Rais Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda wakipozi na maafisa waandamizi aliowaapisha Ikulu jijini Dar leo ambao wako nyuma yao. Toka shoto ni Sethi Kamuhanda (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo) Christopher Sayi (Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji), David Kitundu Jairo kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Jaji Frederick M. Werema (Mwanasheria Mkuu wa Serikali), Prosper Mbena (Katibu wa Rais), Mbarak M. Abdulwakil (Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi), George Masaju kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye kasimama nyuma kabisa. Nyuma Kulia ni Mh. Peniel Lyimo
Katibu mkuu mpya Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Bwana Sethi Kamuhanda akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi katika hafla ambayo Rais aliwaapisha Makatibu wakuu wanne wapya pamoja na Mwanasheria mkuu na Naibu wake Katibu wa Rais Mpya Bwana Prosper Mbena(kulia) akipongezana na katibu mkuu mpya wa wizara ya Nishati na Madini Bwana David Jairo(kushoto) muda mfupi baada ya hafla ya kuwaapisha iliyofanyika ikulu jijini Dar leo. Kabla ya uteuzi mpya Bwana Jairo alikuwa Katibu wa Rais



akitaniana na Bertha Jairo(7) binti wa Katibu Mkuu Mpya wa Wizara ya Madini na
Nishati Bwana David Jairo wakati wa hafla ya kuwaapisha makatibu wakuu wapya wa wizara mbalimbali zilizofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kabla ya uteuzi mpya Bwana Jairo alikuwa katibu wa Rais.






























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. JK ANAPENDELEA SANA HAWA WAKRISTU LAKINI HAWAKAWII KUTOA NYARAKA ZA KANISA KUMSAKAMA.
    KWELI HAKUNA WAISLAM WENYE ELIMU? SABABU ZA KIHISTORIA NDIO KISINGIZIO.AMA HAKIKA TENDA WEMA NENDA ZAKO USINGOJE SHUKRAN ZA WAGALATIA.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi, asante sana kwa kuweka picha hizi za wakubwa. Nakusifu sana kwa umahiri na jinsi unavyoenda na wakati. Ningekuwa na dhamana ya kugawa tuzo, ningekutunuku tuzo ya mwanablog bora. Endeleza uzi huu na usisite kuweka maoni mengi ya ndugu zetu, wawe Wamasai, Wapare, Wachaga, Wamachinga, Wahaya, Wahehe, Wakristo, Wahindu, Waislamu, n.k. Hawa wote pamoja na vijina hivyo ni Watanzania. Chokochoko hizi zinaonesha na kuthibitisha tabia mbaya inayokuwa katika jamii yetu ya ubinafsi. Mungu atunusuru na tusisite kuwasema wenye kuchochea chokochoko hizi. Nawafananisha na mchwa wanaotishia kibanda cha babu na bibi. Kaka Michuzi, naomba uungane nami na Watanzania wanaopenda amani na mshikamano, kukemea tabia ya uchochezi na kulalama. Wengi wetu tunaolaumu Serikali yetu tumekimbia, tunaishi ughaibuni. Unabii gani wa uongo huu? Turudi nyumbani basi tuchangie maendeleo. Ndugu zangu Watanzania tuachane na masimango. Sio haiba yetu hiyo. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Michuzi, umeteleza kidogo. Anayemfuatia Seth Kamuhanda, mwenye tai nyeusi nyuma ya Shein ni Sazi Bundala Salula (Katibu Mkuu, Mambo Ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa) na siyo Christopher Sayi kama ulivyoandika hapo.

    ReplyDelete
  4. Hivi wanawake wa kuongoza Tanzania hakuna au wameisha? Maana naona wamejaa wanaume, nawaza tu

    ReplyDelete
  5. mbona shikamoo jazz tu? ebu ibua yosso!

    ReplyDelete
  6. Maoni kidogo kwa Mdau wa Oct 21 08:01 anayesema kuwa "Wengi wetu tunaolaumu Serikali yetu tumekimbia, tunaishi ughaibuni. Unabii gani wa uongo huu? Turudi nyumbani basi tuchangie maendeleo."

    Katika dunia hii utandawazi watu wote hawawezi kukaa wamerundikana dar es salaam eti kuonyesha uzalendo. watanzania walio nje ya nchi wanachangia sana maendeleo ya nchi, na kwa taarifa yako wanaweza kuwa na uzalendo wa dhati kuliko waliobaki nchini na kufisadi pesa za walipa kodi, walalahoi!! Angaa badala ya kuwaibia walalahoi wanatuma vijisenti kidogo kwa ndugu zao vinavyochangia katika uchumi.

    ReplyDelete
  7. MFUMO DUMEEE.....KUDADADEKI!!

    ReplyDelete
  8. Serikali haina dini. Siyo sababu Kikwete ni Muislamu basa angalie udini. Cha muhimu sasa hivi baada ya uhuru ni kuangalia kwamba balance ya elimu ni kwa wote bila kujali dini n.k. Watanzania wote wanaelewa namna gani elimu ya kikoloni iliwapendelea wakristo. Na ndiyo hao walishika wadhifa mbali mbali serikalini. Nafikiri Waislamu wa Tanzania wamepiga hatua kulingana kama wale wa Ethiopia. Huwezi kuamini kama Ethiopia ina Waislamu wengi kuliko Tanzania. Lakini angalia Huko Ethiopia wanaoshikilia nchi ni Wakristo na wanaotoka nje ya nchi wengi ni wakristo. Ukiongea nao wanajifanya kama Ethiopia hakuna Waislamu.

    ReplyDelete
  9. VIONGOZI HAWA HAKUNA CHOCHOTE NI KUENDELEZA YALE YALE YA ZAMANI. HAWA NI WATU WAMEAMISHWA KUTOKA SEHEMU MOJA KWENDA NYINGINE AU SEHEMU HIYO HIYO NA KUPANDISHWA VYEO. HAKUNA JIPYA HAPA SUIT ZA BURE TU. MTU KAFANYA KAZI OFISI YA MWANASHERIA MKUU TANGU 1984, MIKATABA MIBOVU IMEPITA HAPO AKIWEPO ALIFANYA NINI? KAMA HAKUFANYA CHOCHOTE SASA TUTATEGEMEA ATAFANYA NINI ZAIDI YA KULINDANA TU.

    ISSUE NYINGINE HII NI KWA JK. RAIS MBONA UNAWAPA VYEO WANAUME TU? INA MAANA TANZANIA HAINA WANAWAKE AMBAO WANAWEZA KUFANYA HIZO KAZI? HII NI AIBU SANA KWAKO RAIS KIKWETE. WANAWAKE WALIOSOMA NA WANAENDELEA KUSOMA WATAKUFIKIRIA VIPI WEWE RAIS?

    IN ADDITION, WATU WENGI HAPA WAMEBAKISHA MIAKA MICHACHE WASITAHAFU SERIKALINI HAWA NI WATU WALIOCHOKA HAWANA JIPYA NA WALA HAWATAWEZA KUBUNI MIPANGO YA MUDA MREFU AMBAO NI MUHIMU SANA KWA MAENDELEO. ZAIDI WANAFIKIRIA BADO SI ZAIDI YA MIAKA MITANO NISITAHAFU SASA NIFANYAJE KWA MAISHA YA USITAHAFU. NO IMPACT MR PRESIDENT.

    RAIS UNATAKIWA UCHANGANYE WAZEE NA DAMU CHANGA. DAMU CHANGA INAKUJA NA MAWAZO MAPYA NA MALENGO YA MUDA MREFU.

    MAMBO YAKIENDA HIVI HATUTA PIGA HATUA YEYOTE YA MAANA KWENYE MAENDELEO

    ReplyDelete
  10. - balance mkuu: vijana, wanawake, walemavu, waislamu. upande wa pili wa proportional representation, hii kwatika nyanja ya utawala..ng'oeni mbigiri kabla hazijamea..

    ReplyDelete
  11. Mdau wa Wed Oct 21, 06:27:00 PM,kwani unataka tuwe tunaangalia udini wa mtu kabla ya kuwateua? Mpaka tukahakikishe "usajili" wa dini ya mtu ama kwa shekhe ama maaskofu ndio wateuliwe/kuchaguliwa? Undugu uanataka kuumalizia wapi? Ukimaliza udini kwa kutumia majina(ambayo yote ni ya kugeni), utafuata kubagua kwa kuangalia majina ya kabila gani na huenda ukamalizia na ukoo gani.
    Tanzania ni moja, kwa watu wa dini zote. Hatuwezi kuchambua watu ni dini gani, ina watu wangapi, ngazi gani, mkoa gani, etc.

    ReplyDelete
  12. mdau apo juu ata mie nawaza
    wanawake wasomi hawapo???afu wazee tena waonekana umri wakaribia mboni ndo wamechanguliwa?mana apo labda mdogo kabisa ana miaka 48-50 ana miaka mingapi kustaafu kwa mijibu
    asante kwa uongozi JK

    ReplyDelete
  13. aiseee
    JK anapenda watoto sana,safi sana

    ReplyDelete
  14. KILA NIKIANGALIA SIONI NDUGU YANGU KULA CHEO NIPATE KURUDI BONGO KUJIRUSHA...NA PESA ZA SERIKALI.
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  15. Michuzi huyo mwenye kitenge cha kinigeria ni Agnes Luwago? huyu dada tulikuwa nae jeshini, nadhani ni yeye, please nijulishe kama ni yeye, tumepotezana nae miaka mingi sana. mwambie tuwasiliane kupitia michuzi.

    ReplyDelete
  16. MNALALAMA BURE KAMA NI HIVI!!!!

    Wanawake raia wa Iran kumi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa Maofisa Usalama na Maofisa wa Forodha wa Indonesia baada ya kukamatwa na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya inayokisiwa kuwa na thamani ya US$12.5 million.

    Kwa mujibu wa maofisa wa uwanja wa ndege wa Indonesia wanasema kuwa hiki ni kiasi kikubwa katika historia ya uwanja huo. Jumla ya kilo 26.8 ya unga na Lita 22.8 za madawa mengine yaliyo kwenye hali ya kimiminika yalikamatwa na akina mama hao ambao walikuwa wamevalia Hijab na Baibui Nyeusi ambazo kimsingi huchukuliwa kama ni watu safi.

    Kwa mujibu wa sheria za Malaysia, Brunei, Singapore na Indonesia ukikamatwa na kiwango kinachozidi gramu 200 na kukutwa na hatia mahakamani adhabu yake ni kunyongwa mpaka kufa. gonga hapa kwa habari zaidi.

    ReplyDelete
  17. WE MDAU WA KWANZA JUU KABISA UNADAI JK ANAPENDA SANA WAKRISTO KUWAPA VYEO...WAISLAM WANASOMA MADRASA NA JUZUU, UTAWAPA CHEO GANI???
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  18. wewe mdau monye uk mjinga sana wewe,unafikiri ya duniani yatakufaa sana wewe utakufa utazikwa na utasahuliwa hata elimu yako ya phd..
    akili finyu unaona waislamu wakienda madrasaa hawana phd,master au degree,mshamba sana wewe misifa kujisifu money money kumbe kibaka mkubwa weweee..

    basi kheri ya hao waislamu wanasoma madrasa wanapata kumjua mungu wao kawabiya nini katika mandiko yake matukufu sebuse wewe hata aya zenu za bibilia huzijui mpaka ufunguwe ukurasaa aibu tupu..

    jerekebishe mshamba wewee...waislamu wamesoma ile mbaya wewe hatutaki ukuu wa serikali ya tanzania wewe wala ya majuu.. mimi hapa kwa elimu hunipati na nimuislamu nanimesoma hizo madrasa na pia elimu hapa ndo penyewe nikitua bongo iam a hot cake ajira nje nje watanitafuta mimi hiyo serikali yako..

    mshamba mkubwa weweee....mwenye upeo finyuuu.
    michuzi usibaniye commment hii please.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...