Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mkewe
Baadhi ya wanajumuiya waliojitokeza kuimlaki Mh. Pinda
Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda na Mkewe mama Tunu Pinda wakipozi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi wa New Delhi, Bi Jennifer Sumi
PINDA AIPIGA JEKI YA DOLA ELFU MBILI,





PINDA AIPIGA JEKI YA DOLA ELFU MBILI,
JUMUIYA YA WANAFUNZI WA MJINI NEW DELHI - INDIA.
Waziri Mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Ameichangia jumuiya ya watanzania wanaosoma Mjini New Delhi, kiasi cha Dola ELFU MBILI za kimaraekani kwaajili ya kusaidia na kukuza Jumuiya hiyo yenye wanachama takribani Arobaini na Watano wanaosoma vyuo mbalimbali mjini hapa.
Mheshimiwa Waziri Mkuu ,amesema ametoa mchango huo ili kusaidia jumuiya kuendeleza ushirikiano wao na kuwasisistiza kuishi kwa mshikamano na kupendana kwani ndiyo utamaduni wa watanzania, na kuwasisistiza kujivunia utaifa na nchi yao .
Waziri Mkuu huyo ambaye yuko katika ziara ya kikazi ya siku Nne nchini INDIA, alipata fursa ya kukutana na wanajumuiya hao ambao walihoji maswali mbalimbali juu ya mikakati ya serikali katika maendeleo ya watu wa Tanzania na nchi kwa ujumla sambamba na masuala ya Ufisadi ambayo yamekuwa yakiimbwa kila kukicha.
Hata hivyo Waziri PINDA aliwahakikishia wanajumuiya hao kuwa , Serikali inafanya kila inalowezekana kuhakikisha Nchi inasonga mbele na wananchi wanakombolewa kutokana na matatizo mbalimbali, na kuwataka wanajumuiya hao kusoma kwa bidii na kurudi nyumbani kujenga nchi na kuongeza yeye binafsi pia anawapa hamasa watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi kwani amekiri kuwepo kwa manufaa ya raia wa nchi nyingine kufanya kazi nchi nyingine.
Waziri Pinda, pia alisisitiza mshikamamo na umoja kwa jumuiya hiyo na kusema kuwa, Umoja huo unasaidia kuwaleta Watanzania karibu, na kuondokana na upweke wa kuishi mmoja mmoja na kusisitiza kuimarishwa kwake ,na kuongeza kuwa inatia moyo na faraja kwa viongozi wa nchi wanapotembelea na kukutana na wanajumuiya na kusikiliza maoni na ushauri mbalimbali wa kujenga nchi.
Kwa upande wa wanajumuiya hiyo, baadhi walihoji ,ni vipi serikali imejipanga katika suala la kuhakikisha unafuu wa gharama za mawasiliano na usalama baada ya mtambo wa kusambaza mawasiliano wa FIBRE utakapo kamili , huku wengine wakitoa mashaka yao kwa serikali kwa namna inavyoshughulikia mikataba feki ya uwekezaji wakitolea mfano ule wa TRL na ule wa ATCL sambamba na suala la kuwa na kiwanja cha ndege cha kisasa na usalama wa mali za watu kwenye bandari na uwanja wa ndege .
Pamoja na mambo mbalimbali ya kujenga na kuishauri serikali ambapo Waziri Mkuu Pinda aliwatoa hofu wanajumuiya hao kuwa serikali yao iko makini na inahakikisha inafanya kila linalowezekana kurekebisha pale ilipokosea na kwamba ipo siku Tanzania itafanikiwa kama nchi nyingine katika nyanja mbalimbali kwani serikali hiyo ya CCM inania ya dhati ya kueleta maendeleo kwa wananchi wake.
Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, Mbali na kuambatana na Mkewe mama Tunu Pinda , pia alifuatana na baadhi ya mawaziri na manaibu waziri wa wizara mbalimbali, pamoja na viongozi kadhaa wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.
naona ilikuwa mambo juu ya mambo, manake mtoto na maua kichwani kama flower girl. halafu mama pinda nae akamalizia na mshono wa kitchen party!!!
ReplyDeleteNimependa sana suti ya WM. Mhe Pinda hilo ni vazi zuri sana - achana na ushenzi wa mitai ya kujitia kitanzi kila wakati.
ReplyDeletepinda siku zote anapendeza. suti hazina ubaya. anaweza kuvaa nguo za aina yeyote. huyo mke wake sijui nisemaje ana hitaji mtu wa kumfundisha kuvaa. aangalie jinsi mwenzie salma kikwete anavyo pendeza.
ReplyDeleteMheshimiwa waziri mkuu kwakuwa uko india naomba kwa niaba ya Taifa ujaribu kushinikiza serikali ya India kuweza kuwapa tafu wawekezaji wa TRL maana wameitenda serikali yetu na wametuacha wananchi mahali pabaya especially wale tunaotegemea usafiri wa reli. So baada ya kupokea maua, then hit them hard where it hurts!! Afterwards, tutaweka shida chini na kurusha mikono juu 'kubanjuka' wakati wa Eid!!
ReplyDeletejamani dada mwenyekiti wa wanafunzi mmemuona? kama hajatokea downtown Kibondo Kigoma i don't know where else she from
ReplyDeletemdau inglish course,I love your comments man!
ReplyDeleteMi naona hizo DollarBill 2000. angezitoa msaada kwa wanafunzi maskini wanaoskuli hapa hapa bongo.
ReplyDeletewangelipa ada, na matumizi mengine. walioko india watoto wa vigogo bwana.
... mdau Inglish Kozi, you have summerized it short and clear kazi kwa mkuu kulitia hilo maanani.. na kulifanyia kazi... nchi inazidi kuoza kila kukicha, soon watabeba mpaka reli, wameanza na vichwa vya treni.
ReplyDeleteMizengwe Pinda anajua kukata keki ya bethdei siku hizi...jamani jama!
ReplyDelete