Mshindi wa kwanza na wa pili katika shindano hilo watawakilisha Rwanda katika fainali za Miss East Africa zitakazofanyika Desemba 18 mwaka mjini Dar
Mshindi wa shindano la leo ataondoka na kitita cha faranga za Rwanda milioni moja sawa na karibu sh milioni tatu za kitanzania.
Mshindi wa pili ataondoka na Faranga mia tano sawa na karibu milioni moja na nusu za Kitanzania.
Tayari Kamati ya Miss East Africa makao makuu iko mjini hapa kwa ajili ya kushuhudia shindano hilo ambapo Jaji mkuu usiku wa leo atakuwa Rena Callist, mkurugenzi wa Rena Events.
Pia Miss East Africa, anayemaliza muda wake, Claudia Niyonzima atakuwepo kushuhudia shindano hili pamoja na Miss Burundi wa mwaka jana Alice Kaneza.
Wakati shindano hilo linashirikisha warembo hao 12, mchuano mkali zaidi unaonekana kuwahusisha warembo wanne ambao wanachuana kwa vitu vingi.
Nafasi kubwa sana inaonekana kwenda kwa Sabrina kaganza, Leticia umuizayire, Annet Mahoro na Cynthia Akazuba.
Lakini pamoja na hao wanne msichana mwingine ambaye anaweza kufanya maajabu usiku wa leo ni Viviane Umulisa.
Warembo hao juzi walikutana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa hapa, Joseph Habineza ‘Mr Joe’. Jana pia walikutana na Waziri wa Afrika Mashariki wa hapa Monique Mukaruliza.
Warembo wengine ambao wanashiriki shindano hilo ni pamoja na Clarise Ishimwe, Rita Uwera, Pamela Ungabire, Clarise Ushuti na Sonia Uwambambazi,
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...