Jisajili na M-PESA na uweze kuchangia maendeleo ya timu za Yanga na Simba kupitia M-PESA ili ubahatike kujishindia tiketi MBILI za kwenda kuangalia mechi ya Yanga na Simba 31 Oktoba 2009 uwanja wa Uhuru DSM au jezi ya timu yako.

Kuchangia, fuata maelekezo yafuatayo:


1. Piga *150# kupata orodha ya huduma za M-PESA

2. Bonyeza ‘reply’ na andika namba 5 (Lipa Bili)

3. Bonyeza ‘reply’ na andika namba ya kuchangia ya Simba (500500) au Yanga (200200)

4. Bonyeza ‘reply’ na andika namba ya kumbukumbu - namba ya kadi yako ya uanachama au namba yako ya Vodacom

5. Bonyeza ‘reply’ na andika kiasi unachotaka kuchangia – kuanzia Tsh 2,000 na kuendelea

6. Bonyeza ‘reply’ na andika namba yako ya siri

7. Bonyeza ‘reply’ na andika 1 kwa kuhakikisha.

KUMBUKA

Kujisajili na M-PESA, tembelea Vodashop au wakala yeyote yule wa M-PESA aliyekaribu na wewe ukiwa na kitambulisho chako na ujisajili BURE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Duh Vodacom kweli nyie mnatisha yani siku zote mnapenda maendeleo ya watanzania na sasa kwa kutumia mtandao wenu na Huduma yenu ya M-pesa mmeamua kuboresha hivi vilabu vikongwe Tanzania, Kweli mnastahili pongezi nyingi tu, Hongereni sana.

    ReplyDelete
  2. Yanga oyeeeeeeeeeee, Simba oyeeeeeeeee Vodacom oyeeeeeeee sasa nyie washabiki wa hivi vilabu changieni vilabu vyenu ili muondokane na kuomba omba... na pia mpate kuwa na mipango ya kuendeleza vilabu vyenu Kila la heri

    ReplyDelete
  3. hapo lazima nipate ticket ya kuona hiyo mechi ngoja nichangie timu yangu na najua Vodacom mtanipa VIP ticket au vipi wadau wa Voda?

    ReplyDelete
  4. Yanga Kampuni OyeeOctober 21, 2009

    Vodacom kweli ina majiniasi.

    Naomba nifafanue.

    Simba na Yanga ni brands (majina) kubwa sana hapa nchini. Ni brand ambazo zimeteka nyoyo za Watanzania wengi.

    Tokea utotoni huwa tunajikuta tumeshachagua ama Simba au Yanga. Na tukishachagua huwa hatubadilishi. Ni Simba damu, au Yanga damu. Sijawahi kusikia shabiki amehama toka kuipenda Simba kwenda Yanga ama Yanga kwenda Simba.

    Lakini basi, kutokana na kutokuwa na maono ya mbali, vilabu hivi vimeshindwa kuvuna pesa inayoendana na umaarufu wao.

    Hivyo majiniasi wa Vodacom wameliona hili. Kwa kuunganisha M-Pesa na Simba na Yanga wamefanya "brand association" moja baab kubwa.

    Vilabu aghalabu vimekuwa vikipata pesa toka kwa "wanachama" (ambazo kwa kweli ni vijisenti tu) na wafadhili. Hata hivyo kuna kundi kubwa la mashabiki ambao sio wanachama hivyo hushindwa kuchangia vilabu hivi licha ya kwamba tunavipenda sana.

    Hivyo basi kwa kuweka option ya kutumia simu za mikononi itakuwa rahisi sana kwa mashabiki ambao hawana muda au interest ya kwenda kilabuni, kukata kadi na kulipa ada na michango ya uanachama kwa fedha taslimu kuweza kuchangia vilabu hivi.

    Kikubwa ni vilabu hivi navyo kuamka na kuanza kujiendesha kibiashara.

    Pia vilabu viwe na weledi katika kusimamia mapato na matumizi. Ili vilabu viweze kuhamasisha wanachama kuchangia itakuwa vema vikiweka wazi mapato na matumizi. Endapo pesa zinatumika vema itaongeza hamu ya mashabiki kuchangia.

    Kwa upande mwingine, kadiri watu wengi wanavyoshawishika kuchangia ndipo jina la M-Pesa linavyoimarika.

    Kwa hiyo hawa majamaa wa Vodacom ni majiniasi bwana.

    Heko sana.

    ReplyDelete
  5. mnasema ovyo. me sioni cha ujiniasi ama chochote. kwa nini hadi leo hao wanachama wenye kadi wa yanga/sima hawatoi ada zao. ndo itakua kuchangia?..kuchangia lazima iwepo uwakilishi/viongozi makini; uwajibikaji na ithibati ya maendeleo..ndo maana una friends of simba - hawakuamini kuwapa viongozi wa simba pesa na kadhalika..sipendi kuwa 'nsenene' lakini ndo ukweli wenyewe, kajaribuni tena..

    ReplyDelete
  6. hahaha wewe anony hapo juu lazima utakuwa ni friends of simba, hupendi timu ijitegemee kwasababu unajua timu ikijitegemea kutakuwa hakuna ulaji kabisa, sasa kama hao friends of simba wao ni makini si wawe viongozi ili tujue Moja.... mmefulia mwaka huu uongozi upo na sisi wanachama tutawapa support kwa kuwachangia kwa kutumia M-pesa...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...