Mlinzi wa Nyumba ya jirani Emmanuel Damas, akionesha eneo ambalo Charles Masanja alianguka wakati akijaribu kuruka ukuta wa Nyumbani kwake majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo. Baada ya kuanguka, Masanja alifariki muda mfupi baadae wakati akipelekwa Hospitali.
Mjane wa Marehemu Devotha Masanja(pili Kulia) akiwa na waombolezaji wengine, kulia ni Binti wa Marehemu Mourine.

Watotio wa Marehemu Masanja, Baraka, Mourine (kulia)
na mdogo wao Benadetha wakiwa nje ya nyumba yao.
FlashBack Thursday, August 23, 2007: Meneja wa wanja letu la neshno la zamani Charles Masanja (kulia) akimuonesha Mkurugenzi wa Michezo Mh. Thadeo mchanga wa jangwani ulioletwa maalumu kwa ajili ya kusambazwa uwanjani kabla ya nyasi bandia kubandikwa uwanjani hapo.

FastForward, leo: Charlesa Masanya sasa hatunaye. Amekutwa na mauti usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Kimara Kilungure jijini Dar kwa kile kilichoelezwa kwamba aliangukiwa na ukuta wa nyumba yake.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Mh. Gasper Mwembezi, amethibitisha kifo cha Masanja, ambaye alikuwa pia kocha wa mpira wa miguu ambaye aliiwezesha African Sports ya Tanga na timu zingine kung'ara enzi hizo.
Marehemu Masanja pia alipata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa FAT kabla ya kuundwa TFF, akiwa miongoni mwa viongozi wakongwe wa waliokuja kuweka mambo ya soka nchi hii katika mstari ulionyooka
Habari za mipango ya mazishi zitaletwa baada ya kupatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. Oh, noooo!
    Ni habari za kustua sana, huyu bwana ntamkumbuka kama rafiki na mwanamichezo mwenye spirit ya uanamichezo kweli. Alikuwa mtu mwema na mchapa kazi. Alikuwa muwazi na msema ukweli daima.
    God rest his soul in eternal peace, amen
    Emmanuel M.
    Sports writer

    ReplyDelete
  2. que en paz descance companero, amigo, luchador, compatriota querido Licenciado Charles Masanja. Mola awape nguvu na subra wanafamilia wote katika kipindi hiki kigumu.
    Hasta Siempre hermano.

    ReplyDelete
  3. dah poleni sana na msiba but kitu ninachojiuliza hapo ni kwake kwanini aruke ukuta? but anyway kifo hakina formula rest in peace

    ReplyDelete
  4. R.I.P Charles Masanja, but samahani mbona mimi mazingira ya kifo chake siyaelewi, plz kaka michuzi unaweza kutupa habari zaidi

    ReplyDelete
  5. Rest in Peace Brother C. Massanja. But this is confusing.... why did he have to climb the wall? Mungu amrehemu masikini. Poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  6. Kuruka ukuta inatokea mzee hata kama ni kwako au nyumbani.Mimi mara nyingi nilikuwa naruka ukuta nyumbani ninaporudi mida mibaya.nilikuwa sipendi kumuamsha mama yangu aje kunifungulia geti sababu yeye ndo mtu pekee aliyekuwa nyumbani.Niliacha kuruka ukuta baada ya mama kunionya kuwa sio salama na kuniamuru nimpigie simu nikiwa getini then ataamka na kuja kunifungulia...my lovely mama...Labda masanja hakupenda kumsumbua mkewe...

    ReplyDelete
  7. ni habari za kusikitisha. na iweje aruke ukuta? mh!

    ReplyDelete
  8. i will never forget when he came to our rescue at a time when we (rugby team) had no funds, food and a place to stay for six days. although he was reimbursed for going beyond the call of duty at time, we always felt that the we were indebted to him forever because our lives were changed forever after that particular rugby tournament. most of us left to join various colleges in europe, australia and north america thereafter.

    may he rest in eternal peace.

    ReplyDelete
  9. poleni saana wafiwa. swali ni kwa nini alikuwa anatuka ukuta tena usiku namna hiyo/ hiyo nyumba haikuwa na geti??

    ReplyDelete
  10. Ahhhhhhhhhhh! NO, last week nilikuwa likizo akanipigia anasema tuonane as soon I come back, sasa masikini sitamwona ten. TUTA M- MISS KWA MANFREE KIMARA!!.
    RIP!

    ReplyDelete
  11. RIP rafiki yangu Masanja. Kifo hiki kinatuachia fundisho kubwa sana wana ndoa!!!!

    ReplyDelete
  12. poleni sana wafiwa, ni kweli ni kifo cha kushtusha sana especially kwa vile ameondoka ghafla bila kuumwa.. poleni sana, Mungu ndie ajuaye aina ya kifo kitakachotuondosha duniani, angeweza aruke ukuta asidondoke lakini mlinzi wake amchome mkuki akimdhani mwizi, yote anapanga mola, bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana na libarikiwe

    ReplyDelete
  13. Hay wamama mjifunze kufungulia wamume zenu hata warudi saa 7 usiku matokeo yake it seemz alikuwa bwii akakosea timing.RIP Masanja

    ReplyDelete
  14. Utata tu...kwake aruke ukuta...hii habari mbona wasiiseme kwenye kilio...italeta maswali mengi..hata michuzi mwenyewe kajichnganya...kwamba akiruka ukuta..na paragraph ya mwisho ukasema kuwa kinachosemekana aliangukiwa na ukuta..mbona ni balaa....

    ReplyDelete
  15. Mh utata, inakuwaje mtu anaruka ukuta tena mtu mzima na siyo mtoto/kijana alafu nyumbani kwake? Au ndio za mwizi 40 mama kachoka kumfungulia milango saa saba za usiku kila mara.

    ReplyDelete
  16. kweli ni kwake alirukaje ukuta?

    ReplyDelete
  17. kwanza nawapa pole wafiwa wote na watanzania kwa ujumla Mungu ailaze roho ya marehemu pema peponi - Amen
    Michuzi naomba kuuliza na pia ningependa jibu,
    Hivi marehemu kaangukiwa na ukuta au alikuwa anaruka ukuta na jee kama ni kuruka ukuta umeweza kufanya uchunguzi ni kwa nini aruke ukuta nyumbani kwake, na kama kaangukiwa na ukutu how mbn kama utata hivi??

    Mdau Canada

    ReplyDelete
  18. Que dolor!!! no lo creo ni quiero creerlo .. yote kazi ya mungu.. mola ailaze pema pahala peponi roho ya marehemu Charles C Masanja .. un gran buen amigo, hermano de siempre (dRU)

    ReplyDelete
  19. Celestine Charles Massanja (CCM) My beloved best friend may God rest you soul in Peace... Will always remember you in my prayers Celestino!!!! (dRU)

    ReplyDelete
  20. Poleni wanafamilia na watanzania kwa ujumla.

    Kina baba na Kina mama SOMO hilo. Haijalishi ni sababu gani.

    RIP Masanja

    K.O.R.

    ReplyDelete
  21. Mhhh "Akiruka ukuta wa nyumba yake"? Huenda haikuwa mara ya kwanza!Wakubwa hii tuileweje?

    ReplyDelete
  22. Poleni sn wafiwa and may he rest in peace. Ila hili tukio lina utata. Mimi siamini km kaangukiwa na ukuta maana ht ukiangalia picha hakuna sehemu inayooneshwa ukuta umeanguka. Ni dhahiri kwamba ilianguka baada ya kuruka ukuta. Na hapa ndipo tunapopata maswali mengi kuliko majibu kwamba ilikuaje aruke ukuta tena nyumbani kwake??? Ila naamini kuna wanawake wengine ni wakali mno kwa waume zao na inatokea mwanume akichelewa kurud nyumban ht kugonga afunguliwe anaogopa, na matokeo yake ndio km hayo....

    ReplyDelete
  23. Inasikitisha sana kuondokewa na Masanja.

    Lakini chazo cha kifo kina tia wasi wasi sana.

    Hatajua yeye na Mungu wake kuwa alikuwa ametoka wapi usiku wa manane na kwanini arujuke ukuta mtu mzima tena nyumbani kwake wakati mke na watoto wamelala ndani.

    Kwanini hakupigia hodi wamfungilie mlango?

    ReplyDelete
  24. tuchukulie charles alimpigia wife sim aje kufungua mlango, wife akagoma na mzee mzima coz ni mwanamichezo akaamua kuruka ukuta, bahati mbaya ukuta ukamuangukia na kusababisha kifo...bonge la sooo, kina mama mwajifunza nini na tukio ili??? Unc Charles, sie tulikupenda lkn mwenyezi anakupenda zaidi...upumzike kwa amani..RIP

    ReplyDelete
  25. Poleni sana wafiwa.. ila habari hii inachanganya zaidi:

    Marehemu karuka ukuta, tena kumbe kuna mlinzi wa nyumba yake(maelezo ya picha ya 1).. kama mke amekataa kuamka nadhani mlinzi alikuwa getini angemfungulia.. sielewi?

    R.I.P Masanja...

    ReplyDelete
  26. POLENI SANA WAFIWA MUNGU AWAPE NGUVU ZA KUSUBIRI,

    WAUNGWANA TUKUMBUKE KUWA KILA KIFO HUPANGWA NA MTU ANAKUFA KWA SABABU ZAKE

    SEMA SIO VIBAYA IKIWA TUTAJIFUNZA KWA MATOKEO TUNAYOYASIKIA AU TUNAYOYAONA

    HUYU NDUGU YETU KWA UFUPI WA TAARIFA TULIYOANDIKIWA HAPO NA MKUU WA KIJIJI INAONYESHA WAZI HUYU JAMAA ALIKUWA NA TABIA YA KURUKA UKUTA USIKU

    SABABU HAIWEZEKANI MTU URUKE UKUTA NYUMBANI KWAKO LABDA KAMA ALIFUNGIA UFUNGUO WA GETI KWA NDANI NA ILIKUWA HAMNA MTU NDANI

    AU ALIKUWA AKIRUKA UKUTA KWENDA KUFUKIA SHIMO KWA JIRANI.

    HONGERA MKUU WA KIJIJI KWA KUTUFIKISHIA MAMBO MENGI NAMNA HII SEMA TUNAKUOMBA TUPIGIE PICHA WEZI WA AIRPORT NA TRAFIC WALA RUSHWA TUWANYANYAPAE HAPA KIWANJA CHA KUOSHWA DOMO AU KWA LUGHA NYINGINE KUSUKUTUA KINYWA

    mdau uholanzi kama kawaida nawakilisha usemi.

    ReplyDelete
  27. RIP, jamaa amekuwa meneja wa uwanja wa taifa miaka mingi sana, anaweza kuwa inafika 15.

    Kama wengine walivyosema yote ya Mungu. Kuna yule mtoto aliyepona ndege iliyoanguka miezi 3iliyopita, na hii mtu mzima anafariki kwenye ukuta ambao ni mfupi sana. Habari za TZ haziachi kushangaza lakini.

    ReplyDelete
  28. wafiwa poleni sana, inavyoonekana alikuwa amezoa kuruka ukuta nyakati za usiku maana hata ukiangalia kwenye huo ukuta ameweka ngazi za matofali yaelekea hiyo ndo ilkuwa njia yake. kama mama alikuwa mkali hatujui lakini sioni sababu ya kuweka ngazi za matofali kwenye ukuta hii ni hatari pia maana unawanyesha majambawazi njia rahisi ya kuja kuiba

    ReplyDelete
  29. Naushauri Uongozi wa Uwanja wa Taifa umpe huyu mama ulinzi mkali huko aendako maana wazazi wa Masanja wanaweza wasimuelewe kabisa

    ReplyDelete
  30. MIMINAFIKILI ATAKUWA AMEPIGWA JUJU HAIWEZEKANI UKUTA UMWANGUKUE TU HIVI HIVI KUNA MKONO WA MTU. MIMI NAWASILIANA NA FAMILIA YAKE NINA MGANGA MKALI SANA HUKO SUMBAWANGA LAZIMA KIJULIKANE TU

    ReplyDelete
  31. Dah!kweli kosa ni la wote mama na baba tujifunze jamani!R.I.P

    ReplyDelete
  32. Pole sana wafiwa, huo nikienda likizo nyumbani na nikimpigia simu Massanja, dakika moja tu geti la langu kuu hufunguliwa ili niingize gari.

    Mwisho, hili liwe fundisho kwa kina Mama wengine kutufungia geti njee sisi kina baba tunaporudi usiku wa manane kutoka kutafuta riziki ya wao kulala usingizi mnono.

    ReplyDelete
  33. kazi ya mungu haina makosa,habari za kifo mwana michezo wetu zinasikitisha, nazani mama si wakulaumiwa kwa saa saba,possible jamaa alikuwa blii kwa hiyo aliupalamia ukuta kipombepombe,then itakuwa aliangukia kichwa akaflet na akuna msaada kwa masaa kadhaa,possible alipoteza damu nyingi;poleni wafiwa

    ReplyDelete
  34. Hivi nyie mnaowalaumu kina mama kwa nini msilaumu kina baba kutokurudi usiku wa manane na kutegemea kuwa wake zenu watakuwa watumwa wa kuwafungulia magate? Kwa nini msitoe ushauri wa kutembea na funguo na kupunguza kero na ajali?

    Hata hivyo hamjui hasa nini kilichotokea. Waacheni wafiwa waomboleze na amani.

    ReplyDelete
  35. SIJAFUATILIA SANA STORY HII YA KIFO.HUYU MZEE MAREHEMU AMERUKA UKUTA AKIENDA WAPI???NA KWANINI???POLE SANA WAFIWA.
    MDAU MONEY UK.

    ReplyDelete
  36. WEE 01:02:00 AKILI ZAKO ZINACHENGA NINI? HUYO NI MLINZI WA NYUMBA YA JIRANI, MAANA YA JIRANI SI YAKO NI ILIYO KARIBU NA YAKO. lakini umajaribu kuandika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...