JK ATEMA CHECHE BUTIAMA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonya vikali kuwa taifa la Tanzania linaweza kuingia katika mgawanyiko mkubwa endapo Watanzania wataendelea kupuuza urithi wa Baba wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere wa kupinga ubaguzi kwa misingi yoyote ile.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonya vikali kuwa taifa la Tanzania linaweza kuingia katika mgawanyiko mkubwa endapo Watanzania wataendelea kupuuza urithi wa Baba wa Taifa, Mwalimu JK Nyerere wa kupinga ubaguzi kwa misingi yoyote ile.
Rais Kikwete ameonya kuwa kuchezea umoja wa kitaifa ni sawa na kumwaga na kucheza na petrol kwenye moto.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa njia isapayo zaidi ya kumuezi Mwalimu Nyerere ni kutekeleza kwa vitendo yote aliyosimamia Mwalimu katika uhai wake ambayo ni pamoja na kudumisha uhuru wa Tanzania, kulinda umoja wa Watanzania, kudumisha maadili mema na kupambana na maadui wakuu wa maendeleo.
Rais Kikwete alikuwa akizungumza kwenye Sherehe za Kuzima Mwenge wa Uhuru mwaka huu zilizofanyika leo, Jumatano, Oktoba 14, 2009, kijijini Butiama, Mkoani Mara sherehe iliyokwenda sambamba na Kumbukumbu za Miaka 10 tokea kifo cha Mwalimu Nyerere.
Sherehe hizo kwenye kijiji cha Butiama ambako alizaliwa na kuzikwa Mwalimu, pia zilikuwa zinahitimisha Wiki ya Taifa ya Vijana, na zilihudhuriwa na wageni kutoka Angola, Mozambique, Namibia na Zimbabwe.
Akizungumza kwenye sherehe hizo, Rais Kikwete ametaja mambo ambayo Watanzania wanastahili kuyafanya ili kuthibitisha kweli kuwa wanamuezi Mwalimu, akisisitiza umuhimu usiokuwa na kifani wa kulinda na kudumisha umoja wa taifa, bila kulimegamenga kwa misingi ya udini, ukabila ama rangi.
“Wapo watu wanafanya mchezo na umuhimu wa kulinda na kudumisha uhuru na umoja wa taifa letu.
Tukifanya mchezo na suala la umoja, tutajuta. Tusidanyike ama tusidanganywe na viongozi wetu wa siasa ama dini kutuingiza katika vitendo vinavyoweza kuvuruga umoja wetu kwa misingi ya dini, ukabila ama rangi,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Uhuru na Umoja ndizo zilikuwa kaulimbiu kubwa na muhimu zaidi za Mwalimu Nyerere na hivyo kama kweli tunataka kumuezi ni lazima tudumishe mambo hayo,” amesema Mwalimu Nyerere na kutoa mwito maalum kwa vyombo vya habari:
“Tusaidieni. Mkiendelea kuwa vipaza sauti vya ujumbe huu wa kuvunja umoja wa kitaifa kwa misingi ya dini, siasa ama ukabila tutaingia katika matatizo makubwa,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Pale Rwanda, mauaji yote yale makubwa yalichochewa na kuongozwa na redio moja tu, Millie Collines (RTLM). Nawaombeni, tusichezee na kumwaga moto kwenye petrol.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Tukigawanyika kwa misingi ya kidini, kikabila ama kwa rangi, hakuna mshindi. Mnajua yaliyowapata majirani zetu. Naviomba vyombo vya habari vipuuzed sauti hizi zinazotaka kuigawa nchi yetu kwa misingi hiyo.
Msipowapa nafasi kwenye televisheni zenu, kwenye magazeti yenu, watanyamaza. Tukiwapuuza, wataacha kutugawa kwa sababu hawa wengine wanalipwa, ili washiriki katika kuvuruga umoja wetu.”
Akizungumzia namna ya kumuezi Mwalimu Nyerere, Rais Kikwete amesema kuwa urithi wa Mwalimu Nyerere ni kudumisha yale yote aliyojenga na kuyasimamia Mwalimu Nyerere kwa kuanzia na uhuru.
“Mwalimu alipigania, alitetea na aliulinda uhuru wetu. Ni wajibu wetu na sisi kufanya hivyo. Kama ni lazima tutaupigania na kujitolea mhanga, kama tulivyofanya mwaka 1978.”
Rais Kikwete amesema jambo jingine ambalo Watanzania wana wajibu wa kumuenzi Mwalimu ni katika moyo wa kujitolewa na kujenga na kudumisha umoja wa taifa la Tanzania.
“Kujenga na kudumisha umoja katika nchi hii ni kazi kubwa sana, Nchi yenye makabila mengi namna hii, yenye makabila mengi kiasi hiki. Lakini Mwalimu alijenga, akadumisha na kutetea umoja wa nchi yetu wakati na baada ya kutoka madarakani,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Mafanikio yake yalitokana na msimamo wake wa kuondoa ubaguzi wa aina zote, wa dini, wa kabila na wa rangi. Tukiipuuza misingi hii, tutabakia na nchi yenye vipande vipande, vipande vya dini hii, vipande vya kabila hili ama lile.”
Rais Kikwete amesema kuwa katika kuondoa ubaguzi huo, viongozi wana wajibu mkubwa zaidi na maalum. “Watu wanatusikiliza, watu wanatuamini, watu wanatufuata. Hivyo, tuhimize watu kuishi kwa pamoja.”
Rais Kikwete pia amesema kuwa Mwalimu alisimamia maadili ya uongozi. “Alichukia rushwa, alichukia uonevu.
Wakati huo tulikuwa na miiko ya uongozi. Lakini miiko hii iliundwa kwa msingi ya kijamaa. Sasa tuko katika uchumi wa soko na ndiyo maana tunajaribu kuweka misingi ya maadili ya uongozi inayoendana na mazingira ya sasa. Tunaandaa miswada miwili ya kuleta miiko mipya ya uongozi katika mazingira mapya.”
"Wakati huo tulikuwa na miiko ya uongozi. Lakini miiko hii iliundwa kwa msingi ya kijamaa. Sasa tuko katika uchumi wa soko na ndiyo maana tunajaribu kuweka misingi ya maadili ya uongozi inayoendana na mazingira ya sasa."
ReplyDeleteWaerevu wakang'amua!
Kama mtundikaji wa habari hii amemnukuu vizuri Mhe Rais JK katika hotuba yake, basi tukubali kuwa safari yetu bado ni ndefu!! Tatizo analoliona na kulisititiza zaidi ya mara nne katika hotuba yake ni "tukigawanyika kwa misingi ya kidini, kikabila, ama kwa rangi hakuna mshindi." Tatitizo la taifa letu sio udini wala ukabila wala rangi (hayo yalikwisha yanatumiwa tu kama mada za siasa). Mhe TATIZO NI TABAKA ZA KIUCHUMI KWA MISINGI YA KIFISADI. Ni masikitiko sana Mhe hilo halioni kama ndio tatitizo la msingi!!!!!!!!!!!! Kweli kaaaaaaaaaaaaaaazi hipo
ReplyDeleteI HAD THIS IDEA, NI KWAMBA SIKU HII SIKU ZA MBELENI IASHIMISHWA KWA WATU KUJITOLEA SEHEMU MBALI MBALI KUANZIA WIKI NZIMA INAYOANGUKIA TAREHE HII KAMA VILE KUFAGIA BARABARA, KUSAFISHA MAENEO YA SHULE, MASOKO, MIFEREJI MICHAFU, KUJENGA BARABARA, MADARASA, MISIKITI, MAKANISA, HOSPITALI,KUJENGA VYANZO VYA MAJI NA KUTEMBELEA WAGONJWA NA WAZEE KUWASAIDIA KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE, KUJITOLEA KWA HALI NA MALI KWA WALE WANAOHITAJI MISAADA NA KUMALIZIA KWA SHEREHE KUBWA SIKU YA TAREHE JIONI KWA MIHADHARA TOFAUTI, NA PIA KUWA NA KONGAMANO KATIKA VYOMBO VYA HABARI NA VYUONI WEEK NZIMA, TUONYESHE NA TUJENGE TABIA YA UPENDO/LOVE NA HARAMBEE KWA AJILI YA WATU WALIOMO MASOMONI YAANI KUWASAIDIA VITU KAMA ADA HIVI TOKA VIDUDU HADI UNIVERSITY, WENYE UWEZO WASAIDIE WATU HAWA
ReplyDeleteKWANI NANI KAFARIKI TENA BUTIAMA MBONA NAONA KAMA KUNA MSIBA MZITO MPAKA RAIS WETU ANAKWENDA HUKO? HEE MAISHA KWELI MAFUPI NI NINI TENA JAMANI?
ReplyDeleteUjamaa wa Nyerere hakuwa ule wa Lenin au Stalin au Mao au Kim Il Sung. Ujamaa wa Nyerere uliojengekea kutokana falsafa ya udugu uliruhusu uchumi wa soko na tena huria ila ulizuia uchumi usiendeshwe ovyovyo na hizo nguvu za soko. Hivyo miiko ya wakati ule wa Azimio la Arusha sasa kubwa ni kuiboresha ili iendane na hali ya sasa mfano ule mwiko kiongozi kutokuwa na nyumba ya kupangisha au hisa katika kampuni la kibepari.
ReplyDeleteHili ndilo nililotegemea kutoka kwa rais wetu safi sana ijapokuwa tabaka la umaskini na utajiri hujalizungumzia sijui umeliacha wapi?
ReplyDeleteNdiyo maana watu wanamuita huyu rais wetu kuwa ni MSANII. Huu ni unafiki uliopita kipimo, kwa sababu anajifanya kuzungumzia watu tuache ubaguzi wakati yeye na wenzake wa mtandao walitumia ubaguzi huo huo katika kumfitini na kumuangusha Salim Ahmed Salim kwenye kinyang'anyiro cha urais. Vilevile, huyu mnafiki anaendeleza sana udini, hasa ndani ya CCM. Ukiangalia kamati kuu ya CCM imejaa Waislamu watupu, wenyeviti wa wanawake, vijana na wazazi wote ni waislamu na yeye ndiye kawapigia kampeni mpaka wakachaguliwa.
ReplyDeleteSasa kaka Michuzi naomba usibanie hii comment hangu. Najua unaweza kuona inakuhusu lakini kuwa mstaarabu na uiweke. Amani!
mchangiaji wa kwanza kabisa SWADAKTA
ReplyDeleteKuwepo kwa Mh.JK na hotuba yake naichukulia kama formality si vinginevyo hotuba yake na vitendo vyake pamoja na viongozi wengi wa CCM na serikali haviwianani hata kidogo malecela naweaza kumuelewa amekiri kuumbuka kwa CCM na viongozi wake kwa kuwalinda mafisadi na kukumbuka methali za Baba wa taifa "Obubisibisi buweri ekilo kirimbura" Mfichaficha maradhi kilio kitamfichua ambapo CCM na viongozi wengi hili tayari liko wazi.Ulikua wakati mzuri kwa JK kutubu na kuungama>AMEINGIA MSIKITINI NA VIATU.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
ReplyDelete