ALIYEKUWA Mkurugenzi wa utumishi na utawala wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Amatus Liyumba (pichani),ambaye anakabiliwa na tuhuma za kutumia madaraka vibaya na kuisababishi Serikali hasala ya mabilioni, ndiye aliyekuwa akiagiza kufanyika kwa mabadiliko katika ujenzi wa majengo ya benki hiyo, yaliyoisababishia Serikali kupata hasara.
Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na shahidi wa kwanza kutoka katika upande wa mashitaka wa kesi hiyo, ambayo Liyumba nadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh Bilioni 221, kupitia ujenzi wa majengo pacha ya BoT.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Edson Mkasimongwa, shahidi huyo Seif Mohamed ambaye ni mchunguzi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), alidai mahakamani hapo kuwa Liyumba ndiye aliyekuwa na jukumu la kusimamia ujenzi wa jingo hilo.
Akiongozwa na Wakili wa Serikari Juma Ramadhani, Mohamed alidai kuwa Liyumba alikuwa akitoa maagizo ya kwa aliyekuwa msimamizi wa wakandarasi mkuu wa jengo hilo, juu ya mabadiliko ya jingo bila kupitia kwa bodi ya benki hiyo.
Alidai kuwa Mkuu huyo wa wakandarasi, alikuwa akikubaliana na mabadiliko hayo, na kuidhinisha kufanyika katika jingo, jambo ambalo ni kinyume na makubaliano ya mkataba kati ya benki hiyo na kampuni ya ujenzi wa jengo hilo.
Shahidi huyo alidai kuwa baadhi ya mabadiliko ambayo Liyumba aliyafanya, yalisababisha gharama ya jingo hilo kufikia Dola za Marekani Milioni 357.7, badala ya kiwango kilichoidhinishwa hapo awali cha Dola za Marekani Milioni 73.6.
Aliongeza kuwa katika mkataba ambao BoT iliingia na kampuni ya ujenzi wa jengo hilo, bodi ya ya benki hiyo ilidhinisha gharama hizo za awali kwasabau iliamini kuwa zingetosha kufanyika kwa ujenzi huo.
Kwa mujibu wa shahidi huyo, Liyumba alikuwa akipeleka mapendekezo ya mabadiliko hayo kwa bodi ya benki hiyo, baada ya kuwa mabadiliko kutendeka.
Naye Wakili Hillary Mkate ambaye anamtetea mshitakiwa huyo, alimuuliza shahidi huyo maswali, ambapo Maojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo;
Mkate: maelezo ya mwanzo yalidai kuwa bodi ya BoT iliruhusu mabadiliko hayo kufanyika, je wewe unasemaje juu ya hilo?
Shahidi:hapana Liyumba alikuwa anatoa maagizo, ya mabadiliko na kabla hata ya bodi kuidhinisha na mabadiliko yalikuwa yakifanywa.
Mkate:ni nani ambaye anamamlaka ya kubadili makubaliano yaliyokubaliwa katika mkata?
Shahidi:ni bodi ya benki ndiyo iliyokuwa na uwezo huo, ingawa haikuhusika katika mabadiliko hayo yaliyoisababishia Serikali hasara
Mkate:Imekuwaje Liyumba afanye mabadiliko hayo yanayohusisha mabilioni ya fedha, bila kuihusisha bodi iliyokuwa na mamlaka ya kutoa fedha, wakati yeye alikuwa si mjumbe wa bodi?
Shahidi:Liyumba alikuwa akiidhinisha kwanza mabadiko, kisha alikuwa akirudi kwa bodi na kupeleka taarifa hiyo.
Mkatel:Na bodi hiyo ilikuwa ikisema nini juu ya hilo...???
Shahidi:Mara kadhaa bodi ilikuwa ikimkanya Liyumba kutokana na suala hilo lakini aliendelea kufanya maamuzi bila kuishirikisha bodi.
Wakili Mkate aliendelea kuhoji suala hilo, huku akidai kuwa iweje bodi hiyo ikubaliane na tabia ya Liyumba ya kufanya mabadiliko bila kuishirikisha, na isimchukulie hatua?
Shahidi huyo alionekana kutokuwa na majibu ya maswali hayo.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo, ambapo mahakama hiyo itasikiliza ushahidi wa shahidi wa pili katika kesi hiyo.

Kwanza kabisa pole sana ndugu yangu Michuzi kwa shughuli nzito ya kutuletea habari kila siku. kwa kuchangia tu niliomba kidogo nikupe ushauri wa bure , nilikuwa nakuomba kabla ya kuweka Habari kwenye blog yako ningekuomba uzipitie na kuzisanifu kabla ya kuziweka . hii si mara ya kwanza , Ukirejea kusoma habari uliyoituma utaona umefanya makosa ya lugha si chini ya mara 3 mfano baada ya kuandika Hasara umeandika Hasala( mara 5) ,jengo umeandika jingo( mara 3). sasa Mkuu hapa tunakuwa tunaijenga lugha yetu au tunaibomoa?. ikiwa wewe ni mmoja wa kioo cha jamii hii na pia mwanahabari.
ReplyDeletenawakilisha mdau Leicester UK.
hasala hasala hasala ndio nini mwanzo nilifikiri umekosea tu kuandika lakni kila nikiendelea neno hasala nalikuta ni hiyo inaitwa HSARA HASARA HASARA MWEEEEEEE
ReplyDeleteHe may walk free in the sense that under delegation of tasks to subordnates(the accused),the board of directors remain responsible of any tortuous acts of a delegate.what he had to do was to account.
ReplyDeleteBodi ya Benki kuu kama ilikuwa inaidhinisha kwa nini mtendaji pekee ndio ashitakiwe? Wajumbe wa bodi walitakiwa nao wawe kizimbani.
ReplyDeleteHuyu bwana hana kesi ya kujibu, ukisoma kwa makini flow nzima ya mashitaka unaona "HANA KESI YA KUJIBU".
ReplyDeletehasala HASARA?
ReplyDeleteHakika ni kwamba Ndg A.Liyumba anaonewa sana kwa sababu angalia hata kama alikula pesa lakini majengo ya BOT yanaonekana na kazi ilifanyika. Hakika majengo pacha ya BOT ndio majengo bora kulikoni majengo yote hapa TZ nani anabisha?
ReplyDeleteCha kushangaza ni kwamba mbona watu kama Rostam Azizi na KAGODA yake hajafikishwa mahakamani na hiyo kampuni ya KAGODA imefanya nini kinachoonekana naishauri serikali itende HAKI!!!
Watu tulikuwa tukimcheka bure Kanumba kwa kutokufahamu kiingereza vizuri .Kumbe na hata lugha yetu wenyewe hatuifahamu eti Hasala Hasala .Mmmhhh sasa najua wote kwenye jingo hili la blog ya jamii tupo Hasalani.
ReplyDeleteMI KILIO CHANGU HAPA NI TANZANIA KUWA BADO GIZANI JAMANI INAKERA SANA
ReplyDeleteKIKWETE VIPI BABAAAAAA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
GIZA
Ni yaleyale ya Zombe, ukisoma vizuri mwenendo wa kesi na namna ya maelezo yanayotolewa utagundua kuwa liumba hana kesi ya kujibu. maana kama bodi ilikuwa inakubali kuidhinisha malipo hata baada ya mabadilikomya awali ya ujenzi, basi ni bodi iliyokubali mabadiliko hayo na wala sio Liumba.kesi hizi za kisiasasiasa zitatupeleka pabaya, ikubaliwe tu kuwa kulikuwa na uzembe katika bodi nzima.
ReplyDeleteMAWAKILI WA LIYUMBA NAOMBA MCHUKUE HAYA MASWALI MNISAIDIE KUULIZA HAO MASHAHIDI:
ReplyDelete1. Hiyo hasara ambayo serikali imeingia ni ipi? Je ghorofa ambazo wanadai zimeongezwa alizipeleka nyumbani kwake?
2. Ghorofa zilizoongezeka sasa zinatumika na staff, je TAKUKURU wanataka BoT iendelee kupangisha kwenye majengo ya PPF Tower na NDC?
3. Lipi bora, kujenga nyumba yako mwenyewe au kupangisha floor 3 huko PPF Tower?
4. Ni kwa vipi wajumbe wa bodi hawakujiuzulu kama waliona wanaburuzwa?
Kwa kifupi kwa mwenendo wa mashitaka, Liyumba hana kesi ya kujibu.
Michuzi ni photographer mzuri sana, ila sio mwandishi mzuri. Tafuta mwandishi ktk blog yako or andika ila tafuta mtu wa ku-edit. Hata waandishi wakubwa wa vitabu kama Robin Sharma, Robert Ludlum, Stephen King wana Editore, hawaandiki tu wakachapisha bila mtu mwingine kusaili. Ma-programmer wenzangu mtakubaliana na mimi that huwezi ukaandika code na kuisaili pale inapogoma ku-run, lazma mwenzio aisaili ndo ataliona kosa...we call it "preconception"....so hilo neno hasala ndio vocabulary yake, editer angeiona
ReplyDeleteBig up ANON wa Frid Oct 23,11:47:00AM maana umempa ushauri mzuri na wa kujenga Bw Michuzi pia dogo Michuzi fanyia kazi ushauri uliopewa na mdau ili kuboresha blog yetu hii ya jamii.
ReplyDeleteJamani lakini mjaribu kufirkiria. Mnaposema tafuta mtu wa ku-edit kama Robin Sharma, Robert Ludlum mjue hapo kuna gharama hao watu watataka mishahara ya haja si wana ujuzi na uzoefu wao.
ReplyDeleteBro Mchu ni muandishi wa habari na anataka ujumbe wake uwafikie wadau faster faster sasa nadhani alifanya haraka katika kuandika ndio ikaja hiyo HADALA Upss sorry Hasala Hasala ukichulia pia yeye ni m'bara kwaiyo neno Raah halitumiki sana pia hakuna tofauti ktk Ra na La kwa watu wa bara wengi wetu wazalamo aka wazaramo
ReplyDeleteWajumbe wa Bodi ya BOT walikuwa wanangoja ushahidi tu. Asilimia 80 ya wajumbe hao ni Maprofesor na Madakatari wa fani ya uchumi.
ReplyDeleteInakuwaje watu wa "SYSTEM" mnamgeuka mwenzenu????????????? Au mnataka kututia mchanga wa macho ili tuwaone mmechukua hatua??
ReplyDeleteTunajua mwisho wa kesi mtalazimisha Liyumba afungwe kwa kumuonea tu, lakini nanyie siku zenu zinahesabiwa.
Kama mlimshindwa ZOMBE na ushahidi uliokamilika, huyo jamaa mtamuonea tu. Mbona hamjamsusia majengo yake basi kama amewatia hasara??
ReplyDeleteMzee Lyumba kuwa mwangalifu na hiyo kesi, hao jamaa wana hasira ya kumkosa Zombe................
ReplyDeleteNamkumbuka sana mchizi!!! Kwa nini wanambania lakini? Wezi wengine wote wakubwa wako nje - sielewi.
ReplyDeletehao watu waliomshitaki lyumba pekee inaonesha hawajui wafanyalo, ilipaswa kwanza washitakiwe wanabodi then lyumba angefata baadae.hizi sheria bongo wanasoma wapi vitu vinaonyesha wazi wazi logically.haviitaji form six.hapo ni upuuzi mtupu,mwachieni huyo mzee akapumzike.hiyo mipesa imeshapigwa mgao,huyo mzee ana ubavu wa kuidhinisha mipesa yote bila mkono wa bodi ,mnazidi kupoteza fedha za walipa kodi kuendesha kesi za kipuuzi
ReplyDeletekaka Michuzi, wakili ni Mkatte na sio Mkate, please rekebisha
ReplyDelete...nyambafu...
ReplyDeleteila jamaa yuko fit kinoma mwanaumeee!!cheki icho kifua na kila kesi amebeba chupa ya maji KILIMANJARO
usanii huu?