPOONGEA KWA KISWAHILI NA KUWEKA KI MWANZONI NI UNAMAANISHA UMOJA WA HIKO KITU KWANI SWAHILI IKO MOJA TU HAMNA SWAHILI INGINE MAHALA POPOTE DUNIANI NA KAMA KIKO NDO HICHI HICHI SO THAT IS WHY TONAWEKA KI MWANZONI KAMA VILI KIHAYA, KINGONI. NA KAMA UNAZUNGUMZA KATIKA ENGLISH UNATAMKA SWAHILI KWA VILE KI HAIKO KATIKA LUGHA YA ENGLISH NA LUGHA YA TAIFA NI SWAHILI
ReplyDeleteNdugu zangu wachangiaji ninawashukuru sana kwa kunielimisha wala sitanii. Asante sasa nimeelewa. Kumbe maneno haya ninayaandika kwa Kiswahili and correctly put I have written these words in swahili. Asanteni sana.
ReplyDeletePetro mswahili.
Ni nini asili ya neno 'swahil'?
ReplyDeleteNi neno litokanalo na lugha ya kiarabu 'sahel' likimaanisha 'pwani', 'ufukweni' au 'coastal' kwa kimatumbi cha ulaya. Likiwa ni neno la kuazimwa toka kiarabu, swahili linamaanisha pwani, na mtu aishiye pwani ni m'pwani' au m'swahili'. Halikadhalika, lugha izungumzwayo na watu wa pwani ikaitwa ki'swahili' . Kwa mantiki hiyo, ni sahihi kuita lugha 'kiswahili' regardless which languange is employed.kama kungekuwa na umuhimu wa kuongeza au kupunguza maneno au viunganishi, basi ni bora neno lote linebadilishwa kwa kiingereza (homework kwa waingereza kutafuta neno mbadala la 'swahili' au 'kiswahili' kwa lugha yao!kama ambavyo akina Shaban Robert walivyoyatunga maneno kama 'Uingereza', 'Ureno'etc ambayo hayamo katika kamusi yoyote duniani zaidi ya ile ya kimatumbi.
kaka michuzi chei chei !
ReplyDeletehapa kinachoendelea wengi wameelekeza kuhusu kiswahili ama swahili. kwanza ieleweke nini maana ya swahili. si kila mtu ni mswahili hapa kuna kila aina ya watu hata petro pengine hafai kuitwa mswahili ! swahili maana yake ni mwambao wa pwani ama costal area kwa kimombo sasa kwa vile tanzania imetawaliwa na wa pwani ndo mana ikawa inazungumza kiswahili lugha ya taifa hili wengi hawataipenda lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.
ndio maana ukiangalia maoni mengi utakuta yana matatizo ya uandishi .
sasa kama wewe ni wa pwani ndio mswahili wengine ni wahaya wamasai na lugha zao zitakua kiswahili, kihaya, kimasai na kadhalika HII NI KWA KISWAHILI kama itakua kwa lugha nyengine basi itakua sawa kusema swahili , haya na masai.
mdau kutoka bwagamoyo mzaramo mswahili.
MLIKUWA MNAMCHEKA KANUMBA BURE KUMBE HATA ELIZABETH HAJUI TOFAUTI YA KISWAHILI NA SWAHILI LOL.
ReplyDeleteDADA YETU KACHEMKA HAPO.
ReplyDeleteyote sawa lakini ukisoma lugha ya kiswahili kama somo lako basi utajua ya kuwa Kiswahili kama lugha kinatokana na lugha za mwambao wa pwani ya bahari ya Hindi na waarabu waliita Sawa-hili na hapo wakoloni kwa kushindwa kutamka sawahili walitamka swahili na tukapata Kiswahili nadhani nimeeleweka.
ReplyDeletewabongo saa ingine tuakiamua kuacha kuosha vinywa tuna akili! Hizi komenti za akili sana kama alivosema mdau hapo juu zimeenda shule hasa!
ReplyDeleteTujipe big five kwa kuchangia hoja bila mswaki leo,
subilaga