kikosi cha yanga ambacho kinasemekana ndicho kilichokamilika kila idara enzi za mwalimu. wenye data msaada tutani. majina na kumbukumbu muhimu ya enzi hii ambayo inasemekana itajirudia baada ya miaka 100

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hili ni Yanga la 1976 ambalo 1977 lilifumka na kuzaa Nyota Afrika ya morogoro na baadae wakahamia Dar kisha wakabadili jina na kuwa Pan Afrika. niliowatambua mimi waliosimama wa2 toka shoto Juma Pondamali Mensha. wa4 toka shoto Mohamed Rishard Adolf wa6 toka shoto Omary Kapera wa7 toka shoto Jafari aAbdullahman. wa8 shoto ni Mohamed Mkeche na wa mwisho ni Muhidin Fadhili. waliokaa wa4 toka shoto ni Kitwana Ramadhani manara propaty na wa6 shoto ni Kassim Manara.
    Mdau
    Kisiju Pwani

    ReplyDelete
  2. Ninae mkumbuka ni Kaka Kitwana Manara, Naomba wadau mnisaidie. Mwinyi Mpeku

    ReplyDelete
  3. Yuko Eliyasi, Muhidin, Omari Kapera, Abramani Mwinyijuma, Boi Weekend, Adam Juma,Sunday Manara Adoph Richard, Mkweche, Kitete.Na hao wengine inabidi tuwatafute watoto wa Mzee Mangara ili watupangie hiyo listi.

    ReplyDelete
  4. Mitchu, nilisha sema mahala pengine, hapa najirudia tuu: ni vigumu kuteua timu moja 'adhimu' ila wachezaji bora tangu timu ipoanza. Kwangu mimi, wafuatao ni wale walonikosha sana (kuwaona na wachache kuwasikia, waliobobea kwanza, kwenye mabao 'hawavumi lakini') kwa Yanga ni: 1. Muhiddin Fadhili/Nyaga (pia Riffat Said, Pondamali, Fungo, Hamis Kinye, Sahau Kambi na Dunia Adonis); 2. Boi Idd Wickens/Hassan Gobbos/ Yusuph Ismail Bana (hapa nimeweka watatu 3, maana nimeshindwa kuwapambanua hawa wawili wa mwisho); 3. Ahmed Amasha/Ken Mkapa (pia Juma Shaaban, Minziro Isaya na Ngandou Ramadhani); 4. Athuman Juma Chama/L. Tenga; 5. Jella Mtagwa/Constatine Kimanda (L. Mwalusako, Abdulrahman Juma, Selemani Jongo, Rashid Idd Chama na Athumani Kilambo!);6. Said Mwamba Kizota/Master C Mkwasa/ Juma Jenerali Mkambi (pia Athuman China, Ahmed Amasha, Methodius Mogella, Yanga Bwanga, Issa Athumani na Jumanne Shiengo...); 7. Omari Hussein Keegan/Abdulrahman Lukongo (pia Sekilojo/Kampala/Majungu na Swed Scud); 8. Mwinda Ramadhani/ Ezekiel Greyson Jujuman (pia Dotto Rutta Mokili..., , Muhiddin Cheupe labda na Athuman Iddi...); 9. Gibson Sembuli/Kitwana Ramadhani Manara (pia Makumbi Juma bonga bonga)10. Sunday Manara/Abeid Mziba (pia Nonda Papii)11. Edibily Lunyamila/Abubakar Salum (pia Saleh Hijja, Godian Mapango, Sikinde Mbunga na labda Ngassa? (miaka ijaaaayo!)); Waalimu: Ruud Gutendorf/Tambwe Leya (Dr. Victor/Peter Mandawa/Boi/Mziray?)
    Ningependa kuleta wazo la wadau kuanzisha/chagua ‘hall of fame’. Waafrika wenzangu na lunyasi nao walete mawazo yao. Pia tupeleke swala hili katika wanasoka wa taifa; wanariadha; wanamuziki; bendi za muziki; marefa, watangazaji na waandishi wengine wa habari na hata wanasiasa. Ikiwezekana pia na ‘waliojikongoja’ wanaweza kuanzishiwa listi yao sababu ‘kiza ni ukosefu wa mwanga/nuru’ hivyo vitu hivi siku zote huenda pamoja..naomba kutoa hoja! – UzenG!

    ReplyDelete
  5. ..katika picha hiyo ngoja nijaribu, wale nlowataja kama ‘the greatest/legends’ nimeandika kwa herufi kubwa: toka kulia walosimama: 1 – sikumtambua; 2 – j PONDAMALI mensah; 3 – sikumtambua; 4 – A. RISHARD; 4 – sikumtambua; 5 – JONGO (?); 6 – jaffar abdulrahman; 7 – m MKWECHE; m FADHILI..walochutama toka kushoto: 1 & 2 - sikuwatambua; 3 – TOSTAO (?); 4 – k MANARA popat; wawili baada ya kitwana sikuwatambua; 7 – r. MWINDA (?); 8 – muhaji Mukhi..mitchu, wachekesha saana kusema hi indo yanga bora!.. hii inanuka upanya-panya kweli, itakua ya kati-1974 ama mapema-saaana- 1975..UzenG!

    ReplyDelete
  6. ..mitchu, ondoa u+&%$#*@!(* wako, hii siyo pan kwel hii? haiwezi kuwa yanga..sifikiri j. abdulrahman, muhaji mukhi na wengine wachache walichezea mwafrika..UzenG!

    ReplyDelete
  7. Hii Ni Pan African A.K.A Panya wala Kandambili na Kupenda sehemu zisizopenyeka Pan African Watoto wa Mtaa wa Swahili. au Wajanja wa Mjini.

    ReplyDelete
  8. KITWANA ALIITWA POPATI SI PROPATY

    ReplyDelete
  9. wa2shoto.juma mensah,zitto kiaratu,adolf,adam juma,omar kapera(rwambo)jaffar,mkweche,na muhidin fadhily.waliokaa toka shoto.godian mapango,moshi dayan,tostao,kitwana manara(bapo)chitete,kassim manara,abrahman juma(captain)na muhaji mukhi.mdau challa boy.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...