
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Pepsi Tanzania Limited (SBC) Rashid Chenja(katikati) akifafanua jana jijini Dar es salaam juu azma ya Kampuni hiyo ya kukuza vipaji vya vijana katika mchezo wa mpira wa kikapu (basketball) kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania kupitia soda ya 7 up gharama ya zaidi ya milioni 10. Mchezo huo unatarajia kuanza Novemba 13 hadi Desemba 15 mwaka huu katika eneo la Mlimani City.
Kushoto ni Rais wa Chama cha Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es salaam Simon Msoffe na kulia ni Katibu wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Kikapu Tanzania Salehe Zonga. (Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar)
Rashid,
ReplyDeleteHabari za siku nyingi sana.
Nakupa hint kama utanikumbuka nitafute, Ok?
Tulipokuwa shule uliniuliza
"Mshikaji utapenda kuwa nani?"
Nikakujibu
"Sociologist Criminologist" Huku nimeupinda mdomo. Ukacheka sana.
Lakini haukuwa mzaha miaka saba baadaye nikaingia chuo kikuu kusoma sociology lakini sikusoma criminology nilimakinikia Juvenile Deliquency kwa sababu chuo nilichosoma criminology ilikuwa inasomwa na watu wa sheria lakini nilifanya fieldwork Probation services na nilikutana na vicriminal chipukizi.
Kwa ridhaa yangu sasa hivi nasoma Social Policy an Introduction cha Ken Balemore na Edwin Griggs naangalia mfumo wa sheria (Criminal Justice).
Nakuona Zonga hapo, nakumbuka enzi za Gymkhana Pazi.
ReplyDeleteToka Hasheem aukate basi ndio wameamka...mlikua wapi siku zote hizo .....
ReplyDeletewe unaesema kwamba tangu hashim aukate basi ndio wameamka, wewe ndio umeamka sio msoffe wala zonga. mie nimewafahamu hao kupitia basketball zaidi ya miaka 20 iliyopita. je hashim kaukata miaka ya 80? hashim amewahi kudunda mpira gymkhana? hashim alikuwepo wakati vijana wanaifunga pazi kwa mara ya kwanza februari 1991?
ReplyDeleteRashid Chenja mtoto wa mjini mtu wa watu.nakuomba ugombee ubunge Temeke.kwani watoto wa mjini ndio nyie.
ReplyDeletemdau-London
Aliyesema kuhusu Hasheem alikuwa anamaanisha hao kina Msofe walikuwa wapi siku zote kukuza vipaji hadi leo? Tunajua hao wamekuwepo siku zote kwenye mambo ya kikapu, lakini hakukuwa na jitihada zozote kubwa za maana za kukuza mchezo, hapa hatuongelei tu kuandaa mashindano don bosco, gymkhana au uwanja wa ndani wa taifa (na hapa inaonyesha ni yale yale tu, hamna jipya). Mimi binafsi nadhani njia bora ya kukuza mchezo wa kikapu ni watu wenye uwezo wa kifedha na/au kiwango fulani cha elimu ya mambo ya biashara (siyo lazima mamilionea), kujikusanya katika vikundi vichache,labda watu 5, na kutafuta funds, either kwa kutoa shares, mikopo, au hela za mfukoni mwao na kuziendesha timu mbalimbali. Ushindani utakapoanza kati ya kikundi na kikundi, na kati ya timu na timu, ndiyo itaongeza msisimko wa wapenzi wa mchezo, na ndiyo hapo makampuni yatakapojitokeza kuinvest zaidi kwenye timu hizo, mfano kwa matangazo kweye jezi, wachezaji bora kutoea kwenye matangazo yao n.k. Kuendesha timu ya kikapu ni rahisi zaidi ya timu ya mpira wa miguu.
ReplyDeleteNiko mbioni kuanzisha a sports club. Nitatoa maelezo zaidi hapa kwa bwana Michuzi nikiwa tayari.
anony sun nov 01, 06:23:00 pm, hao watu wawili kwa namna zote ulizozitaja wamekuwa mbele katika kuendeleza basketball tangu miaka hiyo niliyoitaja (na kabla ya hapo) kama wachezaji, makocha, marefa na viongozi wa mpira wa kikapu. hao ni watu ambao wamekuwa wakitumia pesa zao za mfukoni (japo sio matajiri) kwa ajili ya kikapu tanzania. suala la ufadhili ni kitu kingine manake sisi watanzania kuanzia bmt, wizara husika, vyombo vya habari hadi kiongozi mkuu, kwao mchezo ni mpira wa miguu tu. sasa wanaopenda mpira wa kikapu wafanye nini zaidi ya hapo wakati hata kifua cha udhamini, wanapigiwa fat tu? au wasuse na kuendelea kukosoa kama wengine tunavyofanya?
ReplyDeletemnyonge mnyongeni lakini zonga ana mapenzi ya dhati na mpira wa kikapu tanzania.
Hamna tatizo. Sina baya la kusema kuhusu wao, ingawa nadhani kwa mtazamo wangu, mchezo utaendelezwa si tu kwa kuandaa mashindano na kupata misaada ya jezi na viatu hapa na pale, lakini zaidi itakuwa kwa kujenga timu madhubuti zenye ushindani. Kama nilivyosema makampuni yakiona kuna msisimko, hautahitaji hata kwenda kuwapigia magoti kupata udhamini, watakuja wenyewe tu. Nawatakia kila la kheri, najua kukaa kwenye mchezo huo miaka yote lazima wana mapenzi nao.
ReplyDeleteHeshima.