Chura wa Kihansi

Serikali inakabiliwa na changamoto kubwa katika suala zima la hifadhi ya mazingira ya Bonde la mto Kihansi ikiwa ni pamoja na urudishaji wa vyura wa kihansi katika makazi yao ya asili.

Hayo yameelezwa leo na Bwana Dismas Mwikila ambae ni Afisa Mazingira mwandamizi wa Baraza laTaifa la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira (NEMC) alipokuwa akizungumza na viongozi wa serikikali ya vijiji vya Kalengakelu, Udagaji, Chisano Chita na Mgungwe vinavozunguka bonde la mto Kihansi.

Ilikuwa ni wakati wa utambulisho wa mradi wa pili wa hifadhi ya mazingira ya bonde la mto kihansi ambao unahusisha zaidi ushirikishwaji wa wananchi wa maeneo hayo katika hifadhi ya mazingira.

Bwana Mwikila aliongeza kwa kusema kuwa changamoto nyingine kubwa ni ya uchafuzi wa maji utokanao na kilimo cha chakula katika vyanzo vya maji ambacho hupelekea uharibifu mkubwa wa vyanzo hivyo ambao huaribu maji ambayo ni ya manufaa kwa Binadamu na viumbe hai.

Akizungumzia suala la vyura wa Kihansi ambao walipelekwa nchini Marekani, Bwana Mwikila amesema vyura hao wameshazaliana na kufikia zaidi ya elfu tatu ambapo serikali inampango wa kuwarudisha mwishoni mwa mwaka huu (2009) kwa awamu, ambapo awali vyura hao watarejeshwa nchini na kuhifadhiwa katika maabara ya chuo kikuu cha Dar es Salaam katika Idara ya Ziolojia na baadae kupelekwa katika maabara maalum huko Kihansi na hatua ya Mwisho ni ya kuwarudisha katika makazi yao ya asili katika bonde la mto kihansi.

Akizungumzia suala zima la mradi huo, Bwana Mwikila alisisitiza kuwa Mradi huo si wa vyura bali ni mradi wa kuhifadhi mazingira ya bonde la mto kihansi na kuwepo kwa vyura hao ni kiashirio kuwa mazingira hayo yakiboreshwa , watu uzalishaji wa umeme na shughuli za kijamii vyote vitaendelea kwa pamoja na kwa ufanisi.

Awali vyura hao wa kihansi walihamishiwa chini marekani kutokana na uharibifu wa makazi yao ya asili uliotokana na mradi wa kufua umeme uliopelekea maji mengi kutumika katika shughuli hiyo na kupelekea makazi yao kukosa unyevyu vyevu wa kutosha, lakini kwa sasa mradi unaendelea na hali ya kimazingira ni shwari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. aargh! wengine mbona wako shingofeni pale sharifu shamba illa, kwenye madimbwi si bora mkaanze kuwachukua wale sababu wanatufataga mpaka uani, wanatafuta nini kama si uchokozi?! lakini kuwachukua mtabidi muonane na wanaohusika wenyewe maana wanawafuga pale wenyewe ni kama mheshimiwa zungu na wenziwe.

    ReplyDelete
  2. Duu! Churaz Kihansiasis wamepanda ndege na kufika Marekani wakati wadau wamefulia.

    ReplyDelete
  3. Ati mazingira... really?!?! Ili kupata maendeleo lazima tough choices zifanyike... Umeme au chura? Hao vyura wangepigwa picha na historia yao kuandikwa nasi tupate umeme... Kweli kabisa hii kitu mimi hata hainiingii akilini. Wanamazingira mniwie radhi!

    ReplyDelete
  4. dah mambo ya vyura wa nini tena jamani kwanza washafika kwa obama bado wanarudishwa wakaliwe na ze snake huko mwituni ah kweli masikini hazai hata vyura wa bongo wana mikosi kimaisha

    waacheni wale kuku huko unyamwezini mavyura kibao tunayo yanatutosha jamani aaaaaah leteni umeme na maji safi yafike nyumba hadi nyumba mwe!

    mdau uholanzi nasuuza kinywa

    ReplyDelete
  5. Anonymous nadhani kidogo hapo umekosea. Mazingira yakiharibika hata hayo maji ya kuzalisha huo umeme yatakosekana. Na hii ndio inayotokea hivi sasa. Mazingira ni muhimu kwa uhai na maendeleo yetu.

    Anonymous no 2, Mungu aliwaweka hao vyura katika bonde la KIhansi kwa maana yake. Sisi kama binadamu haifai kuamua kuwa'eliminate' kwa visingizio vya maendeleo

    ReplyDelete
  6. Anonymous no. 3, bila ya kutunza mazingira unadhani hata huo umeme utapatikana? Tusijidanganye!

    Anonymous no. 4 Mungu alichagua kuwaweka hawa vyura katika bonde la Kihansi pekee Duniani, kwa hivo definitely alikuwa na sababu zake.

    Jee sisi binadamu tunayo haki ya kuamua kuondoa kiumbe kwa sababu tu tunahitaji umeme? Lazima tuweke balance ili maendeleo yapatikane na mazingira yahifadhiwe

    ReplyDelete
  7. INASEMEKANA HUKO WALIKO HAO VYURA KUNA WATANZANIA WAMECHUKUA VYURA WATOTO NA KUANZISHA PARK ZAO, HUU PIA NI UFISADI, BASI TUREJESHEENI HAO WAZEE WAFIE NYUMBANI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...