JK akikata utepe kuzindua rasmi kliniki inayotembea(Mobile Health Lab) kwaajiloi ya kutoa huduma za upimaji ukimwi na huduma nyinginezo za kimaabara katika uwanja wa Shule ya Msingi Ilembo, Mbeya vijijini.Wengine katika picha kushoto ni Mwakilishi wa Jumuiya ya Ulaya Dr.Inge Baumgarten na kulia ni afisa kutoka taasisi ya jeshi la Marekani ya Walter Reeed Army Institute Bwana Edward Sekonde.
Mganga wa meno katika kliniki ya Meno kata ya Ilembo wilaya ya Mbeya vijijini Dr.Marietha Sanga akimpa maelezo JK jinsi mitambo mipya ya kuhudumia wagonjwa wa meno inavyofanyakazi muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuzindua kliniki hiyo jana.

JK akiongea na wafanyakazi wa kujitolea kutoka taasisi ya American Peace Corps Meesh Santoro(wapili kushoto) anayeishi kata ya Ilembo na Jenna Covey anayeishi Isangati Mbeya vijijini muda mfupi baada ya Rais Kikwete kuwahutubia wakazi wa kata ya Ilembo,wilaya ya Mbeya vijijini jana mchana(picha na Freddy Maro).


Sehemu ya umati wa wananchi wa Kata ya Ilembo wakimsikiliza JK alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya Msingi Ilembo,wilaya ya Mbeya vijijini.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...