Mahakama Kuu leo Shinyanga imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu watatu kwa kupatikana na hatia ya kumwua mtoto wa kiume albino mwenye umri wa miaka 14, Matatizo Dunia, na kumkata miguu yake katika wilaya ya Bukombe katika mkoa wa Shinyanga.

Viungo vya albino hutumiwa katika dawa zinazotumiwa na baadhi ya waganga wa kienyeji wakiwaahidi wateja wao kupata utajiri. Kuna kesi nyingine 50 zinazohusu mauaji ya albino katika mahakama hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. safi sana jino kwa jino
    miss michuzi

    ReplyDelete
  2. Anyongwe, bado mafisadi tu !

    ReplyDelete
  3. way to go! hopefully this will be a wake up call for this ruthless people!

    Mdau wa Juu

    ReplyDelete
  4. Waliomponza mtoto wa watu ni kumwita jina la matatizo dunia, tusiwaite watoto majina yenye kuvuta laana watoto wet tuwaite majina yanye kulenga mema, sio shida, havijawa, havinitishi, taabu

    ReplyDelete
  5. nimefurahi sana kunyongwa. bado mafisadi wangepewa hukumu ya kufungwa maisha mpakandugu wawasahau.na hawa wanao baka jamani wange nyongwa unajua mtu kama mtoto sio wako haikuumi akiwa wako utatamani umuuwe mwenyewe,kama mtoto wa miezi au mwaka na muendelea anabakwa na kuambukizwa ukimwi inauma kama mtoto wako halafu huna msaada wowote mahausigeli kubakwa na baba mwenye nyumba kama sheria ingefuatwa tungekua wamasikini wenye furaha kwa nchi yetu.

    ReplyDelete
  6. hukumu hiyo ingepita kwa mafisadi wadogo wa TRA wanaotunyanyasa kwa kututoza kodi za VAT za 101% badala ya 18%

    ReplyDelete
  7. Kwa mujibu wa hukumu iliyosomwa na jaji, hawa watu hawakuwepo eneo la tukio kwa maana hiyo hawakushiriki moja kwa moja ila ushahidi umeweza kuwatia hatiani moja kwa moja. Swali ni kwamba kwa nini akina Zombe hawakutiwa hatiani kama hawa wakati walikuwa na marehemu wakiwa wazima kwa mara ya mwisho na wakakutwa wamekufa maana mazingira yanashabihiana!!!!!

    ReplyDelete
  8. Watanzania leo mnafurahia HUKUMU YA KIFO kwa Watanzania wenzenu, kweli nchi hii imebadilika.!!

    Wao wameuwa bila HAKI, lakini nani anaipa Serikali/ Mahakama HAKI YA KUTOA MAISHA yA BINADAMU??

    Kama adhabu ya Kifo ingekuwa inapunguza uhalifu wa mauaji kwa nini USA ambako watu wanauliwa na Serikali kila siku lakini Wauwaji bado wapo; tena wengi na wakatili zaidi ya hao wa kwetu huko Shinyanga??

    Hao wangefungwa vifungo vya Maisha...kitendo cha kuwauwa, hakina tofauti na kile wao walichokifanya.

    Umma/Serikali na Mahakama wanapojiwekea uwezo na HAKI ya kuua wanakosa HAKI ya kumzuia raia mwingine kuua...huo ni UNAFIKI.

    "NO TO DEATH PENALTY"

    ReplyDelete
  9. WHY NOT ZOMBE?

    ReplyDelete
  10. MAREHEMU HUWA ANAJUFUNZA NINI BAADA YA KUNYONGWA? NA UMASIKINI UNAOSABABISHA WATU KUFAB=NYA LOLOTE ILI WAAGANE NAO UTAHUKUMIWA NA NA NANI?

    ReplyDelete
  11. Ewe ndugu yangu unaesema No to death penalty. hebu jiulize wewe mwenyewe na halafu ujijibu wewe mwenyewe. Kama aliefanyiwa angekuwa ndugu yako,mama yako au dada yako ungejisikiaje? jibu la swali hilo usinipe mimi. Jiulize wewe mwenyewe na halafu ujijibu wewe mwenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...